Pages

Showing posts with label Tanzia - Msiba - Mazishi. Show all posts
Showing posts with label Tanzia - Msiba - Mazishi. Show all posts

Friday, January 4, 2013

MAZISHI YA MSANII SAJUKI


Picture
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es Salaam leo
Picture
Mke wa Rais, Mama, Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es Salaam leo Januari 4, 2013.
Picture
Picture
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani (nyumbani).
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Rais Kikwete (aliyevaa koti la kijivu, miwani na kushikamanisha vidole) akiwa na baba mzazi wa marehemu (aliyevaa kanzu) na Simon Mwakifamba (aliyevaa shati la rangi ya machungwa) na Meya wa Ilala, Jerry Slaa (aliyevaa suti nyeusi, na miwani) wakati wa shughuli ya maziko ya SaJuKi yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picture
Rais Kikwete akiwa ameshika sepetu kwa ajili ya kuliwekea udongo kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) katika shughuli ya maziko yaliyofanyika mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.
Picture
Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picture
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akiwa ni mmoja ya waombolezaji waliojitokeza katika maziko ya msanii huyo.
Picture
Rais Kikwete akijadiliana jambo na Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu nchini Simon Mwakifwamba mara baada ya mazishi kwenye makaburu ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni baba mzazi wa marehemu Mze Juma Kilowoko.
Picture
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe akifafanua jambo mbele ya baadhi ya Wanahabari kabla ya mazishi
Picture


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2H2hjTvlI

Monday, November 19, 2012

Rais Jakaya Kikwete,Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal,Waziri Mkuu Mizengo Pinda Waongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Hayati Jackson Makwetta Jijini Dar es Salaam


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kutoa heshima zao za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha maomboleza alipofika kutoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu baada ya  akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Makweta Bunju.
  Makamu wa Rais Dkt Ghalib Mohamed Bilali akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
 Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa David Msuya akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
 Spika wa Bunge Mhe Anne Makinda akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
Waziri William Lukuvi  akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali
Mke wa Rais Mama Salma akiwafariji wana familia wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali.Picha na IKULU

Thursday, September 6, 2012

MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA

Marehemu Kardinal Laurean Rugambwa enzi ya uhai wake.
Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake.

*************
MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA

Kanisa katoliki nchini dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali Laurean Rugambwa, aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la Bukoba. Maziko ya Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6 mwaka huu.

Mwili wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi barani Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo Kashozi kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa.

Akizungumza katika kipindi cha Baragumu Channel ten na baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba Askofu Methodius Kilaini , amesema wanataka kumzika kardinali Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa alilopenda kuzikiwa kutokana na kukamilika kwake, lakini kabla ya kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa, alikobatizwa, sherehe zitakazoambatana na kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa kardinali Rugambwa tarehe 7 mwezi Octoba.

"tuna alika watu wengi kuhudhuria kwenye tukio hili..., na pia tunakaribisha michango itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu kwa mchango wake,alisema askofu Kilaini.

Naye mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo , James Rugemalira, alimwelezea Kardinali Rugambwa kama mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye jamii ya watanzania, kuanzia kwenye nyanja za elimu, afya na kiroho.

Marehemu Kardinali Rugambwa ana mambo mengi ya kukumbukwa na jamii ya watanzania hususani watu wa mkoa wa Kagera hasa kwa juhudi zake za kupeleka elimu mkoani humo kwa kuagiza ujengwaji wa shule za msingi na sekondari ikiwemo shule ya kwanza ya wasichana ya Rugambwa ambayo ujenzi wake ulikuwa ni mafanikio ya marehemu huyo kuomba msaada wa ujenzi wa shule hiyo alipohutubia bunge la Ujerumani akiwa mwafrika wa kwanza.

Licha ya mambo hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha mfuko rasmi wa kumuenzi kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la Kardinali Rugambwa ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

Padre Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10 Februari,1952. Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.

Monday, September 3, 2012

MWILI WA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MKOA WA MOROGORO ASHA KIPANGULA WAWASILI MKOANI IRINGA KWA MAZISHI

Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Asha Kipangula
Jeneza likiingizwa nyumbani kwa marehemu mjini Iringa
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, John Chiligati akiagana na baadhi ya waombolezaji kabla ya mwili wa aliyekuwa Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Mayr Chipangula, kuondoka Hospitali ya Taiafa Muhimbili Dar es Salaam,jana asubuhi kupelekwa Iringa kwa ajili ya maziko.
Msafara wa kuupeleka mkoani Iringa mwili wa marahemu Asha Kipangula ukiwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro jana, ukitokea Dar es Salaam, ambapo kwenye ofisi hiyo ulisimamishwa kwa muda kutoa fursa kwa wana-CCM na waombolezaji wenmgine kuaga
Muombolezaji akiangua kilio nyumbani kwa marehemu mjini Iringa
Mmoja wa viongozi wa CCM akilia kwa huzuni baada ya mwili kufika Morogoro jana
Katibu wa CCM, Mary Chatanda akiangua kilio mwili wa marehemu Asha Chipangula ulipofikishwa nyumbani kwao Iringa jana jioni
Sheikh Mohammed Kairo akiongoza dua, mwili wa marehemu Asha Kipangula uliowasili mjini Morogoro jana
Nape akizungumza na baadhi ya waombolezaji mjini Morogoro. Aliyesimama ni Kada wa CCM, Asas
Kiongozi wa msafara, LKatibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itiladi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akijadiliana na baadhi ya viongozi mwili ulipowasili mjini Morogoro. Baadhi ya viongozi hao ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda.Picha na Bashir Nkromo

Tuesday, August 7, 2012

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEKHE MKUU WA KIJIJI CHA MSATA, BAGAMOYO, MKOA WA PWANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa familia ya Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88 pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika kumuombea dua Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88, pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88, pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.

(PICHA NA IKULU)

Tuesday, July 31, 2012

Rais Jakaya Kikwete Ahudhuria Mazishi ya Shemeji Yake mjini Lindi

Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi leo Julai 30, 2012
Rais Kikwete akishiriki katika swala ya kumuombea marehemu mjini Lindi leo Julai 30, 2012.Picha na IKULU
--
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Julai 30, 2012 amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi (45), aliyefariki Jumamosi iliyopita jijini Dar es salaam, na kuzikwa katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.

Friday, July 27, 2012

Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika Mazishi Ya Mwalimu Wa Baba Wa Taifa,Mwalimu James Irenge

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mwalimu James Irenge katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Mwisenge Mjini Musoma, Julai 26, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Tuesday, July 24, 2012

MAZISHI YA BELINDA JOSEPH MWAPINGA

Mwili wa Marehemu Belinda ukiwa umewekwa juu ya nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.
Mwili wa Belinda ukiwa katika kanisa la roman katoliki extenal.
Marehemu Belinda J. Mwapinga enzi za uhai wake.
Baba Padre akitoa heshima yake ya mwisho kwa mwili wa Belinda. J. Mwapinga jana katika Kanisa la Katoliki Extenal Dar es salaam
Joseph Mwapinga mwenye suti nyeusi akiwa na watoto wake alio achiwa na mke wake kipenzi Belinda.
Wafanyakazi wa VODACOM Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Belinda wakiufikisha katika makaburi ya Kinondoni.
Mhandisi Joseph Mwapinga akiweka shada la mauwa kwenye kaburi la Mke wake.
Baba Padre akisali sala ya mwisho kwa ajili ya kumuombea Marehemu Belinda J. Mwapinga katika makaburi ya Kinondoni.kulia kwa Padre ni Joseph Mwapinga na mwenye Tshirt nyekundu ni rafiki wa karibu wa familia, Ndugu Stephen Mapunda.

Marehemu Belinda J. Mwapinga alifariki tarehe 20/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili na mazishi yake kufanyika tarehe 23/07/2012 katika makaburi ya Kinondoni.
Hawa ni baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kwenye safari ya mwisho ya Belinda.

Popular Posts