Pages

Showing posts with label Kambi ya Upinzani. Show all posts
Showing posts with label Kambi ya Upinzani. Show all posts

Tuesday, July 17, 2012

MAAMUZI YA BARAZA KUU CUF YATANGAZWA.JUMUIYA YA VIJANA YAFUMULIWA YASUKWA UPYA

MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UONGOZI
LA TAIFA KILICHOFANYIKA SHABAN HAMISS MLOO
MJINI DAR ES SALAAM TAREHE 14-15 Julai, 2012.

Yametangazwa leo tarehe 17/07/2012,Ofisi za CUF Buguruni mbele ya waandishi wa habari.

Baraza Kuu la Uongozi Taifa la The Civic United Front (CUF- Chama Cha Wananchi) limekutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kikao ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Prof Ibrahim Lipumba na kufanyika katika Ukumbi wa Shabani Hamisi Mloo , Dar es salaam, Tarehe 14-15 Julai, 2012. Katika kikao hicho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limepokea, limejadili na kuzifanyia maamuzi Agenda mbalimbali zilizowasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ikiwa ni pamoja na;

  1. 1. Utekelezaji wa Kazi za Chama kipindi cha Oktoba 2011-juni 2012
  2. 2. Maandalizi ya Uchaguzi mdogo Jimbo la Bububu
  3. 3. Msimamo wa Chama katika mchakato wa Maoni ya Wananchi kuhusu uandikaji wa Katiba mpya ya Tanzania.
  4. Uimarishaji wa Chama kupitia Jumuiya ya Vijana.
  5. Hali ya Kisiasa Nchini.

Baada ya Mjadala wa kina kuhusiana na agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

Utekelezaji wa Kazi za Chama kipindi cha Oktoba 2011-juni 2012

  1. Baraza Kuu limepokea Taarifa ya Kazi za Chama kwa kipindi cha Oktoba 2011 hadi 2012. Baraza limeipongeza Kamati ya Utendaji kwa Kazi ilizofanya na kusimamia kwa kipindi pamoja na changamoto za kiutendaji zinazowakabili. Baraza Kuu limetoa msisitizo kwa Chama kuendelea kujipanga .

Kuhusu Maandalizi ya Uchaguzi Bububu

  1. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeridhia lengo la Chama kushiriki katika Uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Bububu na kuhakikisha chama kinashinda kwa sababu jimbo hilo ni ngome kubwa ya CHAMA na hasa baada ya kutathmini matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Kuhusu uimarishaji wa Chama kupitia Jumuiya ya Vijana

  1. Baada ya kazi kubwa iliyofanywa na jumuiya za chama na kuonekana kuwa zinapaswa kuimarishwa zaidi, hususani jumuiya ya vijana taifa (JUVICUF), Baraza Kuu limejadili na kukubaliana kufanya mabadiliko katika nafasi mbali mbali za Uongozi ndani ya Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilisha baadhi ya wajumbe waliokuwepo awali. Viongozi walioteuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ni hawa wafuatao:-
S/N JINA NAFASI
1 Katani A.Katani M/kiti
2 Yusuph K. Makame M/Mwenyekiti
3 Khalifa A. Ali Katibu
4 Thomas D.C. Malima Naibu Katibu
5 Sonia Magongo Mjumbe
6 Bonifasia Mapunda Mjumbe
7 Kuruthumu Mchuchuli Mjumbe
8 Said Maulid Mjumbe
9 Ashura Mustapha Mjumbe
10 Hamidu Bobali Mjumbe
11 Ahmed Mudhihir Mjumbe
12 Shomvi R Issa Mjumbe
13 Faustin Khalfan Mjumbe
14 Suleiman S. Abdallah Mjumbe
15 Biubwa M. Mselem Mjumbe
14 Pavu J. Abdallah Mjumbe
15 Gora J. Hamis Mjumbe
16 Hafidh A. Hafidh Mjumbe
17 Ayoub Y. Khamis Mjumbe

Kuhusu mgomo wa madaktari nchini;

  1. Baraza kuu limesikitishwa na mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini kwa zaidi ya miezi saba sasa bila Serikali ya CCM kuwa na mkakati wenye malengo ya kuondoa tatizo lililopo. Kuendelea kwa mgomo huo kumesababisha kusuasua kwa huduma za Afya kunakowasababishia mateso makubwa wananchi wa tabaka la hali ya chini na wengine kufa kwa kukosa tiba katika kipindi muafaka.
  2. Baraza Kuu linawasihi Madaktari wote warejee kazini ili kuokoa maisha ya Watanzania wenzao wasio na uwezo wa kwenda kutibiwa hospitali zinazotoa pesa nyingi, sambamba na hilo tunaiomba Serikali iwaombe Madaktari wote waliosaini kuacha kazi warejee kazini.
  3. Kuendelea kuwafukuza na kuwatishia si kutatua tatizo hili kwa sababu limekuwepo muda mrefu na madaktari wana madai ya msingi ya kuboresha mazingira ya kazi na huduma kwa wananchi pamoja na mishahara yao, madai haya yasidharauliwe kwa sababu yana mantiki kubwa japokuwa hayapaswi kutumiwa kupoteza roho za watu kwenye mgomo. Tunaitaka Serikali ya CCM ihakikishe inatekeleza madai yote ya msingi yanayolalamikiwa na Madaktari, pia kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za Afya.
  4. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limelaani kitendo cha kutekwa, kuteswa na kuhujumiwa kwa kiongozi wa madaktari ndugu. Ulimboka , Baraza Kuu linaitaka serikali iunde tume huru ya wataalam na isiyohusisha usalama wa taifa wala Jeshi la polisi ili suala hili lichunguzwe na matokeo ya uchunguzi yawekwe hadharani.
  5. Mgomo wa madaktari umechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari haidhuru ni sehemu ndogo ya huduma za afya. Watanzania wachache sana wanaopata fursa ya kuonana na daktari. Wengi wanategemea huduma za zahanati na vituo vya afya ambavyo vina hali mbaya sana. Hakuna huduma ya afya ya msingi ya kukidhi mahitaji ya wananchi. Maeneo mengi ya nchi yana theluthi moja tu au chini ya hapo ya mahitaji yao. Tanzania haina wahudumu wa afya wa kutosha. Shirika la Afya la Dunia linakadiria kuwa Tanzania inahitaji wafanyakazi wa sekta ya afya wasiopungua 92000 wakati wafanyakazi wote waliopo ni 25400. Sera ya serikali ni kuwa na wafanyakazi 140,500 ifikapo mwaka 2019. Vyuo vyote vya afya vinafundisha wafanyakazi 4000 kwa mwaka. Kwa sababu ya mazingira mabovu ya kufanyia kazi asilimia 30 ya wahitimu wote (wafanyakazi 1200) wa sekta ya afya wanaacha kazi mwaka wa kwanza baada ya kuhitimu. Zahanati, Vituo vya afya na hospitali nyingi hazina wafanyakazi wenye ujuzi na ari ya kutoa huduma.
  6. Uchambuzi wa mgawanyo wa matumizi halisi ya serikali kisekta yanaonyesha kuwa miaka yote sekta ya afya inatengewa chini ya asilimia 10 ya matumizi yote ya serikali na hakuna dalili ya jitihada zozote za kutenga asilimia 15 ya matumizi ya serikali katika sekta ya afya kama ilivyokusudiwa na sera ya afya ya 2007. Mgao wa matumizi ya serikali katika sekta ya afya umepungua toka asilimia 8.2 mwaka 2008/09 na kufikia asilimia 5.4 mwaka 2010/11.
  7. Watanzania wengi bado wanaathirika na maradhi mengi yanayoweza kuzuiliwa kwa gharama ndogo. Vipaumbele vya matumizi ya fedha za serikali viwe katika kinga na tiba ya maradhi ya kuambukiza na kuhakikisha watoto wote wanapata lishe bora. Maradhi yanayohusiana na kupumua, malaria, kuharisha na ukosefu wa lishe bora ndiyo chanzo cha vifo vingi vya watoto. Maradhi haya yanaweza kuzuwiwa kwa gharama ya wastani. Matumizi makubwa ya serikali yanatengwa kuwatibu watu wachache. Gharama kubwa inatumiwa kuwapeleka wagonjwa wachache hasa viongozi nje ya nchi.

Kuhusu suala la Bajeti ya Mwaka 2012-2013

  1. Baraza Kuu limebaini kuwa malengo ya bajeti ya 2011/12 hayakufikiwa. Katika hotuba ya bajeti ya juni 2011, ilieleza kuwa “Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wananchi katika kupambana na makali ya maisha. Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, pamoja na mambo mengine, inalenga katika kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo.” Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa wakati waziri wa fedha anasoma hotuba ya bajeti, mfumko wa bei Juni 2011 ulikuwa asilimia 10.9. Mfumko wa bei uliongezeka na kufikia asilimia 20 mwisho wa mwaka 2011 na umepungua kidogo sana na kuwa asilimia 18.2 mwezi Mei 2012.
  2. Mfumko wa bei wa vyakula ni wa juu zaidi. Takwimu za serikali zinaonyesha mfumko wa bei uliongezeka toka asilimia 12 mwezi Juni 2011 mpaka kufikia asilimia 26 mwezi desemba 2011 na Mei 2012 ulikuwa asilimia 24.5. Mfumko wa bei ni matokeo ya matumizi makubwa ya serikali yasiyokuwa na tija. Sekta ya kilimo haijatengewa fedha za kutosha kwa madhumuni ya kuongeza tija na uzalishaji wa chakula na mazao mengine ya kilimo. Mgao wa matumizi ya serikali kisekta unaonyesha kuwa sekta ya kilimo ilitengewa asilimia 2.92 mwaka wa fedha 2010/11 na asilimia 1.65 mwaka 2011/12. Taarifa za hali ya uchumi wa taifa zinaonyesha kuwa, kwa muda wa zaidi ya miaka 20 iliyopita, sekta ya Kilimo, misitu na uvuvi kwa pamoja imekuwa inatengewa chini ya asilimia 5 ya matumizi yote ya serikali. Makubaliano ya nchi za SADC ni kutenga alau asilimia 10 ya matumizi ya serikali kwenye kilimo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uzalishaji wa mazao ya chakula na kupunguza umaskini uliokithiri vijijini. Sekta ya kilimo imekua kwa asilimia 3.6 wakati ongezeko la watu linakadiriwa kuwa asilimia 2.9. Nafasi muhimu ya serikali katika kuleta mapinduzi ya kilimo ni katika maeneo ya utafiti wa mbegu bora, mbolea inayofaa kwa mazao katika maeneo mbali na madawa ya kuua wadudu, huduma za ugani na elimu kwa wakulima, miundombinu ya umwagiliaji maji na usafiri.
  3. Kilimo kipo hoi na bei ya bidhaa za wakulima ikiwemo korosho haiwasaidii wakulima na bado wanaendelea kukopwa kwa utaratibu wa ‘stakabadhi gharani.’ Bei ya pamba imepungua toka shilingi 1100 kwa kilo msimu uliopita na sasa ni shilingi 660/ kwa kilo msimu huu.
  4. Katika mwaka 2011/12 Serikali ililenga kukusanya asilimia 17.2 ya pato la taifa kuwa mapato ya serikali. Imefanikiwa kukusanya asilimia 16.9. Ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na mapato yasiyokuwa ya kodi ndiyo hayakufikia kiwango kwa asilimia kubwa. Serikali inalenga kukusanya asilimia 18 ya pato la taifa kama mapato yake. Inakadiriwa kuwa misamaha ya kodi ni asilimia 2.5 ya pato la taifa. Ukwepaji wa kulipa kodi ni asilimia 2-3 za pato la taifa. Sekta ya madini haichaingii ipasavyo katika mapato ya serikali. Serikali makini inaweza kukusanya asilimia 22-25 ya pato la taifa kuwa mapato ya serikali.
  5. Sera za kukusanya mapato zimejikita katika kodi za vinywaji na sigara. Sentensi moja inaniudhi kuisikia katika bajeti kila mwaka nayo ni “Ushuru wa “Cigar” unabaki kuwa asilimia 30.” Hivi cigar ngapi zinazovutwa Tanzania mpaka zistahiki kuwa ndani ya hotuba ya bajeti kila mwaka! Bajeti haizungumzii kabisa hatua zinazochukuliwa kuhakikisha sekta ya madini inachangia vya kutosha mapato ya serikali.
  6. Katika kukabiliana na upungufu wa umeme serikali iliahidi kuchukua “hatua kadhaa za kukabiliana na upungufu huu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100 Dar es Salaam na ule wa megawati 60 Mwanza.” Katika bajeti ya mwaka huu bado inaeleza “Serikali ilisaini Mkataba wa mkopo wa Euro milioni 61 na Benki ya HSBC. Mkopo huu umeelekezwa kugharamia ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawati 60 Nyakato Mwanza.” Bajeti tano mfululizo zimekuwa zinaeleza utekelezaji wa mradi huu. Mpaka sasa haujakamilika. Fedha zinazotengwa kila mwaka kukamilisha ufuaji wa umeme, Nyakato Mwanza zinakwenda wapi? Hali ya umeme bado ni tatizo kubwa nchini mbali na mwaka 2008 kutengwa 1.7 trilioni kama mfuko wa kichocheo cha kufufua uchumi (stimulus package) utekelezaji wake hauelezwi uliyeyukia wapi na fedha hizo zilizotengwa zimekwenda wapi! Serikali ya CCM, imeshindwa kutatua tatizo hili na kuisababishia nchi kupata hasara kubwa kwa kudhoofisha uchumi wa nchi. Hali hiyo imezorotesha uzalishaji viwandani na bidhaa zimepanda bei na kusababisha ukali wa maisha kwa watanzania, huduma za mahospitalini, katika sekta ya elimu, upatikanaji wa maji, KUPOROMOKA KWA SHILINGI na mengi mengineyo. CUF tunaamini bila ya umeme wa uhakika nchi haiwezi kupata maendeleo.
  7. Serikali pia iliahidi kuweka mazingira mazuri ya kuongezeka kwa ajira. Mpaka sasa tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa mno na halielekei kutatuliwa. Katika nchi yenye nguvukazi ya zaidi ya watu milioni 22, walioajiriwa katika sekta rasmi ya viwanda ni watu 115000 tu.
  8. Tatizo kubwa la bajeti yetu ni kuwa matumizi ya serikali hayatekelezi bajeti ya maendeleo iliyopitishwa na bunge. Matumizi ya miradi ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2011/12 yatakuwa chini kwa shilingi bilioni 600 ukilinganisha na bajeti iliyopitishwa na Bunge. Baadhi ya sekta, matumizi halisi ya maendeleo ni chini ya asilimia 50 ya fedha zilizoidhinishwa.
  9. Bajeti ya Maendeleo ya 2012/13 ni ndogo. Matumizi yote ya serikali yameongezeka toka shilingi trilioni 13.1 na kufikia shilingi trilioni 15.1 bajeti ya maendeleo imepunguzwa toka shilingi trilioni 4.9 mwaka 2011/12 na kufikia shilingi trilioni 4.5 mwaka 2012/13. Bajeti ya Maendeleo mwaka 2011/12 ilikuwa asilimia 36.4 ya matumizi yote ya serikali. Matumizi halisi ya bajeti ya maendeleo katika mwaka 2011/12 yatakuwa asilimia 33.3. Mwaka 2012/13 Bajeti ya Maendeleo ni asilimia 30 ya bajeti yote. Matumizi ya kawaida yameongezwa kwa asilimia 23.2 na bajeti ya maendeleo imepunguzwa kwa asilimia 8.1. Ukizingatia mfumko wa bei matumizi halisi ya bajeti ya maendeleo yatapungua mwaka 2012/13 ukilinganisha na mwaka 2011/12. Ili kuweka msukumo katika ukuaji wa uchumi bajeti ya maendeleo iwe alau asilimia 40.
  10. Matumizi ya kawaida yanakua kwa kasi kubwa kwa sababu ya kuongeza gharama za utawala kama vile kuanzisha wilaya na mikoa mipya, safari nyingi za nje za Rais na viongozi wengine wa serikali, ukubwa wa Baraza la Mawaziri, posho za semina na makongamano. Hatua za maksudi zinahitajiwa kuchukuliwa kubana matumizi ya utawala.
  11. Baraza kuu limeshtushwa na hali ya MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA kama ilivyoainishwa na taarifa iliotolewa na Msimamizi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Serikali Kuu, halmashauri mbalimbali nchini na mashirika ya umma, mabilioni ya shilingi ya fedha za walipa kodi wanyonge wa Tanzania zimetafunwa na watendaji wachache bila hatua stahiki kuchukuliwa dhidi yao. Baraza Kuu linaitaka Serikali ya CCM na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuchukua hatua za kuwakamata wahusika wote waliotajwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Matumizi ya Rasilimali za mafuta, gesi, madini

  1. Kuhusu matumizi ya Rasilimali za mafuta, gesi, madini ya uranium na madini mengine nchini, Baraza kuu linaitaka serikali kuweka utaratibu mzuri wa mchakato wa matumizi ya rasilimali hizi ili ziweze kuwanufaisha watanzania wenyewe kwani uzoefu inaonyesha kuwa nchi nyingi dunia zimeingia katika matatizo makubwa kutokana na ufisadi mkubwa wa watu wachache waliohodhi rasilimali hizo kwa maslahi yao.
  2. Baraza Kuu la linatoa wito kwa Watanzania wote, pale Tume ya Kukusanya Maoni itapopita kwenye Wilaya zao, kutoa Maoni juu ya sehemu ya Mapato yanayopatikana toka kwenye mauzo ya Mali ya Asili kama vile gesi, dhahabu na madini mengine yagawiwe kwa Wananchi moja kwa moja ili yaweze kupunguza makali ya maisha na kuleta ulinzi shirikishi wa Rasilimali za Nchi na mali ya Asili ya Nchi yetu katika kukuza na kuimarisha dhana ya Utawala Bora.

Mpasuko wa kisiasa ndani ya serikali ya CCM

  1. Kuhusu mpasuko wa kisiasa ndani ya serikali ya CCM unaathiri na kuiyumbisha nchi na ustawi wa maisha ya watanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na makundi makubwa ya nani awe mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015. Jukumu la msingi la chama kinachounda serikali inayounda kufahamu kuwa nchi yetu inahitaji mabadiliko. Baraza Kuu linatoa wito kwa Watanzania kuzinduka na kufahamu kuwa nchi yetu inahitaji mabadiliko. CUF na viongozi wake wako tayari kuwaongoza Watanzania kuelekea katika mabadiliko wanayoyataka. CCM imeshindwa kuiongoza Tanzania. Na tujiandae kuishughulikia kikamilifu mwaka 2014/15 ili CUF iweze kuunda serikali makini itakayoweza kuweka mipango thabiti ya kiuchumi na maendeleo ya Taifa yetu.

Kuhusu suala la Vitambulisho vya Mnzanzibar Mkaazi ZAIN ID

  1. Baraza Kuu la Uongozi Taifa linaipongeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar juu ya maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Wawakilishi kuhusu kushghulikia suala la Vitambulisho vya mzanzibari mkaazi ZAN-ID. Baraza Kuu linawaomba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuona haja ya kutatua tatizo hili la Vitambulisho vya Mzanzibar Mkazi ili kuendeleza Ummoja uliopatikana kwa siku za Karibuni.

Kuhusu suala la Sensa

  1. Baraza kuu linaitaka serikali kudhibiti utoaji wa Takwimu ili kuepusha migongano isiyo ya lazima ndani ya Nchi. Baraza kuu linaona kuwa mgogoro uliopo sasa baina ya Waislamu na serikali katika suala la Sensa unatokana na serikali kutodhibiti utoaji wa takwimu za idadi ya watu kwa taasisi zisizohusika. Baraza Kuu limesikitishwa na namna serikali imelishughulikia tatizo ikiwemo vyombo vya serikali kutoa takwimu potovu na kuwa na dodoso la sensa linalohesabu nyumba za ibada bila kuhesabu waumini wa madhehebu husika. Linatoa wito kwa Rais Kikwete kukutana na viongozi wa dini zote kuwasikiliza hoja zao na kutafuta maridhiano kuhusu dodoso la dini katika sensa kwani ikiwa sehemu ya jamii itahamasishwa na kususia sensa, zoezi hili lenye gharama kubwa halitafanikiwa na nchi itakuwa na takwimu zisizo sahihi.

Msimamo wa Chama katika mchakato wa kutoa Maoni ya Wananchi kuhusu uandikaji wa Katiba Mpya ya Jamuhuri Muungano

  1. Baraza Kuu limewapongeza Viongozi wa Chama kwa jitihada zilizofanyika za kudai Katiba Mpya na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na kufanikiwa kuishinikiza Serikali kuanzisha mchakato wa kukusanya Maoni ya wananchi juu mabadiliko ya Katiba mpya. Sera ya CUF ni kuwa na Muungano wa Serikali tatu. Sera hiyo imezingatia ukweli kwamba muundo Mpya wa Muungano ndio unaoweza kutoa ufumbuzi wa kudumu kwa changamoto (Kero) za muda mrefu za muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili. Serikali ya Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya mambo yake kuhusu Zanzibar. Ikiwemo uamuzi wa mwisho kwa matumizi ya mali asili (Mafuta, gesi na Madini) na matumizi ya kiuchumi ya bahari.
  2. Baraza kuu limeona ni vizuri Serikali ya Muungano ihusike na mambo ya jumla ambayo wananchi wa Serikali mbili zinazounda Muungano watakubaliana. Hata hivyo kwa kuwa Muungano sio wa vyama na umekuwepo kabla ya kuungana kwa TANU na ASP1977, na kwa kuheshimu demokrasia ya wananchi wa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar) waliofanya Muungano uwepo mwaka 1964, CUF- Chama Cha Wananchi kinasisitiza kuwa Tume isikilize na kuyaheshimu maoni ya Wananchi na isiyachakachue.
  3. CUF- Chama cha Wananchi tunawahimiza wanachama na wananchi kwa ujumla wao kutoa maoni yao kwa UHURU ili kufanikisha jambo hili kwa mustakabali wa Nchi yetu. Baraza Kuu limesisitiza kusimamia na kuheshimu Sera ya Chama ya kutaka Muundo wa Serikali tatu ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwepo na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Baraza kuu linawaomba Watanzania kushiriki kutoa Maoni yatakayowezesha kuandikwa Katiba Bora ikayotujengea Tanzania Tuitakayo.

Kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi

  1. Baraza Kuu linaitaka Serikali kuanzisha Mchakato wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi sambamba na Mchakato wa ukusanyaji wa Maoni ya Katiba ili Uchaguzi wa 2015 uweze kufanyika chini ya Tume itayokubaliwa na Watanzania wote ili kuipa muda Tume hiyo kuweza kupitia Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kuhusu suala la Haki ya Kumiliki Ardhi

  1. Baraza Kuu la uongozi linatoa wito kwa serikali kuwamilikisha Watanzania ardhi yao hasa ukizingatia mchakato wa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki na wimbi la kutafuta na kupora ardhi linalofanywa na nchi zenye fedha lakini zinaagiza chakula toka nje. Katiba mpya iwape Watanzania haki ya kumiliki ardhi yao.

Mwisho;

Baraza Kuu la Uongozi Taifa linawatakia watanzania wote ushiriki mwema katika utoaji wa Maoni yatakayowezesha kupatikana kwa Katiba Mpya.

Imetolewa na

Prof.Ibrahim Lipumba

Mwenyekiti CUF Taifa

HAKI SAWA KWA WOTE

HOTUBA YA MSEMAJIMKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSUMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 WIZARA YA MAMBO YANDANI YA NCHI

HOTUBA YA MSEMAJIMKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA VINCENT JOSEPHAT NYERERE (MB), KUHUSUMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 WIZARA YA MAMBO YANDANI YA NCHI


(Kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)

UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, napenda kuchukua fursa hii kuwasilishamaoni yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndaniya nchi kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Aidha, napenda kuwashukuru askari wa Jeshila Polisi na Jeshi la Magereza wanaoishi Kambi iliyoko katika Kata ya Mkendokwa kunichagua kuwa Diwani wao. Vile vile, nawashukuru wananchi wote wa vyamavyote na dini zote Jimbo la Musoma Mjini kwa kunichagua kuwa Mbunge na mteteziwao. Pia napenda kumshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwaimani yake kubwa kwangu kwa kuniteua kuwa Msemaji Mkuu wa Kambi katika Wizarahii.

Kwa upekee kabisa, Mheshimiwa Spika,kwa wanaoeneza propaganda kwamba CHADEMA inachukia au kudharau askari polisi wetu,naomba nitoe shukrani zangu kwa mke wangu Helen[o1] V. Nyerere, ambaye pia ni askari waJeshi la Polisi.
UTEKELEZAJI WAAHADI ZA SERIKALI
Mheshimiwa Spika, Katikamwaka uliopita wa fedha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilihoji matukio mbalimbali ya mauaji ya raia yaliyowahusisha askari wa Jeshi la Polisi pamoja na wavyombo vingine vya dola. Aidha, tulihoji matukio mengi ya ukiukwaji wa haki zabinadamu za wananchi wetu hasa katika maeneo yenye migodi mikubwa ya dhahabukama vile Nyamongo, Arusha na kwingineko katika nchi yetu. Vile vile, tulihojisababu za Serikali kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria na za kiutendajiwatuhumiwa wa makosa haya makubwa.
Mheshimiwa Spika,Wakatianatoa hoja yake ya kuahirisha Mkutano wa Bunge la Bajeti la mwaka jana, WaziriMkuu aliahidi kwamba Serikali ingefanya uchunguzi wa matukio yote ya mauaji kwamujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (The Inquests Act), Sura ya 24 ya Sheriaza Tanzania. Kwa maneno yake mwenyewe, Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema:“vifo ... ambavyo vimetokea katika mazingira ya kutatanisha chini ya mikono yaVyombo vya Dola, ni lazima vichunguzwe.”Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, hadi wakati tunaandika maoni haya, hakunaMahakama ya Korona hata moja ambayo imeitishwa kwa lengo la kuchunguza vifo vilivyotokanana matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali kutoa kauli rasmi mbele ya Bunge hili tukufu kama kauli yaWaziri Mkuu ilitolewa kwa lengo la kuwahadaa Watanzania. Aidha, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inaitaka Serikali itamke ni lini Serikali itaunda Mahakama zaKorona ili kuchunguza matukio yote ya mauaji ya wananchi katika maeneo yotetuliyoyataja mwaka jana.

Mheshimiwa Spika,Kwasababu ya Serikali kutotimiza ahadi yake ya kuchunguza matukio ya mauaji kwamujibu wa Sheria tajwa, vitendo vya mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vimeendeleakutokea katika nchi yetu. Kwa mfano, katika taarifa yake ya Haki za Binadamukwa Mwaka 2011, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinaripoti kwamba “mwenendowa matukio ya ukatili wa polisi na mauaji yanayofanywa kinyume cha sheria navyombo vya dola umeendelea kuongezeka katika nchi yetu. Kati ya Januari naDesemba 2011 tayari watu 25 wamekwisharipotiwa kuuawa wakiwa mikononi mwapolisi na maafisa wengine wa usalama, wakati ambapo watu wengine 50walijeruhiwa.” Taarifa hii inaungwa mkono na taarifa ya Hali ya Haki za Binadamu kuhusu Tanzania iliyotolewa mwaka huu na Wizaraya Mambo ya Nje ya Marekani (State Department)inayoonyesha kuwa bado yapo mauaji yanayotokea mikononi mwa vyombo vya dolaikiwemo jeshi la polisi, utesaji na wananchi wanaotuhumiwa kujikuta wakipatavipigo kinyume na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia.
MAUAJI YENYE SURAYA KISIASA
Mheshimiwa Spika,Kutokana na Serikali kutochukua hatua kukabilianana matukio ya mauaji yanayohusishwa na vyombo vya dola, sasa limezuka wimbi lamauaji na matukio ya majaribio ya mauji yenye sura ya kisiasa katika maeneombalimbali nchini. Matukio hayo ni pamoja na mauji ya kada wa CHADEMA MbwanaMasudi yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Igunga,na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River, Marehemu Msafiri Mbwambo,mara baada ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Aidha, Mheshimiwa Spika, kumekuwa na majaribio ya mauaji ambapo wabunge waCHADEMA Mheshimiwa Highness Kiwia wa Jimbo la Ilemela na Mheshimiwa SalvatoryMachemli wa Jimbo la Ukerewe, walioshambuliwa kwa mapanga mbele ya maafisapolisi na watu wanaosadikiwa kutumwa na makada wa CCM mkoani Mwanza. Vile vile,Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) alivamiwana wafuasi wa CCM wanaodaiwa kutumwa na Iddi Chonanga, Diwani wa Kata ya Nduli (CCM)katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Mheshimiwa Spika, Matukio ya mauaji au majaribio ya mauajiyenye sura ya kisiasa yamewahusu pia watu ambao sio wanachama au viongozi wavyama vya siasa lakini wanaonekana kupinga matakwa ya watawala. Haya yamemkuta Mwenyekitiwa Jumuia ya Madaktari Dr. Steven Ulimboka ambaye alitekwa nyara na kuteswa kwakikatili na watu ambao taarifa za vyombo vya habari zimewataja kuwa maafisa wavyombo vya dola. Kwa mara nyingine tena, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iamuru kukamatwa kwa watuhumiwawote ambao wametajwa kuhusika na utekaji nyara na jaribio la kumuua Dr.Ulimboka ili kufuta dhana kwamba vyombo vya dola viko juu ya sheria na vinawezakuua au kutesa wananchi bila mkono mrefu wa sheria kuwaangukia.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 14 Julai 2012, mtu anayesemekanakuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM katika Kata Ndago, Jimbo la IrambaMagharibi, Yohana Mpinga, ambaye pia ni mtoto wa Mwenyekiti wa CHADEMA katikaKata ya Urughu alifariki dunia kufuatia vurugu zilizotokea baada ya kumalizikakwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na viongozi wa CHADEMA katika Kata ya Ndago.Kwa vile, tayari baadhi ya Wabunge na viongozi wa Serikali ndani ya Bunge hilitukufu wanaelekea kuwa wameshapitisha hukumu kwamba CHADEMA inahusika na kifocha Marehemu Yohana Mpinga, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina haya ya kuelezakuhusiana na tukio hili.
Kwanza, mkutano wa hadhara wa CHADEMAulihudhuriwa pia na maafisa polisi waliokuwepo wakati wote wa mkutano huo.Pili, licha ya kuwepo kwa maafisa polisi hao, kundi la wahuni wanaodaiwakukodiwa na makada wa CCM wa Jimbo la Iramba Magharibi walivuruga mkutano huokwa kupiga mawe watu waliohudhuria mara mbili lakini mara zote polisiwaliokuwepo hawakuchukua hatua zozote dhidi ya kundi hilo la wahuni. Aidha,mara ya wahuni hao kuvuruga mkutano mara ya pili, viongozi wa CHADEMA walitoataarifa rasmi katika Kituo cha Polisi cha Ndago na kufunguliwa jalada nambaNDG/RB/190/2012.

Tatu, mara baada ya kutoa taarifa hiyo kwapolisi, mkutano wa hadhara uliendelea bila fujo yoyote hadi ulipomalizika na msafarawa viongozi wa CHADEMA kuondoka eneo la Ndago na kuelekea Kinampanda ambakokulikuwa na mkutano mwingine wa hadhara. Wakati huo, kundi la askari polisi waKikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) kutoka Kiomboi walishafika katika eneo lamkutano na kukuta mkutano umemalizika. Nne, kwa vile mkutano wa hadhara waCHADEMA ulimalizika kwa amani mbali na matukio ya kihuni yaliyoripotiwa kwa Jeshila Polisi, na kwa vile kulikuwa na kikosi cha FFU na askari polisi wenginekatika eneo la mkutano baada ya msafara wa CHADEMA kuondoka, ni wazi kwamba watuwanaotakiwa kutoa maelezo ya jinsi Marehemu Yohana Mpinga alivyofikwa na mautini Jeshi la Polisi lenyewe.

Aidha, Mheshimiwa Spika, ni Jeshi la Polisi pekee linaloweza kuwaelezaWatanzania kwa nini kikundi cha wahuni waliowarushia mawe viongozi wa CHADEMAna wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara hawakuchukuliwa hatua zozotena polisi waliokuwepo kwa muda wote wa mkutano huo au askari wa FFU waliofikabaada ya msafara wa CHADEMA kuondoka. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwasana na mauaji ya kijana huyo na inatuma salamu za pole na rambi rambi kwafamilia, ndugu na jamaa wa marehemu. Hata hivyo, Kambi yetu inasikitishwa nakushangazwa sana na ushabiki wa kisiasa ambao umejitokeza humu Bungeni na kauliza kutoa hukumu ambazo zimetolewa na baadhi ya Wabunge na viongozi wa Serikalibila hata kusubiri uchunguzi kamili juu ya jambo hili.
MASLAHI YA POLISI NA MAGEREZA
Mheshimiwa Spika, Katikamaoni yake ya mwaka jana Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ililalamikia utamaduniwa Serikali kupuuza maslahi ya askari polisi na wale wa Jeshi la Magereza. Utamadunihuu ni wa muda mrefu sana. Kwa mfano, katika hotuba ya bajeti ya Waziri wa Mamboya Ndani kwa mwaka wa fedha 2006/2007, aliyekuwaWaziri wakati huo alikiri kwamba “... kutokana na kipato kidogo cha askari polisi,inawawia vigumu kukopa katika mabenki nchini kutokana na riba kuwa kubwa nakukosa dhamana za uhakika. Hivyo, askari polisi hawana mahali popote wanapowezakupata fedha za kujiendeleza kiuchumi. Aidha, mishahara na posho wanayolipwaaskari bado haikidhi hali halisi ya mahitaji yao na familia zao.”

Mheshimiwa Spika,Tokawakati huo hadi sasa, maslahi ya askari polisi yamekuwa mabaya zaidi kutokanana kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumuko wa bei hasa za vyakula kupandawakati ambapo mishahara yao haijaongezeka sambamba na ongezeko la gharamahalisi za maisha. Aidha, katika hali inayoonyesha kutokujali kabisa maslahi nahali za maisha za askari wetu, Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yakeiliyotolewa tarehe17 Novemba, 2011 na aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa KhamisSued Kagasheki, aliyeliambia Bunge hili tukufu kwamba “... posho yaaskari imepandishwa na ... kwamba (inatakiwa) itoke kwenye shilingi laki mojampaka shilingi laki moja na hamsini.... Ni jambo ambalo tunalo na tumelifanyiakazi na tuna uhakika kwamba, litaweza kutimia….”

Mheshimiwa Spika, Ni ukweli usio na mjadala kwamba askaripolisi na magereza bado wanapokea posho ya kujikimu ya shilingi laki mojabadala ya shilingi laki moja na elfu hamsini iliyoahidiwa na Serikali mbele yaBunge hili tukufu. Aidha, katika mazingira yakushangaza kabisa, mara baada ya Serikali kutoa ahadi Bungeni juu ya poshohiyo, uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi ulituma maelekezo kwa Makamanda waPolisi wa Mikoa kufanya uchunguzi ili kubaini askari wote waliokuwa wanadaiwalipwe posho ya shilingi laki moja na nusu kama ilivyoahidiwa ili askari haowafukuzwe kazi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaSerikali ilieleze Bunge lako tukufu ni lini italipa malimbikizo ya baki yashilingi elfu hamsini kwa mwezi kwa kila askari polisi na magereza ambayohaijawalipa askari hao hadi hivi sasa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali ianze kuwalipa askari polisi na magereza posho ya kujikimu yashilingi laki moja na nusu kwa mwezi kuanzia mwaka huu wa fedha, kwa vile ahadiya Serikali iliyotolewa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani haijawahikukanushwa, kubatilishwa au kubadilishwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika,Sio tukwamba Serikali haitekelezi ahadi inazotoa Bungeni juu ya malipo ya askaripolisi na magereza. Serikali pia imekuwa inawakopa watumishi hao bila ridhaayao. Kwa mfano, randama ya fungu la 29 inaonyesha kuwa Jeshi la magerezalinadaiwa jumla ya shilingi bilioni 23.65. Kati ya fedha hizo, watumishi waJeshi la Magereza wanaidai Serikali jumla ya shilingi bilioni10.34 ambazo nimalipo ya stahili zao mbali mbali kama vile fedha za likizo, uhamisho, mafunzo,n.k. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli mbele yaBunge hili kama, na lini, italipa madeni haya ya askari magereza wetu wanaokeshamagerezani usiku na kushinda juani mchana wakiwalinda wafungwa na mahabusuwaliojaa katika magereza ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Kuna hatari kwa askari wa Jeshi la Magereza kufanyakazi katika mazingira magumu ambayo tumeyaeleza katika maoni haya. Mfano ni katikaJimbo langu la Musoma Mjini. Mbali na makazi duni ya askari magereza, vile vilekuna umbali mrefu kati ya kambi ya askari magereza ya Nyasho na Gereza la Mkoalililopo Kata ya Mkendo na askari magereza wamekuwa wakitembea kwa miguu usikuwanapokuwa zamu gerezani. Hii inahatarisha usalama wao kwani wanaweza kuvamiwana kudhuriwa na wafungwa au mahabusu waliokwisha kumaliza adhabu zao lakiniwakawa na visasi na askari hao. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaSerikali iwapatie gari askari wa kambi ya Nyasho na makazi mengine ya askarimagereza yaliyoko mbali na magereza wanakofanyia kazi ili kunusuru maisha yaaskari magereza wetu.

Mheshimiwa Spika,Katikamaoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya mwaka jana, tulipendekeza kwamba “...utaratibu wa sasa wa polisi wa ngazi za chini kukatwa shilingi 5,000 kila mwezikwenye mishahara yao, kwa ajili kugharamia mazishi yao na wategemezi wao,ufutwe mara moja, kwani unawanyonya kwa sababu vipato vyao ni vidogo. Badalayake ... serikali ibebe jukumu hilo.” Hata hivyo, hadi tunaandika maoni haya,Serikali imeendelea kupuuza mapendekezo haya kwa kisingizio kwamba ‘mfuko wa kufa na kuzikana’ ni wa hiariilhali askari polisi wanaendelea kukatwa mishahara yao kwa lazima. Kwa mara nyingine tena Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inatamka kwamba kukata mshahara wa mfanyakazi bila ridhaa yakewakati hadaiwi chochote na mwajiri wake ni kinyume cha sheria husika za nchiyetu na kitendo cha jeshi la Polisi kuendelea kukata mishahara ya askari polisikwa ajili ya ‘mfuko wa kufa na kuzikana’ bila ridhaa ya askari polisi wenyewekikome mara moja.

Mheshimiwa Spika,KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inafahamu kwamba askari polisi wanaofanya kazi zalindo katika mabenki yote ya biashara hapa nchini hulipwa posho ya shilingielfu kumi kwa siku. Hata hivyo, Serikali haijawahi kutamka hadharani kiasiambacho mabenki hayo hulipa serikalini kwa ajili ya kazi hiyo ya kulindamabenki binafsi. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaSerikli kulieleza Bunge lako tukufu kiasi ambacho mabenki ya biashara hulipaserikalini kwa ajili ya huduma ya ulinzi inayotolewa na askari polisi ili Bungelako lifahamu kama askari polisi wanaofanya kazi hiyo wanalipwa inavyostahili.
VITENDEA KAZI VYAPOLISI
Mheshimiwa Spika, Kwamujibu wa ripoti ya Hali ya Uchumi wa Taifa,makosa ya jinai yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchiniyalikuwa 62,133. Ripoti inasema kwamba kwa mwaka 2011 makosa 63,703 ya jinaiyaliripotiwa katika vituo vya polisi nchini.Kwa kiasi kikubwa, ongezeko hili la uhalifu linasababishwa naaskari wa doria kushindwa kufika kwenye maeneo ya matukio ya uhalifu kwa harakapindi wapatapo taarifa kwa kisingizio cha kukosa mafuta kwa ajili ya magari yadoria.

Hatahivyo, Mheshimiwa Spika, nyaraka zaSerikali zinaonyesha kwamba Bunge lako tukufu limekuwa likiidhinisha fedhanyingi kwa ajili ya mafuta ya magari ya Jeshi la Polisi. Kwa mfano, kwa mujibuwa randama ya Fungu la 28 kwa mwaka huu wa fedha, matumizi halisi ya mafuta kwaajili ya Jeshi la Polisi kwa mwaka wa fedha 2010/2011 yalikuwa shilingi bilioni2.81. Aidha, katika mwaka wa fedha uliopita Bunge lako tukufu liliidhinishashilingi bilioni 2.61 kwa ajili ya mafuta, wakati ambapo kwa mwaka huu wa fedhaSerikali inaomba Bunge liidhinishe shilingi bilioni 2.56 kwa ajili ya mafuta yamagari ya Jeshi la Polisi.

WakatiBunge limekuwa lkiidhinisha mafungu haya makubwa ya fedha kwa ajili ya mafuta,askari polisi wamekuwa wakilalamika kwamba hawapewi fedha za mafuta kwa ajiliya magari ya doria hivyo kusababisha askari polisi kushindwa kufanya kazi zaohizo ipasavyo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali ielezezinakopelekwa fedha za mafuta kwa ajili ya Jeshi la Polisi kama gari moja ladoria linapatiwa lita 5 za mafuta kwa kutwa na/au usiku.
IDARA YA UHAMIAJINA PAKACHA LA MIPAKA
Mheshimiwa Spika,Mipakayetu na nchi jirani zinazotuzunguka imekuwa pakacha linalovuja. Ndio maanakatika hotuba yetu ya mwaka janatuliliambiaBunge lako tukufu kwamba “... kumekuwana ongezeko la wageni wengi kutoka nchi za nje ... kiasi cha kujiuliza kamanchi hii ina utaratibu wowote wa kuratibu na kudhibiti uingiaji wa wageni hapanchini.” Tulionyesha jinsi ambavyo kumekuwa na ongezeko la wageni haramu kutokanchi za Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Burundi, Rwanda, Kenya,Uganda, Pakistan, Nigeria, China, India na Bangladesh “ambao wanaishi Tanzaniakwa mfumo usio rasmi, bila ya kuwa na hati zinazowaruhusu kufanya hivyo.”Tulitahadharisha kwamba “utaratibu wa kuachia kila mgeni kuingia Tanzania nakuishi atakavyo bila ya vyombo husika kujua kuwepo kwake ni hatari kiusalama,hasa katika zama hizi za kusambaa kwa ... ugaidi na uharamia wa kimataifakatika masuala ya fedha, biashara za binadamu ...” n.k.

Mheshimiwa Spika, Manenona tahadhari zetu ziliangukia kwenye masikio ya Serikali kiziwi. Na sasa yaletuliyoyasema yameanza kutimia kwani ni mwezi mmoja tu umepita tangu wahamiajiharamu zaidi ya arobaini kutoka Ethiopia kukutwa wamekufa ndani ya lori lamizigo ambalo kwa vyovyote vile lilitokea nchi jirani. Watu hawa waliingiajenchini na kusafiri hadi katikati ya nchi yetu bila kujulikana na maafisa waUhamiaji, polisi wa usalama barabarani na usalama wa taifa kama kweli nchi yetuiko salama? Ni afisa gani wa Idara ya Uhamiaji aliyewapitisha katika mpaka wetuwa Namanga au Horohoro au Sirari au Kogaja au Borogonja? Na ni askari polisigani aliyewasindikiza hadi Kongwa? Aidha, ni afisa mizani gani wa TanRoadsaliyepitisha lori walimokuwa watu hao bila kulikagua na kujua kilichokuwamo?
KambiRasmi ya Upinzani Bungeni ilitegemea – kwa kuzingatia ukubwa na uzito wa kashfahii – viongozi waadilifu katika Wizara, Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi wangewajibikakutokana na uchafu huu. Hata hivyo, hakuna hata mmoja ambaye amefanya hivyo.Kwa vile uwajibikaji wa hiari unaelekea kushindikana, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inamtaka Rais Kikwete kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuwawajibishawale wote waliohusika kuanzia viongozi wa Wizara walioko humu Bungeni nauongozi wa juu wa Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi ili kuondokana na aibuhii ya nchi yetu kuwa transit routeya biashara ya kusafirisha binadamu katika sehemu hii ya Bara la Afrika.

Mheshimiwa Spika,Matatizoya ongezeko la wahamiaji haramu katika nchi yetu linatokana na Idara yaUhamiaji kuendekeza vitendo vya kifisadi katika kuajiri, kupandisha madaraja auvyeo wa maafisa wa Idara hiyo. Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, ajira katikaIdara ya Uhamiaji haizingatii tena elimu, uwezo na weledi wa maafisa husika.Bali, kwa mujibu Taarifa ya Utafiti waMpango Mkakati wa Mageuzi Katika Utumishi wa Uhamiaji (Immigration Service Reform Programme Strategic Plan Research Report)iliyochapishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 27 Novemba, 2011, “mara nyingi mgawanyo ya kazi (katika Idara)hautegemei sifa bali unategemea upendeleo, rushwa, kujuana na urafiki vituambavyo viko kinyume na maana halisi ya mgawanyo wa kazi.” (“Most of the timeplacement is not based on merits but depends on nepotism, bribery and technicalknow-who, friendship and favouritism that have been contrary to the wholemeaning of placement.”)

Mheshimiwa Spika, Ushahidiwa kauli hii unapatikana katika Taarifa hiyo ya Utafiti inayoonyesha kwamba maafisawengi wa ngazi za juu katika Idara ya Uhamiaji ni watu wenye uwezo mdogokielimu kulinganisha na maafisa wa ngazi za chini wa Idara hiyo. Kwa mfano, katikangazi ya Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji kwenda juu hadi kwa Kamishna Mkuu, kunamaafisa kumi wenye shahada ya uzamili (masters degree), wawili wenyepost-graduate diploma (PGD), ishirini na nne wenye shahada ya kwanza, tisawenye stashahada, saba wenye diploma, kumi na moja wenye kidato cha sita na 248wenye elimu ya kidato cha nne. Katika maafisa hawa wa ngazi za juu, kunaKamishna mmoja mwenye elimu ya kidato cha nne wakati kuna Makaimu Kamishna 216wenye elimu hiyo ya kidato cha nne na Kamishna Wasaidizi Wakuu 31.

Kwaupande mwingine, Mheshimiwa Spika, kuanziangazi ya Mrakibu Mwandamizi (Senior Superintendent) kwenda chini mpaka koplokuna maafisa wenye shahada ya uzamili 36, wenye post-graduate diploma wakosaba, wenye shahada ya kwanza wako 340, wenye stashahada wako 78, diploma wakokumi wenye cheti (certificate) wako 52, waliomaliza kidato cha sita wako 585wakati waliohitimu kidato cha nne wako 337. Katika mazingira ambayo maafisawenye uwezo mkubwa wa elimu hawapewi nafasi za juu katika Idara badala yakeuongozi wa juu umejazwa na wenye elimu za mashaka kama inavyoonyeshwa katikaTaarifa ya Utafiti ya Wizara, ni wazi kwamba matukio kama ya maafa ya wahamiajiwaliokutwa wamekufa Jimboni kwa Naibu Spika wa Bunge hili tukufu hayawezikuepukika!

Aidha,Mheshimiwa Spika, katika mazingiraya upendeleo na rushwa katika ajira ya Idara ya Uhamiaji ya aina hii, maafisauhamiaji hawawezi kuacha kutumiwa na wanasiasa wa chama tawala kuwatuhumu washindaniwao kisiasa kuwa sio raia wa Tanzania ili kuwaondoa katika kinyang’anyiro chachaguzi zetu. Hivi ndivyo ilivyotokea kwa Mheshimiwa Ali Mohamed Keissy alipotakakugombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA na kuzushiwa tuhuma kuwa siyo raia. Hatahivyo, alipojiunga na CCM bila ridhaa yake tuhuma za kutokuwa raia ziliyeyukana sasa ni Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini katika Mkoa anakotokeaWaziri Mkuu!

Mheshimiwa Spika,KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa kauli rasmi mbele ya Bungehili tukufu juu ya mambo haya ambayo yamethibitishwa na Ripoti ya Utafiti yaWizara ya Mambo ya Ndani. Aidha, Kambi inaitaka Serikali itoe kauli kama kunahaja yoyote ya kutumia mamilioni ya fedha za wananchi kusomesha maafisa wa Idaraya Uhamiaji ambao baada ya kufuzu hawapatiwi vyeo na majukumu yanayolingana nauwezo wao wa kielimu.
JESHI LA ZIMA MOTO NA UOKOAJI
Mheshimiwa Spika, Ni dhahiri kuwa umuhimu wa Jeshi hili unaonekana paleyanapotokea majanga ya moto, mafuriko au maafa mengine kama vile tetemeko laardhi ambapo athari za matukio haya ni makubwa sana na mara nyingi hupelekeawananchi kupoteza maisha. Malalamiko ya wananchi katika maeneo mbalimbali juuya Jeshi la Zimamoto kuchelewa kufika katika maeneo ya tukio yamekuwepo kwa miakamingi na yamepigiwa kelele sana hapa Bungeni. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inarudiaushauri wake kuwa Serikali iboreshe mfumo mzima wa zimamoto katika nchi yetuili kukabiliana na majanga ya moto yanayoongezeka kutokana na kupanuka na kukuakwa miji yetu.

Mheshimiwa Spika, Baadaya maelezo na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ninaombakuwasilisha.
.....................……………………… ……………..

VINCENTJOSEPHAT NYERERE


MSEMAJI MKUU WA


KAMBI RASMI YAUPINZANI BUNGENI


WIZARA YA MAMBO YANDANI YA NCHI


17/07/2012

Friday, July 6, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza swali kutoka kwa kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza swali kutoka kwa kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Mjini Dodoma Julai 6,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Popular Posts