Pages

Showing posts with label Habari za Mahakamani. Show all posts
Showing posts with label Habari za Mahakamani. Show all posts

Thursday, November 8, 2012

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI DHIDI YA RUFAA YA LEMA



IMG-20121108-WA0003
Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mhe. Godbless Lema wakiwa mahakamani leo.
IMG-20121108-WA0007
Godbless Lema akiwasili katika viwanja vya Mahakama ya Kuu jijini Dar leo.
Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai  ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.

Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za waliokata rufaa. Mawakili wa Mhe. Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.

Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi. Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu.
IMG-20121108-WA0006
Wapenzi wa Chadema wakimlaki Mhe. Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama leo.
IMG-20121108-WA0004
Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi.
IMG-20121108-WA0002
Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
IMG-20121108-WA0005
Katibu wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama Kuu leo. Habari / Picha kwa hisani ya ARUSHA255 BLOG

Thursday, October 18, 2012

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda na Wengine 50 Wapandishwa Kizimbani Jijini Dar es Salaam


 Picha juu na chini ni washaktakiwa zaidi ya 50 wakiwa pamoja na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda wakiwa ndani ya karandimnga la polisi 
 Baadhi ya akina mama wanaounganishwa kwenye mashtaka hayo pamoja na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda (wa tatu kulia)leo akiwa ndani ya mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo na wenzake 50 kujibu mashtaka mbalimbali pamoja na kuwashawishi baadhi ya Waislamu kuvamia eneo la Kiwanja katika eneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam, kuwashawishi Waislamu kutojitokeza katika zoezi la Uandikishaji katika Sensa ya Watu na Makazi.

Saturday, August 11, 2012

Papaa Msofe Alivyopandishwa Kizimbani Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Saalam Kwa Tuhuma za Mauaji

Papaa Musofe akipanda gari ya polisi kurejea mahabusu baada ya kusomewa shitaka la mauaji kwenye mahakama ya Kisutu
Marijani Abubakar Msofe ‘Papaa Musofe’ (58) akiingia kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, kwa ajili ya kusomewa mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili
Papaa Musofe akipandisha ngazi za mahakama ya Kisutu kwenda kusomewa shitaka la tuhuma za mauaji linanomkabili
Papaa Musofe akielekea mahakama ya Kisutu kwenda kusomewa shitaka la tuhuma za mauaji linanomkabili
Papaa Musofe akindikisha jina kwa maofisa wa Polisi mahakamani hapo
Papaa Musofe wa pili kulia, akiwa amekaa kwenye gari ya polisi chini ya uangalizi mkali, tayari kwa safari ya kurudi mahabusu.Picha Zote na Mdau Francis Dande

Monday, July 23, 2012

Wananchi wa Mgodi wa Buhemba Kuishitaki Serikali Ya Tanzania Kwa Jumuia za Kimataifa

Mgodi wa Buhemba
Diwani wa kata ya Buhemba Boniphace Masero akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
---
Augustine Mgendi, BUHEMBA
WANANCHI vijiji Vitatu wanaozungukwa na Mgodi wa Buhemba wilaya ya Butiama mkoani Mara wanakusudia kuishitaki Serikali ya Tanzania katika Taasisi za Umoja waMataifa zinazohusika na haki za binadamu ikiwa ni shinikizo la kulipwa fidia ya shilingi Bilioni 30.

Mbali na kusudio hilo la kuelekea umoja wa Mataifa lakini pia wananchi hao wamesema kuwa wanakusudia kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kumueleza madhara yaliyosababishwa na Mgodihuo ambao ulidaiwa kumilikiwa na Serikali kupitia Kampuni ya Meremeta.

Wananchi hao kutoka vijiji vyaTarani,Biatika na Magunga huku wakiomba Wabunge kuungana na kutoipitisha Bajetiya Wizara ya Nishati na Madini had hapo Serikali itakapo wafidia.

Akiongeana waandishi habari katika eneo hilo la Buhemba,Diwani wa kata ya BuhembaBoniphace Masero amesema kuwa Mgodi huo umeachia athari kubwa kutokana namachimbo yaliyoachwa kuleta athari kubwa huku Ardhi yao ikiwa haina rutuba kutokanana Kemikali zilizomwagwa katika eneo hilo

Amesema athari zingine zilizoletwa na Mgodi huo nipamoja na Shule iliyokuwa katika eneo hilo kubomolewa lakini walishindwakuijenga kama walivyokuwa wameahidi wahuska hao wa mgodi huku miundombinu yabarabara nao ikiwa haifai kutumika.



“Huu Mgodi umetuachia madhara makubwa sana maanaMashimo hayakufukiwa,Milima inaleta uchafuzi wa Mazingira,shule iliyokuwaimejengwa hapa ilibomolewa,Nyumba zikabomoka kutokana na Baruti za mgodi,katikahili sisi tunakusudia kumuona Rais ili tumueleze haya Manyanyaso tunayoyapata”alisema diwani huyo

Diwani Masero ameongeza kuwa athari nyingine nipamoja na baadhi nyumba za wakazi wa eneo hilo kubomoka kutokana na barutizilizokuwa zikipigwa katika Mgodi huo lakini mpaka sasa hawajalipwa fidia nahivyo wanawaomba Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakutoipitisha Bajeti ya wizara ya Nishati na Madini mpaka walipwe fidia yao

Aidha Pasta wa Kanisa la Anglikana SamweliNyakarungu alisema kuwa mgodi huo wa Buhemba ulikuwa ni Mgodi wa kitapeliambapo wahusika hao wamechuma raslimali za Taifa na kushindwa kufanya shughuliza Maendeleo katika Jamii.

Pasta Nyakarungu alisema kuwa mbali na wawekezajihao wa Kitapeli kuiba mali ya Watanzania lakini pia wamesababisha madharamakubwa kwa jamii ya Buhemba kwa kushindwa kujenga miundombinu ya barabara,kujengashule kama inavyotakiwa.

Kutoka na adha hiyo Pasta huyo alisema kuwa Serikaliimeshindwa kuwajali wananchi wake na hivyo wanawaomba Wabunge wa Bunge laJamhuri ya Muungano kutoipitisha Wizara ya nishati na Madini mpaka hapowananchi wa eneo hilo watakapopata fidia yao.

“Hawa wawekezajimimi naona hawakuja hapa kwa lengo la kumsaidia mtu wa Buhemba huu Mgodi naonaulikuwa wa Kitapeli kabisa,wamechuma raslimali za Taifa na kushindwa kumsaidiamtu anayezungukwa na mgodi na hata kurekebisha miundombinu huska na hiiinaonyesha jinsi Serikali isivyojali wananchi wake” alisema Pasta Nyakarungu

Naye Mwalimu mstaafu Sita Nyamhanga na bi HadjaYasini walisema kuwa mgodi huo umewaachia matatizo makubwa ikilinganishwawalivyokuwa wameahidiwa wakati wanaanza uchimbaji katika mgodi huo.

“Tunavyojuani kwamba wawekezaji wanapowekeza eneo lolote lazima watu wanaozungukwa naMgodi ule wanufaike lakini hapa Buhemba sisi wananchi ndiyo tumepat tabu kabisakwani mpaka sasa hatuna shule,barabara inayopitika muda wote,eneo letu limebakiJangwa huku wakina mama wanapata tabu kutafuta maji kutokana na vyanzo vingivya maji kuchafuliwa na mgodi” alisema Mwalimu mstaafu huyo.

Kwa upande wake Bi Hadja Yasini alisema kuwawanapata tabu hata kutafuta kuni kutokana na eneo kubwa la Buhemba kubakiJangwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Kulingana na adha hiyo Bi Hadja alisema kuwa nivyema Waziri mwenye dhama huska akawasaidia watu wa Buhemba ili waweze kupatafidia zao kutokana na madhara waliyoyapata kutokana na mgodi huo.

Mgodi wa Buhemba ambao ulianza kuchimbwa mwaka 2002ni moja ya mgodi ambao ulikuwa ni mkubwa hapa nchini ukielezwa kumilikiwa naSerikali na kufungwa mwaka 2006 huku ukiacha eneo hilo la Buhemba kupotezarutuba yake

Tuesday, July 17, 2012

WAFUASI WA CHADEMA WALIOPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWENYEKITI WA UVCCM

Afisa sera na utafiti CHADEMA Makao makuu, Waitara Mwita akifurahi na wanachama wa CHADEMA, baada ya kupata dhamana mjini Singinda
Mwita Waitara akizungumza na wanahabari mjini Singida baada ya kuwekewa dhamana ya wadhamini wawili
Mwita Waita (wa kwanza kushoto), akifurahi na wafuasi wa CHADEMA mahakamani mjini Singida, baada ya kupata dhamana ktk kesi ya mauaji.
VIJANA sita, Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti UVCCM Yohana Mpinga wa Kata Ndago Iramba Singida, wakipandishwa kwenye gari la polisi.Picha na Habari na Elisante John
--

WATU sita wamepandishwa kizimbani Mjini Singida, kujibu shitaka la mauaji ya Mwenyekiti UV-CCM Kata ya Ndago Wilaya Iramba,Yohana Mpinga, katika vurugu zilizohusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM.Wamesomewa shitaka hilo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Neema Mwanda mbele ya hakimu mfawidhi mahakama ya Mkoa Singida, RuthMassam.
Walioshitakiwa ni Manase Daudi (40), Williamu Elia (33), Frank Stanley (20), Charles Leonard (36), Tito Nintwa na Fillipo Edward (30), wakazi wa Ndago, Wilaya Iramba.
Wamedaiwa kufanya kosa hilo Julai 14, 2012 saa kumi alasiri, katika kijiji cha Nguvumali, kwa kutumia mawe na fimbo.
Hawakutakiwa kujibu lolote, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo na itatajwa tena Julai 30, 2012.
Pia kesi nyingine iliyosomwa na mwanasheria wa Serikali Seif Ahmad, imemhusisha afisa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Waitara Mwita (37) mkazi wa jijini Dar-es-salaam, akidaiwa kutoa lugha ya matusi mkutanoni.
Waitara anadaiwa kutoa lugha hiyo ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, Julai 14, 2012 saa kumi jioni katika kijiji cha Ndago, Wilaya Iramba Mkoani Singida. Yupo nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja mwenye Sh.800,000 na itatajwa tena Julai 30, 2012.

Sunday, July 15, 2012

WALIOBOMOLEWA MBEZI BEACH KWENDA MAHAKAMANI

*Wadai wanamiliki maeneo yao kihalali na wameonewa

Na Joachim Mushi wa Thehabari.com

WAKAZI 32 wa eneo la Mbezi Beach Kata ya Kilongawima wanakwenda mahakamani kupinga kitendo cha Serikali kuwabomolea nyumba zao hivi karibuni, kitendo ambacho wanadai wameonewa kwani wao wanamiliki maeneo hayo kihalali, huku baadhi yao wakiwa na nyaraka muhimu za umiliki na baraka kutoka Serikali za Mtaa husika.

Wakizungumza na vyombo vya habari leo wakazi hao wamesema wanasikitishwa na kitendo hicho cha mabavu kufanywa na Serikali tena kwa kuvizia ilhali kulikuwa na taratibu za kisheria za kufuatwa kabla ya zoezi hilo kama kulikuwa na haki ya kufanyiwa hivyo.

Akitoa tamko la wakazi wa eneo hilo leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa wakazi hao, Antony Mseke alisema madai ambayo Serikali kupitia Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) imeyatoa kuwa wao wamevamia eneo la mikoko na kujenga maeneo yasioruhusiwa hayana msingi wowote kwani eneo hilo lipo mbali na mikoko hiyo.

Alisema wanakwenda mahakamani kutafuta haki yao kwa kuwa kilichofanyika ni uvunjaji wa sheria na huenda kuna sababu nyingine wanazo na si kama ilivyotamkwa na waliobomoa.

Mseke alisema eneo hilo kuna mabango ya NEMC ambayo yanaainisha ni eneo gai lisiloruhusiwa kujengwa ambamo imo mikoko ya bahari, lakini katika nyumba zote zilizobomolewa zipo nje na mbali na mipaka ya taasisi hiyo ya mazingira.

“Tumeonewa kupita kawaida tunaiomba Serikali isiwe ikifanya kazi kwa hali kama hii ya mabavu…tunakwenda mahakamani kutafuta haki yetu maana tunaamini tupo hapa kihalali,” alisema kiongozi huyo na mwakilishi wa waathirika wa bomoa bomoa hiyo.

Akifafanua zaidi Mchungaji wa Kanisa la Christian Chapel la Dar es Salaam, George Makala ambaye naye ni mmoja wa wakazi waliokubwa na adha hiyo alisema baadhi yao wamekuwepo eneo hilo tangu mwaka 1992 bila matatizo yoyote huku wakitambuliwa na Serikali za mitaa kihalali.

Alisema anashangaa kuona NEMC kujitokeza na kuwabomolea majengo yao tena bila taarifa kitaratibu. Ameongeza zoezi hilo linaulakini kwani yapo majengo mengine ambayo ni ramani moja eneo hilo lakini hayakubomolewa jambo ambalo linazidi kujenga mazingira ya uonevu.

Alisema pamoja na mambo mengine alama za ‘X’ ziliwekwa Julai 8, 2012 na watu wasiojulikana na baada ya wao kuanza kufuatilia Julai 10, 2012 wavamizi walikuja na silaha kali na kufanya ubomoaji jambo ambalo limewatisha.

“Sisi hatukuwa na mgogoro na Serikali wala kugoma chochote, eneo ambalo mara zote lilikuwa na mvutano lilikuwa mbele yetu tena ni mbali nasi…siku zote tulitambua hilo hata baadhi ya viongozi wa Serikali wanalijua hilo, tunashangaa kuona leo tunabomolewa hivi,” alisema mchungaji huyo ambaye licha ya jingo lake kubomolewa na Kanisa analochunga pia limebomolewa.

Naye Mwanasheria wa Wakazi hao, Living Kimaro kutoka Kampuni ya L & K. Law Chambers ya jijini Dar es Salaam amesema zoezi hilo halikufanyika kitaratibu wala na mamlaka husika hivyo wanakwenda mahakani kudai haki yao.

Tuesday, July 10, 2012

MAHAKAMA MKOANI SINGIDA YATEKETEZA BANDI YENYE THAMANI YA MILIONI 5

Matukio mbalimbali ya uchomaji wa Bangi yenye kilo zaidi ya 350 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.2 iliyokuwa ikisafirishwa na Pascal Dogii (31) mkazi wa Nzega mjini mkoani Tabora kuipeleka jijini Dar-es-salaam, ikiteketezwa kwa moto nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.Pascal hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka kumi jela baada ya kukiri kosa la kumiliki madawa ya kulevya aina ya Bangi.Picha na Nathaniel Limu

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania , Dk Namala Mkopi Mahakamani

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wakati akiingia Mahakamani leo Jijini Dar es Salaam kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini..
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi akiwa na mama yake mzazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Kuibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini..
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi (kulia) akiongozana na baba yake mdogo, Hilary Chinendachi mara baada ya kupata dhama katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi akipeana mikono na baadhi ya madaktari waliofika kujua hatma yake baada ya kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kukaidi amri ya Mahakama ya kutaka kusitisha mgomo wa madaktari.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi akiwa na mama yake mzazi (katikati), pamoja na baba yake mdogo, Hilary Chinendachi mara baada ya kuapata dhama katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.Pihca Zote na Mdau Dande Francis

Popular Posts