MAAMUZI KUHUSU  RUFAA
 DHIDI YA MAAMUZI YA KAMATI ZA UCHAGUZI VYAMA VYA MPIRA WA MIGUU MKOA WA
 MBEYA (MREFA), MKOA WA SHINYANGA (SHIREFA) NA MKOA WA DAR ES SALAAA 
(DRFA).
  
1.                   Kwa mujibu wa Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), Kanuni za Uchaguzi  za wanachama wa TFF, Ibara  ya  10(6), 12(1) na 26(2) na (3), Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika
 vikao vyake vilivyofanyika tarehe 12 na 18 Oktoba 2012 ilijadili 
michakato ya chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa ya Mbeya 
(MREFA), Shinyanga (SHIREFA) na  Dar es Salaam (DRFA) na  kutoa maamuzi kama ifuatavyo:
 
(a)                 Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA)
 
(i)                  Rufaa ya Ndg. Charles Makwaza: Kamati ilijadili rufaa iliyowasilishwa na Ndg. Charles Makwaza dhidi
 ya Kamati ya Uchaguzi ya MREFA, iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF 
kubatilisha uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya MREFA kumpitisha Ndg. John 
Mwamwaja kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa MREFA, kwamba hakutekeleza 
wajibu wa kikatiba wa kuitisha Mkutano Mkuu wa MREFA kwa muda wa miaka 
3.
 
Baada ya kupitia maelezo ya warufani na warufaniwa, Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilijiridhisha kuwa vielelezo na maelezo ya Ndg. Charles Makwaza yaliyowasilishwa mbele ya Kamati kwa kiwango kikubwa hayakuwa ya kweli. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa rufaa hiyo.
 
(ii)                Rufaa ya Ndg. Lusekelo E. Mwanjala: Kamati ilijadili rufaa iliyowasilishwa na Ndg. Lusekelo E. Mwanjala ikipinga  maamuzi ya  Kamati ya Uchaguzi ya MREFA kuliondoa jina lake kugombea  nafasi ya Mwenyekiti wa MREFA, kwa kigezo cha kutokuwa na uzoefu wa uongozi wa mpira wa Miguu.
 
Kamati
 ilipitia vielelezo kuhusu rufaa na kujadili maelezo ya Mrufani na 
Mrufaniwa na ilijiridhisha kuwa Ndg. Mwanjala anakidhi kigezo cha 
uzoefu. Kamati inakubaliana na rufaa ya mrufaa dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya MREFA na hivyo imemrejesha Ndg. Mwanjala kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa MREFA. 
 
(iii)              Rufaa ya Ndg. Thadeo T. Kalua: Kamati ilijadili rufaa iliyowasilishwa  mbele yake na Ndg. Kalua ikipinga  maamuzi ya  Kamati ya Uchaguzi ya MREFA kuliondoa jina lake kugombea  nafasi
 ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, kwa kigezo cha kutokuwa Mkazi wa Mkoa
 wa Mbeya. Kamati ilipitia vielelezo kuhusu rufaa hii na kubaini kuwa 
Katiba ya MREFA iliyosajiliwa haina sharti hilo kwa waombaji uongozi.  Kamati inakubaliana na maombi ya
 
(iv)               mrufaa na inamrejesha Ndg. Thadeo Kalua kugombea nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF. 
 
(v)                 Uchaguzi wa MREFA utafanyika Jumamosi, tarehe 27 Oktoba 2012 kama ulivyopangwa.
 
(b)                Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA).
 
(i)                   Rufaa ya Ndg. Ibrahim Magoma: Kamati ilijadili rufaa iliyowasilishwa na Ndg. Magoma ikipinga maamuzi ya Kamati
 ya Uchaguzi ya SHIREFA kuliondoa jina lake kugombea nafasi ya Katibu wa
 SHIREFA, kwa kigezo cha kuingilia Mchakato wa Uchaguzi kunyume na 
Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na pia kutozingatia matakwa ya 
Kanuni hizo katika kujaza fomu za maombi ya uongozi wa SHIREFA.
 
Kamati
 ilipitia vielelezo kuhusu rufaa ya Ndg. Magoma na kujadili maelezo ya 
Mrufani na Mrufaniwa na ilijiridhisha kuwa Ndg. Magoma  aliingilia
 mchakato wa uchaguzi wa SHIREFA kunyume na Kanuni za Uchaguzi za 
wanachama wa TFF akiwa Katibu Mkuu wa SHIREFA kwa kushiriki kuivunja 
Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA iliyokuwa ikendelea na mchakato wa 
uchaguzi wa SHIREFA.  Kamati inakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA wa kumwondoa Ndg. Magoma kugombea nafasi ya Katibu wa SHIREFA.  Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa rufaa hiyo.
 
(ii)                 Uchaguzi wa SHIREFA umesogezwa Mbele kwa siku nne. Uchaguzi huo utafanyika Alhamisi, tarehe 25 Oktoba 2012, mjini Shinyanga.
 
(c)                 Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA).
 
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilijadili Mchakato wa Uchaguzi wa DRFA na rufaa dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA  na kuamua kama ifuatavyo:
 
(i)                   Marekebisho na usajili wa Katiba ya DRFA: Hoja
 ya rufaa iliwasilishwa na Ndg. Michael R. Wambura ilikihoji uhalali wa 
marekebisho na usajili wa Katiba ya DRFA, kwamba usajili wa Katiba ya 
DRFA si halali. Kamati ilibaini kuwa marekebisho ya Katiba hiyo 
yalifanyika kwa kufuata maagizo ya TFF na kwamba DRFA ilizingatia 
maagizo hayo. Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliridhika kuwa Katiba ya DRFA 
imesajiliwa na Msajili wa vyama na vilabu vya michezo baada ya kuridhiwa
 na TFF, na hivyo, Kamati iliitupa hoja hiyo ya Mrufani kuhusu uhalali na usajili wa Katiba ya DRFA.
 
(ii)                 Kuundwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF : Hoja
 ya rufaa ya Ndg. Michael R. Wambura iliomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF 
kutoa tamko kuwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA imeundwa bila kufuata Kanuni
 za Uchaguzi Ibara ya 3(2). Kamati iliridhika kuwa Kamati ya Uchaguzi ya
 DRFA iliteuliwa kabla ya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi  za wanachama wa TFF hususan, Ibara ya 3(2), hivyo uteuzi wa wajumbe wa Kamati hiyo haukukiuka Kanuni za Uchaguzi. Kamati iliitupa rufaa hiyo.
 
(iii)                Wapiga kura wa Mkutano Mkuu wa DRFA: Hoja za rufaa za Ndg. Michael R. Wambura na Ndg. Juma Jabir ziliomba
 kuyaondoa majina ya Ndg. Abeid Mziba, Ndg. Salehe Ndonga, Peter Muhinzi
 na Ndg. Daudi Kanuti katika orodha ya wapiga kura wa Mkutano Mkuu wa 
DRFA na uongozi wa wanachama wa DRFA, kwamba hawana sifa kwa mujibu wa 
Kanuni za Uchaguzi na Katiba za wanachama wa DRFA. Kamati ya Uchaguzi ya
 TFF haikupata vielelezo kuhusu hoja iliyowasisilishwa mbele ya Kamati 
na hivyokuitupa hoja hiyo ya mrufani.
 
(iv)               Rufaa dhidi ya Ndg. Mohamed Salim (Bakhressa) kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa DRFA.  Rufaa
 dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA wa kumpitisha Ndg. Amin 
Mohamed Salim (Bakhressa) kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa DRFA 
iliyowasilishwa na Ndg. Michael R. Wambura na Ndg. Juma Jabir iliomba
 jina la Ndg. Amin Mohamed Salim (Bakhressa) liondolewe katika orodha ya
 wagombea uongozi wa DRFA kwa nafasi ya Mwenyekiti, kwa kuwa hana elimu 
ya kiwango cha kidato cha nne na hivyo kutokidhi matakwa ya Katiba ya 
DRFA Ibara ya 29(2) inayotamka kwamba ‘Mtu
 yeyote anayegombea nafasi yoyote ya DRFA hana budi awe na kiwango cha 
elimu kisichopungua kidato cha nne (Academic Certificate of Ordinary 
Secondary Education).
 
Kamati
 ya Uchaguzi ya TFF ilipitia vielelezo kuhusu rufaa dhidi ya maamuzi ya 
Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na kujadili maelezo ya Warufani, Kamati ya 
Uchaguzi ya DRFA naNdg. Amin Mohamed Salim na ilijiridhisha kuwa Ndg. 
 
Amin
 Mohamed Salim (Bakhressa) hana elimu ya kiwango cha kidato cha nne na 
hivyo hakidhi matakwa ya Katiba ya DRFA Ibara 29(2). Kwa kutokidhi 
matakwa hayo ya katiba ya DRFA, Ndg. Amin Mohamed Salim (Bakhressa) 
hastahili kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa DRFA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inakubaliana na maombi ya Warufaa.
 
(v)                 Rufaa kupinga kuenguliwa kugombea Uongozi DRFA:  Ndg. Evans Elieza na Ndg. Juma Jabir waliwasilisha rufaa  wakiomba
 Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutengua uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA
 wa kuwaengua kugombea uongozi kwa madai ya kugushi sahihi ya Katibu wa 
Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA). 
 
Katika
 vielelezo mbalimbali vilivyoletwa mbele ya Kamati na baada ya kuwahoji 
warufani, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, Katibu wa KIFA, Ndg. Seif Ally Mailo aliyeshuhudia maelezo
 ya fomu za waombaji uongozi DRFA na baadhi ya waombaji uongozi ambao 
kupitishwa kwao na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kulilalamikiwa, Kamati 
ilibaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za 
uchaguzi zilizofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na pia ama KIFA au 
wagombea wenyewe.
 
Kutokana
 na mkanganyiko, maelezo yenye utata kutoka kwa warufani na warufaniwa 
na maamuzi ya utata ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA yameufanya mchakato wa
 uchaguzi wa DRFA kupoteza hadhi ya uchaguzi unaozingatia Kanuni za 
Uchaguzi na misingi ya demokrasia na uwazi kama ilivyoainishwa kwenye 
Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilijiridhisha 
kwamba:
 
·         Kamati
 ya Uchaguzi ya DRFA iliwapitisha wagombea Ndg. Gungurugwa Tambaza, Ndg.
 Mohammed Bhinda, Ndg. Benny Kisaka na Ndg. Hamisi Ayoub Mpapai bila 
kuwa na vielelezo vinavyothibitisha kuwa wana kiwango cha elimu 
kisichopungua kidato cha nne (Academic Certificate of Ordinary Secondary Education).
 
·         Hoja ya kughushi saini ya Katibu wa KIFA katika kushuhudia maelezo ya  baadhi ya wombaji uongozi, ambayo  ilitumiwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kuwaondoa kugombea uongozi waombaji uongozi watano (5)  Ndg. Hamis Ambar, Ndg. Hamisi Kisiwa, Ndg. Andrew Tupa, Ndg. Evans Elieza na Ndg. Juma Jabir  haikutumika kuwaondoa baadhi wagombea ingawa fomu za waombaji uongozi saba zilisainiwa na Ndg.  Ndg. Seif Ally Mailo.
 
·         Ndg. Seif
 Ally Mailo ambaye si mwajiriwa na si kiongozi wa KIFA hakuwa na mamlaka
 ya kushuhudia maelezo ya wagombea kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.
 
·         Kulikuwa na hali ya kumficha Ndg. Seif
 Ally Mailo aliyesaini fomu za wagombea walioenguliwa kwa kigezo cha 
kughushi saini asifike kwenye kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa maelezo 
kuhusu ushiriki wake katika mchakato wa uchaguzi wa DRFA.
 
·         Fomu
 za wagombea Ndg. Said H.Tully na Ndg. Shaffih Dauda zilizojadiliwa na 
Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na hivyo kupitishwa na Kamati hiyo 
zilichezewa (tempered-with) kwa kunyofolewa baadhi ya kurasa na kuwekwa 
kurasa zenye maelezo na saini ambazo si za Ndg. Said H.Tully na Ndg. 
Shaffih Dauda. Wagombea hao ambao walikuwa wamepetishwa na Kamati ya 
Uchaguzi ya DRFA kwa maelezo kwamba fomu zao zilikuwa zimeshudiwa kwa 
sahihi halali ya Ndg. Ndg. Seif Ally Mailo
 
 
 
walikana
 kwa maandishi na kutoa vielelezo vilivyothibitisha kwamba fomu zao 
zilichezewa na maelezo yaliyo kwenye kurasa zilizobadilishwa siyo wao 
walioyandika na kusaini.
 
·         Kamati
 ya Uchaguzi ya DRFA iliwaondoa baadhi ya waombaji uongozi kwa maelezo 
kwamba maelezo kwenye fomu za wagombea hao hayakushuhudiwa na viongozi 
vyama wanachama wa DRFA wenye mamlaka ya kushuhudia maelezo ya waombaji 
uongozi lakini bila kuzingatia matakwa hayo ya kikanuni ikawapitisha 
kugombea Ndg. Muhsin S. Balhabou na Ndg. Benny Kisaka ambao maelezo ya 
kwenye fomu zao hayakushuhudiwa na kiongozi wa chama mwanachama yeyote 
wa DRFA.
 
·         Kamati
 ya Uchaguzi ya DRFA inahusika kwa kiwango kikubwa katika ukiukwaji wa 
Kanuni na taratibu za uchaguzi na kutozingatia matakwa ya Katiba ya DRFA
 katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa DRFA.
 
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara  ya  10(6), 12(1) na 26(2) na (3):
 
(i)                   Imeifuta
 Kamati ya Uchaguzi ya DRFA. DRFA inaagizwa kuteuwa Kamati mpya ya 
Uchaguzi itakayoandaa na kutekeleza majukumu yake ikizingatia Kanuni za 
Uchaguzi za wanachama wa TFF na Katiba ya DRFA. Uteuzi wa Kamati mpya ya
 Uchaguzi ya DRFA ufanyike kabla ya tarehe 25 Oktoba 2012
 
(ii)                 Imefuta
 mchakato wa Uchaguzi wa DRFA. Mchakato wa uchaguzi utaanza upya tarehe 
29 Oktoba 2012 na uchaguzi utafanyika tarehe 08 Desemba 2012.Wagombea
 wote waliokuwa wamelipia Fomu za maombi ya uongozi (Fomu Na. 1) 
wanaokidhi sifa za kugombea uongozi kwa mujibu wa Katiba ya DRFA na 
Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF wajaze upya Fomu Na.1 bila 
kutozwa ada kwa nafasi zinazoendana na zile walizokuwa wameomba 
kugombea.