Pages

Showing posts with label Tamko kwa Umma - Press Release. Show all posts
Showing posts with label Tamko kwa Umma - Press Release. Show all posts

Monday, January 7, 2013

Taarifa ya BAVICHA kwa vyombo vya habari kuhusu kuwavua uanachama wanachama wake


Taarifa kwa Vyombo vya habari juu maamuzi ya kikao cha Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA)


Ndugu waandishi wa habari, baadhi yenu mnafahamu kuwa Baraza la Vijana la Chadema Taifa (BAVICHA), limefanya kikao cha kawaida cha Kamati Tendaji, juzi 5 Januari 2013, katika Hotel ya Benzi Garden jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili masuala matatu mazito.

Kwanza, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina suala la kuporomoka kwa elimu nchini, ambapo serikali imepunguza alama za viwango vya kufaulu, jambo ambalo limesababisha mamia ya wanafunzi waliochaguliwa kutokuwa na sifa.

Pili, Kamati Tendaji ilijadili jinsi Bavicha itakavyoshiriki katika maandilizi ya utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema yalioeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma.

Tatu, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina “Tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa Chadema na Baraza kwa ujumla.”

Ndugu waandishi wa habari, yapo baadhi ya vyombo vya habari jana na leo vimeripoti kwa upotoshaji mkubwa wa baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kikao hicho.

Kwa mfano, gazeti moja la kila siku limemtaja mwanachama wetu mmoja kuwa ndiye aliyekuwa mtoa taarifa wetu muhimu na kusema mbunge mmoja wa CHADEMA alijadiliwa katika kikao hicho kuwa ni miongoni mwa kundi hili la MASALIA na kufika mbali zaidi kwa kusema, “…sasa amekalia kuti kavu.”

Lakini ukweli wa kilichojadiliwa kikaoni ni huu ambao tunaueleza sasa:

Kwanza, kuhusu ajenda ya kuporomoka kwa elimu: Kamati Tendaji imeagiza kuwa utafiti uliofanywa na BAVICHA katika ngazi ya sekondari, ambao umegundua madudu mbalimbali, uongezwe hadi shule za Msingi na taarifa yake ililetwe kwenye kikao kijacho cha Kamati Tendaji.

Kwenye ajenda ya pili: Kamati ya Utendaji BAVICHA, ilipokea na kujadili agizo la Kamati Kuu ya Chama iliyoeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma.

Katika ajenda ya tatu juu ya tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa CHADEMA, na Baraza, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya Kamati Ndogo ya Kamati Tendaji iliyoundwa Septemba mwaka jana kwenye kikao chake kilichofanyika mjini Morogoro. Kamati ilipewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha kazi hii.

Katika hili, watuhumiwa wakuu walikuwa ni kama ifuatavyo:


  1. Juliana Shonza, Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa
  2. Habib Mchange, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  3. Mtela Mwampamba, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  4. Gwakisa Burton Mwakasendo, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  5. Joseph Kasambala, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA


Aidha, baada ya Kamati iliyoundwa kuwahoji baadhi ya watuhumiwa na wanachama wengine mbalimbali, ilibaini kwamba wapo baadhi ya wanachama wa BAVICHA ambao wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika tuhuma hizi. Hao ni pamoja na Ben Saanane – maarufu kama Eight Oclock.

Katika orodha hiyo, wakatajwa pia Exaud Mamuya lakini kamati ikashindwa kumpata Mamuya kwa kuwa hakukuwa na mawasiliano ya kutosha.

Ndugu waandishi wa habari, hizi sasa ni tuhuma za kila mmoja:

Ndugu Juliana Shonza:

Alituhumiwa akiwa katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, amekuwa akishirikiana na baadhi ya watu kupanga njama na kufanya usaliti dhidi ya Baraza, Chama na vijana wenzake wapenda mabadiliko nchini.

Amekuwa akifanya mikutano na vikao vya siri, kwa manufaa ya CCM, akiwakusanya vijana wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliosimamishwa masomo au kufukuzwa vyuoni kwa kutimiza wajibu wao wa kudai haki zao za msingi na uwajibikaji wa serikali na ambao ni wanachama wa CHASO.

Juliana alifanya kazi yake hiyo kwa ushawishi wa hongo, ili wakubali kuitisha mkutano na waandishi wa habari, watoe matamko machafu dhidi ya CHADEMA na viongozi wake wakuu, akiwamo Dk. Willibrod Slaa na Freeman Mbowe.

Mfano dhahiri hapa ni kikao alichofanya Baa ya Highland iliyoko maeneo ya Makumbusho, majira ya saa 9 hadi saa 11, ambapo aliwaita viongozi wa CHASO, akawashawishi kuwa watakuwa na maisha mazuri, watarudishwa vyuoni na kutunzwa vizuri hapa mjini kama anavyoishi yeye, endapo tu watakubali kufanya press conferences na kuisema CHADEMA kuwa inawavuruga vijana walioko vyuoni.

Tarehe 6, Desemba, 2012 Hotel MIC, kuanzia saa 10 hadi saa 12, aliwaita baadhi ya vijana ambapo yeye na wenzake walipanga njama za kukichafua chama na kutukana viongozi, kwa manufaa ya CCM.
Ifuatayo hapa chini ni moja ya sms ambazo Juliana Shonza alikuwa akiwaandikia vijana katika ushawishi wake wa usaliti kwa mapambano haya ambayo chama chetu kinafanya, kuwapigania Watanzania maskini na wanyonge katika nchi yao;

“jembe chukua bodaboda basi jamaa washatia timu hela yako yakulinda mfuko wako utaikuta tumempa eddo mnaetoa naye tamko tutalindana tu jembe usijali.”

Huu ni moja tu kati ya ushahidi mwingi, wa meseji, simu, sauti, video, picha na vikao kadhaa katika maeneo mbalimbali, unaomwingiza Shonza na wenzake wengine katika sifa mbaya ya usaliti wa chama, baraza na viongozi wake na wanachama wenzao na umma wa Watanzania kwa ujumla.

Hapo alikuwa akimwandikia mmoja wa viongozi wetu ili ashiriki katika press conference ambayo yeye Makamu Mwenyekiti kwa kushirikiana na wenzake wengine, walikuwa wameiandaa kwa nia ya kuchafua chama, kulichafua baraza, kutukana viongozi waandamizi pamoja na kuvuruga na kuchonganisha wanachama wa CHADEMA.

Matokeo ya kikao hicho cha MIC Hotel, yalionekana siku moja baada ya kikao hicho, ambapo mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Edo Mwamalala, aliyeshiriki kikao hicho cha MIC Hotel, aliitisha mkutano na waandishi wa habari, akijitambulisha kuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA, cheo ambacho hakuwa nacho.

Aidha, Shonza amekuwa akikutana na kufanya vikao vya siri na wenzake, wakipanga njama za kufanya kazi na majukumu ya CCM kuhujumu BAVICHA pamoja na CHADEMA. Mikakati ya kuvuruga baraza, kuchonganisha wanachama na kutukana chama na viongozi wakuu, kwa siri na hadharani, imekuwa ikipangwa katika vikao hivi.

Amebainika kukiuka kipengele cha 10.1(x) cha Maadili ya Viongozi, cha Katiba toleo la mwaka 2006, kinachomtaka kiongozi yeyote asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali, kwa kuzingatia taratibu na kanuni za chama.

Ameonesha ubaguzi wa kikabila na kikanda kupitia maandiko yake kwenye mtandao kwa kutumia jina lake, anapungukiwa na sifa muhimu na mahsusi za kuwa kiongozi, kwa mujibu wa kipengele cha 10.1(iv) kinachomtaka kiongozi yeyote asijihusishe na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda vinavyolenga kuleta ubaguzi ndani ya chama.

Kwa kushiriki vikao vya kuanzisha chama kipya kinachoitwa CHAUMMA, kushiriki katika makundi yaitwayo MASALIA na PM7 ambayo yote yalikuwa na lengo la kuvuruga chama na wanachama, kukosanisha na kutukana viongozi wa chama, ndugu Shonza amevunja kipengele cha 10.1(i),(viii)(ix) na ibara ya 10.2(iv).

Kwa kushiriki vikundi hivyo hapo juu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya BAVICHA wamejiridhisha pasi na shaka kuwa Shonza haendani na katiba, falsafa, sera na maadili ya chama makini na tumaini la watu, CHADEMA. Hivyo kwa mujibu wa ibara ya 5.1.4 na 5.1.5 anakosa sifa za kuwa mwanachama wa Baraza la Chama.

Kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi ya wanachama na viongozi wenzake, ameendelea kuvunja kanuni za uendeshaji kazi za chama ibara ya 10.1(viii).

Amehusika katika kuanzisha, kujihusisha na kuratibu moja kwa moja kundi la vijana waliokuwa wakizunguka mikoani na kushawishi viongozi wa vijana kutoa matamko kwa kutumia jina la CHADEMA kufanya kazi na majukumu ya CCM ya kukichafua chama, kugombanisha wanachama na kumtukana Katibu Mkuu kwa kutumia propaganda za CCM.

Kamati Ndogo ilimuita Ndugu Shonza ili kumhoji. Lakini aligoma kwa madai kuwa haitambui kamati hiyo na wala hajui kuwa kuna mgogoro, jambo ambalo limetushangaza wengi kwa kuwa Ndugu Shonza alikuwapo katika kikao cha Morogoro kilichounda Kamati hii.

Ndugu Shonza pia hakuhudhuria kikao cha Kamati Tendaji cha juzi kwa madai kuwa amebanwa na shughuli za familia. Baada ya kupitia maelezo yote hayo, Kamati Tendaji iliamua yafuatayo:

Ndugu Juliana Shonza, amepoteza sifa na uhalali wa kuwa mwanachama wa Chadema kwa kukiuka ibara ya 5.3.4 na ibara ya 10.1(ix) ya katiba ya CHADEMA na hivyo imeamua kumuondoa katika nafasi yake ya makamu mwenyekiti na kumfuta uwanachama wake.

Hivyo basi, kwa maamuzi hayo ya Kikao cha Kamati ya Utendaji ya BAVICHA, kuanzia juzi tarehe 5 Januari 2013, Ndugu Juliana Shonza, si mwanachama wa BAVICHA na hivyo moja kwa moja amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa baraza na kwa nafasi yake aliyokuwa nayo ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara.

Habib Mchange:

Huyu alituhumiwa kutoa tuhuma za uongo, zikiwemo za mauaji, kinyume na maadili ya Wanachama (kipengele cha 10.3(3); kuunda vikundi vinavyojulikana kwa majina ya MASALIA na PM7 – Pindua Mbowe.

Pia Ndugu Mchange alituhumiwa kuwavuruga wanachama, kuwachonganisha na kuwatukana viongozi, kisha kushiriki vikao vya kuanzisha chama kingine cha siasa cha CHAUMMA.

Alituhumiwa pia kupotosha maamuzi halali ya vikao vya chama na Baraza hivyo kuendelea kukipaka chama matope.

Kamati ilimuita Mchange, na kumhoji juu ya tuhuma zinazomkabili. Hakufika. Badala yake, aliandika barua kueleza kuwa hana imani na kamati:

Aidha, pamoja na Mchange kugoma kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Kamati Tendaji, Sekretarieti ya Kamati Tendaji Taifa, ilimuita Ndugu Mchange kuhudhudhuria mkutano wa Kamati Tendaji ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mwaliko huu ulifanywa kwa njia ya barua na simu. Njia hizo ndio zilizotumika kualika wahusika wote wakiwamo wajumbe wa Kamati Tendaji,

Ndugu waandishi wa habari, baadhi yenu mnafahamu kwamba Ndugu Mchange alikuwa miongoni mwa wanachama wa BAVICHA waliotaka kuwania nafasi ya uenyekiti wa taifa wa baraza hili. Jina lake liliondolewa na Kamati Kuu ya CHADEMA, kutokana na kukosa maadili ya uongozi.

Kamati Tendaji baada ya kusikiliza hoja yake hii, ikajiridhisha kuwa mtuhumiwa ameamua kuibuka hoja hiyo ili kutaka Kamati Tendaji isimjadili ili aendeleze mradi wake wa kukichafua chama akiwa ndani ya chama.

Hivyo Kamati Tendaji imefanya yafuatayo: Imempata na hatia ya kuvunja ibara ya 10.3(iii) na kwenda kinyume na kanuni za uendeshaji wa chama ibara ya 10.3(4), kinyume na Maadili ya Wanachama (kipengele cha 10.3(3); uendeshaji wa chama ibara ya 10.3(4) na kwamba mambo yote haya yanadhihirisha kuwa Ndugu Mchange hayuko tayari kushirikiana na viongozi wake kama mwanachama, hivyo kukiuka katiba ya chama ibara ya 5.3.4 na kuafikiwa uamuzi wa kumfukuza uwanachama wa Bavicha na Chadema.

Mtela Mwampamba:

Huyu ametuhumiwa kutoa tuhuma nzito za uongo hadharani, zikiwemo za mauaji, kinyume kabisa na Maadili ya Wanachama (kipengele 10.3(3).

Kuvunja katiba ya chama ibara ya 5.3.4 na Kanuni za Uendeshaji kazi za chama Ibara ya 10.3(4) kwa kupotosha maamuzi halali ya vikao vya chama na baraza na kukipaka matope chama pamoja na kudhihirisha kuwa hayuko tayari kushirikiana na viongozi wake kama mwanachama.

3.Amevunja Katiba ya CHADEMA ibara ya 5.3.3 na 5.3.4 kwa kutoa kauli za kichochezi dhidi ya chama, kuwachonganisha wanachama na kuwatukana viongozi.

4.Kwa kujiunga na vikundi vinavyoitwa MASALIA NA PM7 na baadae kushiriki vikao vya kuanzisha chama cha CHAUMMA, Ndugu Mwampamba amevunja ibara ya 10.3(iii).

5.Kinyume na ibara ya 5.3.3 na 5.3.4 ya Katiba ya CHADEMA na Ibara ya 4.3(g) na (i) ya kanuni za BAVICHA, zinazopinga ubaguzi wa aina yoyote ile, Ndugu Mwampamba ameonesha hisia za ubaguzi wa kikabila na kikanda.

Gwakisa Burton Mwakasendo:

Huyu amekuja kwenye kikao na kukiri kutenda makosa yake ambayo takriban yote ni sawa yanayowahusu watuhumiwa waliotangulia hapo juu. Mbele ya kikao cha Kamati ya Utendaji alikiri kushiriki vikao, akisema kuwa ‘lakini’ alilazimika ‘kuikimbia’ dhambi kwa kuondoka katika baadhi ya mikutano na watu hao, wakati mwingine hata nyumbani kwake hakuweza kulala akihisi ‘dhambi’ hiyo anayoikimbia itamfuata nyumbani.

Kamati Tendaji, iliamua kumpa adhabu ya kuwekwa chini ya uangalizi kwa mwaka mzima, katika wakati wote huo amezuiwa kugombea nafasi yoyote ndani ya BAVICHA na onyo kali la barua.

Ben Saanane:

Huyu pamoja na kwamba hakuwa miongoni mwa watuhumiwa alipewa adhabu ya onyo kali na uangalizi wa miezi 12, kutokana na makosa yafuatayo. Kutoa tuhuma nzito, zinazomhusu pia Kiongozi wa juu mwandamizi wa chama, Ben amekiuka Maadili ya Wanachama (kipengele 10.3(3).

Kukiri kuwa mmoja wa waanzilishi wa vikundi vinavyoitwa MASALIA na PM7 na kisha kushiriki vikao vya kuanzisha chama kingine cha CHAUMMA, amevunja ibara ya 10.3(iii), kwa nia ya kuvuruga chama na kutukana viongozi wake:

Mbele ya Kamati Tendaji, Ben alikiri makosa na akaomba radhi.

Aidha, Ben alitoa ushirikiano mkubwa kwa Kamati Ndogo jinsi ya kupatikana kwa taarifa na ushahidi wa namna wanachama wa BAVICHA walivyokuwa wanafanya kazi za kundi hili la MASALIA na PM 7 na hasa juu ya majina wanayotumia katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wakifanya juhudi za kuivuruga CHADEMA, kuvuruga BAVICHA, kutukana viongozi na kuwavuruga wanachama, lakini kikubwa wakionesha kila dalili ya tabia ya usaliti.

Exaud Mamuya:


Huyu hajapata nafasi ya kusikilizwa kwenye vikao. Hivyo suala lake litaendelea kufanyiwa kazi na uongozi wa BAVICHA.

Aidha, kikao cha Kamati ya Utendaji pia kilipitisha kwa kauli moja, moja ya maazimio ya BAVICHA Mkoa wa Mwanza, waliopendekeza kufukuzwa uanachama kwa aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Mwanza, Salvatory Magafu, kwa tuhuma za kukiuka Kanuni ya 10.1(xii) kwa kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kwa nia ya kumfarakanisha Katibu Mkuu na wanachama wa CHADEMA na umma wa Watanzania, ikiwa ni sehemu ya uratibu wa kundi lililokuwa likiendeshwa na watuhumiwa wengine hapo juu.

Kamati ya Utendaji pia ilimkuta na makosa ya kiuongozi katika tuhuma zilizowasilishwa vikaoni na kufanyiwa kazi na Kamati Ndogo, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala na hivyo amepewa adhabu ya onyo kali.

Hitimisho
Tunaomba kuwahakikishia vijana wenzetu wa CHADEMA na wengine wote wapenda mabadiliko nchini, hakuna kijana mwanachama wa BAVICHA, atafanya kazi za kuhujumu baraza na chama kwa ujumla na kusaliti matumaini pekee ya Watanzania, akifanya kazi za mahasimu wetu, kisha akaachwa.

Ni lazima na muhimu tuoneshe kuwa tuna uthubutu kwa kuchukua hatua kadri inavyotakiwa, pale panapotakiwa. Tuliopewa dhamana za uongozi, tutatimiza wajibu kuhakikisha hakuna mtu ataonewa wala kupunjwa haki yake katika kusimamia utendaji na utoaji utumishi bora wa baraza kwa wanachama wake na chama kwa ujumla.

Daima tutasimamia katiba ya chama, maadili, kanuni, taratibu, itifaki na miongozo ya mabaraza. Baraza hili halitakuwa tayari kuwa sehemu ya kuruga matumaini makubwa ya Watanzania waliyonayo juu ya CHADEMA.

Baraza liko imara. Wanachama wetu wasifadhaishwe na upotoshaji unaofanywa na wasaliti kuwa tumevurugika au ‘kumechafuka’. Hatuwezi kuchafuka wala kuvurugika kwa kuchukua maamuzi dhidi ya watu wabinafsi wanaotaka kukwamisha mapambano ya awamu ya pili, kupigania mabadiliko ya kweli ya kimfumo na kiutawala, kwa ajili ya Watanzania.

Historia inatuonesha kuwa mara zote ambapo mapambano yamefikia hatua ya juu ya kutimiza malengo, ndipo ambapo wasaliti hujitokeza. Hivyo vikwazo hivi vya baadhi yetu kuanza kugeuka nyuma ni dalili za mwisho mwisho kuwa ushindi unakaribia. Ni lazima kama vijana tuendelee kujenga imani na matumaini ya Watanzania waliyonayo juu ya CHADEMA kutukabidhi dola mwaka 2015.

Mwisho

Imetolewa leo Januari 7, 2013, Dar es Salaam na;
John Heche
Mwenyekiti wa Taifa,
Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA)

Saturday, January 5, 2013

TAMKO LA JUVICUF JUU YA UTAPELI WA KUTOA GESI MTWARA

M'Kiti wa Jumuiya ya Vijana Ya Chama Cha Wananchi-CUF, Leo ameongea na Vyombo vya Habari. Na haya ndio Maelezo ya Press ya Leo.
NI HAKI YA MSINGI KABISA WANANCHI WA MKOA WA MTWARA KUANDAMANA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR ES SALAAM.WAKATI HAWAJUI HATIMA YAO.
TAREHE: 05/01/2013

Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaendelea kuunga mkono harakati zinazoendelea mkoani Mtwara za kupinga mpango wa serikali wa kujenga bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka mtwara hadi dare s salaam, jumuiya ya vijana CUF taifa inaamini gesi inahamishwa kwa matakwa ya watu Fulani na sio kwa manufaa ya taifa kama inavyoelezwa na serikali, jumuiya haioni sababu ya kiuchumi ya kuhamisha gesi Mtwara kupeleka Dar es salaam au sehemu nyingine yeyote ile kwa kuzingatia yafuatayo:-

1. Uamuzi wa kuhamisha gesi sio wa kiuchumi na haukuzingatia misingi ya kiuchumi kwani kama serikali ingeamua kujenga mitambo ya kufulia gesi (Plants) mkoani Mtwara ingeokoa mabilioni ya pesa yanayotumika kusafirishia gesi asilia toka Mtwara kwenda Dar es Salaam, inasemekana bomba moja la mita tano (5) inagharimu fedha za kitanzania takribani bilioni tatu (3), hii ni hatari tujiulize umbali uliopo kati ya Mtwara na Dar nikilometa ngapi? Kwani ni zaidi ya kilometa 560 mara hiyo bilioni 3 tunazani ni pesa kiasi gani zitatumika kwa ajli ya mradi huo?kwanini wasifanye opportunity cost ya kujenga hizo plants Mtwara? ili kuokoa gharama za usafirishaji wa gesi wanasafirisha na wanaenda kujenga plants nyingine Dar hivi hatuoni Taifa linaingia gharama mara mbili?

2. Ujenzi wa vinu vya kufulia gesi asilia Mtwara utasaidia kuchochea maendeleo ya mikoa ya kusini kwa kuwahakikishia ajira vijana ambao kila siku wanapanga mikakati ya kwenda Dar kutafuta ajira na maisha bora! Lazima Taifa lifanye diversification of economy kwani hata mataifa ya Ulaya na Marekani yalifanikiwa kwa kufanya diversification of economy sio kila mradi tuupeleke Dar es Salaam, tunasababisha population na kufanya uchumi kuwa concentrated in a single area hii ni hatari kwa mipango ya muda mrefu ya taifa hili.

3. Kujengwa kwa mitambo hiyo katika mikoa ya kusini itasaidia kuchochea maendeleo ya miundo mbinu mbalimbali kama barabara, bandari, na reli kwa lazima serikali itajenga miundo mbinu imara kwa ajili ya kusafirisha gesi iliyo tayari kwa kutumiwa na watumiaji mbalimbli kutoka mikoa tofauti tofauti, Taifa linahitaji mawazo yakinifu ya kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini hasa wanaotoka mikoa ya kusini.

Jumuiya ya vijana inashangazwa na kauli tata inayotolewa na viongozi wa Serikali ya CCM kwani ikumbukwe kuwa tarehe 25/07/2011 kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa Rais Kikwete aliwahutubia wananchi wa Mtwara na kuwahakikishia kuwa katika utawala wake atainua mikoa ya kusini kiviwanda na kumtaka Meya wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani kutenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji, wananchi wanahoji utawala wake unaelekea ukingoni hauna hata dalili ya kiwanda kimoja badala yake kunazoezi la kutaka kuhamisha gesi hiyo na kupelekwa Dar es Salaam, je hivi kweli Rais Kikwete na CCM yake wana mapenzi ya dhati na watu wa kusini?
Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaendelea kushangazwa na taarifa ya Waziri wa nishati na madini Mheshimwa Sospeter Muhongo kwa kudai kuwa eti asilimia kumi na nne (14%)tu ya gesi iliyogunduliwa ndiyo inatoka Mtwara, kwanini sasa wasipeleke mradi huo wa bomba la kusafirishia gesi sehemu nyingine badala ya Mtwara? Jumuiya inasisitiza kuwa wanamtwara hawapingi gawio la pato linalotokana na gesi kutumika sehemu nyingine yeyote ya nchi, kwani ikumbukwe kuwa hata kwenye ushuru wa zao la korosho ambalo limekuwa zao la pili kuingizia ushuru wa Taifa mwaka jana wananchi hawajahoji lolote juu gawio la ushuru huo?

Kwa hiyo Jumuiya ya vijana CUF Taifa inashangazwa na kauli ya viongozi wa CCM ya kusema kuwa wanamtwara wanahitaji gesi iwanufaishe wao wakati ukweli ukijulikana kuwa kilio cha wanamtwara nikutaka uwekezwaji unaotokana na gesi ufanywe Mtwara na Lindi kama ilivyofanywa kwenye viwanda vya sukari, kwani miwa inalimwa Tuliani, Mtibwa, na Kilombero – Morogoro na viwanda viko huko kwa nini gesi iwe Mtwara plant iwekwe Dar es Salaam?

Kwa hiyo Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaunga mkono gesi kutosafirishwa kupelekwa Dar es Salaam.

Imetolewa na,
Jumuiya ya Vijana CUF Taifa,

Friday, January 4, 2013

UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI






Ndugu Deogratius Kisandu aliyeshika Kadi, Kulia kwake ni Ndg. Florian Rutayuga ( Afisa Utawala wa Chama) na Katikati ni Ndugu Faustin Sungura (Kaimu Katibu Mkuu) 



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI
Ndugu wanahabari,
Mimi ninaitwa Deogratius Kisandu, nimehitimu katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa huko Lushoto (SEKUCO) nina Shahada ya Elimu Maalum, Siasa na Utawala.
Nilikuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA katika nafasi za; Katibu wa Wilaya ya Lushoto na Katibu wa Vijana wa Mkoa wa Tanga (Bavicha).
Mwaka 2010 niligombea ubunge katika jimbo la Lushoto, nilishika nafasi ya pili kwa kupata kura 5000+ dhidi ya mgombea wa CCM aliyepata kura 14000+ .
Ndugu wanahabari, 
Kwa muda mrefu nikiwa ndani ya CHADEMA, tumekuwa katika maelewano mabaya na hata pengine kujengewa chuki na fitina pale nilipojaribu kuhimiza viongozi wenzangu kufuata katiba ya Chama chetu.
Mwishoni mwa mwaka jana (2012) niliamua kujivua uanachama ndani ya CHADEMA na kuahidi kujiunga na Chama kingine.Vile vile nilisema siku hiyo nitaeleza sababu za msingi zilizonifanya nijivue uanachama na kukabidhi kadi ya Chama hicho.


1. Mnamo mwaka 2012 nilitangaza nia yangu ya kugombea urais kupitia CHADEMA. Msimamo huo umenijengea chuki na uhasama kwa viongozi wakuu wa CHADEMA akiwemo muasisi wa Chama hicho Mzee Edwin Mtei, kupinga vijana kuonesha dhamira zao.
Nimejiridhisha kwamba, CHADEMA ina watu wake inaowataka wagombee urais na hususan watu wa Kaskazini mwa nchi hii.
Yaliyonikuta mimi pia yamewahi kuwatokea marehemu Chacha Zakayo Wangwe, Zitto Zuberi Kabwe na John Magane Shibuda pale walipojaribu kuwania nafasi hiyo ndani ya Chama.
Inasikitisha sana kwa watu wanaotaka kugombea urais wanasakamwa, wale ambao hawataki kugombea na wala kutangaza kugombea urais ndiwo wanaolazimishwa kugombea nafasi hiyo.
Itakumbukwa kwamba, Dkt. Wilbroad Peter Slaa hakuwahi kujitangaza kuwa anataka kugombea urais, bali amekuwa analazimishwa kugombea urais, hata juzi Mwenyekiti wa CHADEMA ameonekana kumlazimisha Dkt. Slaa kugombea urais (2015).
2. Mnamo mwaka 2012, Dkt. Slaa ametangaza na kukiri kuwa anamiliki Kadi ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba Kadi hiyo ililipiwa ada kwa miaka 20 hadi mwaka 2017.
Ninajua kuwa Dkt. Slaa anayo haki ya kuwa na Kadi hiyo kwa sababu aliinunua kwa fedha zake na hivyo ni mali yake.
Binafsi siridhiki na vitendo vya Dkt. Slaa, amekuwa anahamasisha watu wanaotoka CCM wamkabidhi Kadi za CCM. Je, hao nao hawakununua kwa fedha zao? Je, hawataki nao kuwa na kumbukumbu kama yeye? Bila shaka kuna siri kubwa imejificha nyuma ya pazia.
3. CHADEMA haitaki kuona vijana wanaochipukia wanakuwa na umaarufu ndani ya Chama hicho. Kwenye ziara za M4C wamekuwa wanawatumia watu wasioijua CHADEMA, wanazunguka nao Mikoani, wanawaacha vijana waliokipigania Chama hadi kikafika hapa kilipo.
Watu wanaopata nafasi nyeti ndani ya Chama hicho ni wale tu wenye udugu au uhusiano na viongozi wakuu wa Chama. Mfano mzuri ni mgawanyo wa vitu maalum vya ubunge.
Zaidi ya nusu ya viongozi wa juu wa Chama wamehakikisha ndugu zao au wake zao ndio wamepata nafasi hizo, zingine zinagawiwa kwa njia za kudhalilishana. Hivi sasa kuna mmoja wa wabunge wa viti maalum ana ujauzito wa mmoja wa viongozi wakuu wa Chama.
Ndugu wanahabari, 
Yapo mambo mengi na ambayo siwezi kuyamaliza kwa leo, ila kwa ufupi nianze na hayo ili yakikanushwa ndipo nitaeleza mengine.
Baada ya kusema hayo, ninatangaza sasa rasmi kuwa, kuanzia leo tarehe 04/01/2013 nitajiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi.


SABABU ZA KUJIUNGA NA NCCR-MAGEUZI
1. Ni Chama kikongwe, waasisi na waanzilishi wa mageuzi hapa nchini. Ni Chama kilichopitia migogoro na misukosuko mingi ambacho ninaamini kimekomaa.
2. Ni chuo kizuri cha wanasiasa,watu wengi wamepitia hapa, wakafundwa na baadaye wakatamaniwa hata vyama vingine. Mifano michache ni Dkt. Masumbuko Lamwai, Dkt. Festus Limbu, Steven Wasira (CCM) na Ndesamburo, John Mnyika, Joseph R. Selasini, Chiku Obwao, Suzana Kiwanga, Profesa Mwesigwa Baregu, Mabere Marando nk.
Ninaamini kwamba, kujiunga kwangu na Chama hiki nitajifunza mambo mengi.
3. NCCR-Mageuzi ni Chama na kipimo cha demokrasia kwa vitendo. Ni Chama ambacho hakina mtu mmoja tu kwa ajili ya nafasi ya za uongozi, yeyote ana nafasi ya kugombea nafasi anayotaka na mkutano mkuu wa Chama ndio uamue nani anafaa kuwa mgombea urais.
Mfano, Mwaka 1995 Chama kilimsimamisha ndugu A.L. Mrema kugombea urais. Mwaka 2000 Chama kilimsimamisha ndugu Edith S. Lucina kugombea urais. Mwaka 2005 Dkt. E.A. S. Mvungi aligombea urais na mwaka 2010 Chama kilimsimamisha ndugu Hashim S. Rungwe aligombea urais. Hii ni tofauti na baadhi ya vyama vingine.
4. Nilipotangaza kugombea urais kupitia CHADEMA, niliwekewa mizengwe, nikajengewa chuki. Nilitangaza kugombea urais, lakini sikutangaza kwa mwaka gani, kwani mwaka 2015 umri wangu wa kikatiba wa kugombea urais hauniruhusu, nilikusudia baada ya mwaka 2015, lakini kwa CHADEMA inaonekana wana wagombea wao wa Kaskazini kwa miaka hamsini ijayo.
Ninaamini ndani ya NCCR-Mageuzi, umri wangu ukifika, mkutano mkuu ndio utaamua na siyo kiongozi mmoja.
Baada ya kusema hayo, ninaomba sasa nikabidhiwe Kadi ya NCCR-Mageuzi.


----------------------------------04/01/2013
D. KISANDU

Wednesday, January 2, 2013

KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUFAFANUA KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI

1.0   UTANGULIZI

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi wa miradi ya Gesi Asilia ambayo itatekelezwa kwa kushirikiana na wawekezaji katika Sekta ndogo ya Gesi Asilia na kueleza manufaa makubwa yatakayopatikana kwa wananchi wote wa Tanzania wakiwemo wale wa Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Siku ya Alhamisi, tarehe 27 Disemba 2012, baadhi ya Vyama vya Siasa vya Upinzani viliratibu na kuhamasisha baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara, wengi wao wakitokea Mtwara Mjini kufanya maandamano ya kudai raslimali ya Gesi Asilia iwanufaishe wakazi wa Mtwara na kupinga mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa Wa-Tanzania wote kwa kupitia vyombo vya habari.

Tokea Uhuru, uchumi wa Tanzania umetegemea kilimo cha mazao ya biashara kama vile katani (Tanga na Morogoro), pamba (Mwanza, Mara na Shinyanga), kahawa (Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma na Mara), chai (Iringa) na tumbaku (Tabora). Fedha za mazao haya zimewanufaisha wakazi wa mikoa yote ya nchi yetu bila ubaguzi wo wote wala wakulima wa kutoka mikoa hiyo hawajawahi kufanya maandamano wakidai upendeleo (dhidi ya Wa-Tanzania wengine) wa aina yo yote ile.

1


Mapato yatokanayo na uchimbaji wa dhahabu (Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga na Tabora), almasi (Shinyanga) na tanzanite (Manyara) yamewanufaisha Wa-Tanzania wote bila ubaguzi wo wote ule! Minofu ya samaki wa Ziwa Victoria (Mara, Mwanza na Kagera) imeliingizia Taifa letu fedha nyingi ambazo zimetumiwa na wakazi wa nchi nzima bila ubaguzi wo wote.

Aidha kuna mikoa ambayo inazalisha mazao ya chakula kwa wingi kwa manufaa ya Wa-Tanzania wote. Mahindi kutoka Rukwa, Mbeya, Ruvuma na Iringa yanasafirishwa kwenda mikoa yote ya nchi yetu bila kujali eneo yanakolimwa na wakazi wa mikoa hiyo hawajawahi kudai mahindi hayo ni kwa ajili ya watu wa mikoa hiyo pekee. Sukari ya Kilombero, Mtibwa na Kagera inatumiwa na wakazi wa mikoa yetu yote bila ya kuwepo madai ya mikoa inayozalisha sukari hii kupewa upendeleo wa aina yo yote ile. Maji ya Mto Ruvu yanatumiwa na wakazi wa Dar Es Salaam bila manung’uniko yo yote kutoka kwa wakazi wa eneo la chanzo cha Mto Ruvu.

Umeme wa kutoka Mtera, Kidatu na Kihansi (Dodoma na Morogoro), Hale (Tanga), na Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro) unatumiwa na wakazi wote wa Tanzania bila ubaguzi au malalamiko ya wenyeji wa sehemu ambazo umeme huo unafuliwa na kusafirishwa kwenye Gridi ya Taifa. Kwa hiyo, kutokana na mifano hii michache, ni wajibu wa wazalendo na wapenda maendeleo wa kweli na hasa Wa-Tanzania wanaopinga ubaguzi wa aina yo yote ile kujiuliza kwa kina sababu zilizopelekea Vyama Siasa vya Upinzani kupanga, kuhamasisha, kushabikia na kuongoza maandamano ya tarehe 27 Disemba 2012 pale Mtwara Mjini.

2.0   RASLIMALI YA GESI ASILIA TANZANIA

Gesi Asilia ilianza kugundulika hapa nchini tangu mwaka 1974 kwenye Kisiwa cha Songo Songo, Mkoani Lindi. Baada ya hapo Gesi Asilia imegundulika maeneo ya Mtwara Vijijini, yaani Mnazi Bay (1982) na Ntorya (2012), Mkuranga (Pwani, 2007), Kiliwani (Lindi, 2008). Kiasi cha Gesi Asilia iliyogunduliwa katika maeneo haya inakadiriwa kuwa Futi za

2


Ujazo Trilioni 4.5 – 8. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji Mafuta na Gesi Asilia uliojikita zaidi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari. Kiasi cha Gesi Asilia iliyogundulika katika kina kirefu cha maji inafikia takribani Futi za Ujazo Trilioni 27. Kiasi cha wingi wa Gesi Asilia yote iliyogunduliwa nchi kavu na baharini inafikia takribani Futi za Ujazo Trilioni 35.

Kufuatana na Sheria za nchi yetu zinazotumiwa kugawa mipaka ya mikoa iliyopo kando kando mwa bahari (isivuke 12 nautical miles au 22.22 km kuingia baharini), Gesi Asilia iliyogunduliwa hadi sasa katika

Mkoa wa Mtwara pekee ni asilimia 14 tu ya gesi yote iliyogundulika nchini. Kwa kutumia kigezo hicho cha Sheria za mipaka ya ki-utawala ya mikoa yetu, Lindi inayo 7% ya gesi yote, Pwani 1% na huku Kina Kirefu cha Bahari (Deep Sea) ndicho chenye gesi nyingi (78%) kuliko mikoa yote ikiwekwa pamoja! Kwa hiyo, hakukuwa na haja ya kufanya maandamano kwa sababu Gesi Asilia nyingi inapatikana kwenye bahari ya kina kirefu ambayo iko ndani ya mipaka ya nchi yetu bila kujali mipaka ya mikoa yetu. Isitoshe Gesi Asilia imegundiliwa kwenye miamba tabaka (sedimentary rocks) yenye umri wa Miaka kati ya Milioni 199.6 hadi 23.03. Mipaka ya Bara la Afrika, ya nchi yetu na ile ya mikoa yetu haikuwepo wakati huo!

Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia pia unaendelea tukiwa wa mategemeo makubwa ya upatikanaji wa raslimali hizi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Kigoma, Mbeya, Njombe, Rukwa, Katavi, Morogoro na Tabora pamoja na kwenye kina kirefu cha maji baharini kuanzia mpaka wetu na Msumbiji hadi mpaka wetu na Kenya. Hatutarajii mikoa hii nayo ifanye maandamano ya kutaka kuhodhi raslimali za Gesi Asilia na Mafuta zitakapogunduliwa mikoani mwao.

3.0      MATUMIZI YA GESI ASILIA YA MNAZI BAY (MTWARA) NA SONGO SONGO (LINDI)

Mpaka hivi sasa Gesi Asilia inayozalishwa na kutumika nchini ni kutoka Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) na Songo Songo (Kilwa, Lindi). Gesi ya Mnazi

3


Bay kwa sasa huzalisha umeme kwa ajili ya Mikoa ya Mtwara na Lindi tu. Mitambo ya kufua umeme kutokana na Gesi Asilia iliyopo Mtwara Mjini inao uwezo wa kuzalisha MW 18 lakini matumizi ya umeme ya Mikoa ya Mtwara na Lindi haijavuka MW 12. Umeme huo wa Mtwara unafuliwa na TANESCO huku Kampuni za Wentworth na Maurel & Prom zikizalisha Gesi Asilia (inayotumiwa na TANESCO) kiasi cha Futi za Ujazo Milioni 2 kwa siku. Ikumbukwe kwamba ufuaji wa umeme wa hapo Mtwara Mjini ulikuwa mikononi mwa Kampuni ya Artumas iliyofilisika. Tangu Desemba 2006 hadi leo hii kiasi cha gesi kilichotumika kufua umeme kwa ajili ya mikoa hiyo miwili ni chini ya asilimia 1 ya gesi yote iliyogundulika Mnazi Bay (Mtwara Vijijini). Vilevile ikumbukwe kwamba kuna visima vinne vya Gesi Asilia pale Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) na kinachotumika kwa sasa na tena kwa kiwango cha chini kabisa ni kimoja tu!

Aidha ni vizuri ndugu zangu Wa-Tanzania wakaelewa kuwa Gesi Asilia hii inatafutwa na kuchimbwa na wawekezaji wenye mitaji mikubwa, wataalamu na teknolojia ya utafutaji na uchimbaji wa Gesi Asilia ambao wanapaswa kurejesha mitaji yao. Uchorangaji wa kisima kimoja cha utafutaji wa Gesi Asilia nchi kavu unahitaji Dola za Marekani Milioni 40, na kwenye kina kirefu cha maji baharini zinahitajika zaidi ya Dola za Marekani Milioni 100. Ikumbukwe kwamba, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Mafuta la Tanzania (TPDC), inatumia fedha za walipa kodi wa nchi nzima kwa shughuli za kuvutia, kuratibu na kusimamia utafutaji na uendelezaji wa Gesi Asilia nchini kote ikiwemo Mikoa ya Mtwara na Lindi. Walipa kodi Wa-Tanzania bado hawajalalamika wala hawajafanya maandamano ya kudai fedha zao za kodi zisitumike huko Mtwara!

Ni muhimu pia tukaelewa kwamba Gesi Asilia iliyopo Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) inazalisha umeme peke yake kwa ajili ya Mikoa ya Mtwara na Lindi. Gesi Asilia ya Songo Songo (Kilwa, Lindi) ndiyo inayotumika kuzalisha umeme kwa ajili ya Gridi ya Taifa, na pia kwa ajili ya wananchi wa Kisiwa cha Songo Songo (Lindi), maeneo ya Somanga

4


Fungu (Lindi) na viwandani (Dar Es Salaam). Tangu Oktoba 2004 ambapo mitambo ya kufua umeme ilipoanza kazi hadi leo hii, kiasi cha Gesi Asilia ya Songo Songo kilichotumika ni asilimia 7 tu ya Gesi Asilia yote iliyogunduliwa huko. Kwa hiyo, takwimu zinaonyesha kwamba hata uchumi wa Jiji la Dar Es Salaam unatumia kiasi kidogo sana cha Gesi Asilia (7%) iliyopo Songo Songo (Kilwa, Lindi). Ikumbukwe kwamba waajiriwa kwenye viwanda vya Dar Es Salaam wamo wanyeji wa kutoka Mtwara Mjini ambako maandamano yalifanyika na vilevile wamo wafanyakazi ambao ni wanachama wa Vyama vya Siasa vya Upinzani vilivyopanga, ratibu na kushabikia maandamano ya Mtwara Mjini ya tarehe 27 Disemba 2012.

4.0      MIPANGO YA MATUMIZI YA GESI ASILIA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5 HADI 10

(a)     Ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia hadi Dar Es Salaam:

Kuuza Gesi Asilia Jijini Dar es Salaam, kitovu cha uchumi wa Tanzania (80% ya mapato ya nchi yetu yanazalishwa Dar Es Salaam) ni uamuzi mzuri wa ki-uchumi. Tayari kuna viwanda

34 vinatumia Gesi Asilia ambavyo vinahitaji kupanua shughuli zao endapo gesi zaidi itapatikana. Soko kubwa la Gesi Asilia lipo tayari Dar es Salaam (na siyo Mtwara), ambapo ipo mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta. Serikali inatumia fedha nyingi za kigeni kununulia mafuta ya kufua umeme tunaoutumia kila siku. Takribani Dola za Marekani Bilioni Moja (sawa na Shilingi Trilioni 1.6) kwa mwaka zitaokolewa kutokana na mitambo iliyopo nchini ikifua umeme kwa kutumia Gesi Asilia na kuachana na mafuta ambayo ni ya bei kubwa sana. Bei ya umeme kwa uniti moja (KWh) ya umeme unaofuliwa kutumia dizeli na mafuta ya aina nyingine ni kati ya Senti za Marekani 30 hadi 45 na huku bei ya uniti moja hiyo hiyo ni Senti za Marekani 6-8 kwa umeme utokanao na Gesi Asilia na zinapungua na wakati wa matumizi.

Vilevile, takribani Dola za Marekani millioni 202 kwa mwaka zitaokolewa iwapo Jiji la Dar Es Salaam litatumia Gesi Asilia badala ya mafuta katika magari, taasisi na majumbani. Fedha

5


hizi zikiokolewa zitatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa letu kwa manufaa ya Wa-Tanzania wote wakiwemo wale waliondamana na wale walioratibu maandamo ya Mtwara Mjini ya tarehe 27 Disemba 2012.

(b) Umeme mwingi zaidi kutokana na Gesi Asilia:

Bomba la Gesi Asilia linalojengwa litasafirisha gesi nyingi zaidi ambayo itawezesha mitambo mipya itakayojengwa Kinyerezi (Dar Es Salaam) kufua umeme wa zaidi ya MW 990. Umeme mwingine utafulia Somanga Fungu (Lindi) wa kiasi kisichopungua MW 520.

(c)  Usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini mwetu:

Dar es Salaam ndiko kuna miundombinu mikubwa ya usafirishaji na usambazaji wa umeme kuliko mikoa mingine yote, hivyo ni uamuzi wa ki-uchumi unaotulazimisha kusafirisha Gesi Asilia kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara na kuipeleka Dar Es Salaam ambako itatumika kufua umeme, na kutumika moja kwa moja viwandani, majumbani na kwenye magari.

(d) Kwa   kuzingatia   mahitaji   ya   Gesi   Asilia   yatakayojitokeza:

Bomba la kusafirisha gesi litawekewa matoleo ya kuchukulia gesi (tie-off) katika maeneo ya Mtwara, Lindi, Kilwa na Mkuranga ili kuhakikisha kuwa miji hii inakuwa na Gesi Asilia ya uhakika wakati wowote itakapohitajika. Kwa hiyo kuweka mitandao ya usambazaji wa gesi kutoka kwenye Bomba la Gesi Asilia linalojengwa kutarahisisha matumizi ya Gesi Asilia viwandani na majumbani katika Mikoa ya Mtwara na Lindi, na kwenye mikoa mingine kwa siku za baadae.

(e)Serikali   imetenga   maeneo katika pwani ya Mikoa  ya  Kusini

(Lindi na Mtwara) kwa ajili ya uanzishwaji wa maeneo ya viwanda (Industrial Parks/Estates) vikiwemo viwanda vya mbolea, Liquefied Natural Gas (LNG) na Petrochemicals.

Ujenzi wa kiwanja cha sementi uko katika hatua za mwisho za maandalizi.

(f)  Ili kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ya Gesi Asilia na Mafuta kwa kampuni za huduma, malighafi na vitendea kazi, Serikali imetenga eneo maalumu Mtwara, ambalo litawekewa

6


miundombinu ya msingi ili kutoa vivutio mbalimbali kwa makampuni hayo. Eneo hilo litapewa hadhi ya Ukanda Huru wa

Bandari (Freeport Zone).

Ni lazima shughuli za kusafisha na kusafirisha Gesi Asilia zitatoa ajira katika maeneo husika. Kwa mfano kwa mitambo ya kusafishia gesi inayojengwa Madimba (Mtwara Vijijini) na SongoSongo (Kilwa, Lindi), kila mtambo utahitaji wafanyakazi na wengine watatoka Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Watanzania wanakumbushwa kuwa raslimali zilizopo nchini ikiwemo gesi asilia, madini, makaa ya mawe, wanyama pori, misitu, milima ya utalii, mito, maziwa, bahari n.k ni za Wa-Tanzania wote kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Raslimali hizi zinapatikana, zinatunzwa na kuzalishwa maeneo mbalimbali nchini mwetu na mapato yake yanatumika kwa maendeleo ya Wa-Tanzania wote bila kujali maeneo raslimali hizo zilipo.

Tusikubali kuvunja nchi yetu vipande vipade kwa kisingizio cha raslimali zilizopo mikoani mwetu. Tusikubali kuvunjavunja mikoa yetu kwa kisingizio cha raslimali zilipo kwenye wilaya zetu. Tusikubali kuvunjavunja wilaya zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye tarafa zetu. Tusikubali kuvunjavunja tarafa zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye kata zetu. Tusikubali kuvunjavunja kata zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye vijiji vyetu na mitaa yetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, DUMISHA UHURU NA UMOJA WETU

Prof Dr Sospeter Muhongo (Mb)

WAZIRI YA NISHATI NA MADINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Thursday, December 27, 2012

MAAMUZI YA BARAZA LA MADAKTARI KUHUSU MADAKTARI WALIOGOMA


TAARIFA  KWA UMMA JUU YA MAAMUZI YA BARAZA LA  MADAKTARI KUHUSU MADAKTARI WALIOGOMA 

UTANGULIZI

Kutokana na mgomo wa madaktari uliotokea kati ya tarehe 23 na 29 mwezi juni 2012.Wizara iliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la madaktari Tanganyika ili lifanye uchunguzi kuhusu madaktari hao .Idadi ya madaktari wote waliogoma walikuwa 394, kati yao madaktari 376 walikuwa ni madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo (Interns) kutoka hospitali za Muhimbili, K.C.M.C. Bugando, Mbeya Rufaa, St.Francis - Ifakara, Dodoma, Temeke, Mwananyamala, Amana, Haydom na Sekou Toure. Aidha, Madaktari waajiriwa(Registrar) 18 walishiriki katika mgomo huo kutoka hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Baraza lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo.  Adhabu hizo zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo, onyo kali na kusimamishwa udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na miezi sita.Vile vile kuna Madaktari ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki katika mgomo na hivyo walifutiwa mashtaka.
MCHANGANUO WA ADHABU
  • Waliofutiwa mashitaka madaktari 49
  • Waliopewa onyo  madaktari 223
  • Waliopewa onyo kali madaktari 66
  • Kusimamishwa kwa muda madaktari 30
  • Mashitaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria madaktari 4
  • Mashitaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza madaktari 22
Wizara inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la Madaktari.   Wizara pia imeridhia kuwapa Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa.  Hata hivyo fursa hii haitawahusu Madaktari wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo watakapomaliza kutumikia adhabu zao.

HITIMISHO
Kwa taarifa hii madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii barua kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa usajili  na kuruhusiwa kuendelea na mafunzo kwa vitendo. Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ili kupewa barua zao kulingana na Adhabu walizopewa.  Barua hizi zitatolewa  kuanzia tarehe 2 Januari, 2013.Madaktari wote walio katika mafunzo kwa vitendo wanatakiwa kuanza kazi katika vituo vyao vya awali  ifikapo tarehe 14 Januari, 2013.Hakuna muda utakaoongezwa kwa kipindi kilichobakia cha mafunzo kwa vitendo. Kwa wale wote waliopewa adhabu wataanza kutumikia adhabu hizo kuanzia tarehe ya adhabu hiyo ilivyotolewa.

Nsachris Mwamwaja
Msemaji
WIZARA YA AFYA NA USTAWI  WA JAMII
27/12/2012

TAMKO LA MAASKOFU WA TANZANIA KUHUSU AMANI YA TANZANIA


TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF)
MKUTANO MKUU WA NNE WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA (TCF)

TAMKO RASMI 

“ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA”

Utangulizi
Katika Mkutano Mkuu wa Nne wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, Tanzania Christian Forum – TCF, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Desemba, 2012; Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja na kutathmini juu ya wajibu wa Kanisa na Utume wake wa Kinabii kwa taifa letu.

Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha taasisi kuu za Umoja wa Makanisa nchini kama ifuatavyo;-
Jumuiya ya Kikristo Tanzania - CCT
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC
Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania - PCT
Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (observers)

Tafakari
Tafakari yetu ilianza kwa kujiuliza yafuatayo:
1. Ni mwenendo gani uliotusibu hivi karibuni kusababisha kukutana kwetu hapa?
Vikundi vya kihalifu vikiongozwa chini ya mwavuli wa waamini wa Kiislamu vimekuwa vikishambulia kwa ukali na kikatili sana imani, mali, majengo na makanisa ya Wakristo kwa jeuri na kujiamini.

2. Kwa mwenendo huo ni kitu gani kilicho hatarini?

Vitendo na mienendo yote ya namna hiyo inahujumu sana Amani, Mapatano na Uelewano kati ya watu wote nchini mwetu. Tunaelewa kwamba ni waamini wachache tu wenye kutenda maovu hayo, lakini mienendo ya kikatili ya namna hii huchochea shari miongoni mwa walengwa wa ukatili husika na kutaka kulipiza kisasi hata kusababisha uvunjifu wa amani.3. Ni athari gani kwa nchi, katika muda ujao, iwapo mienendo hiyo haitadhibitiwa na kukomeshwa kabisa?

Katika nyakati zetu hizi, tunashuhudia fadhaa na migogoro mingi ya kijamii. Kuna hasira kubwa ya chinichini inayotokana na kasoro nyingi za kiutendaji katika mihimili mikuu ya uongozi na utando mkubwa wa ufukara wa kutupwa kwa wananchi wengi usio na matumaini ya kumalizika hivi karibuni. Hatari ya hali hii ni dhahiri kwamba makundi nyemelezi (kisiasa, kiuchumi na kidini), kwa kutumia vikundi halifu vilivyo katika hali ya ufukara na migogoro, yatavielekeza kimapambano na kiharakati kutetea kijeuri ajenda hasimu za wale walio madarakani au washindani wao kwa maslahi ya wanyemelezi. Hali tunayoelezea sio ya kufikirika kwani ndiyo inayotokea huko nchini Nigeria, Kenya na nchi za Afrika ya Kaskazini hivi sasa. Tanzania haina kinga ya kipekee kuiepusha kukumbwa na maovu ya namna hiyo bila utaratibu na vyombo thabiti kuhimili mienendo hasi kama hii. Kutokana na matukio na kauli zinazotolewa na watu mbalimbali hapa nchini, inawezekana tayari wanyemelezi wako kazini wakiongoza vikundi kusukuma ajenda za kutekeleza maslahi yao.4. Masuala yanayotakiwa kufafanuliwa na kudhibitiwa na Dola mapema ili yasiendelee kupotoshwa:

  • Hali ya mahusiano kuzorota pamoja na kashfa dhidi ya Kanisa.

Huu ni wakati wa kukubali kwamba misingi ya Haki, Amani na Upendo katika Taifa letu imetikiswa kwa kiwango kikubwa. Uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi na makusudi unaofanywa na baadhi ya waamini wa dini ya Kiislamu, ukiendeshwa na kuenezwa kupitia vyombo vyao vya habari vya kidini (redio na magazeti) mihadhara, kanda za video, CD, DVD, vipeperushi, makongamano, machapisho mbalimbali na kauli za wazi za viongozi wa siasa na hata viongozi wa dini husika (ushahidi wa mambo yote haya tunao) pasipo Serikali kuchukua hatua yeyote huku bali imekuwa ikibakia kimya tu. Ukimya huu unatoa taswira ya Serikali kuunga mkono chokochoko hizi. Jambo hili linavyoendelea kuachwa hivi hivi linaashiria hatari kubwa ya kimahusiano siku zijazo.
  • Hadhi ya Baba wa Taifa kuhifadhiwa.

Huyu ni kiongozi aliyetoa maisha yake kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu akitetea Watanzania wote bila ubaguzi wowote, akiimarisha umoja wa Kitaifa, amani na upendo kwa watu wote. Kashfa, kejeli na habari za uongo dhidi yake ni kukipotosha kizazi hiki na hata vizazi vijavyo kwa kuondoa moja ya alama muhimu ambazo kiongozi huyo alisimamia kwa ajili ya umoja wa kitaifa.
  • Memorandum of Understanding” (M.o.U) ya mwaka 1992, kwa ajili ya huduma za kijamii zitolewazo na Makanisa kwa Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na huduma za hospitali, vituo vya afya na zahanati na shule mbalimbali zinazoendeshwa na Makanisa nchini kote. Ni vema ikaeleweka wazi kwamba makubaliano hayo (M.o.U) yalikuwa ni kati ya Makanisa ya Tanzania na Makanisa ya nchini Ujerumani ambapo Serikali ya Tanzania ilihusishwa tu, kwa vile raia wake ndio wangenufaika na misaada hiyo ambayo nchi ya Ujerumani ingeitoa kupitia Makanisa hayo. Kanisa limeendelea kujishughulisha na huduma hizi kwa jamii hata kabla ya uhuru na baada ya uhuru pasipo ubaguzi. Ikibidi ni vema kuondoa hali hii, ya Kanisa kuendelea kutukanwa, chuki na kukashifiwa viongozi wake kutokana na huduma hizi kwa jamii yote. Jukwaa la Wakristo Tanzania tunaitaka Serikali itoe tamko la ufafanuzi juu ya M.o.U hiyo, maana yake, makusudi yake na manufaa yake kwa Watanzania wote.


  • Hujuma ya kuchomwa Makanisa na mali za Kanisa, ni tukio la uvamizi na uchokozi wa wazi, ulioyakuta makanisa yetu na waamini wake wakiwa hawana habari na bila maandalizi yoyote. Ni muhimu kuanzia sasa, Wakristo wote wakae macho na wawe waangalifu zaidi.


  • Dhana ya kuwa Tanzania inaendeshwa kwa mfumo Kristo ni potofu na potevu.

Maneno hayo ni ushahidi wa uwepo wa ajenda za waamini wenye imani kali na waliojiandaa kwa mapambano maovu kutetea dhana potovu kinzani na misingi ya demokrasia na haki za binadamu kama ilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa na kuridhiwa na Serikali yetu. Jukwaa la Wakristo nchini tunakanusha wazi wazi na kueleza bayana kuwa, nchi hii haiongozwi kwa mfumo Kristo!. Kwa watu walio makini hakuna kificho kuwa viongozi wote waandamizi wa ngazi ya juu Serikalini awamu ya sasa, asilimia 90 ni Waislamu (Rais wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu, Makamu wa Rais, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi). Kwa mantiki hiyo haiingii akilini kueleza watu kuwa nchi hii inaendeshwa kwa mfumo Kristo! Kwa upande wa Zanzibar asilimia 100 ya viongozi ngazi za juu Serikalini ni Waislamu, na sio kweli kwamba Zanzibar hakuna Wakristo wenye sifa za kuongoza. Kisha, hata uwakilishi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, theluthi mbili ya wajumbe wake ni Waislamu. Tunayo mifano mingine mingi iliyo wazi, na hii ni baadhi tu. Watanzania wanapaswa kuelewa wazi kuwa, nchi hii inaongozwa kwa misingi ya Utawala wa Kisheria na sio vinginevyo.
  • Matumizi hasi ya Vyombo vya Habari vya Kidini:

Vyombo vya habari vya kidini vinatumiwa na viongozi wa dini ya Kiislam kuukashifu Ukristo na kuwachochea Waislamu hadharani kupitia vyombo hivyo wakiwataka wawaue Maaskofu na Wachungaji, iwe kwa siri au hadharani. Japo Serikali imesikia kashfa na uchochezi huo hatarishi, imendelea kukaa kimya, na kuwaacha wachochezi hao wakiendelea kuhatarisha amani bila kuwadhibiti. Jambo hili linatia mashaka makubwa juu ya umakini wa Dola kuhusu usalama wa wananchi nchini mwao. Imani kali za namna hii huchochea vitendo viovu vya uasi na hujuma sio tu dhidi ya waamini na viongozi wa dini fulani, bali hata na kwa Serikali na viongozi waliopo madarakani, endapo waamini wa dini fulani katika taifa kama Tanzania lililo na waamini wa dini nyingi tofauti, hawataheshimu na kutendeana kiungwana baina yao na wale wasio wa dini na mapokeo yao. Hali hii inapelekea kujiuliza kama je,huu ni wakati mwafaka kwa kila raia au kiongozi wa dini kujilinda yeye mwenyewe na waamini wake dhidi ya wenye imani kali?
  • Matukio yanayosababisha hasira na kutenda maovu:

Tumejionea matukio kadhaa ambayo kwayo vikundi vya watu wenye hasira vilisababisha hujuma na uharibifu mkubwa wa mali za watu wengine. Hivyo ni viashiria tosha vya uchovu na unyonge mkubwa katika jamii yetu, ambamo jambo dogo tu na hata la kupuuzwa, likitendwa na afikiriwaye kuwa hasimu wa watu fulani, wahalifu hujipatia fursa ya kuonesha hasira yao kwa vitendo vya hujuma na shari, wakiharibu hata kuteketeza mali na nyenzo za maisha ya jamii. Suala hili lataka uchambuzi yakinifu na wa kiroho ili kupata majibu na maelezo sahihi na wala sio kwa kutumia nguvu za ziada za kijeshi au kwa majibu mepesi ya kisiasa. Hili ni suala lihusulo tunu na maadili ya jamii yote ya Watanzania katika ujumla wao. Kila mmoja wetu ni mhusika na sote tukitakiwa kuwajibikiana katika ujenzi wa amani iletayo mapatano na uelewano kati yetu.

Mapendekezo:
Kutokana na muono wetu huo tunapendekeza yafuatayo:

  • Tabia na mienendo ya kukashifiana ikomeshwe kabisa na badala yake tujengeane heshima/staha tukizingatia utu wa kila mmoja katika utofauti wetu.
  • Tumwendee Mungu wetu na kumwomba atuongoze sote kufuata utashi wake tukitafuta huruma yake iliyo sheheni upendo wake mkuu, ili atujalie umoja wa kuishi pamoja kwa amani nchini mwetu.
  • Tunaitaka Serikali yetu na vyombo vyake vya usalama, sheria na amani kutenda mara moja na bila kuchelewa, katika nyakati ambazo vikundi halifu kisiasa au kidini vinapoanza uchochezi ili kupambanisha wanajamii. Tabia ya kuachia uchochezi wa kidini kuendelea pasipo hatua mathubuti kuchukuliwa na Dola ni udhaifu mkubwa wa uongozi na uwajibikaji. Ikithibitika kwamba uharibifu uliofanywa ulitokana na kikundi mahususi chini ya uongozi wa dini au chama cha kisiasa au asasi isiyo ya kiserikali, basi taasisi husika iwajibishwe na kulipa fidia kwa uharibifu uliofanywa.
  • Lianzishwe Baraza mahsusi lililo huru lisiloegemea chama chochote cha kisiasa wala dini yoyote na litamkwe na kuwezeshwa kikatiba likiwa na dhumuni kuu la kuilinda na kuiongoza Serikali kuto fungamana na dini yoyote na kuhakikisha kwamba dira na dhana ya utu katika mfumo wa uchumi wenye kujali maslahi ya wote havipotoshwi. Baraza hilo liwe na uwezo wa kuvichunguza vyombo vya sheria na usalama itokeapo matatizo makubwa yaashiriayo uvunjifu wa haki na kuteteresha usalama wa nchi.
  • Na sisi viongozi wa dini za Kikristo, Kiislam, Kihindu na nyinginezo tuwajibike katika kufundisha, na katika majiundo ya waamini wetu, hasa vijana, ili kuwajengea uelewa na utashi wa kuvumiliana kwa upendo. Katika kushuhudia na kuadhimisha imani na ibada zetu sote tutambue , tulinde na kukuza maadili, tunu na desturi za imani za watu wengine wanazo ziheshimu na kuzitukuza. Vikundi vya imani kali na pambanishi kwa kutumia kashfa potoshaji sharti vidhibitiwe kwa weledi mkubwa wa viongozi wa dini husika wakisaidiana na usalama wa taifa. Stahamala [kustahimiliana] ni fadhila inayopaswa kufundishwa na kupenyezwa katika mifumo ya uongozi na maisha ya jamii na ihifadhiwe kwa kufuatiliwa kwa karibu sana.


Hitimisho: 
Kwa sasa Kanisa liko katika vita vya Kiroho, hivyo ni vyema Waamini wote wakakumbuka kuwa, katika mapambano kama hayo Mungu mwenyewe, Mwenye enzi yote ndiye mlinzi wa watu wake na Kanisa lake.
JIBU LITAPATIKANA TU, KWA NJIA YA SALA, KUFUNGA NA MAOMBI!
Hivyo siku ya Jumanne tarehe 25 Desemba 2012, inatangazwa rasmi nchini kote kuwa siku ya sala na maombi kwa Wakristo wote na Makanisa yote nchini, pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kuomba kwa imani, amani katika nchi yetu, na kumkabidhi Mungu ashughulikie mipango yoyote iliyopo, ya wazi na ya kisirisiri ya kutaka kuondoa amani ya taifa hili na kuyashambulia Makanisa nchini Tanzania ishindwe na kuanguka pamoja na wale wote walio nyuma ya mipango hiyo.

1. Askofu Bruno Ngonyani (TEC) - Mwenyekiti
2. Askofu Dkt. Israel Mwakyolile (CCT) - Mjumbe (Mwenyekiti Mwenza)
3. Askofu Daniel Aweti (PCT) - Mjumbe (Mwenyekiti Mwenza)
4. Askofu Oscar Mnung’a (CCT) - Mjumbe
5. Askofu Elisa Buberwa (CCT) - Mjumbe
6. Askofu Stephen Mang’ana 
(CCT) - Mjumbe
7. Askofu Dkt. Peter Kitula 
(CCT) - Mjumbe
8. Askofu Alinikisa Felick Cheyo 
(CCT) - Mjumbe
9. Askofu Christopher Ndege 
(CCT) - Mjumbe
10. Askofu Michael Hafidh 
(CCT) - Mjumbe
11. Askofu Charles Salala 
(CCT) - Mjumbe
12. Askofu Dismus Mofulu 
(CCT) - Mjumbe
13. Mchg. Conrad Nguvumali 
(CCT) - Mjumbe
14. Mchg. Ernest Sumisumi 
(CCT) - Mjumbe
15. Mchg. William Kopwe 
(CCT) - Mjumbe
16. Askofu Thaddaeus Ruwa’ichi (TEC) - Mjumbe
17. Askofu Paul Ruzoka 
(TEC) - Mjumbe
18. Askofu Norbert Mtega 
(TEC) - Mjumbe
19. Askofu Severine Niwemugizi 
(TEC) - Mjumbe
20. Askofu Michael Msonganzila 
(TEC) - Mjumbe
21. Askofu Castorl Msemwa 
(TEC) - Mjumbe
22. Askofu Eusebius Nzigilwa 
(TEC) - Mjumbe
23. Askofu Renatus Nkwande 
(TEC) - Mjumbe
24. Askofu Bruno Ngonyani 
(TEC) - Mjumbe
25. Fr. Antony Makunde 
(TEC) - Mjumbe
26. Fr. Sieggried Rusimbya 
(TEC) - Mjumbe
27. Fr. Ubaldus Kidavuri 
(TEC) - Mjumbe
28. Askofu Dkt. Paul Shemsanga (PCT) - Mjumbe
29. Askofu Ability Samas Emmanuel 
(PCT) - Mjumbe
30. Askofu Nkumbu Nazareth Mwalyego 
(PCT) - Mjumbe
31. Askofu Batholomew Sheggah 
(PCT) - Mjumbe
32. Askofu Dkt. Mgullu Kilimba 
(PCT) - Mjumbe
33. Askofu Renatus Tondogosso 
(PCT) - Mjumbe
34. Askofu Emmanuel Mhina 
(PCT) - Mjumbe
35. Askofu O.S. Sissy 
(PCT) - Mjumbe
36. Askofu Jackson Kabuga 
(PCT) - Mjumbe

Popular Posts