Pages

Showing posts with label Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Tanzania. Show all posts

Monday, September 3, 2012

TAMKO LA TEF KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI

TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF) KWA VYOBO VYA HABARI KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI

UTANGULIZI:

1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

2. Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

3. Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.

4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

5. Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.

6. Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.

MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF

Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:

1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.

2. Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.

3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.

4. Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.

5. Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.

7. Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.

8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.

9. Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.


IMETOLEWA NA:


NEVILLE MEENA,

KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)

SEPTEMBA 3, 2012

Wednesday, August 15, 2012

Tanzania Second EITI Reconciliation Report

Source: TEITI
Date: 2 May 2012

Download the second Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative reconciliation report (in PDF).

It covers the period 1 July 2009 to 30 June 2010 and was carried out from 6 October 2011 to 15 April 2012 by BDO East Africa, Tanzania in association with Paulsam Geo-Engineering Limited in accordance with terms of reference as established in the Request for Proposal referenced ME/008/TEITI/C/06.

Saturday, July 28, 2012

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUSUDIO LA WALIMU KUGOMA

SERIKALI kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo, Ijumaa, Julai 27, 2012 majira ya saa tisa alasiri, imepokea notisi ya saa arobaini na nane (48) ya kusudio la walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kugoma kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 saa moja na nusu asubuhi.

Kabla ya notisi hii kutolewa, Serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi za kujadiliana na viongozi wa CWT kuhusu jinsi ya kuboresha maslahi ya walimu kwa nia ya kumaliza suala hili kwa maelewano kwa kutumia vyombo na ngazi mbali mbali za kisheria.

Kwa sasa, shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku ya Ijumaa tarehe 27 Julai, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote mbili zilifika Mahakamani, na Mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne tarehe 31 Julai, 2012 saa sita mchana, ili kuiwezesha Mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi.

Kwa hiyo, Mgomo huu siyo halali kwa sababu shauri hili bado liko Mahakamani.

Kwa msingi huo hatua ya CWT kutoa notisi ya kuanza kwa mgomo kabla ya kukamilika kwa shauri hili ni kukiuka taratibu halali za Kimahakama ambazo kila mmoja anawajibika kuziheshimu.

Serikali inapenda kuwafahamisha walimu wote kuwa kujihusisha na mgomo huu ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi. Hivyo, walimu wanapaswa kupima madhara ya mgomo huu usiokuwa halali na Serikali inawataka walimu kupuuza mgomo huo na kutokujihusisha nao. Walimu wote wanatakiwa waendelee na kazi kama kawaida.


Peniel M. Lyimo
KAIMU KATIBU MKUU KIONGOZI

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
27 Julai, 2012

Friday, July 27, 2012

Emmanuel Shija Wa Tanzania Kupanda Ulingoni Agosti 19 Nchini Ugiriki

Bondia wa mchezo wa Kick Boxer Mtanzani, Emmanuel Shija (kushoto) akipozi kwa picha na mpinzani wake wakati wa utambulisho wa pambano lao linalotarajia kufanyika Agosti 9, mwaka huu mechi ya MMA UF3 ULTIMATE FIGHTING ndani ya Greece Thassalokia AHOY SUMMER NIGHT CLUB 19. 08.2012 LIVE ON INTERNET ww.XpowerSport.eu.
Shija akipozi na mpambe wake.
Shija (kushoto) akiwa na mabondia wenzake wanaoshiriki katika mapambano hayo yaliyodhaminiwa na Everlast.

Wednesday, July 25, 2012

Wildebeest Migration: Kenyans are big liars

PRESS RELEASE

Reference is made to Daily Nation of 23rd July, 2012 that is published in Kenya under the headline “Arson halts wildebeest migration”. It was published that migration to Kenya is being blocked following fire that was set by local communities that reside in the northern part of Serengeti Game Reserve (it is a National Park and not a game reserve). However, the Management for Tanzania National Parks (TANAPA) is hereby refuting the published allegations for the following facts:

Annual calendar of migration
Usually wildebeest and zebra do cover 1000 km in their course of migration throughout the year. These migratory animals do spend very little time in Masai Mara which is almost two months of a year and the rest ten months the wildebeest do spend their time in Serengeti as it can be observed on the below scientifically proven migration calendar. These animals are too many (1.5 millions) and therefore cannot stay in one area, they must move in search of new pasture and exchanging males to avoid inbreeding. As per the annual migration calendar, it suffices to state that is not yet time of main migration to be in Masai Mara, the right time is September and October. Currently the Main migration is still on movement from Western towards Northern part of Serengeti.

Early Burning
What was intended to be published is what is known scientifically as Early Burning. The General Management Plan of Serengeti National Park has in place a Fire Management Plan which allows the practice of early burning. This is type of fire which is set early while grasses are still green is known as ‘early burning’. The fire is practiced for several reasons which include reducing number of destructive insect e.g. tsetse fly; is set to reduce amount of litter that can catalyze fire during dry season; also early burning do facilitate new forage for animals as some seeds can only germinate after been burnt and also when old grasses are burnt new one do germinates. In line with this, early burning was practiced in some parts of Northern zone namely as Wogakuria towards Nyamalumbwa plains. These areas were selected following high number of tsetse fly and large amount of litter. This excursion is being undertaken every year and has never affected phenomena of migration.

To recap the above, Tanzania National Parks wish to inform the public that the Wildebeest Migration has not been affected as claimed and that the time for the migration to cross in to the other part of Masai Mara per the migration calendar will be in September or October. Also what is happening in the northern part of Serengeti is Early Burning which has taken place in an area of not more than 0.5 square kilometers and which actually has no impact at all in wildlife movement patterns which has been practiced for years without affecting the migration which we are sure our neighbors in the other part of Serengeti who are also conservationists are aware of this.

Pascal Shelutete
Public Relations Manager
TANZANIA NATIONAL PARKS
P.O.BOX 3134
ARUSHA

SERIKALI YA TANZANIA : HATUJADHULUMU MALIPO YA WAHANGA

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

SERIKALI imesema kuwa hakuna malipo ya kiasi kidogo cha fedha kilicholipwa kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu ya Kambi ya jeshi ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila wiki la hapa nchini hivi karibuni.

Akizungumza na Idara ya Habari( MAELEZO) jana ofisini kwake , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema hakuna fidia ya Shs. 1400 na Shs. 2500 iliyotolewa kuwa ni ya uharibifu wa jumla ya fidia za malipo kwa wahanga hao, bali malipo hayo ni tofauti ya kiasi cha fedha kilichokuwa kinadaiwa na wahanga hao ambacho kilichobakia.

‘’ Unajua malipo ya wahanga hao yalifanyika katika awamu mbili. Hivyo kiasi cha fedha cha malipo hayo yaliyotolewa katika hundi hizo , ambayo iliripotiwa katika gazeti hilo ni malipo ya awamu ya tatu. Malipo hayo ni tofauti ya fedha kilichokuwa kinadaiwa na si kweli kuwa wahanga hao walilipwa fedha hizo kama jumla ya fidia za malipo yao,’’ alifafanua Mkuu huyo wa Mkoa.

Mkuu huyo wa Mkoa, aliongeza kuwa habari hiyo iliyoandikwa sio sahihi na haikufuata maadili ya uandishi wa habari kwani hakuweka wazi usahihi wa taarifa hiyo.Serikali haijamdhulumu mtu yeyote, bali inalipa kutokana malipo stahili.

‘’Ninaomba waandishi wa habari waandike habari walizozifanyika utafiti wa kina wa pande zote ilikuepusha utoaji wa taarifa zisizosahihi,’’ alisisitiza.

Aidha Mkuu huyo alisema malipo ya waathirika hao yanatolewa kwa awamu tofauti na kwa idadi ya watu maalum, kwa sababu ya kuepusha utoaji wa malipo yasiyostahili. Hivyo aliwataka waathirika hao kuvuta subira kwa kuwa malipo hayo bado yanaendelea.

Naye Mtathimini Mkuu wa malipo hayo, Victor Ndonne akizungumzia kuhusu suala hilo alisema hundi za malipo ya sh. 1000 na zilizotajwa hapo juu ni za tofauti ya kiasi cha fedha kilichobakia baada ya wahanga hao kutoridhika na malipo hayo yaliyotolewa katika awamu ya kwanza na awamu ya pili.

‘’ Fedha hizi zimelipwa baada ya kufanyika kwa tathimini mpya Agosti 18 mwaka 2011, ambapo ilioneka baadhi ya wahanga hawakurithika na fidia walizolipwa,’’ alisema Ndonne .

Alifafanua kuwa orodha ya wahanga wanaodaii malipa yao ni 2,575, hivyo hundi zilizotolewa hadi sasa ni 295 kwa ajili ya malipo hayo, ambapo hundi 244 zimeshakabidhiwa kwa wananchi husika, hundi nyingine 18 majina yamebandikwa katika eneo la Mbagala Kuu na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke, zaidi ya wiki moja iliyopita na wanasubiri wananchi waende kuchukua.

Ndonne alisema hundi 32 zimeonekana kuwa na matatizo mbalimbali mfano majina ya vitambulisho vyao ni tofauti na yaliyoandikwa katika hundi na majina mengine ya hundi hizo wahusika wameshafariki dunia. Aidha aliongeza kuwa hundi moja imeonekana majina yamejirudia.

Alisema kuwa hundi za malipo ya fedha ya wahanga hao zilitolewa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha uliopita. Malipo ya fedha zingine zitatolewa mwaka huu wa fedha wa 2012/2013 mara baada ya Serikali kuidhinisha.

Saturday, July 14, 2012

Basketball Legend Tim Hickey Visits Tanzania


TBF Vice President Magesa left with Tim Hickey right , Basketball Legend who taught and coached many TZ basketballers in the sixties , he is in TZ to visit the schools he taught in Dar and Moro and meet some of his players in the 60's like Hamidu Alekwa, Jaji Ramadhani (former CJ), Henry Ramadhani (former Dirctor of Sports), Mustafa Nyanganyi (former Minister and Ambassador), John Zembetakis, Wakili Hamidu Abuzeleni, Saleh Zonga , Mohamed Majura just to mention a few.. there are many more.


He has coached many Athletes in TZ and US.. Last time he visited TZ was 1970.
All who remember him at schools and courts please come and meet him and from Tuesday he will be in Morogoro for 4 days and then Back to Dar for 4 more days before departing to US.

Call me to get his contacts.
Phares MagesaTBF - VP.
+255 784 618320+255 767 618320
+255 713 618320

Wednesday, July 11, 2012

VODACOM KUTOA TUZO KWA WAANDISHI MAHIRI KUMI WA MITANDAO YA JAMII NA TOVUTI TANZANIA

Waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na mafanikio yao. Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom”Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao.

Tuzo hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”, zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni kwa mala ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom.

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.

Wapo waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.

Baadhi ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii, Kuzingatia ueledi wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.

Waandishi wa mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.

Kampuni ya Vodacom Tanzania pia itaanzisha mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali, Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.

“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”, Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”

Sunday, July 8, 2012

Lives on Hold : AgriSol's Land Deal in Tanzania


image 20.png 2


Lives on Hold
AgriSol's Land Deal in Tanzania Creates an Uncertain Future for More than 160,000 People

A new report provides details from the ground as the investor faces the Iowa Ethics Commission


Oakland, CA - A new report by the Oakland Institute, Lives on Hold, exposes the consequences of Iowa-based AgriSol Energy LLC's plans to lease more than 800,000 acres in Tanzania. The project initiated in 2007-2008 has moved forward without public debate or consent, and will evict more than 160,000 long-term residents of Katumba and Mishamo, who remain in the dark over compensation and relocation plans. The AgriSol land deal is a part of Kilimo Kwanza, or Agriculture First, the Tanzanian government's scheme to promote agricultural development through public-private partnerships.

In June 2011, the Oakland Institute revealed how Iowa-based Bruce Rastetter, CEO of AgriSol Energy, leveraged the involvement of Iowa State University's College of Agriculture and Life Sciences to provide legitimacy to this deal. Initially masquerading the project as responsible agricultural investment, the university completely withdrew any support or association with it in February 2012 under growing public pressure. While AgriSol claims to have halted operations in Katumba and Mishamo until the refugees have been relocated, Lives on Hold depicts how the relocation is to be accomplished.

"Caught in the crossfire of this egregious land deal are more than 160,000 newly naturalized Tanzanians--former Burundian refugees who fled civil war more than 40 years ago. Initially promised citizenship, the residents still await their papers, conditional on them vacating their homes and lands in order to make way for the foreign investor. The residents have been banned from cultivating crops including perennial crops such as cassava or building new homes and businesses, leaving them with no other option but to consider moving. This is how the situation will be resolved for AgriSol," said Anuradha Mittal, Executive Director of the Oakland Institute and coauthor of the report.

A Katumba resident, a farmer and house builder, who's name has been withheld to ensure his safety told the research team: "I'm greatly disappointed by the decision that forbids us from making progress. Our livelihoods, activities have been stranded."

Lives on Hold documents how the residents of the Katumba settlement contribute to the economic and agricultural well-being of the region. While initially referred to as "abandoned refugee camps" by AgriSol, OI's field work depicts the Katumba settlement as a thriving community with well-established homes, farms, places of worship, and businesses. Yet the policy of Kilimo Kwanza is being misused to subject the villagers to human rights abuses, which range from the burning down of houses and crops and violation of their freedom of speech to inequities in social services.

Amid the announcement of relocation in a town hall-style meeting with the authorities in 2010, several villagers reported threats and arrests by the security forces for demanding fair compensation; the argument against their inquiry amounted to "Katumba is not your land for you to start asking questions." But residents of the settlement have called Katumba their home for the last 40 years.

"It is true that the Tanzanian government donated the land for the camp. But this is a case of good will gone wrong," said Mittal. There has been significant value added to the land by the refugees during the past 40 years. Currently, the compensation stands at $200 per person in a family. This paltry payment is for the land their livelihoods depend on, upon which their houses have been built, where the crops that feed them and the neighboring communities are grown, and where they have built churches and other community infrastructure.

Lives on Hold also reveals how AgriSol plans to develop large-scale monocrops, use high levels of chemicals, and even ask for changes in the national biosafety regulations so that genetically modified crops can be grown--all within a protected forest reserve and the Malagarasi-Moyowosi wetland system, one of the wetland sites protected by the international Ramsar Convention on Wetlands.

AgriSol's model of industrial agriculture poses a high risk to biodiversity, with the pollution of rivers and drying out of water sources being highly likely, which will affect the health of the people downstream and also wildlife in the area. The protected forest reserve and its biodiversity will be sacrificed for a large-scale plantation for exports. The Oakland Institute is asserting that the needs of the Burundian Tanzanians in Katumba must be met clearly, efficiently, and fairly while preserving one of the world's most important and fragile waterways and landscape.

Earlier this month, an Iowa-based group, Iowa Citizens for Community Improvement, filed an official conflict of interest complaint against Rastetter with the Iowa Ethics and Campaign Disclosure Board, and are lobbying for Bruce Rastetter to be removed as Iowa Board of Regents President Pro Tem.

The Oakland Institute first exposed AgriSol's land investment deal in June 2011. View the June 2011 report and related documents here.

The Oakland Institute is an independent policy think tank, bringing fresh ideas and bold action to the most pressing social, economic, and environmental issues of our time.

###
We need your help to prevent deals like this from ever being on the table.


That the AgriSol deal has gone sour is just one example of how research with a purpose can change the world. That's what we do at the Oakland Institute.

The Oakland Institute research has been critical in empowering local communities and decision makers in many countries so they can make informed choices about the investment they need to develop their agriculture and overcome hunger and poverty. By providing information and analysis, sponsoring radio programs in local languages, and hosting events on the ground around agricultural investments, the Institute is working to ensure people have a say in their own future. This work has already resulted in popular mobilization in countries such as South Sudan and Sierra Leone as well as increasing awareness for many decision makers across the world.

We are committed to a world free of hunger, which requires policies and investments that will benefit the people, not just a handful of businessmen, investors, and politicians. It is our mission to unearth and publish information that propels activism and builds change. To continue this work, we look to individuals and foundations that are committed to the same work and goals for support.

We hope that we can count on your continued support and ask you to make a generous gift to the Institute today so we can continue our shared work and build coalitions to make real change.


Thank you!




Become a Fan on Facebook: www.facebook.com/oak.institute

Follow us on Twitter: @oak_institute

To unsubscribe from this listserve, please send a message to info@oaklandinstitute.org

Wednesday, July 4, 2012

Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Mugosi Kabaka azungumza Umoja wa Mataifa

Mhe. Gaudentia Mugosi Kabaka ( MB) Waziri wa Kazi na Ajira akizungumza wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa unaojadilini pamoja na mambo mengine tatizo la ajira na hasa kwa vijana, Mhe. Kabaka anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huu wa wiki moja, ukiwashirikisha mawaziri wanaohusika na masuala ya ajira, fedha na uchumi, mambo ya nje , ILO na wanazuoni. katika mchango wake kuhusu changamoto hiyo ya ukosefu wa ajira, Mhe. Waziri Gaudentia Kabaka anasema kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazoendelea. Tanzania pia inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira na kwamba serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kujaribu kulikabili tatizo hilo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa mataifa tajiri na maskini pia na ni bomu ambalo limeshaanza kufuka moshi.
Baadhi ya ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu unaojadili tatizo la ajira, ni mkutano ambao umeandaliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii maarufu kama ECOSOC. Walio kaa mbele ni Kamishna. Ahmed Makame Haji, kutoka Tume ya Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Omar Hamisi Same kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Bi. Aziza J. Ali, Mkuu wa kitengo kinachoratibu misaada, Idara ya Fedha za Nje, Serikali ya Mapinduzi Zanziba na Bw. Humphrey Shangarai, mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
--
Na Mwandish Maalum
Wakati Jumuia ya kimataifa ikiendelea kukuna vichwa kutafuta mbinu na mikakati ya kukabiliana na hatari inayotokana na ongekezo kubwa la ukosefu wa ajira na hususani kwa Vijana. Tanzania inasema kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo imeanza kuandaa mikakati endelevu ya kulikabili janga hilo.
Akizungunza katika siku ya pili ya mkutano unaowakutanisha kwa pamoja mawaziri wanaohusika na masuala ya ajira, wataalamu wa masuala ya fedha , uchumi na wanazuoni. Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudentia Mugosi Kabaka ( Mb) anasema Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazoendelea inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira.
Mhe. Waziri Kabaka anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa wiki moja unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Mkutano huo ambao umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon mwanzoni mwa wiki, umeandaliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii (ECOSOC).
“Kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazo endelea duniani, nchi yangu pia inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira na hasa kwa vijana. Na tatizo hili linasababishwa kwa kiasi kubwa na uboreshaji wa elimu yetu hadi ngazi ya elimu ya juu, uboreshani na upanuzi ambazo hauendani sambamba na ongezeko la ajira”.
Amewaeleza wajumbe wamkutano huo kwamba, tatizo la ajira pia lipo zaidi kwa upande wa mijini na hii ni kutoka na wimbi la vijana kuhamia mijini.
“ licha ya kwamba vijana wengi wanahamia mijini na hivyo kuchangia katika ukosefu wa ajira, lakini pia hivi sasa tunashuhudia vijana wale wa vijijini kukoa ajira kutokana na athali za mabadiliko ya tabia nchi , mabadiliko ambayo yamekuwa na athari kubwa kwa upande wa kilimo” akabainisha Kabaka.
Akaitaja baadhi ya mikakati inayofanywa na serikali ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana, kuwa ni pamoja na mpango wa kurasimisha mali za wanyonge ( Mkurabita) ili mali hizo ziweze kutumika kupata mikopo, upanuzi vya vyuo vya ufundi stadi ili vijana waweze kujiajiri wenyewe, na kuanzishwa pamona na mambo mengine sheria ya hifadhi ya jamii, mifuko ya jamii, mifuko ya bima ya afya, na vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa ( SACCOS)
Aidha akasema, serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ziwamo taasisi za kitaifa na kimataifa, imekuwa ikiratibu mafunzo mbalimbali yakiwamo ya uwezeshaji katika eneo la kilimo ili vijana wawe kujiajiri katika eneo hilo na kwamba mipango yote inalenga katika kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya millennia.
Aidha akasema, Tanzania pia inaendelea na jukumu la kuhakikisha kwamba ajira kwa watoto inakomeshwa, kuwapo kwa ajira zenye tija, endelevu na zenye hadhi na kwa sababu hiyo akauomba Umoja wa Mataifa kupitia ECOSOC, kuisaidia Tanzania katika eneo la teknolojia.
Mada kuu ya mkutano huu ni kukuza uwezo wa uzalishaji wa ajira kwa vijana, na kazi zenye heshima kwa lengo la kuondokana na umaskini na kukuza uchumi endelevu ili kufikira utekelezaji wa MDGs.
Mkutano huo unatoa fursa kwa nchi wanachama wa UMum kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ambayo ni changamoto kubwa kwa usalama wa dunia. Na hususani wimbi hilo la ukosefu wa ajira kwa vijana, wimbi ambalo limesha onesha kwamba lisipotafutiwa mikakati ya kudumu ni bomu ambalo tayari limeshaanza kufuka moshi.

Sunday, July 1, 2012

HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 30 JUNI, 2012

Ndugu Wananchi,

Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari.

Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini

Ndugu Wananchi;
Bila ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43 za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012. Pamoja na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi. Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma. Maiti 22 zilipelekwa Dodoma na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa wale walionusurika zimebainisha kuwa watu hao ni raia wa Ethiopia ambao walikuwa safarini kwenda Malawi na baadaye Afrika ya Kusini ambako wangetengenezewa utaratibu wa kwenda kuishi Marekani na Ulaya. Kwa mujibu wa maelezo yao, safari yao ilianza miezi mitano iliyopita. Mwezi mmoja waliutumia Ethiopia na miezi minne waliitumia Kenya kabla ya kuletwa Arusha ambako walipakiwa kwenye lori na kuanza safari ya kuelekea Malawi lakini ikaishia Chitego. Lori walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha vifo kwa kukosa hewa.

Tukio la Chitego, Dodoma la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea hapa nchini. Kwa jumla, katika kipindi cha takriban miaka 10 sasa kumekuwepo na tatizo kubwa la wahamiaji haramu kuingia nchini. Kwa mfano, kati ya mwaka 2005 na hivi sasa jumla ya wahamiaji haramu 19,683 wamekamatwa. Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu watu 1,500 tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa makwao. Wengi wa watu hao wanatoka Ethiopia na Somalia na baadhi kutoka Pakistan na Bangladesh.

Wahamiaji haramu wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi. Wapo wanaotumia nchi kavu hasa kupitia mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Na, wapo wanaopitia baharini kwa kutumia fukwe za Pemba, Unguja na za mikoa ya ukanda wa Pwani ya Tanzania Bara yaani Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.

Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa kauli zao, watu hao wamekuwa wanaeleza kuwa hawaji nchini kuhamia bali wao ni wapita njia tu. Wanaelekea Afrika ya Kusini ambako wameahidiwa kuwa watatengenezewa mipango ya kuhamia Marekani na Ulaya. Watu hao pia wamethibitisha kuwepo kwa watu maalum wanaojihusisha na usafiri wao tangu nchi watokako na zote wanazopitia mpaka kule waendako. Aidha, wamesema kuwa wao wanawalipa watu hao ili wawasafirishe na hakika si kiwango kidogo. Kwa jumla ni kwamba hili si suala la uhamiaji haramu bali ni la biashara haramu ya kusafirisha binadamu.

Ndugu Wananchi;
Kufuatia vyombo vyetu vya usalama kuwa makini na watu wengi kukamatwa ndipo wasafirishaji walipobuni njia za kuwasafirisha kama mizigo. Makontena, malori yaliyofunikwa nyuma na matenki ya mafuta na ya maji yamekuwa yanatumika kwa ajili hiyo. Usafiri wa aina hiyo ndiyo uliosababisha vifo vilivyotokea Dodoma tarehe 26 Juni, 2012 na vya watu 21 vilivyotokea mwezi Desemba, 2011 Mkoani Morogoro, na vile vya watu 12 vilivyotokea katika matukio mawili ya Mkoa wa Mbeya, mwezi Mei, 2012.

Ndugu Wananchi;
Tarehe 27 Juni, 2012 nilikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzungumzia tukio la Chitego na suala zima la biashara hii haramu na hasa mbinu mpya inayotumiwa na wasafarishaji. Nilitoa pongezi kwa vyombo vya dola kwa kazi nzuri waifanyayo kudhibiti shughuli za biashara hii haramu hapa nchini. Tulielewana kuwa waendelee kuimarisha udhibiti huo kwa lengo la kukomesha kabisa biashara hii.

Niliagiza pia kwamba kikundi kazi nilichokiunda mwaka 2006 kushughulikia ujambazi sasa kielekeze sehemu ya nguvu zake kukabili tatizo hili. Aidha, kwa pamoja tulikubaliana kuwa nchi yetu ishirikiane na wenzetu wa Ethiopia, Kenya, Malawi, Msumbiji na Afrika ya Kusini kutambua mawakala na kuwabana kwa mujibu wa sheria. Tayari nimeshaanza kufanya mawasiliano na baadhi ya Wakuu wa Nchi hizo kuhusu ushirikiano huo. Nashukuru wote wameafiki nchi zetu zishirikiane kwa pamoja kuvunja mtandao huu mchafu na kutokomeza biashara hii haramu na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.

Ndugu Wananchi;
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wenzetu, wakazi wa vijiji vya Chitego na Mkoka kwa kazi nzuri walioifanya. Kwa kweli, wenzetu wameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutoa taarifa mapema juu ya jambo lenyewe, lakini pia wameonesha utu kwa kuwajali wageni waliokumbwa na janga hili. Naushukuru pia uongozi wa Mkoa wa Dodoma na Morogoro ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulishughulikia tatizo hilo kwa umakini mkubwa. Nimefurahishwa sana na ushirikiano ulioonyeshwa na vyombo na taasisi mbalimbali za Serikali katika kushughulikia suala hili.

Mgomo wa Madaktari
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ni kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa. Nilipozungumza na Wazee wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 12 Machi, 2012, kuhusu mgomo wa Madaktari uliokuwa unaendelea wakati ule pamoja na kuelezea chimbuko la mgomo na hatua iliyokuwa imefikiwa, nilielezea mazungumzo yangu na viongozi wa Chama cha Madakari wakiwemo pia viongozi wa Jumuiya ya Madaktari. Nilitoa taarifa kuwa tumeelewana kuwa watasitisha mgomo na watarudi kwenye meza ya majadiliano na Serikali. Siku ile pia nilielezea matumaini yangu kuwa mgomo ule utakuwa wa mwisho katika nchi yetu. Bahati mbaya matumaini yangu hayo hayakuwa na hivi sasa tunashuhudia tena wagonjwa wakiteseka, kuhangaika na wengine kufa kwa sababu ya kukosa huduma wanazostahili kwa vile madaktari wao wamegoma tena.

Ndugu Wananchi;
Kama walivyoniahidi, madaktari waliacha kugoma na viongozi wao walirudi kwenye mazungumzo na Serikali. Kama ilivyoagizwa na Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi tarehe 8 Machi, 2012, kwa mujibu wa Sheria ya Mahusiano Kazini, Namba 6 ya mwaka 2004. Chama cha Madaktari na Serikali walifika katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Commission for Mediation and Arbitration) kwa ajili ya majadiliano. Kwa pamoja na kwa ridhaa yao wote, pande hizo mbili ziliiomba Tume hiyo iwape fursa ya kuzungumza wao wenyewe na wakimaliza mazungumzo wataenda kusajili makubaliano yao. Tume ikawakubalia. Ni vizuri ikakumbukwa kuwa siku ile ya tarehe 8 Machi, 2012 Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ilitoa zuio la mgomo pamoja na kuagiza kuwepo mazungumzo baina ya pande mbili.

Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari. Katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari yalizungumzwa. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

1.Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
2.Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3.Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4.Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
5.Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6.Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
7.Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
8.Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9.Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje.
10.Madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini.
11.Huduma za afya ziboreshwe nchini.
12.Posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.

Ndugu Wananchi;
Katika mambo hayo 12 pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba. La kwanza, ni kuhusu usafiri wa kwenda na kurudi kazini. Serikali ilieleza kuwa upo utaratibu kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 3 wa mwaka 2011 wa kuwakopesha wafanyakazi wa Serikali fedha za kununulia magari au pikipiki, samani na matengenezo ya magari. Ilikubaliwa kuwa madaktari waitumie fursa hiyo.
Jambo la pili, ni kuhusu madaktari kupatiwa Green Card za Bima ya Afya. Jambo hili lilikubaliwa na Serikali na Wizara ya Afya imekwishachukua hatua za utekelezaji wake.

Jambo la tatu, ni kuhusu hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya. Kwa pamoja walikubaliana kuwa suala hilo liko nje ya mamlaka ya Kamati yao ya pamoja, waziachie mamlaka husika za uteuzi. Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya. Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona. Kwanza walisema hawaoni sababu kwa vile wameyazungumza na Kamati yake kwa miezi mitatu bila ya mafanikio
Jambo la nne walilokubaliana ni kuhusu viongozi kulazimisha kupewa rufaa ya kutibiwa nje. Walikubaliana mambo mawili. Kwanza, kwamba maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa madaktari wazingatie maadili ya kazi zao na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili awe kiongozi au asiwe kiongozi. Pili, walikubaliana kuwa hospitali zilizopo ziboreshwe ili viongozi watibiwe hapa nchini. Ukweli ni kwamba kufanya hivyo ndiyo sera ya Serikali. Nililieleza hili mwezi Desemba 30, 2005 katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza nchi yetu.

Tumeiongeza sana bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka 2011/12 na imekuwa ya tatu baada ya miundombinu na elimu. Tumeziimarisha hospitali za Mikoa kwa vifaa tiba na wataalamu wa afya. Kazi inaendelea katika hospitali za Wilaya. Tumewekeza katika Hospitali ya Muhimbili. Hospitali hiyo ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka sita nyuma. Na kazi inaendelea hasa katika maeneo ambayo tunapeleka wagonjwa nje. Matunda yake yanaanza kuonekana kwa upande wa figo, moyo, kinywa na mipango inaendelea kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu. Tunaendelea kuimarisha mafunzo ya madaktari na madaktari bingwa, yote kwa nia hiyo hiyo. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba,Muhimbili kinachukua wanafunzi wengi zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma na makazi mapya ya chuo yanaendelea kuandaliwa ili kuchukua wanafunzi wengi zaid. Mwaka 2005 tulikuwa na madaktari bingwa 46 mwaka huu tunao 520.

Ndugu Wananchi;
Jambo la tano ambalo pande zote mbili zilikubaliana ni kuhusu madaktari waliofukuzwa. Hawa ni wale Interns waliokuwa wamerudishwa Wizarani kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Lugalo. Hili ni jambo ambalo lilikuwa limemalizika kitambo na wote walikuwa wamerudi Muhimbili.

Jambo la sita ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya afya. Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini sera na mpango wa afya ya msingi, bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha viwango vya ubora wa madaktari na kadhalika. Serikali imeyaafiki mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.

Jambo la saba, ambalo pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti. Hili ni jambo jipya halikuwepo mwazoni. Hata hivyo, Serikali imelikubali na posho hiyo imeongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi kufikia shilingi 100,000/= kwa daktari na shilingi 50,000/= kwa wasaidizi wake.

Ndugu Wananchi;
Kuna masuala matatu ambayo yamekuwa na muafaka kwa kiasi fulani na kutoafikiana kwa baadhi ya mambo. La kwanza ni suala la kufanya kazi katika mazingira hatarishi. Serikali imekubali hoja ya kuchukua hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi. Serikali iliwaeleza kuwa watumishi wa kada zote za afya watapatiwa chanjo dhidi ya maambukizi ya Hepatitis B na fedha zimetengwa katika bajeti ya 2012/13.

Aidha, Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili. Utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike. Madaktari wamekataa hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja.

Jambo la pili ambalo wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi. Serikali imekiri wajibu wake wa kuwapatia madakari nyumba za kuishi. Aidha, imeeleza mpango ulioanza wa kujenga nyumba 700 za madaktari kote nchini na kwamba hivi sasa ujenzi wa nyumba 90 unaendelea, 50 katika mkoa wa Mtwara na 40 katika mkoa wa Rukwa.

Kwa maeneo ambayo madaktari wanalipwa posho ya pango Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba. Jambo hilo limekataliwa na Madakari na kutaka lazima walipwe asilimia 30 ya mshahara kama posho ya nyumba. Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na kuwasihi wakubali wanayotendewa wafanyakazi wengine wote wa umma.

Jambo lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu. Pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao. Serikali imekubali wajibu wa kuweka utaratibu wa kuboresha maisha ya watumishi katika maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, Serikali itatoa mwongozo kwa mamlaka za ajira kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi hao kupunguza makali ya maisha katika kila eneo badala ya kutegemea posho peke yake.

Kuhusu posho, Serikali imeeleza kuafiki kuwepo posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya uchambuzi wa kuainisha mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama zake.

Madaktari hawajakubali kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali ilipe posho hiyo sasa. Tofauti hapa si posho hiyo kuwepo, bali ni rai ya Serikali ya kubaini maeneo yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya posho kulingana na mazingira halisi ya maeneo. Madaktari hawaoni haja ya kufanya hayo.

Ndugu Wananchi;
Mambo mawili hayakuwa na muafaka kabisa kati ya pande zetu mbili. Jambo la kwanza ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance). Kwanza sina budi kueleza kuwa Serikali imekubali kuongeza posho hiyo. Tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi shilingi 25,000/= kwa daktari bingwa (Specialist), shilingi 20,000/= kwa dakari mwenye usajili wa kudumu (Registrars) na shilingi 15,000/= kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo kazini (Interns). Viwango hivyo vya posho vinatumika hivi sasa.

Madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara. Ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa kazini. Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa. Hili haliwezi kuwa sahihi kufanya. Linaweza kuwafanya baadhi ya madaktari kutokutimiza wajibu wao kwa vile wana hakika mwisho wa mwezi malipo yako pale pale.

Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ambalo muafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari. Madaktari wanataka uwe shilingi 3,500,000/= wakati Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi. Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha. Kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi 1,100,000/= na 1,200,000/= kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa. Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000/=.

Ndugu Wananchi;
Huo ndiyo mlolongo wa mambo yaliyozungumzwa na pande zote mbili na matokeo ya mazungumzo yenyewe. Katika kikao cha sita kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2012, upande wa Chama cha Madaktari ulisema kuwa kwa vile hoja ya nyongeza ya mshahara haina mabadiliko hawakuona haja ya kuendelea na majadiliano mpaka watakapowasiliana na wenzao. Waliahidi kutoa taarifa ndani ya wiki mbili. Tarehe 12 Juni, 2012, Rais wa MAT aliandika barua kwa Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano kwa upande wa Serikali, kuwa Madaktari wameikataa taarifa na ufafanuzi waliopewa kutoka Serikalini kwa ujumla wake.

Ndugu Wananchi;
Baada ya majibu yale ya madaktari, tarehe 19 Juni, 2012, Serikali na Madaktari walikwenda kwa Msuluhishi (CMA) kutoa taarifa kuwa mgogoro umekosa usuluhishi kama sheria inavyotaka. Kwa pamoja pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lifikishwe Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Wakati pande zote zinasuburi mgogoro huu kufikishwa ngazi hiyo ya juu, upande wa Madaktari ukatangaza kuwepo kwa mgomo kuanzia saa sita ya usiku tarehe 23 Juni, 2012. Hatua hiyo haikustahili kwani suala lenyewe halijafika mwisho wa kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za Mahusiano ya Kazi nchini.

Ndugu Wananchi;
Tarehe 22 Juni, 2012, Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaenda Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kulifikisha suala la tishio la mgomo na kuomba zuio la muda kufanywa. Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuagiza kuwa mgomo usitishwe. Juhudi za kumtafuta Rais wa MAT, Dkt. Namala Mkopi na viongozi wengine wa MAT hazikufanikiwa, Ofisi ya MAT ilikuwa imefungwa na simu zote za viongozi wa MAT zilikuwa zimezimwa. Hatimaye tarehe 25 Juni, 2012, alipatikana na kupewa amri hiyo ya Mahakama. Tarehe 26 Juni, 2012, Dkt. Mkopi alifika Mahakamani ambapo alikana kuwa yeye hahusiki na kuitisha huo mgomo lakini hakumtaja aliyehusika. Pamoja na rai hiyo, Jaji alimuamuru Rais wa MAT akawatangazie wanachama wake kusitisha mgomo. Dkt. Namala Mkopi hajafanya hivyo hadi leo na mgomo umekuwa unaendelea kinyume cha Sheria.

Ndugu Wananchi;
Wagonjwa wanateseka na wengine kupoteza maisha kwa mgomo huu usiokuwa halali kisheria ambao pia haustahili kuwepo hata kwa mujibu wa maadili ya udaktari. Viongozi wa MAT na wenzao wanawaingiza Madaktari katika mgogoro na Mahakama na waajiri wao isivyostahili. Ni vyema viongozi wa Madaktari na madaktari wakatambua kuwa wanashiriki katika mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana Mahakamani kuwa hahusiki nao. Madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao wanaziweka hatarini. Mfanyakazi ana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa kushiriki mgomo unaokubalika kisheria. Huu siyo. Watapoteza ajira, hawana pa kukimbilia, hawana cha kiwalinda. Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali. Lazima watafakari sana kwa hayo wafanyayo.

Ndugu Wananchi;
Napenda kurudia maneno niliyoyasema tarehe 12 Machi, 2012, kuwa kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi ni Sera ya Serikali yetu kwa maelekezo ya Ilani ya Chama Tawala (CCM). Tumeitekeleza kwa vitendo sera hiyo, hata hivyo ni ukweli ulio wazi kuwa nia yangu njema tu pekee haitoshi, lazima uwezo wa kufanya hivyo uwepo. Kwa kulingana na uwezo uliopo, tumeendelea kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi hatua kwa hatua tangu tuingie madarakani. Tumefanya hivyo kwa jumla kwa wafanyakazi wote na kwa kada mbalimbali za watumishi wa umma.

Miongoni mwa wafanyakazi wa umma walionufaika na hatua hizo za Serikali ni madaktari na watumishi wa kada nyingine za huduma ya afya. Tena nadiriki kusema madaktari tumewapa upendeleo mkubwa kuliko watumishi wengine wa umma. Upendeleo upo kwenye mafunzo ambapo wanafunzi wa udaktari wanagharimiwa na Serikali kwa asilimia mia moja wakati wanafunzi wenzao wa taaluma nyingine hawako hivyo.

Ndugu Wananchi;
Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=, mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa sasa. Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100/=.

Tunafanya hivyo kwa kutambua na kuthamini nafasi maalum ya madaktari katika jamii na ukweli kwamba bado tunayo safari ndefu ya kuziba pengo la madaktari nchini. Lakini inaonekana juhudi zetu zote hizo hazithaminiwi.

Ndugu Wananchi;
Sina budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa. Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile.
Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.
Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.

Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.

Ndugu Wananchi;
Napenda kuwathibitishia kwamba dhamira ya Serikali ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo madaktari iko wazi. Tumekuwa tunafanya hivyo, na tutaendelea kufanya hivyo kulingana na uwezo wa kibajeti. Ni vyema watumishi wa umma wakatambua kuwa hatuwezi kutumia fedha zote au kiasi kikubwa mno cha pesa za umma kulipana mishahara. Tukifanya hivyo, Serikali itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ambao ndiyo wengi na wanastahili kuhudumiwa. Hata hizo huduma za afya tunazosema ni duni tuziboreshe, hatutaweza kuziboresha kama tutatumia sehemu kubwa ya pesa za Serikali kuwalipa mishahara wafanyakazi.

Hivi sasa matumizi ya mishahara ni asilimia 48 ya bajeti ya Serikali. Kiwango hicho ni kikubwa mno. Uwiano mzuri ni kuwa na matumizi ya mishahara yasiyozidi asilimia 35 ya bajeti na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa. Sisi tumezidi kwa asilimia 13. Hivyo, hatuna budi tukubali kujinyima kwa manufaa ya walio wengi.

Suala la Dkt. Steven Ulimboka

Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.

Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.

Ndugu Wananchi;
Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana. Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana. Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa. Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.

Ndugu Wananchi;
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.

Naomba kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini. Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.


Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.

Friday, June 29, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MAMA MZAZI WA WAZIRI STEPHEN WASSIRA

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mama wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira (kushoto) , Marehemu Esther Mgaya Mankaba, leo nyumbani kwa Mhe Wassira jijini Dar es salaam leo Juni 29, 2012. Baada ya heshima za mwisho mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea wilayani Bunda kw mazishi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Waqrioba, Waziri wa Kazi na Ajira Mhe Gaudencia Kabaka, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, na wanafamilia wa wafiwa wakitoa heshima za mwisho kwa mama wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira (kushoto) , Marehemu Esther Mgaya Mankaba, leo nyumbani kwa Mhe Wassira jijini Dar es salaam leo Juni 29, 2012. Baada ya heshima za mwisho mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea wilayani Bunda kw mazishi.Picha na IKULU

Wednesday, June 27, 2012

Picha za Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Steven Ulimboka Steven Baada ya Kuokotwa Maeneo ya Mabwepande

Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa
Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu Dk Hellen Kejo(kushot)akiwa na Dr. Steven Ulimboka muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi
Dr. Steven Ulimboka alipokua akieleza jambo kwenye mkutano wao(madaktari na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Hivi Karibuni
....
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.
---
UPDATE:

Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------

Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.

Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.

Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.

Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.

SHEREHE ZA MIAKA 35 ZA UHURU WA DJIBOUTI


Pichani juu na chini ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akiongea machache kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 35,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo mabalozi kutoka sehemu mbalimbali,hafla hiyo imefanyika jioni ya jana nyumbani kwa balozi huyo,jijini Dar.
Sehemu ya baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba fupi iliyokuwa ikitolewa na Balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo,kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 35 ya jamhuri ya Djibout iliyofanyika jioni ya jana jijini Dar.
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo,Pichani kati ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo,wakisherehekea hafla fupi ya kutimiza miaka 35 ya jamhuri ya Djibout iliyofanyika jioni ya jana jijini Dar.
Burudani kama hivi ilikuwepo kwa wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo.
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akimpokea mgeni rasmi wa hafla hiyo,Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi alipokuwa akiwasili nyumbani kwa balozi huyo.
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo akimkaribisha Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons) mara alipokuwa akiwasili kwenye hafla hiyo.
Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons) akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi jioni ya jana kwenye viunga vya balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akizungumza machache na machache na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi ,shoto ni Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons)
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo sambamba na Mkewe Mariam Shamo wakiwa na mmoja wa wageni wao,Mwamvita Makamba kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
Balozi Shamo na Mkewe wakiwa na wageni wao waalikwa waliofika kujumuika nao kwenye hafla hiyo.
Mke wa Balozi,Mariam Shamo (wa nne shoto) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwa na Mkewe Juhayna Kusaga wakifurahia jambo kwenye hafla hiyo
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi akizungumza jambo na Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons).
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi akizungumza machache kuhusiana na hafla hiyo kwa baadhi ya wanahabari waliohudhuria ,shoto ni Sir Andy Chande.

Popular Posts