Pages

Showing posts with label Mbeya. Show all posts
Showing posts with label Mbeya. Show all posts

Friday, January 4, 2013

Dkt. Mwakyembe akagua uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya


Picture
Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika uwanja wa Ndege wa Songwe, Mbeya amesema kuwa uwanja huo una hadhi ya Kimataifa na ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru, ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro (KIA).

(picha zote na maelezo, credit: Mbeya Yetu blog)
Picture
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimwelezea Dkt. Harrison Mwakyembe jinsi uwanja wa ndege wa Songwe unavyofanya kazi toka uzinduliwe mwezi wa 12 mwaka jana na kuwa sasa uwanja huo umebaki kukamilisha maeneo ya maegesho ya ndege kubwa kama Boeing 737.
Picture
Hili ni eneo la kutua ndege na kurukia barabara hiyo ya ndege yenye urefu wa zaidi ya kilometa 3.5 km
Picture
Huu ni mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja hicho
Picture
Mwongoza ndege mwandamizi John Chambo akimwezea waziri Mwakyembe jinsi wananvyofanya kazi ya kuongoza ndege katika mnara huo
Picture
Sura ya mbele ya uwanja wa Songwe
Picture
Maegesho ya zimamoto
Picture
Hili ndilo eneo la maegesho ya ndege kubwa aina ya Boeing 737 ambalo mwishoni mwamwezi huu linatarajiwa kuwa limekamilika


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2H2wxliuB

Saturday, August 4, 2012

wajipanga kuirejesha Tukuyu Stars Ligi Kuu

Wadau wa timu ya Tukuyu Star Banyambala ya Mbeya wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea Tukuyu kwa ajili ya Kongamano la Kuifufua upya timu hiyo iliyovuma miaka ya 1980 na 1990 katika soka la Tanzania na ilifanikiwa kuchuka ubingwa wa Bara mwaka 1986. katika picha kulia ni Kocha Kenny Mwaisabula Mzazi wa pili kutoka kulia waliosimama ambaye ndiyo kiongozi na Makamu mwenyekiti wa Tukuyu Star Family, Fullshangweblog itakuwa ikikumuvuzishia moja kwa moja matukio ya kongamano hilo kutoka mjini Tukuyu Kesho. yakirushwa na Kamanda wa Fullshangweblog John Bukuku
Hapa wadau hao wakipozi kwa picha kabla ya uanza safari hiyo maeneo ya Ubungo jijini
Dar es salaam.

Saturday, July 28, 2012

KUHUSU MUINGILIANO WA MASAFA YA TELEVISHENI ULIOTOKEA MKOANI MBEYA

MWINGILIANO wa masafa ya televisheni uliotokea hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Mbeya umeelezwa kusababishwa na masafa yaliyokuwa yakitumika kuchukuliwa na wamiliki wake halali walioyanunua.

Hayo yamebainishwa leo na Meneja wa mamlaka ya mawazsiliano nchini(TCRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Deogratius Moyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Moyo amesema kuwa masafa hayo hivi sasa yanatumika kutolea huduma za Interneti kwa makampuni yanayotoa huduma hiyo nchini.

Amesema kwa watumiaji wa dishi ya Setilaiti wanatakiwa kufanya marekebisho ya madishi yao ili waweze kupata masafa sahihi yanayorusha matangazo kwenye masafa yaliyotengwa kwa ajili ya matangazo
ya Televisheni.

Akifafanua zaidi, Meneja huyo amesema masafa ya sataelaiti katika C-Band huanzia 3.7GHZ hadi 4.2GHZ yametengwa kwa ajili ya intaneti barani Afrika huku masafa hayo katika C- Band huanzia 3.4GHZ hadi 3.6GHZ ni kwa ajili ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumzia tatizo la masafa katika jiji la Mbeya, Moyo amesema kuwa kwa kuwa wananchi wengi walifunga kifaa cha kunasa mawimbi (NLB) kwenye uelekeo wa masafa ya intaneti ambayo wamiliki wake walikuwa hawajaanza kuyatumia, na kuwa baada ya wamiliki halali kuyachukua imesabaisha baadhi ya watu kukosa matangazo ya televisheni.

Meneja huyo amesema masafa hayo kwa hivi sasa yanatumiwa na kampuni ya simu ya Vodacom, hivyo watumiaji wengine hawana budi kuhama na kubadilisha kifaa cha kunasa matangazo kwa njia ya sataelaiti (LNB).

Amesisitiza wananchi kujiunga na mfumo wa digitali kwa kuwa ifikapo Desemba 31, mwaka huu mitambo ya kurushia matangazo kwa njia ya analojia itazimwa nchini huku akiusifia mfumo mpaya akisema ni salama, hauna madhara wala gharama kubwa kwa mtumiaji.

Kwa hisani ya Joachim Nyambo

Friday, July 27, 2012

MAFUNZO YA INTANETI KWA WAANDISHI HABARI WA MBEYA

Waandishi wa mkoa wa Mbeya wakiwa makini kufuatilia mafunzo ya kompyuta jijini Mbeya


Waandishi wa Habari Gordon Kalulunga(TANZANIA DAIMA), Johnson Jabir(MBEYA FM) na Lina Mwambungu (BARAKA FM).


Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango naye alikuwepo katika semina hiyo

MAFUNZO ya Intaneti kwa waandishi Habari leo yameingia siku yake ya pili katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC) tawi la Mbeya chini ya Mwalimu Mdegela kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam.

Tuesday, July 24, 2012

MAANDALIZI YA SIKU YA MASHUJAA MKOANI MBEYA

Askari wa JWTZ wa kikosi cha 44 KJ wakiwa mazoezini kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa jijini Mbeya

Ukumbusho wa askari waliokufa vitani 1939 1945


Askari wa JWTZ wa kikosi cha 44 KJ wakiwa mazoezini kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa jijini Mbeya





Monday, July 23, 2012

Rais Jakaya Kikwete Afuturu na Viongozi Mbalimbali wa Dini mkoani Mbeya

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya magharibi muda mfupi kabla ya futari ambayo aliwaalika viongozi mbalimbali wa dini mjini Mbeya jana
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya magharibi muda mfupi kabla ya futari ambayo aliwaalika viongozi mbalimbali wa dini mjini Mbeya jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali aliowaalika katika futari katika ikulu ya mjini Mbeya jana jioni.Picha na Freddy Maro-IKULU

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI MBEYA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo katika Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(wapili kushoto), balozi wa jumuiya ya ulaya nchini Cerian Philberto Sebregondi(kushoto),Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji safi na mazingira Mjini Mbeya.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(Watau kushoto) na Waziri wa Maji Profesa JumANNE Maghembe wakikagua chanzo cha maji eneo la Swaya mjini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mradi maji safi na mazingira mjni humo.

Saturday, July 14, 2012

UJENZI WA BARABARA YA TUNDUMA MPAKA SUMBAWANGA WAENDELEA

Barabara ikiwa tayari imeshaanza kuwekewa lami
Daraja la MPUI
Daraja la LAELA
Vijana wakiwa kazini kurekebisha mifereji kwenye barabara hiyo mpya.Picha zote na Mdau Adam Mzee

Wednesday, July 11, 2012

SHIRIKA LA NYUMBA MBEYA LAENDELEA KUTOA VYOMBO NJE WADAIWA SUGU

VYOMBO VYA WAPANGAJI WA SHIRIKA LA NYUMBA VIKIWA VIMETOLEWA NJE

DALALI NA AFISA MTENDAJI WA KATA YA SISIMBA WAKISIMAMIA ZOEZI LA UTOAJI VYOMBO VYA WAPANGAJI HAO




Friday, July 6, 2012

Waziri wa Elimu na Ufundi Apiga marufuku wanafunzi kushika Chaki

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo akiongea na wakuu mbalimbali wa elimu mkoani Mbeya


WALIMU waliozoea kuwapa chaki na notsi wanafunzi ili wakawaandikie wenzao madarasani sasa watawajibishwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi watakapobainika.

Naibu waziri wa wizara hiyo Filipo Mulugo ametoa agizo hilo katika mkutano wake na viongozi mbalimbali wa idara ya elimu kanda,mkoa na wilaya pamoja na wakuu wa shule za sekondari za mkoani Mbeya na wakuu wa shule za msingi katika halmashauri ya jiji.

Kadhalika Mulugo amekataza mamonita wa madarasa kuitisha majina ya mahudhurio ya wanafunzi wenzao akisema mwenye jukumu hilo ni mwalimu wa darasa husika na itakapobainika mwalimu huyo pamoja na mkuu wa shule husika watawajibishwa.

Amesema shughuli zote hizo si za mwanaafunzi na zinazorotesha ufanisi katika utendaji kwakuwa walimu wanakaimisha majukumu hayo na wao wakibaki wanapiga soga ofisini mwao na walimu wenzao

Waziri wa Elimu na Ufundi Apiga marufuku wanafunzi kushika Chaki

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo akiongea na wakuu mbalimbali wa elimu mkoani Mbeya


WALIMU waliozoea kuwapa chaki na notsi wanafunzi ili wakawaandikie wenzao madarasani sasa watawajibishwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi watakapobainika.

Naibu waziri wa wizara hiyo Filipo Mulugo ametoa agizo hilo katika mkutano wake na viongozi mbalimbali wa idara ya elimu kanda,mkoa na wilaya pamoja na wakuu wa shule za sekondari za mkoani Mbeya na wakuu wa shule za msingi katika halmashauri ya jiji.

Kadhalika Mulugo amekataza mamonita wa madarasa kuitisha majina ya mahudhurio ya wanafunzi wenzao akisema mwenye jukumu hilo ni mwalimu wa darasa husika na itakapobainika mwalimu huyo pamoja na mkuu wa shule husika watawajibishwa.

Amesema shughuli zote hizo si za mwanaafunzi na zinazorotesha ufanisi katika utendaji kwakuwa walimu wanakaimisha majukumu hayo na wao wakibaki wanapiga soga ofisini mwao na walimu wenzao

Wednesday, July 4, 2012

MWANACHUO WA ST AGREY AUWAWA KWA TUHUMA ZA WIZI

Samahani kwa picha hizi



Hii ndiyo pikipiki inayodaiwa mwanachuo huyo kuiiba

Hiki ni kitambulisho cha mwana chuo huyo



Mwananchuo wa chuo cha ualimu cha ST Aggrey kilichopo uyole jijini mbeya anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma zakuiba pikipiki zakusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati 25 mpaka 30 .

Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo july 2 mwaka huu majira ya saa 8 za mchana katika daraja lilopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea isanga jijini mbeya.

Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa taarifa za kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya JOSEPH KAPASI(23)mkazi wa Ilomba jijini hapa

 
Kwaupande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri alitokomea nayo na marabaada ya hapo alipatikana eneo la isanga akielekea barabara ya chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na wanainchi wenye hasira kali nakuanza kumpa kichapo ambacho kimemfanya azirai.

picha na Mbeya yetu

Tuesday, July 3, 2012

KONGAMANO LA UTOTO WA MTAKATIFU WA YESU KANDA YA KUSINI

Askofu mkuu wa jombo la Songea Mhashamu Norbert Mtega akiongoza maandamano hayo kuingia kanisa la Hija Mbeya



Maandamano ya watoto wa utakatifu wakiingia kanisa la hija kwa maandamano


Askofu mtega akipokwea na watoto katika kanisa la hija jijini Mbeya


Picha na MbeyaYetu

Popular Posts