Pages

Showing posts with label Mara. Show all posts
Showing posts with label Mara. Show all posts

Friday, August 3, 2012

MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) TAIFA- SANGOGUNGU KASERA

PRESS STATEMENT

HOTUBAYA MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) TAIFA- SANGOGUNGU KASERA

2August 20112

Ndg:Wanahabari
Ndg: wanaUVCCM wenzangu

Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kutoa salamu zangu za dhati kwa Watanzania na vijana wenzangu wanchi hii pamoja nanyi waandishi wa Habari kwa kushiriki nami katika safari hiiinayolenga kuunganisha na kujenga hatua za mabadiliko ya maisha ya Vijana waTanzania. Kwa namna ya pekee kabisa niwashukuru na kuwaomba mshikamano vijanawenzangu wa Chama cha Mapinduzi ambao kupitia kwao ninatumia nafasi hii kuomba ridhaa yao ili nipate nafasi ya kuwa chemchem ya mafanikio na mabadiliko katika maisha yetu kwa kuanzia na chama chetu. Leo hii naungana na vijana wenzangu hawa wa ndani ya CCM, kufanya jambo moja kubwa, jambo la kuchukua fomuya kuwania moja ya nafasi kubwa katika jumuiya ya Vijana wa CCM Tanzania. Ninafanya kazi hii leo nikitambua mambo yafuatayo:

Kwanza, ninalenga kuleta mabadiliko yanayotazama aina ya vijana tuliopo sasa, aina ya maisha tunayoishi na aina ya changanoto zinazotukabili mimi nikiwa mmojawapo.

Pili kwa upekee mkubwa, nachukua fomu hii nikibaini hali ya vijana huko tulikotoka na , changamoto tulizopitia na hatari inayotukabili mbele kama hatua stahiki hazitaanza kuchukuliwa na vijana wa aina yangu ambao tuna uzoefu wa kutosha wa maisha ya kawaida ambayo yanahitaji nguvu na akili zetu na za wenzetu waliotutangulia katika kuboresha maisha yetu ili tuweze kuwa raia wema katika nchi yetu na wanachama waadilifu wa chama chetu na jumuiya zake.

Ndugu Waandishi wa Habari;

Kazi hii ya kuchukua fomu ninayoifanya leo hii na kisha kuanza zoezi la kutafuta kuungwa mkono. Ni kazi inayohitaji ushirikiano mkubwa kwa uongozi wa Jumuiya yetu pamoja na vijana mbalimbali bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa. Nasema hivi kwa kutambua kuwa UVCCM ndiyo Jumuiya pekee yenye kubeba taswira na matarajio ya vijana wa Tanzania na ambayo siku zote inatakiwa kusimamia maslahi na matakwa ya vijana wa Tanzania na kwakuwa jumuhia hii ni jumuhia ya chama kinachoongoza si chama tawala .

Ndugu zangu wanahabari na wana CCM tunafahamu tofauti kati ya kuongoza na kutawala ndio maana nimetumia neno kuongoza, na Kama kazi hii ilikuwa haifanyiki huko nyuma na kama ilifanyika bila kuridhisha, mimi nimeamua kwa moyo mkunjufu kuingia kuonesha namna jumuiya yetu itakavyoweza kuwatumikia vijana wa Tanzaniana kukiboresha chama cha Mapinduzi ili kitambue wajibu wake kwa vijana wote waTanzania na kwa kufanya hivi kiweze kusimamia misingi iliyolijenga Taifa hili na kuachwa na waasisi wa Taifa letu Hayati Baba Wa Taifa na Hayati Rais Karume ambao walilijenga taifa letu katika misingi ya haki, usawa na ustahimilivu.

Ndugu wana habari; Katika kipindi hiki chakutafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi hii nitabakia kuongozwa na Moto isemayo: Vijana kwanza kwa taifa lenye amani na maendeleo. Bila vijana kuangaliwa na kupewa yale wanayostahiki, ni wazi taifa lenye amani na maendeleo halitakuwepo. Natambua fika kuwa vijana wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa ile inayolenga kubaini ndoto ya maisha yao ya sasa na siku zijazo. Naamini mimi ni mmoja wa vijana hawa ambaye pia ninahitaji kuona vijana walio katika kilimo basi wanaweza kupata soko la mazao yao. Vijanawabeba mikokoteni nao wanafanya kazi hiyo kwa miaka kadhaa na kisha kuboreshaajira zao.

Vijana wanaosoma basi wanahitimu vema na kupata ajira wanazostahiki na pia walio makazini na waliopata nafasi za kuongoza wanaonesha mfano wakufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii ili kuonesha kuwa vijana tunaweza na hatuwezi kuliangusha taifa. Natambua haya ninayoyazungumza ni mambo magumu lakini pia natambua yanahitaji mbinu nyingi ili kukabiliana nayo. Kwa sasa natumia nafasi hii kukiomba Chama changu, kuiomba Jumuiya Yetu ya Vijana kutambua kuwa nina dhamira, nina nia, nina sifa za kutosha, nina uwezo wa kufanya majukumu haya ninayoyaomba na ninafahamu kazi za majukumu haya.

Tena nina rekodi katika umri wangu huu wa kufanya mambo ya kutukuka ambayo rekodi yake inaweza kutazamwa pote nilipobahatika kutoa utumishi wangu. Kwa namna isiyoonyesha kuyumba naomba kuwaeleza vijana wenzangu kuwa kutokanana mshikamano wa vijana wenzangu kwangu ni wazi tumejiandaa kushinda katika nafasi hii ili tuweze kuleta mwanga wa mabadiliko katika jumuiya yetu na chama chetu katika maandalizi ya chaguzi zijazo. Ndugu wanahabari ninatambua zipo changamoto nyingi zinazoikabili UVCCM na changamoto hizi zinahitaji kiongozi ambaye atakuwa na uthubutu wakuweza kukabiliana nazo, changamoto kuuni kitaswira, kimuundo, kiimani, kimadhumuni kama ambavyo zimehainishwa kwenyekanuni za ummoja wa vijana. Nina maanisha nini ninapozungumzia taswira ya UVCCM.Taswira ya UVCCM Taifa leo siotaswira ya kimapambano.

Historia yetu ipo wazi jumuiya ya vijana ilishiriki katika mapambano ya kuleta Uhuru, Umoja na mshikamano mtakumbuka wakati TANU Inahangaika na kutafuta Uhuru wa Tanganyika na Afro-Shirazi party ikipambana kuleta Uhuru wa Zanzibar vijana waliunganishwa na jumuiya za umoja wa vijana wa vyama hivi viwili ambavyo ni TANU YOUTH LEAGUE na ASP YOUTH LEAGUE, zinafahamika kazi zilizofanywa na wabeba mizigo wa Kariakoo mfano Mzee Rajabu Diwani, leo UVCCM sio tena yawabeba mizigo, sio tena ya wamachingasio tena ya wakulima ,sio tena jumuiya ya wafanyakazi ni jumuiya ya wafanyabiashara, watoto wa vigogo ama wenyenasaba nao ama rafiki zao, inahitaji viongozi wenye dhamira ya dhati ambao watarudisha jumuiya hii kwa vijana wakitanzania na kurudisha taswira ya kimapambano ambayo ni mapambano ya kiuchumi, kazi ya Uhuru imeshafanyika imebakia jukumu la kuleta Uhuru wa kiuchumi na kuwa kimbilio la vijana wote.

Ni dhamirayangu ya kugombea nafasi hii ni kuhakikisha awamu ya pili ya mapambano ya kiuchumi ya umoja wa vijana inaanza rasmi. Nafahamu zipo changamoto za kiutawala, kiuchumi na jumuiya kuendelea kuishi kwa kutegemea misaada na Ruzuku kutoka kwenye chama, nafahamu watendajiwana hali mbaya kiuchumi hasa katika mawilaya, nafahamu ofisi zetu za wilaya zina upungufu wa vitendea kazi ni dhamira yangu kubadili mwelekeo wa utendajiwa jumuiya yetu kutoka “Business as usual” kuvalisha skafu viongozi na kuimba nyimbo, kuwa jumuiya yenye dira namwelekeo sahihi wa kuwaunganisha na kumkomboa kijana wa kitanzania.

Ndugu waandishi wa Habari; Ninafahamu matarajio yavijana wa kitanzania yatafikiwa kupitia CCM imara na CCM inatokana na uimara wajumuiya zake kuwa imara na hili inawezekana kwa kupatikana viongozi Imara na mimi nina amini ni mmoja waviongozi ambao wataifanya jumuiya yetu kuwa Imara.

Kwa kuhitimisha Hotuba yangu naomba kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kunifanikisha kuwananyi hapa, niwashukuru wana familia yangu, marafiki na nyie ndugu zanguwaandishi wa Habari kwa kukubali kujumuika nami kunisikiliza leo. Niwaombe Vijana wenzangu wa CCM kuniunga mkono katika azma hii kubwa niliyo nayo na niwakumbushe tu kuwa, zoezi hili la kuchukua fomu nililofanya hapa leo si langu bali la vijana wote wa Tanzania wakiwakilishwa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi.

Ni imani yangu kuwa, wana UVCCM hawatakubali kuangusha taa hiiwaliyoiwasha kule Rorya mkoa wa Mara wao wenyewe na badala yake wataungana namibega kwa bega ili kuufikia ushindi. Tutapitisha fomu hii pamoja nao, tutachujwa pamoja nao na kisha tutashinda pamoja nao na kisha kuanza kuwaongoza vijana wa Tanzania pamoja nao. Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma atubariki na kutupa nguvutufanikishe azma hii muhimu pamoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi

Asanteni kwa kunisikiliza.

Mimi Ndg Sango Gungu Kasera- Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM (W) Rorya

Kauli mbiu
MbiuVijana kwanza kwa taifa lenye amani namaendeleo’’.

Tuesday, July 10, 2012

Four Seasons Sets Up Camp in Tanzania’s Serengeti National Park

Four Seasons Hotels and Resorts has signed a long term management agreement with the owners of Bilila Lodge, a resort in the Serengeti National Park, and is now operating the property, which will be upgraded and renamed Four Seasons Safari Lodge Serengeti, Tanzania in fall 2012.

“We have long wanted to expand into Sub-Saharan Africa and offer new outdoor adventure experiences to our guests,” says Kathleen Taylor, president and CEO, Four Seasons Hotels and Resorts. “Now, we’re thrilled to have an outstanding location and partners who share our vision to create a world class lodge like no other in the heart of Africa’s finest safari region.”

Four Seasons veteran James Kostecky has been appointed General Manager as the property transitions to Four Seasons Safari Lodge Serengeti. Most recently General Manager at Four Seasons Resort Chiang Mai and Four Seasons Tented Camp Golden Triangle in Thailand, he has previous experience in Kenya with a hotel group based in Nairobi.

“It’s great to be back in Africa, where each day brings a new wonder,” says Kostecky, an avid photographer with a keen sense of adventure. “This Lodge will be an excellent opportunity for first time safari travellers, families and groups to experience the natural beauty, astounding wildlife and fascinating culture of the Serengeti.”

Development in Africa and Other Ecologically Sensitive Regions

“This is the first step in a bold development project that will see three diverse Four Seasons experiences in what are considered to be three of the most important and attractive destinations in Tanzania,” says Scott Woroch, executive vice president worldwide development at Four Seasons. “The responsibility of taking over such as irreplaceable asset within the Serengeti National Park is one that we take very seriously. This is an extremely rare opportunity forFour Seasons in that no other property of this size or scale exists, or is likely to ever be developed again in the Park. With the future development of a luxury tented safari camp in the Ngorongoro Conservation Area and an exclusive beach resort on the island of Zanzibar, Four Seasons will offer some of the finest holiday experiences in Tanzania.”

As with the company’s award-winning Four Seasons Tented Camp Golden Triangle in Thailand, Four Seasons in Tanzania will offer guests opportunities to get close to wildlife in a safe and ecologically responsible environment while still being pampered in a lodge set amid unspoiled wilderness.

About Four Seasons Safari Lodge Serengeti, Tanzania

A UNESCO World Heritage Site, Tanzania’s Serengeti National Park covers 14,763 square kilometres (5,700 square miles). The landscape features the largest concentration of plains animals in Africa, and is acclaimed for the best game drives and abundant year-round wildlife, including the famous migrating herds of wildebeest, zebra, antelope and gazelle as well as lions, leopards, cheetahs, elephants, buffalo, rhinoceros, hippopotamuses, crocodiles and abundant birdlife.

Four Seasons Safari Lodge Serengeti is located in the Central Serengeti, entirely within the Park. The property boasts 60 rooms, 12 suites and 5 villas – all of which have direct views over the Serengeti. Designed with contemporary African architecture sympathetic to the natural landscape, the centrepiece is a two-story great house, including several dining options with indoor and outdoor seating, a Spa and an infinity-edge swimming pool overlooking an active watering hole. Guests have the opportunity to witness nature at its best, day or night, including a herd of nearly 30 elephants that are frequent visitors. Elevated wooden walkways connect the great house to guest rooms, free-standing villas and the Spa complex.

Sunday, June 24, 2012

SAFARI YA MWISHO YA MHARIRI WILLY EDWARD OGUNDE

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo akiiongoza familia ya marehemu Willy Edward kuweka udongo kwenye kaburi wakati wa maziko.
Watoto wa marehemu Willy Edward, Colman na Careb wakiweka shada la maua kwenye kaburi la babao.
Mdogo wa marehemu Willy Edward, Essey Ogunde (kushoto) na kakao, wakiweka shada la maua
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda (katikati), akiwaongoza baadhi ya wahariri kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Willy Edward wakati wa maziko yaliyofanyika Molotongo, Mugumu.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo (kushoto) na Askofu John Adiema wa Dayosisi ya Rorya wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Willy Edward.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni tayari kwenda ktuo heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Willy Edward.
Waombolezaji wakiwa katika msiba wa marehemu Willy Edward nyumbani kwao,

Popular Posts