Pages

Showing posts with label Airtel Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Airtel Tanzania. Show all posts

Thursday, August 16, 2012

Airtel Tanzania : SHULE 93 ZA SEKONDARI KUFAIDIKA NA MRADI WA VITABU

Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanoyo kama 'AIRTEL SHULEYETU' iliyofanyika katika ofisi za Airtel na kupata shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huo. Kulia anaefuatilia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda (shoto). Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110
Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanoyo kama ' AIRTEL SHULE YETU' iliyofanyika katika ofisi za Airtel na kupata shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huo. Kulia anaefuatilia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi.
---
Airtel Tanzania, imeendeleza dhamira yake katika kuboresha elimu kwa kuchezesha droo iliyochagua shule za sekondari 93 zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel wa kusaidia jamii unaojulikana kama Airte shule yetu kwa mwaka 2012 -2013 Akiongea katika mkutano na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Airtel Kitengo cha Mawasiliano Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Mwaka huu.

Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu shule za sekondari 93, Mradi huu utafaidisha shule 3 kutoka katika kila mkoa Tanzania bara na visiwani.

Shule 93 zilizo chaguliwa leo ni matokeo ya droo iliyochezeshwa na kuzichagua shule hizo kutoka shule 3,000 zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule ambazo zina uhitaji mkubwa wa vitabu na kushauri ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule
yetu.

"Toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka saba iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa yote na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.

Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110, hivyo kila shule iliyopatikana kwenye droo hii watapata Vitabu alisema Mallya.

Bi Mallya aliongeza kwa kusema "tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zitakazoingia kwenye Mradi huu wa Shule yetu tunayatimiza kwa kuwapatia vitabu vya mitaala ya masomo yao kama ilivyopendekezwa na Wizara"

"Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuisaidia jamii hapa Tanzania hasa kwa kuchangia sekta ya elimu kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo Vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Mwaka jana pia Airtel ilisaidia Vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 104 tsh kwa shule za sekondari kwa kupitia droo iliyohusisha jumla ya shule 502" alisema Bi, Mallya.

Nae Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda aliongea kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ulimu (TEA) alisema "Mamlaka ya Elimu Tanzania tunawashukuru sana Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuinua kiwango cha elimu hapa nchini " Mradi wa Airtel Shule Yetu ni mradi mzuri sana kwa jamii yetu kwa kuinua kiwango cha elimu na maisha ya watanzania"

Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo watanzania wote pamoja na waalimu mtakaopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu tuvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini" aliongeza kwa
kusema Bw. Nyirenda

Mbali na shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huu wa vitabu mwaka huu, pia Airtel Tanzania imeshamaliza kukarabati shule ya msingi ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la DSM kando kando na barabara ya bagamoyo ilichaguliwa mwaka jana 2011 huku mipango mingine ya mwaka huu ikiendelea ili kupata shule nyingine itakayofaidika kwa kujengwa na kukarabatiwa na Airtel shule Yetu Airtel bado itaendelea kushirikiana wizara ya elimu kwa wadau wengine kuweza kushiriki katika kuinua kiwango cha elimu hapa Tanzania.

Saturday, August 11, 2012

KIKOSI CHA WACHEZAJI NYOTA WA AIRTEL RISING STARS CHAENDA NAIROBI

Afisa Habari wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jane Matinde(kushoto) akizungumza na waadishi wa habari wakati wa kutangaza kikosi cha timu ya soka cha Airtel Rising Stars kitakachoshiriki michuano ya Inter-continental yatakayofanyika Nairobi, Kenya mwezi huu. Amefuatana na na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando(kulia)
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jackson Mmbando(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kikosi cha timu ya Airtel Rising Stars kinachokwenda kushiriki michuano ya Inter-continental itakayofanyika Nairobi, Kenya baadaye mwezi huu. KAtikati ni Afisa Habari wa kampuni hiyo Jane Matinde na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA).
---
Airtel Tanzania kupitia mpango wake maalum wakuvumbua na kukuza vipaji vya soka nchini ujulikanao kama Airtel Rising Stars leo wametangaza kikosi cha wachezaji 16 watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel yatakayofanyika Nairobi kuanzia Agosti 19 hadi 25, 2012.

Wachezaji hao walichaguliwa na jopo la makocha kwa kushirikiana na shirikisho la mpira TFF na chama cha mpira cha Dar es Saalam DRFA wakati wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam mwezi Juni na kushirikisha timu kutoka mikoa ya Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Temeke na Kinondoni.

Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za TFF leo, Afisa Maendeleo wa mpira wa miguu nchini Salum Madadi aliwataja vijana watakaowakilisha Tanzania kuwa ni Denis Richard, Juma Hamza, Abdul Selemani, Ishaka Shekolowa na Bakari Ally kutoka mkoa wa kisoka wa Temeke.

Wengine ni Abdulatif Mohamed, George Joseph na Badilu Said (Lindi), Said Kassim, Amos Ikungula, Paul Balama na Goodluck Mabiku (Ilala), Joel Kasimula na Ibrahim Mtenga (Mbeya), Sntkony Angelo na Suleiman Yunus (Arusha).
Mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkali yatashirikisha wachezaji wengine nyota wa ARS kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, DRC, Congo Brazzaville, Nigeria, Ghana, Zambia, Niger, Gabon, Burkina Fasso, Sierra Leone, Chad, Madagascar na Tanzania.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kimataifa ni kuwapa vijana fursa zaidi ya kuendeleza vipaji vyao na kupata uzoefu. "Vile vile Airtel Rising Stars inatoa nafasi kwa wanasoka hawa chipukizi kuweza kupanua jiografia yao na kujenga urafiki na vijana wenzao kutoka nchi mbali mbali", alisema Singano.

Michuano hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo pia itafanyika Nairobi chini ya walimu wa soka la vijana kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United ya Uingereza. Kliniki kama hii ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa kisasa wa soka jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya, Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.

Katika kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji sita miongoni mwao ni wavulana watatu na wasichana watatu ambao walioibuka kuwa wachezaji bora wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam mwezi Juni.

Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wanaochipukia barani Afrika. Walengwa ni wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata fursa ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya waatalum wa mpira wa miguu
wa kitaifa na kimataifa.

Monday, July 23, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA SECONDARY MTIPA WILAYA YA SINGIDA MJINI

Meneja Huduma kwa Jamii wa Kampuni ya Simu za Mikononi Tanzania ya Airtel, Hawa Bayuni (kushoto) akikabidhi vitabu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwakilishi wa Shule ya Sekondari
Mtipa iliyopo mkoani Singida, Bi. Mary Haiki ambaye alitembelea makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu ya Airtel jijini Dar es salaam
---
Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora nchini kote, leo imetoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari Mpita ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salam kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mtipa wilaya ya Singida mjini. Mwawakilishi wa shule hiyo ambaye ni mzawa wa eneo hilo bi Mary Hiki alikabidhiwa msaada huo wa vitabu na Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayuni. Shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilling milioni mbili.

Vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Hisabati, Phisikia, Biolojia, Kiswahili. ambapo vimekuwa na uhitaji mkubwa shuleni hapo.

Akiongea wakati wa makabithiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salaam Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayuni alisema" Airtel kwa kupitia kampeni yake ya kusaidia jamii imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule ya sekondari wilayani Singida na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hii Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza Bayuni.

Mwakilishi wa Shule hiyo bi Mary Hiki mzawa wa Singida alisema tunayo fuhara kuona Airtel inajito katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni
kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Singida anatoka graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika
kutimiza malengo tuliojiwekea.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, mwezi uliopita Airtel ilitoa msaada wa kutoa computer 4 na Vitabu vyenye dhamani ya millioni tano kwa shule ya sekondari Mazombe iliyokokilomita nne kutika Iringa mjini . Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.

Thursday, July 5, 2012

FAIDA ZA AIRTEL SUPA 5

1.Hivi inakuaje bado haujawaweka mabesti wako wa tatu kwenye dili na ulipe nusu shilingi kwa sekunde?
2. Kwanini ulipie facebook wakati unaweza kuperus kwa BURE na Airtel?
3. Kwanini usitumie fursa ya kuperuz intanet BURE usiku?
4. Usipoteze pesa bureee kwenye mitandao huku hakuna longo longo, ukiwa Airtel pia unaongea na yeyote kwa ROBO shilling kwa sekunde,usiku kuchwa!!
5. Kubwa zaidi unapata sms 200 Bure , Baada ya kutuma sms 10 kwa shs 30 kila moja…halafu ufurahie kuchat na washkaji KIBAO siku nzima

Hili ndo DILI 5 ya SUPA 5 kwa watu SUPA kama sisi,,,.unasubiri nini.???.Jiunge sasa

Piga *149*99# au ANDIKA neno ‘SIKU’ kisha number 3 za marafiki utakazopigia kwa nusu shillingi na utume kwenda 15548

Popular Posts