Pages

Showing posts with label Masuala ya Elimu - Education. Show all posts
Showing posts with label Masuala ya Elimu - Education. Show all posts

Thursday, August 16, 2012

Airtel Tanzania : SHULE 93 ZA SEKONDARI KUFAIDIKA NA MRADI WA VITABU

Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanoyo kama 'AIRTEL SHULEYETU' iliyofanyika katika ofisi za Airtel na kupata shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huo. Kulia anaefuatilia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda (shoto). Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110
Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanoyo kama ' AIRTEL SHULE YETU' iliyofanyika katika ofisi za Airtel na kupata shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huo. Kulia anaefuatilia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi.
---
Airtel Tanzania, imeendeleza dhamira yake katika kuboresha elimu kwa kuchezesha droo iliyochagua shule za sekondari 93 zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel wa kusaidia jamii unaojulikana kama Airte shule yetu kwa mwaka 2012 -2013 Akiongea katika mkutano na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Airtel Kitengo cha Mawasiliano Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Mwaka huu.

Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu shule za sekondari 93, Mradi huu utafaidisha shule 3 kutoka katika kila mkoa Tanzania bara na visiwani.

Shule 93 zilizo chaguliwa leo ni matokeo ya droo iliyochezeshwa na kuzichagua shule hizo kutoka shule 3,000 zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule ambazo zina uhitaji mkubwa wa vitabu na kushauri ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule
yetu.

"Toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka saba iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa yote na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.

Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110, hivyo kila shule iliyopatikana kwenye droo hii watapata Vitabu alisema Mallya.

Bi Mallya aliongeza kwa kusema "tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zitakazoingia kwenye Mradi huu wa Shule yetu tunayatimiza kwa kuwapatia vitabu vya mitaala ya masomo yao kama ilivyopendekezwa na Wizara"

"Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuisaidia jamii hapa Tanzania hasa kwa kuchangia sekta ya elimu kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo Vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Mwaka jana pia Airtel ilisaidia Vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 104 tsh kwa shule za sekondari kwa kupitia droo iliyohusisha jumla ya shule 502" alisema Bi, Mallya.

Nae Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda aliongea kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ulimu (TEA) alisema "Mamlaka ya Elimu Tanzania tunawashukuru sana Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuinua kiwango cha elimu hapa nchini " Mradi wa Airtel Shule Yetu ni mradi mzuri sana kwa jamii yetu kwa kuinua kiwango cha elimu na maisha ya watanzania"

Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo watanzania wote pamoja na waalimu mtakaopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu tuvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini" aliongeza kwa
kusema Bw. Nyirenda

Mbali na shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huu wa vitabu mwaka huu, pia Airtel Tanzania imeshamaliza kukarabati shule ya msingi ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la DSM kando kando na barabara ya bagamoyo ilichaguliwa mwaka jana 2011 huku mipango mingine ya mwaka huu ikiendelea ili kupata shule nyingine itakayofaidika kwa kujengwa na kukarabatiwa na Airtel shule Yetu Airtel bado itaendelea kushirikiana wizara ya elimu kwa wadau wengine kuweza kushiriki katika kuinua kiwango cha elimu hapa Tanzania.

Tuesday, August 14, 2012

MJADALA WA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU 2012/2013 UDSM

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa
Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo
Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo
Kutoka kushoto ni Meneja Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli, Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo.
Baadhi ya maofisa kutoka taasisi ya HakiElimu.
Dk. Kawambwa akiwa 'live' Dar.
Bajeti ya elimu 'live' Dar.
Wadau wakiwa busy katika mjadala huo.
Wadau anuai wa elimu wakifuatilia hotuba kutoka Dodoma kabla ya mjadala.
Wadau wa elimu wakifuatilia hotuba hiyo 'live' kabla ya mjadala.
Wadau anuai wa elimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya Dk. Shukuru Kawambwa kutoka Dodoma.
----
Na Joachim Mushi, Thehabari.com

TAASISI ya HakiElimu leo jijini Dar es Salaam imewakutanisha baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walimu pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ambapo waliishuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu ikiwasilishwa ‘live’ mjini bungeni mjini Dodoma kabla ya kutoa maoni yao.

Wadau hao wa elimu kwa pamoja waliishuhudia kupitia king’amuzi bajeti ya Wizara ta Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwasilishwa ‘live’ wakiwa kwenye mkutano kisha baadaye kutoa maoni yao jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2012/13, Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo alisema ameshangaa bajeti hiyo kutouona mgomo wa walimu wa juzi pamoja na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ni tatizo kwa elimu na kuiingiza kama changamoto.

“Binafsi kati ya vitu ambavyo vimenishangaza ni bajeti hiyo kutotaja mgomo wa walimu katika bajeti iliyopita kuwa ni miongoni mwa changamoto za wizara hiyo…na hata migomo ya vyuo vikuu,” alisema Dk. Mkumbo alipokuwa akijadili katika mkutano huo.

Alisema wizara imetaja kufanya vizuri katika elimu upande wa msingi na sekondari kwa kidato, lakini imekwepa kutoa mafanikio kwa kidato cha tano na sita eneo ambalo limefanya vibaya kwa matokeo ya hivi karibuni. Alikosoa kiwango cha uwiano kati ya wanafunzi na walimu kilichotatolewa kwa sasa (1:46) kwani idadi kubwa ya walimu wapo shule za mjini huku hali mbaya ikiwa vijijini.

Aidha aliongeza kuwa wizara pia imeshindwa kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ya mara kwa mara ni changamoto hivyo kushindwa kueleza katika bajeti yake. “…karibu asilimia 80 ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu imesababishwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, lakini hili halikutajwa katika bajeti ya waziri,” alisema msomi huyo.

Kwa upande wake Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM akizungumza katika mkutano huo alisema bajeti iliyowasilishwa ni ya kawaida hivyo ni vigumu kumaliza changamoto lukuki za elimu zinazoikabili wizara hiyo.

Alisema bajeti imejivunia ongezeko la idadi ya vyuo vikuu lakini imeshindwa kuonesha ubora wa vyuo hivyo jambo ambalo ni hatari endapo litaachwa, bila udhibiti. “…Twaweza kuwa na vyuo vingi lakini suala la ubora ni tatizo lingine. Pia uandikishaji wa idadi kubwa ya wanafunzi unatakiwa kulinganishwa na waliokusudiwa kuandikishwa…maana twaweza jivunia kiwango kinapanda kumbe tunadanganywa na ongezeko la idadi ya watu,” alisema msomi huyo.

Akizungumza kwenye mjadala Meneja wa Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli alisema Serikali haiwezi kufanikisha elimu bora bila kuaandaa walimu bora katika utoaji wa elimu husika. “Huwezi kutegemea elimu bora pasipo na walimu bora, binafsi sijaona mkakati wowote mahususi wa kuboresha elimu,” alisema Shuli.

Ameishauri wizara ya elimu kujiandaa vizuri kimipango kabla ya kutekeleza mpango wa kuwa na shule ya kidato cha tano na sita kwa kila tarafa ili kuepuka madudu yaliojitokeza katika mpango wa uanzishwaji shule za kata.

Hata hivyo kabla ya kuishuhudia bajeti hiyo ikiwasilishwa Dk. Mkumbo na Mkenda wakiongozwa na mhadhiri mwenzao kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano, Ayoub Rioba waliwasilisha mada zilizokuwa zikiiangalia elimu ya Tanzania na majaliwa yake.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu tayari imewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2012/13 ambapo jumla ya sh. 724,471,937,000 ili zitumike kuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake. Huku sh. 18,561,689,000 zikiwa ni fedha za ndani na sh. 74,019,627,000 kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Friday, July 27, 2012

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA CHUO CHA NELSON MANDELA MKOANI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo na Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kwa pamoja wakifurahia mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Video unaowawezesha wanafunzi kuonana na kuzungumza na kuchangia masomo kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya mkoa huo wa Arusha, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo, kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Chuo kipya cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati leo akitembelea mazingira ya Chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni kilichopo Jijini Arusha. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati akimfafanulia kuhusu kazi za maabala mpya inayoandaliwa katika Chuo hicho wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo, kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho. Kushoto kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.

Monday, July 23, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA SECONDARY MTIPA WILAYA YA SINGIDA MJINI

Meneja Huduma kwa Jamii wa Kampuni ya Simu za Mikononi Tanzania ya Airtel, Hawa Bayuni (kushoto) akikabidhi vitabu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwakilishi wa Shule ya Sekondari
Mtipa iliyopo mkoani Singida, Bi. Mary Haiki ambaye alitembelea makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu ya Airtel jijini Dar es salaam
---
Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora nchini kote, leo imetoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari Mpita ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salam kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mtipa wilaya ya Singida mjini. Mwawakilishi wa shule hiyo ambaye ni mzawa wa eneo hilo bi Mary Hiki alikabidhiwa msaada huo wa vitabu na Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayuni. Shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilling milioni mbili.

Vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Hisabati, Phisikia, Biolojia, Kiswahili. ambapo vimekuwa na uhitaji mkubwa shuleni hapo.

Akiongea wakati wa makabithiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salaam Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayuni alisema" Airtel kwa kupitia kampeni yake ya kusaidia jamii imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule ya sekondari wilayani Singida na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hii Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza Bayuni.

Mwakilishi wa Shule hiyo bi Mary Hiki mzawa wa Singida alisema tunayo fuhara kuona Airtel inajito katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni
kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Singida anatoka graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika
kutimiza malengo tuliojiwekea.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, mwezi uliopita Airtel ilitoa msaada wa kutoa computer 4 na Vitabu vyenye dhamani ya millioni tano kwa shule ya sekondari Mazombe iliyokokilomita nne kutika Iringa mjini . Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.

Thursday, July 12, 2012

WANAFUNZI KUTOKA UN CLUBS KUIWAKILISHA TANZANIA KONGAMANO LA MANDELA AFRIKA KUSINI.


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akimkabidhi barua Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Azania Rahim Rajab ambaye ni mmoja wa kati ya wanafunzi wawili wajumbe wa UN Clubs waliochaguliwa kuhudhuria Kongamano la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela litakalofanyika Johannesburg Afrika Kusini ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 18.

Wanafunzi hao wamepewa duhamini wa Tiketi za kwenda na kurudi na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways-SAA).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akimkabidhi barua ya kuchaguliwa kushiriki Kongamano hilo Afrika Kusini Mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa Nuru Kessy ambaye ni Mwanachama wa Un Clubs.
Bw. Phillippe Poinsot (kulia) akimfafanulia Mwanafunzi Nuru Kessy kuwa katika Kongamano hilo watakutana na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali duniani wenye umri kati ya miaka 13-18 na kuwa wanahitaji kufanya utafiti kuhusiana na maisha ya Mandela ikiwemo miaka ya mwanzo, maisha yake ya jela, maisha ya uraisi kama mtu aliyepokea tuzo ya Amani ya Nobel, kustaafu kwake na mchango wake kama kiongozi maarufu duniani.
Wanafunzi hao wakitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot (kulia) na Head, Management Support Strategy and Partnership wa UNDP Ishmael Dodoo (kushoto).
Wanafunzi ambao ni wananchama wa UN Clubs wanaoelekea Afrika Kusini katika Kongamano la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Nelson Mandela kwa udhamini wa shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa UNDP. Kushoto ni Reference Assistant kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Harriet Macha, IT Associate Alice Chopeta, Head, Management Support Strategy and Partnership wa UNDP Ishmael Dodoo, Wanafunzi Rahim Rajab na Nuru Kessy, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot na Information Officer UNIC Stella Vuzo.

Tuesday, June 12, 2012

Rais Jakaya Kikwete apokea Kitabu Cha Kwanza Cha Fasihi Simulizi ya Jamii ya Wakwere

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI Dkt.Aldin Mutembei akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu cha kwanza cha fasihi simulizi ya jamii ya Wakwere ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya historia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Kapepwa Tambila. Dkt.Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti za Tamaduni lugha na fasihi za makabila ya Tanzania alikabidhi pia kamusi Asisi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiarabu.Picha na Freddy Maro-IKULU

Monday, June 11, 2012

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA WAJITOLEA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi na timu yake nzima wakati walikuja kufungua zoezi la kujitolea damu kwa hiari kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) zoezi lililoandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuoni Hapo
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe akitoa neno fupi kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma waliofika katika Zoezi la Kujitolea Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula (Wa Pili Kushoto) akiwa amesimama wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe aliyeongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma, Na Balozi Job Lusinde katika zoezi la kujitolea damu kwa hiari lililofanyika siku ya leo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na Kuandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuo Hapo.
Afisa Mahusiano wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi Beatrice alipokua akitoa damu kwa hiari katika Zoezi la Kuchangia Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo huku Akishuhudiwa na Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Manongi(Mwenye Miwani)
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao Pia Wamemaliza Muda wao rasmi leo Wakiwa katika zoezi la Uchangiaji Hiari wa Damu zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo ambalo liliandaliwa na Taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosoholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO). Kutoka Kushoto Ni Emmanuel Mwakibinga akifuatiwa na Stefano Saimon.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akiaga wanafunzi na wafanyakazi waliojitoa katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) lililofanyika chuo hapo leo.Picha Zote Na Josephat Lukaza wa
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa Wanasubiri Kwenda Kutoa damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma

Saturday, June 9, 2012

shule za kata wilayani Kilwa zimeanza kuwekeza katika maabara

Wanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari ya Kinjumbi wilayani Kilwa wakisoma kemia kwa vitendo katika maabara ya shule.Shule hii ipo rtakribani kilometa 70 toka Kilwa Masoko
Hivi ndivyo tukichanganya inatokea kwenye 'test tube'
Hii ni result ya huu mchanganyiko.Mananisikia?Mwanafunzi akiwaelekeza wanafunzi wenzake juu ya mchanganyiko alioufanya kwenye 'test tube' na reaction iliyotokea.
Majaribio ya maabara yakiendelea.wanafunzi hawa ni wa kidato cha nne na wanategemea kufanya mtihani wao wa Chemistry,Biology na Physics kwa vitendo.
Embu leye hiyo test tube.ingawa hatuna groves na miwani kwaajili ya kujikinga kama reaction mbaya itatokea.
tunaendelea hivi


Unaona inavyokuwa?Tunachanganya hivi







Chumba cha maabara ya shule ya sekondari ya Kinjumbi

Friday, June 8, 2012

KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2012

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2012

1.0 UTANGULIZI

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita 2012 yaliyotangazwa rasmi tarehe 01/05/2012. Tarehe 28/5/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipokea barua kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu yenye Kumb. Na. BSK/W/012/01 ya tarehe 22/5/2012 iliyoeleza kutoridhika na ufaulu wa watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge kwa kuwa waliona matokeo yaliyotangazwa hayakuwa na uhalisia wa uwezo wa wanafunzi. Kutokana na barua hiyo, Serikali ilifanya uchunguzi kwa kuangalia mambo yafuatayo:

• Kulinganisha alama za watahiniwa zilizojazwa katika vituo vya usahihishaji mitihani na zile zilizohifadhiwa katika Kompyuta, yaani database ya Baraza la Mitihani ili kubaini kama kuna tofauti yoyote; na

• Kulinganisha alama za somo la Islamic Knowledge zilizochakatwa na Mfumo wa Kompyuta na sampuli ya alama zilizokokotolewa kwa kutumia kikokotozi (calculator).


2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI

• Baada ya kupitia hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji wa matokeo, ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la Islamic Knowledge zilizokokotolewa na Mfumo wa Kompyuta ZILITOFAUTIANA na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi. Uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo

kwenye Mfumo wa Kompyuta ulionesha kuwa uchakataji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya “Paper” tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.

1

• Kutokana na mabadiliko ya Fomati ya Mtihani wa somo la Islamic Knowledge yaliyoanza kutumika rasmi katika Mtihani wa Kidato cha Sita 2012, mtihani huo kwa sasa una “paper” mbili na siyo “paper” tatu. Hivyo, tofauti ya alama iliyobainika imetokana na Mfumo wa Kompyuta kuendelea kutumia “paper” tatu katika kupata wastani wa alama za mwisho badala ya kutumia “paper” mbili.

3.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI

• Baada ya kugundua dosari hiyo kwa somo la Islamic Knowledge, uhakiki ulifanyika kwa masomo yao yote ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2012 yaliyokuwa na “paper” zaidi ya moja ili kujiridhisha endapo uzito sahihi ulitumika katika kupata wastani wa alama za watahiniwa. Matokeo ya uhakiki huo yalionesha kuwa alama sanifu zilizokokotolewa na mfumo wa kompyuta ni sawa na alama zilizokokotolewa na Kikokotozi. Hivyo hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo mengine.

• Matokeo ya somo la Islamic Knowledge yaliyotangazwa awali yamerekebishwa kwa kutumia Paper mbili kama inavyotakiwa ili kuendana na mabadiliko ya Fomati ya somo hilo. Marekebisho hayo yaliridhiwa na Baraza la Mitihani katika Kikao chake Maalum kilichofanyika tarehe 31/05/2012. Aidha, Kikao kati ya wajumbe wa Baraza la Mitihani na wawakilishi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu kilifanyika tarehe 31/05/2012 ambapo walielezwa kuwa Wakuu wote wa Shule wenye watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge wataandikiwa barua rasmi kufahamishwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika na barua hizo ziliandikwa tarehe 01/06/2012. Pia walifahamishwa kuwa matokeo yao yote ya masomo mengine hayana dosari yoyote na yanabaki kama yalivyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Matokeo hayo yamewekwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani na pia yatatangazwa kwenye magazeti.

• Pamoja na marekebisho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaunda Kamati ya wataalamu kuiwezesha serikali kujiridhisha zaidi na hatua zilizochukuliwa na Baraza la Mitihani ili kuepuka dosari ya aina hiyo isijitokeza tena kwa siku zijazo.

• Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya

2

Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.


4.0 HATMA YA WANAFUNZI WALIOREKEBISHIWA MATOKEO KATIKA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU

Wizara inapenda kuwahakikishia watahiniwa waliorekebishiwa matokeo yao kwamba, kwa kuwa zoezi la usajili bado linaendelea hadi tarehe 30/06/2012, waliorekebishiwa matokeo yao watapata fursa ya kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu endapo wana sifa stahiki. Aidha, kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, maombi ya mikopo hufanyiwa kazi rasmi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu kukamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu. Hivyo, hapatakuwa na athari yoyote kwa watahiniwa husika kupata mikopo endapo watakidhi vigezo vinavyotakiwa.


5.0 HITIMISHO

• Napenda kuhitimisha kwa kuwasihi wazazi, walezi, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa na imani na Baraza la Mitihani la Tanzania kama chombo chetu chenye dhamana kisheria ya kuendesha mitihani nchini. Hapakuwa na hujuma yoyote iliyofanyika kwa watahiniwa ambao matokeo yao yamerekebishwa. Kosa lililojitokeza ni la kibinadamu, halikufanywa kwa makusudi wala kwa lengo lolote la kuhujumu kundi fulani la watahiniwa. Marekebisho yameshafanyika na matokeo stahiki yameshatolewa. Aidha, uhakiki uliofanyika kwa masomo yao mengine unaonesha kuwa hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo yote.

• Kutokana na dhana ya baadhi ya watu kuwa kunakuwa na upendeleo kwa baadhi ya watahiniwa wa makundi fulani katika usahihishaji

napenda kuwakumbusha kuwa wakati wa mitihani, watahiniwa
huandika namba zao za mitihani na siyo majina. Katika taratibu za

usajili wa Baraza la Mitihani hakuna kipengele chochote kinachomtaka mtahiniwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa. Vilevile, utaratibu unaotumika kuwapata wasahihishaji huzingatia uwezo wao kitaaluma na uzoefu kazini. Aidha, katika fomu ya mapendekezo ya uteuzi wa wasahihishaji hakuna mahali popote ambapo Mkuu wa Shule hutakiwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa ya mwalimu

anayependekezwa kusahihisha mitihani.


• Utaratibu unaotumika kusahihisha mitihani hautoi mwanya wa upendeleo. Katika kudhibiti uwezekano wa kupendelea mtu yeyote kila msahihishaji husahihisha swali moja tu na kisha humpatia msahihishaji mwingine asahihishe swali linalofuata. Aidha, kila msahihishaji hutakiwa kuweka vifupisho vya majina yake (initials) ili ufuatiliaji uweze kufanyika kadri itakavyohitajika. Pia uhakiki wa usahihishaji hufanyika kwa lengo la kujiridhisha na usahihi wa kazi na kuhakikisha kuwa kila mtahiniwa amepata alama anazostahili. Dosari zinazobainika zimekuwa zikirekebishwa katika mchakato wa usahihishaji na wasahihishaji wanaobainika kuhusika na dosari hizo wamekuwa wakichukuliwa hatua stahiki mara zinapobainika.

• Pamoja na hayo niliyoyaeleza nina taarifa kuwa yanapangwa maandamano ambayo yanalenga suala hili hili la kutoridhika na matokeo ya awali ya somo la Islamic knowledge. Kwa kuwa suala hili limeshapatiwa ufumbuzi, nawasihi wananchi wajiepushe kushiriki maandamano hayo kwa sababu suala la msingi lililo wafanya watake kuandamana limeshatolewa maelezo. Hivyo, maandamano hayo hayatakuwa na tija.

IMETOLEWA NA DKT SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAREHE 07/06/2012

UZINDUZI WA KITABU CHA 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING)

Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya akitoa neno wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING) kilichoandikwa na Hopolang Phororo kinachozungumzia Mateso na manyanyaso ya wasichana wadogo wakati wa malezi yao na haki ya msingi ya jinsia ya kike katika jamii.
Mmoja wa washiriki wa uzinduzi huo Bi. Chansa Kapaya akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Hopolang Phororo na haki za msingi za wanawake wanaokutwa na matatizo ya unyanyasaji wa Kijinsia Tanzania.
Mtunzi wa Kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' Bi. Hopolang Phororo akielezea simulizi ya kweli iliyomkuta kama mwathirika wa unyanyasaji wa Kijinsia wakati wa usichana wake na moyo, uvumilivu aliokuwa nao wa kuweka uzoefu huo katika maadishi ili jamii ijifunze na madhara ya unyanyasaji wa Kijinsia unaokua kwa kasi nchini Tanzania.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho akitoa nasaha zake wakati uzinduzi rasmi wa kitabu hicho jijini Dar es Salaam. Alisema 66% ya wanawake na 20% ya wanaume nchini wameshawahi kukutwa na majanga ya unyanyasaji wa Kijinsia katika maelzi yao ambapo kwa sasa Dar es Salaam na Mbeya zinaongoza.
Mgeni rasmi Dkt. Mrisho na Mtunzi wakionyesha Kitabu kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari. Kitabu hiki kinapatikana katika Maduka ya MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS yaliyopo jijini Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi 10,000/=.
Jopo la Wataalam wa Mambo ya Jinsia Tiba na Vitabu wakiwa kwenye picha pamoja.
Mkurugenzi wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Mzee Bugoya akibadilishana mawazo na Dkt. Mrisho pamoja na Bi. Kapaya wakati wa uzinduzi
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo baada ya uzinduzi.

Popular Posts