Pages

Showing posts with label Wizara ya Uchukuzi. Show all posts
Showing posts with label Wizara ya Uchukuzi. Show all posts

Thursday, July 26, 2012

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. DKT. CHARLES TIZEBA (MB) BANDARI YA DAR ES SALAAM


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi (aliyavaa suti ya mikono mifupi), Dkt. Charles Tizeba (Mb), wakati wa ziara ya siku moja katika Bandari ya Dar es Salaam leo, kulia kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. John Mngodo, aliyevaa kofia nyeupe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kupakua na kupakia Makontena (TICTS), Bw. Neville Bisett na Aliyevaa kizibao cha Kijani ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam,Bi. Winnie Mulindwa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba akifafanua jambo kwa uongozi wa Wizara, Bandari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kupakia na kupakua makontena TICTS, kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Naibu Waziri ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi Winnie Mulindwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo(aliyevaa tai ya blue), Mhandisi Omar Chambo, na Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kupakua na Kupakia Makontena (TICTS), Bw. Neville Bisett.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Charles Tizeba (Mb),akiongea na baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(hawapo pichani),wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam,Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo (wa pili kushoto),Bw. John Mngodo. Na aliyevaa Kizibao ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam,Bi. Winnie Mulindwa.
Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Winnie Mulindwa, akitoa taarifa ya namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (aliyeshika kichwa), ambaye amefanya ziara ya siku moja katika Bandari ya Dar es salaam. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo, Kulia kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Meneja Bandari Msaidizi ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi,Bi. Tumpe Mwaijande.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kupakua na kupakia makontena Bandarini (TICTS), Bw. Neville Bisett akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (Mwenye Suti ya Mikono Mifupi),wakati alipofanya ziara ya siku moja kuangalia ufanisi wa Kampuni hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam leo.Kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Bw. John Mngodo.Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe Azindua Huduma Za Safari za Anga Za Qatar Aiways Kutoka KIA Kuelekea Sehemu Mbali Mbali

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh lakizungumza machache na pia kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo mapema leo iliofanyika kwenye uwanja wa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akimpa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison zawadi ya yenye nembo ya ndege ya shirika hilo la Qatar.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar zawadi ya picha yenye kivuli cha Mlima Kilimanjaro .
Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat,Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakijadiliana jambo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika hilo aina ya Ndege namba QR546,shoto kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki
Wakuu wa uzinduzi wakipga makofi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akipiga makofi wakati kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza,shoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat

Wednesday, July 11, 2012

Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe Akutana na Viongozi wa TRL na Wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli TRAWU

Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akitambulishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kwa viongozi wa TRL na wale wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli TRAWU mara alipowasili katika Karakana ya TRL.
Waziri Mwakyembe akipata maelezo ya jinsi ya ukarabati wa mabehewa 14 unavyoendelea kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu wa kwanza kulia.
Viberenge viwili malum vikijitayarisha kuondoka kuelekea Ubungo wakati wa ukaguzi wa njia ya reli ambayo itatumiwa na treni ya abiria ya Wakazi wa jiji la Dar es Salaam inayotarajiwa kutoa huduma hapo Oktoba mwaka huu.
Baadhi ya mabehewa yanayokarabatiwa kwa ajili ya huduma ya usafiri kwa Wakazi wa jiji la Dar.
Viberenge viwili malum vikijitayarisha kuondoka kuelekea Ubungo wakati wa ukaguzi wa njia ya reli ambayo itatumiwa na treni ya abiria ya Wakazi wa jiji la Dar es Salaam inayotarajiwa kutoa huduma hapo Oktoba mwaka huu.

Popular Posts