Pages

Showing posts with label BOT Bank of Tanzania Benki Kuu ya Tanzania. Show all posts
Showing posts with label BOT Bank of Tanzania Benki Kuu ya Tanzania. Show all posts

Saturday, August 11, 2012

BOT : HATUJAWEKA SHUGULI/OPERESHENI ZA NBC CHINI YETU

Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa “Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu”. Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na utawala bora.

Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.

IMETOLEWA NA
BENKI KUU YA TANZANIA
11AUGUST 2012

Thursday, August 9, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akutana na Uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania

Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BOT Tawi la Zanzibar Bwana Joseph Mhando akiwasilisha mchango wa Shilingi 10,000,000/- kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya mfuko wa Maafa hapo Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
2.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania BOT uliofika ofisini kwake Baraza la Wawakilishi Mbweni kutoa mkono wa pole kufuatia ajali ya meli ya M.V. Skagiti hivi karibuni.

Popular Posts