Pages

Showing posts with label Ofisi ya Waziri Mkuu. Show all posts
Showing posts with label Ofisi ya Waziri Mkuu. Show all posts

Monday, August 27, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akagua shuguli za maendeleo Wilaya ya Mlele

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua uenzi wa daraja la Msyada linalounganisha vijiji vya Mwamapuli na Chamalendi wilayani Mlele Agosti 26,2012.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na vijana wa kijiji cha Kavuddo wilayani mlele wakati alipokagua eneo litakapojengwa daraja linalounganisha eneo la Majimoto na Inyonga wialyani Mlele Agosti 26,2012.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua mashine ya kukoboa mpunga na kupanga madaraja ya mchele katika kijiji cha Mwamapuli wilayani Mlele Agosti 26,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Tuesday, August 7, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Atembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma 2012

Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu baada ya kuwasili katika banda la Wizara katika maonyesho ya Wakulima ya Nanenane kitaifa yanayoendelea mkoani, Dodoma. Wazir Mkuu Mhe. Mizengo Pinda atembelea maonyesho ya Nyuki katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii , katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Mhe. Waziri MKuu akitoa maelezo baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu anaendesha mafunzo maalam ya ufugaji nyuki yanaqyotolewa ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mhe. Waziri MKuu akiangalia sampuli za asali kutoka kwa moja ya wadau wa bidhaa za Nyuki wanaoshiriki maonyesho ya nane nane ndani ya banda la wizara ya Maliasili na Utalii.
Mhe. Waziri Mkuu akiangalia mzinga wa nyuki wasiouma katika shamba darasa la ufugaji nyuki

Sunday, July 29, 2012

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwapongeza Waziri wa Nishati na madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kushoto),NaibuWaziri wa Wazara hiyo, Stephen Masele (wapili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Eliachim Maswi baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo Mjini Dodoma Julai 28,2012. Picha na Ofisi ya Waziri mkuu

Friday, July 27, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika Mazishi Ya Mwalimu Wa Baba Wa Taifa,Mwalimu James Irenge

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mwalimu James Irenge katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Mwisenge Mjini Musoma, Julai 26, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Monday, July 23, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni Mjini Dodoma 23/07/2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 23, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mpanda Kati Said Arfi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 23, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 23, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mpanda Kati , Said Arfi na Mbunge wa Viti Maalum, Agripina Buyogela, Kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma July 23,2012.Picha naOfisiya Waziri Mkuu

Sunday, July 15, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akutana na Bw.Aliko Dangote

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Mwekezaji kutoka Nigeria, Bw.Aliko Dangote (kulia) ambaye anakusudia kujenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, baada ya mazungumzo yao jijini Dar es salaam Julai 15,2012.Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini, Dr. Ishaya Manjabu.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Wafanya Mkutano wa Kamati ya Sensa ya Kitaifa

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif wakiteta katika Mkutano wa Kamati ya Sensa ya Kitaifa uliofanyika Mjini Zanzibar , Julai 14,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kamati ya Sensa ya Kitafa, Mjini Zanzibar Julai 14,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Thursday, July 12, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ashiriki Mazishi Ya shemeji yake, Mzee Sadik Ismail

Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa Mzee Sadik Ismail Katila, shemiji yake Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika mazishi yaliyofanyikaMjiniMpanda Julai 10, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka udongo kwenye kaburi la shemeji yake, Mzee Sadik Ismail Katila katika mazishi yaliyofanyika mjini Mpanda Julai 10,2012. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Tuesday, July 10, 2012

BABA MZAZI WA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFARIKI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amefiwa na baba yake, imefahamika.Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Jenista Mhagama alitoa taarifa hiyo bungeni mchana huu wakati akiahirisha kikao cha asubuhi cha mkutano uliokuwa ukijadili hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji.

Mhe. Jenista alisema kuwa Pinda hatakuwepo bungeni kwa vile amekwenda kushughulikia msiba wa baba yake. Akaongeza kuwa kwa sababu ya msiba huo, Waziri Mkuu amemteua Waziri wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni kuanzia leo (Julai 10) hadi Julai 15.
--
Viongozi Mbalimbali Walimtembelea Baba Mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya kuku kutoka Mama Albertina Kasanga ambaye ni Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda wakati Rais Kikwete alipowatembelea akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Mpanda, Rukwa. Kushoto ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda, Baba yake Waziri Mkuu.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Exavery Kayanza Pinda, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi Februari 20. 2012. Kulia nia Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitaniana na Mzee Kayanza Pinda alipokuwa anamuaga kuelekea kwenye mahafali ya Shule ya Sekondari Usevya ambapo alienda kumuwakilisha Waziri Mkuu aliyekuwa amealikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali hayo. Miongoni mwa utani alioutoa Mzee Pinda ni pamoja na kumuita Mkuu huyo wa Mkoa "Mnyatomato" kumaanisha kuwa ni Mtoto wa Manyanya ambapo nyanya kwa kiingereza ni Tomato. Hahahahaaah!

Friday, July 6, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 6, 2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongokwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 6, 2012.

wanachuo wa Chuo cha Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa Wakutana na Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wa Chuo cha Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 7,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wednesday, June 27, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Viwanja vya Bunge Juni 26 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma Juni 26, 2012
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo (kushoto ) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni Juni 26,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida (katikati) na Mbunge wa Mchinga,Said Mtanda kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 26,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Monday, June 25, 2012

WAZIRI MKUU KATIKA SHUGULI MBALIMBALI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia (kulia) na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua zabibu wakati alipotembelea shamba la Tendaji Agro lililopo katika kijiji cha Chikopelo wilayani Bahi, Dodoma juni 24, 2012
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mbunge wa Lindi Mjini , Salum Baluany kwnye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25,2012. Kulia ni Mtoto wa Waziri Mkuu, George Bush.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisoma Hotuba ya Bajeti ya Ofisi yake

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisoma Hotuba ya Bajeti ya Ofisi yake , Bungeni Mjini, Dodoma Juni 25, 2012.

Tuesday, June 5, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa China nchini, Lu Youqing

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa China nchini, Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Juni 5,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa China nchini, Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Juni 5,2012.Picha na Ofisi Ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akutana na Balozi wa Canada Jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago cha faru, Balozi wa Canada nchini, Robert Orr ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar salaam Juni 5,2012 kuaga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Afisa wa Masuala ya Siasa katika ubalozi wa Canada nchini, Sebastien Lanthier (kulia) na balozi wake, Robert Orr (katikati) ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuaga, Juni 5,2012.

Popular Posts