Pages

Showing posts with label Maonyesho ya Sabasaba. Show all posts
Showing posts with label Maonyesho ya Sabasaba. Show all posts

Sunday, July 8, 2012

Rais Jakaya Kikwete Atembelea Maonyesho ya Sabasaba 2012

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya bidhaa zitokanazo na Wannyamapori wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mali asili na utalii katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya bidhaa zitokanazo na Wannyamapori wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mali asili na utalii katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa PPF Bwana William Eriyo akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mradi wa uwekezeaji wa hoteli ya kisasa iliyojengwa na shirika la PPF mjini Mwanza wakati Rais alipotembelea banda la PPF katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana.Picha na Freddy Maro-IKULU

Thursday, July 5, 2012

BANDA LA ARTI-TZ MAONYESHO YA SABASABA 2012

Pia mkaa unaotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa unapatikana.
Epuka kuhangaika na giza, Sola zinapatikana.
Wateja wakipatiwa huduma.
Muonekano wa banda lao.
Programe Director wa Arti- Tanzania, Dennis Tessier akiwa ndani ya banda lao.
Meneja wa mambo ya mkaa, Allan Shahidi akitoa somo kwa wateja waliofika bandani hapo.

Twiga Bancorp Katika Maonyesho ya Saba Saba 2012

Wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp ambao wapo kwaajili ya kutoa huduma katika banda la Benki hiyo viwanbja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Saba Saba wakilamba picha ya pamoja mbele ya Banda lao linalotoa huduma kamili za Kibenki
Afisa Masoko wa Twiga Bancorp Limited, Adelbert Archerd Tibikunda akiwa amekamatia tuzo ya Century International Gold Quality ERA waliyo ipata Genever kwa huduma bora .
Katika Banda la Twiga Bancorp wateja wanapata fursa ya kuweka fedha zao papo hapo baada ya kufanya mauzo ndani ya Saba Saba. Yanini utembee na fedha nyingi wakati Benki ya twiga ipo nawe pale ulipo.
Fedha katika ATM ni kwa saa 24, siku 7 za wiki, mwezi mzima na siku 360. Huduma hii katika banda la Twiga hafungwi mwaka mzima.
Utoa huduma bora ndio nguzo na ngao ya Twiga Bancorp, pichani ni mteja akiwa na furaha wakati akizungumza na Afisa Mwandamizi Mwendeshaji wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Lydia Matembel, alipotembelea banda lao katika viwanja vya Maonesho Saba Saba.
Afisa wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Ernest Kikwasi, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo jana juu ya akaunti maalum ya watoto. Twiga Bancorp ni miongoni mwa benki zinazoshiriki katika Maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere barabara ya Kilwa huku wakitoa huduma kamili za kibenki
Mmteja wa Twiga Bancorp akitoka kupata huduma katika banda la Benki hiyo kwa furaha baada ya kufanikiwa kutimiza alichotaka kwa wakati.
Wateja wakipata huduma ya kubadili fedha katika banda la Twiga bancorp.

BANDA LA MeTL MAONYESHO YA SABASABA 2012

Moja ya Bango ndani ya banda hilo linaloonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
Mafuta aina ya ‘Safi’ yanayopatikana katika banda la hilo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Maji safi ya kunywa aina ya ‘Maisha’ ambayo pia yapatikana kwa bei rahisi katika banda la MeTL kwenye maonyesho ya Sabasaba.
Vitengee, Khanga venye ubora navyo vinapatikana.
Muonekano wa banda la MeTL kwa nje ukionyesha wateja kadhaa wakitoka baada ya kujipatia mahitaji yao.
Mmoja wa wafanyakazi katika banda la kampuni ya Mohammed Enterprses Tanzania Limited (MeTL) akionyesha unga wa ‘Safi’ unaotengenezwa na kampuni hiyo.

KIJADALA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI VIWANJA VYA SABASABA

Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja akiwa amekamatwa na vijana wa skauti mara baada ya kukamatwa huku akiwa ameiba simu ndani ya Maonyesho ya SabaSaba 2012 jijini Dar.
Mpeleke mpelekeeeee...
Kitu cha Tanganyika jeki kikiwa kimekolea.
Wananchi mnatakiwa kuwa makini sana mnapokuwa mmetembelea maonyesho ya SabaSaba 2012 maana kuna vibaka wa kutosha japo vijana wa skauti wamekuwa wakijitahidi kulinda usalama.

Wednesday, July 4, 2012

Banda la ASAS Dairies , Maonyesho ya Sabasaba 2012


DAIMA huwezi zungumzia bidhaa za maziwa bila kutaja bidhaa za ASAS Dairies IRINGA ambao huzalisha bidhaa za aina mbalimbali zitokanazo na Maziwa halisi ya Ng’ombe.Maonesho ya 36 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanaendelea katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam ASAS DAIRIES wapo katika banda la KARUME fika hapo na ujipatie mahitaji yako ya Maziwa.
Bidhaa zimesheheni na vinavyostahili kuliwa vya Baridi utavipata baridi kwa fleva za kila namna
Wateja wakubwa kwa watoto wakijipatia bidhaa za maziwa bora kutoka banda la ASAS ndani ya Maonesho ya Saba Saba.
Karibuni katika Banda la Bodi ya Maziwa Tanzania na utawakuta ASAS DAIRIES kwa bidhaa bora za Maziwa.

Tuesday, July 3, 2012

Vodacom Tanzania Katika Maonesho ya Sabasaba 2012

Wakala wa Vodacom M PESA akitoa huduma ya M- PESA kwa mteja alietembelea maonesho ya sabasaba jijini Dar es salaam Kampuni ya Vodacom Inashiriki katika maonesho hayo kama mdhamini rasmi wa mawasiliano.
Wateja waliojitokeza katika maonesho ya biashara ya Kimaifa Dar Es salaam (sabasaba) wakipewa maelekezo na wafanyakazi wa kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania,namna ya kutumia simu ya ZTE 502 inayouzwa kwa shilingi elfu 13 katika maonyesho hayo.
Mteja aliejitokeza katika maonesho ya sabasaba akipata maelezo ya namna ya kutumia simu ya ZTE 502 pia iliyokuwa na muda wa maongezi wa shilingi elf 6000 na kuuzwa kwa shilingi elfu 13 ikiwa ni ofa maalum katika maonesho hayo ya sabasaba.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania wakimpa maelekezo mteja alienunua simu aina ya ZTE 502 inayouzwa kwa shilingi elfu 13 katika maonesho ya Biashara ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam

Monday, July 2, 2012

UMOJA WA MATAIFA KATIKA MAONESHO YA SABA SABA

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi walio telea Banda hilo leo.



Maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Saba saba yameanza Juni 28, 2012 katika viwanja vya Maonesho vya JK Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania wanashiriki maonesho hayo makubwa Tanzania, huku serikali na taasisi zake nyingi zikiwa moja ya washiri katika maonesho hayo yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzanaia.

Pia taasisi za Kimataifa na mashirika makubwa duniani yanashiriki maonesho hayo, miongoni mwa mashirika hayo ni Umoja wa Mataifa ambao upon a taasisi zake zote zaidi ya 21. UN Tanzania wapo katika Banda la Ali Hassan Mwinyi na elimu mbalimbali juu ya Umoja huo wa Mataifa ambao Tanzania ni mwanachama wake unapatikana.
Afisa habari wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Austin Makani akiwa na Afisa Habari wa Umoja wa Umoja wa Mataifa (UN) Hoyce Temu.
Mjasiriamali, Bi Magreth Msuya kutoka Kikundi cha MATA Woman Group cha Tabata jijini Dar es salaam ni moja ya watu wanaofaidika na UN, na hapa anashiriki maonesayo ndani ya Banda la UN. Kulia ni mteja anaeangalia bidhaa zake na kto ni Afisa Habari wa UN Tanzania, Hoyce Temu.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa wananchi walio telea Banda hilo leo.
Banda la umoja wa Mataifa.

Wizara ya Maliasili na Utalii katika maonyesho ya sabasaba 2012

Mwonekano wa Banda la Wizara ya maliasili na utalii katika maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa Dar es Salaam mwaka huu.

Hapa ni mapokezi.






Popular Posts