Pages

Showing posts with label Sumbawanga. Show all posts
Showing posts with label Sumbawanga. Show all posts

Friday, November 23, 2012

Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana Aung'uruma Sumbawanga na Kuhudhuria Kikao Cha Shina


Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Chipukuizi wa CCM, wakati wa mapokezi yake kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa, alipowasili mkoani Rukwa, jana, akiwa katika ziara yake ya siku nne kujitambulisha, kukagua na kueleza kwa wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.
Kinana akimsalimia aliyekuwa mbunge wa Sumbawanga mjini Hilary Aeshi, kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa, jana.
Kinana akimsalimia Mwanasiasa mkongwe, Chrisant Mzindakaya, kwenye Uwanja wa Ndege wa sumbawanga, mkoani Rukwa, jana
Mjumbe wa Shina namba moja la Kisesa mkoani Ruwa,  Simoni Kibona akimsalimia kwa furaha, Kinana alipofika kwenye tawi hilo, jana na kushiriki kikao cha hilo ikiwa ni sehemu ya kuhimiza viongozi kutembelea mashina na matawi ya CCM ili kuimarisha chama.
Wajumbe wa mkutano wa shina namba moja la Kisesa mkoani Rukwa wakimsikiliza Kinana wakati akiwahutubia, aliposhiriki mkutano wao uliofanyika jana.
Kinana akifurahia ngoma ya kina mama wa shina la Isesa, mkoani Rukwa
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggry Mwanri  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nape akihutubia  mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib akisalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wananchi wakiwa na ujumbe wao kwenye bango katika mkutano wa CCM uliofanyika Sumbawanga mjini mkoani Rukwa jana.
Wana-CCM wakiwa na bango la kumpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdylrahman Kinana, mpongeza Kinana katika mkutano uliofanyika jana Sumbawanga mjini mkoani Rukwa.Picha na Bashir Nkromo-idara ya itikadi na Uenezi-CCM

Wednesday, July 18, 2012

Daraja la Kaingesa Sumbawanga mkoani Rukwa

Daraja la Kaingesa likiwa kwenye hatua za kukamilika hapa Sumbawanga mkoani Rukwa,Daraja hili ni moja ya madaraja kadhaa yanayojengwa kwenye barabara kuu ya kutoka Tunduma kwenda Sumbawanga.

Sunday, July 15, 2012

Ziara ya Katibu wa Itikadi na Uenezi(CCM) Nape Nnauye na Viongozi Wa Serikali Walivyotua Mkoani Sumbawanga, Rukwa Kuimarisha Chama

Kiongozi wa Kikundi cha Chipukizi wa Manispaa ya Sumbawanga Samira Samir akimfunga skafu Katibu wa Itikadi na uenezi Taifa Ndugu Nape Nnauye. Nape atakuwepo Sumbawanga kwa siku mbili katika ziara ya kuimarisha Chama.
Bi Rahel Ndegeleke Katibu wa Mkoa wa Rukwa, Mwigulu Nchemba(Mb) katibu wa NEC Uchumi na Fedha (katikati) na Nape Nnauye Katibu wa NEC itikadi na Uenezi (kulia) mara baada ya kufika katika uwanja wa Ndege wa manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Waziri wa Maji na Mbunge wa Mwanga Mhe. Jumanne Maghembe akisalimiana na wakazi na viongozi wa Chama Mkoani Rukwa Ndugu Emanuel Seleman m-NEC (katikati) pamoja na Mzee Abdillah(wa kwanza kulia) waliokuja kuwapokea uwanja wa Ndege wa Sumbawanga mjini, Mhe. Maghembe ameongozana na Mhe Nape Katika Ziara yake hiyo.
Nape akisalimiana na wenyeji wa Sumbawanga waliojitokeza uwanja wa Ndege kumpokea. Katika Ziara yake hiyo Mheshimiwa Nape ameongozana na Viogozi wa Chama na Serikali akiwemo Mhe. Mwigulu Nchemba(katibu wa NEC- Uchumi na Fedha) Mhe. A. Mwanry (NW Tawala za Mikoa), Prof Jumanne Maghembe, Mb (Waziri wa Maji), Mhe. Benedictor Ole Nangoro Naibu Waziri wa Ujenzi., Dr Tizeba Charles (Mb,Nw Uchukuzi) Adam A. Malima(Naibu Waziri Kilimo)

UZINDUZI WA KITUO CHA UWEKEZAJI NA KITEGA UCHUMI CHA CCM, SUMBAWANGA MJINI.

Katibu wa itikadi na uenezi Taifa, Ndugu Nape Moses Nnauye akihutubia wananchi waliojitokeza katika Ufunguzi wa Kitega Uchumi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika manispaa ya Sumbawanga leo 14 july 2012. Kitega uchumi hiko kinajumuisha milango ya maduka 37 na kituo cha mafuta ''petrol station'' ambako kipo maeneo ya sabasaba katika manispaa hiyo, Nape atakuwepo Mkoani Rukwa kwa siku mbili kwa Ziara ya Kuimarisha Chama.

Katibu wa Halmshauri kuu (NEC) Ndugu Nape Nnauye akifungua kitega Uchumi Cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa.

Saturday, July 14, 2012

UJENZI WA BARABARA YA TUNDUMA MPAKA SUMBAWANGA WAENDELEA

Barabara ikiwa tayari imeshaanza kuwekewa lami
Daraja la MPUI
Daraja la LAELA
Vijana wakiwa kazini kurekebisha mifereji kwenye barabara hiyo mpya.Picha zote na Mdau Adam Mzee

Popular Posts