Pages

Showing posts with label Vodacom. Show all posts
Showing posts with label Vodacom. Show all posts

Monday, January 7, 2013

Vodacom Tanzania yasaidia Sober House Pemba


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa Mratibu wa Vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo (Sober House) za Wete Pemba Abdulwaheed Said kwa niaba ya Vodacom Foundation. Wanaoshuhudia ni Menejja wa Vodacom Foundation Grace Lyon Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kushoto). Hafla hiyo ilifanyika wkishoni mwa wiki Chakechake Pemba.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi dumu la dawa ya kusafishia choo kwa Meneja wa kituo cha kutibu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) cha Mjini Chake Chake Kisiwani Pemba Mohammed Kassim. Wanaoshuhudia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kulia) na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa pili kushoto). Vodacom Foundation imevipatia vituo vinne vya Wete na Chakechake vyakula na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya program yake ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Mratibu wa vituo vya kutibu watumiaji wa dawa za kulevya kuacha kutumia dawa hizo (Sober House) vya Wete Pemba Abdulwaheed Said akishukuru kwa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kutoka Vodacom Foundation vilivtolewa kwa Sober House nne za Kisiwani Pemba. Kutoka Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa,Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon. Meneja wa Sober Hosue ya Chakechake Mohammed Kassim na Meneja wa Mahusiano ya Nje Salum Mwalim.Mkabidhiano hayo yamefanyika kwmishoni mwa wiki Mjini Chakecahke 04.
  Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kulia) akishiriki chakula cha mchana na mateja wanaopata tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya katika Sober House ya Chakechake Pemba. Chakula hicho kiliandaliwa na Vodacom Foundation.
Sehemu ya watu wanaopata tiba ya kuachana na matumiz ya dawa za kulevya katika Sober House za Wete na Chakecahke Kisiwani Pemba wakimsikiza kwa makini Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(hayupo pichani)akizungumza nao wakati Vodacom Foundation ilipofika kituoni hapo kusaidia vyakula na vitu mbalimbali mwishoni mwa wiki. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa 06.
--
Vodacom mwishoni mwa wiki imetembea vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na dawa hizo - Sober House Kisiwani Pemba ziara iliyomjumuisha Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa.

Ziara hiyo ililenga kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo vyakula na vitu vingine vya matumizi ya ndani ikwemo dawa za kusafishia vyoo, sabuni katika kwa Sober House nne zilizopo Chakechake na Wete.
Akizungumza katika Sober House ya Chakechake Waziri Profesa Mbarawa aliwataka wateja wa vituo hivyo ambao wengi wao ni vijana kuhakikisha matumaini waliyoyaonyesha ya kutaka kuachana na matumzi ya dawa za kulevya hayapotei.

Waziri Prof Mbarawa amesema uamuzi waliouchukua wa kutaka kuachana na matumiz ya dawa za kulevya ni wa msingi na unawawezesha kurudi katika maisha yao ya kawaida sanjari na kutimiza ndoto za maisha walizokuwa nazo hapo kabla ya kujitumbukiza katika matumizi ya adwa za kuelvya na kuwapotezea dira ya maisha "Nimejulishwa kwamba kuingia katika nyumba hii ni lazima mtumiaji mwenyewe ukubali kuwa yupo tayari kuachana na dawa kulevya hilo ni jambo jema na linalonyesha kwamba mnayo matumaini ya kurudi katika maisha ya kawaida yasiyohusisha matumizi ya dawa za kulevya na aina nyengine ya vilevi."Alisema Prof. Mbarawa "Mnayo mifano ya mafanikio ya wale ambao wameshapitia program hizi na wamefanikiwa na hata nyie hapa mpo ambao tayari mna siku nyingi za usafi bila kutumia dawa ama kilevi cha aina yoyote hivyo ni rai yangu kwenu kuendelea kuamini katika matumaini mliyo nayo."Aliongeza Profesa Mbarawa Akizungumzia juhudi za serikali katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya nchini Waziri huyo amesema serikali imekuwa ikifanya kila juhudi katika kukomesha biashara hiyo.

"Serikali na hata Rais Kikwete(Jakaya)binafsi amekuwa akifanya juhudi kubwa katika kukomesha biashara hii na amekuwa akitukalisha chini mawaziri na kutuelezea mikakati mbalimbali ikiwemo kutuonesha mikanda ya video inayoonyesha athari za dawa za kulevya ambazo zinasikitisha mno."Alisema Waziri Prof Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema changamoto kubwa inayokabili vita hii ni namna ya kukamalisha udhibiti dhidi ya mhalifu au washukiwa wanaojihusisha na biashara hizi haramu ili kuwafikisha mahakamani na hatimae sheria kuchukua mkondo wake lakini hata hivyo juhudi zipo na kuwaomba wateja hao wanaopata nafuu kutoa ushirikiano huku akkiwapongeza Vodacom.

"Nawapongeza sana Vodacom kwa kufika hapa na kuwasaidia vijana hawa ambao bado wanaweza kuwa na mchango mkubwa kwa taifa.Mimi ni mara yangu ya kwanza kutembelea Sober House, nimeguswa na naahidi kuwaleta wadau zaidi kusaidia nyumba hizi ili kazi inayofanyika humu iimarike na kutoa mchango zaidi katika mapambanao dhidi ya dawa za kuelvya nchi."Alisema Prof. Mbarawa Awali Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon alisema Vodacom imefika katika nyumba hizo ikitekeleza kwa vitendo dira yake ya kusaidia makundi yenye uhitiji kupitia program ya Pamoja na Vodacom inayotekelezwa kwa michango ya wafanyakazi na kampuni.

"Hatukifika hapa kwa bahati mbaya tunajua kazi kubwa inayofanyika katika nyumba hizi na kwa makusudi tumezijumiisha katika makundi yakunufaika na program yetu ya Pamoja na Vodacom ili kuunga mkono kazi hiyo na kuonesha upendo wetu kwenu."

"Tatizo la dawa za kulevya sio la mtu mmoja linatugusa sote kama sio ndani ya familia basi kuna ndugu, jirani au hata rafiki."Alisema Lyon na kuongeza "Wito wangu mkubwa ni kuwaomba kujitahidi kuhakikisha hamrudii kutumia dawa za kulevya na aina nyengine za vilevi mara mnapokamilisha matibabu yenu na kurudi uraiani."

Kwa upande wake Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom amepongeza utayari wa wale ambao walikuwa watumiaji kabla ya kuacha na kuona umuhimu wa kusaidia wenzao ili nao waache na kurudi katika maisha mema na masafi.

"Waanzilishi wa nyumba hizi(Sober House) ni watu wenye ujasiri na upendo mkubwa katika jamii wameliona tatizo na wamekuwa tayari kutoa ujuzi, nguvu, mali na muda wao kusaidia wengine, naamini hii ni silaha moja muhimu katika mapambano dhidi ya dawa kulevya nchini."Alisema Mwalim Wakizungumza kupitia risala yao iliyosomwa kwa niaba yao na Abdala Hassan watu hao walio katika tiba maarufu wateja wanaopata nafuu wamesema haikuwa rahisi kwao awali kuamini kuwa wangeweza kubadilika na kurudi katika maisha ya kawaida ya kutotumia dawa za kulevya.

"Na sisi tulio mele yenu ni wateja tunaopata nafuu kwa hiari zetu bila ya kulazimishwa na mtu yeyote tumeamua kubadilika kutoka janga la dawa za kulevya baada ya kuchoshwa na hali za kudhalilika,kupoteza utu wetu, kutoheshimiwa, kuwa mzigo katika familia na jamii."Alisema Hassan "Ni kweli tulikuwa hatuna maadili mema kila mmoja ana historia yake ya nyuma. Tuna shukrani kubwa kwa waasisi wa umoja huu wa N.A (Narcotics Anonymous) na Sober House kwa sababu sasa tunaishi kwa amani, upendo, utulivu bila kufanya uhalifu wa aina yoyote na tunamatumaini na matarijio ya kurejea kuwa wazalishaji bora katika jamii."Aliongeza Hassan Katika kisiwa cha Pemba zipo jumla ya Sober House tano zilizo chini ya uongozi na usimamizi wa watu binafsi ambazo Vodacom Foundation ilizipatia chakula na mahitaji mengine.Hata hivyo warataibu wa Sober House wameiomba seriklai kuzitupia macho na kuziwezesha.

Vodacom Foundation iliandaa pia chakula cha mchana kwa ajili ya wateja wanaoptaa nafuu walio katika vituo hivyo mlo ambao ulimhusisha pia waziri Profesa Mbarawa na wafanyakazi wa Vodacom waliotembelea.
Mwisho.

Monday, November 12, 2012

VODACOM YATOA MIKOPO YA MWEI KWA AWAMU YA PILI BUIGIRI DODOMA


Mwanachama wa kikundi cha Upendo katika kijiji cha Buigiri mkoani Dodoma, Diria Yaledi  Mtumwa (kushoto) akihesabu  fedha  baada ya kukabidhiwa ikiwa ni mkopo unaotolewa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Mikopo ya jumla ya kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 17 ilitolewa kwa wanawake wa Buigiri  kwenye makabidhiano hayo  ya awamu ya pili ya mikopo ya MWEI yalifanyika  jana kijijini Buigiri mkoani Dodoma jana .
Mwanachama wa kikundi cha Upendo katika kijiji cha Buigiri mkoani Dodoma, Diria Yaledi  Mtumwa (kushoto) akipokea fedha ikiwa ni mkopo unaotolewa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Mikopo ya jumla ya kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 17 ilitolewa kwa wanawake wa Buigiri na kukabidhiwa na Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon (kulia) huku  Afisa wa Vodacom Ally Mbuyu (wa pili akishuhudia). Makabidhiano hayo  ya awamu ya pili ya mikopo ya MWEI yalifanyika jana kijijini Buigiri mkoani Dodoma jana.
Mwanakijiji wa Buigiri mkoani Dodoma Nyendo Yohana Chisoma akihesabu fedha  baada ya kukabidhiwa ikiwa ni mkopo unaotolewa na kampuni ya Mawasiliano ya  Vodacom Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Mikopo ya jumla ya kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 17 ilitolewa kwa wanawake wa Buigiri  kwenye makabidhiano  hayo  ya awamu ya pili ya mikopo ya MWEI yalifanyika jana kijijini Buigiri mkoani Dodoma .
Wanakijiji Buigiri mkoani Dodoma wakipata malekezo kutoka kwa Meneja wa Vodacom Foundation,Grace Lyon (kulia) juu ya  mikopo inayotolewa  na Vodacom kupitia mpango wake wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Mikopo ya jumla ya kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 17 ilitolewa kwa wanawake wa Buigiri  kwenye makabidhiano hayo  ya awamu ya pili ya mikopo ya MWEI yalifanyika  jana kijijini Buigiri mkoani Dodoma jana.

Thursday, November 8, 2012

VODACOM WAKISHIRIKIANA NA BUSINESS PARTNER WAKE FTS SERVICES LTD WAWAPELEKA WATEJA WAO KISIWA CHA MBUDYA KILICHO BAHARI YA HINDI


Hapa ndio Kisiwa cha Mbudya ambapo Vodacom imewapeleka wateja wake kwa ajili ya mapumziko ya week end jumamosi ya jana.
Wateja na wafanyakazi wa vodacom
Kushoto ni Steve Goyayi kutoka Stanbic Bank, wa tatu kutoka kushoto Asubisye Mwakatobe kutoka Vodacom na wengine ni baadhi ya wageni washiriki kutoka world Bank
Katikati ni Abdallah Singano kutoka Stanbic na kulia ni CEO wa MSD
Kutoka kushoto Steve Goyayi, Henry Kapinga na Abdallah Singano
Baadhi ya wafanyakazi kutoka Vodacom 
Kushoto ni Idd Mbita Mkurugenzi wa FTS Services akiwa na Joseph Kusaga CEO wa Clouds FM na TV mwenye Tshirt ya kijani.
Wateja na wafanyakazi wa vodacom wakishuka kwenye boti maalum iliyokodiwa kwa ajili yao.
Kulia ni Henry Kapinga meneja mauzo wa FTS Services ltd akipiga picha ya kumbukumbu na CEO wa Clouds Joseph Kusaga
Wadau kutoka Vodacom wakipata vinywaji ndani ya kisiwa cha Mbudya
Rosalynn kutoka vodacom akiwashukuru wateja kwa kushiriki
Idd Mbita kutoka FTS Services akiwashukuru wateja kwa kushiriki na kuwaomba tudumishe ushirikiano wetu.
Vodacom Tanzania wakishirikiana na Business Partner wake FTS Services jana waliwapeleka wateja wao katika Kisiwa cha Mbudya kilicho katika bahari ya Hindi.

Tuesday, September 11, 2012

Vodacom Tanzania na TFF zasaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu kwa miaka mitatu

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,Rene Meza akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi , Said Abeid mkataba wa udhimini wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara,katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,Rene Meza akimfafanulia jinsi mkataba ulivyo wa udhamini wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ,Said Abeid,katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam,wanaoshuhudia wapili toka kushoto Makamu wa pili wa Rais wa TFF, . Nasibu Nyamlani,Ofisa Mkuu wa maswala ya Sheria wa Vodacom Bw.Wallarick Nittu.
--
. Klabu ya Simba Sports Club ndio bingwa mtetezi.
.Msimu wa ligi kuanza Septemba 15, na kushirikisha timu 14.
. Polisi Morogoro, Tanzania Prisons na Mgambo JKT ni timu mpya katika ligi.
-
Dar es Salaam, 11 Septemba, 2012…….
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo limeingia katika mkataba wa udhamini kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wakati maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania yakielekea ukingoni.
Kampuni ya Vodacom imekuwa mdhamini wa ligi kuu kwa miaka mitano iliyopita, na sasa imeingia mkataba mpya wa udhamini kwa miaka mitatu na TFF, mkataba utakao liwezesha shirikisho hilo kupoea fedha za udhamini kwa miaka mitatu.
Ligi kuu ya Vodacom itaanza tarehe 15 ya mwezi huu, ikitarajia kushuhudia michezo 182 ikichezwa katika viwanja mbalimbali na kushirikisha timu 14, zikiwemo timu za Dar es Salaam Young Africans, Kagera Sugar na Simba Sports Club ambaye ndie bingwa mtetetzi wa kombe hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema kuwa kampuni ya Vodacom iko katika mstari wa mbele katika kuunga mkono maendeleo na shughuli mbalimbali za kimichezo ndani ya nchi.
“Wanamichezo wote ni mabalozi wazuri katika nchi. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunawaunga mkono katika kutambua na kukuza vipaji vyao kadri tutakavyo weza,” alisema Meza na kuongeza kuwa, “Kama jina linavyojulikana ligi kuu ya Vodacom, kombe hili linashuhudiwa na mashabiki zaidi ya milioni 10 katika mechi 182 zitakazo chezwa sehemu mbalimbali za Tanzania bara.”

Meza amejivunia kampuni hiyo kuwa wadhmini wa ligi kuu kwa kipindi kingine, na kufafanua kuwa mpira wa miguu ndio unaongoza kitaifa na unapendwa na Watanzania wengi.
Michuano ya mwaka huu itashuhudia timu mpya tatu ambazo ni timu ya Polisi Morogoro, Tanzania Prisons na Mgambo JKT. Mkataba huu umehusisha pande zote ambazo ni kampuni ya Vodacom Tanzania, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kamati ya ligi.

Kwa upande wake makamu wa Rais wa TFF, Nasibu Nyamlani, ameipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania akisema kuwa anaamini kuwa maendeleo ya sasa yatalenga zaidi katika kuunga mkono vipaji vipya na vilivyopo ndani ya nchi.

“Kwa niaba ya TFF, napenda kuwashukuru Vodacom Tanzania kwa kuonyesha nia na kuendelea kuunga mkono mpira wa miguu nchini. Nasi tunaahidi kuendelea kuthamini vipaji vya wachezaji wetu na kuhakikisha tunapata mafanikio zaidi,” alisema Nyamlani.
Mwisho …

Tuesday, August 14, 2012

VODACOM TANZANIA RAMADHAN CARE & SHARE MKOANI LINDI

Baadhi ya watoto wa shule ya Msingi ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini wakiwa wamebeba mfuko wa sembe mara baada ya kukabidhiwa msaada huo na Mkuu wa Kitengo cha odacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule hayupo pichani ikiwa ni mwendelezo wa kutoa misaada na kufuturisha watoto yatima na wasiona katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa kupitia kampeni ya Ramadhan Care and Share wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi Wilaya ya Lindi Bi.Mnyangala Kaguta akipokea msaada wa mbuzi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule kwa niaba ya watoto walemavu wasiona na wanaoona wa shule ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi mbuzi wawili Bi.Rafael Mohamed kwa niaba ya wakina mama wenzake ambao ni walemavu wasioona wa kijiji cha Mnamba kata ya Nyangao Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,anaeshuhudia wapili toka kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula John Swai kwa niaba ya watoto wenzake ambao ni walemavu wasiona na wanaoona wa shule ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini Mkoani humo,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,alieshikilia mbuzi kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi katoni ya chumvi Mtoto mwenye ulemavu wa kutokuona Husna Rajabu, kwa niaba ya watoto wenzake ambao ni walemavu wasiona na wanaoona wa shule ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,alieshikilia mbuzi kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon akisalimiana na baadhi ya wakina mama ambao ni walemavu wasioona wa kijiji cha Mnamba kata ya Nyangao Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi ya watoto ambao ni walemavu wasioona wakifuturu wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Meneja Mahusiano ya umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu akiteta jambo na baadhi ya watoto ambao ni walemavu wasioona wa shule ya msingi Nyangao Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa shuleni hapo kwa ajili ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Wednesday, August 8, 2012

Vodacom Tanzania Yazindua Kinyang’anyiro Cha Watengeneza Programu Wa Kujitegemea

Vodacom yazindua mashindano mapya kwa watengenezaji wa programu wa kujiteg emea. Mashindano yatatoa fursa kwa watengenezaji hao kuonyesha vipaji vyao.Mashindano kuwa katika awamu mbili, ndani na nje ya nchi.

Mshindi kupata dola 20,000. zaidi ya shilingi Milioni 30 za kitanzania. Dar es Salaam, Waendelezaji wa programu za kiteknolojia wa Tanzania sasa watapata fursa ya kuonesha vipaji vyao katika mashindano yaliyo anzishwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, yaliyopewa jina la AppStar Challenge.

Mashindano hayo yameanzishwa ili kuwapa motisha washiriki ambao wanaendeleza ubunifu wa kiteknolojia katika simu na mawasiliano na kutoa nafasi kwa washiriki kuonyesha uwezo katika kuvumbua vifaa mbalimbali vya kiteknolojia ambavyo vinaweza kutumika katika nchi zinazoendelea na kutatua matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii.Washindi watakao patikana katika mashindano ya awali ndani ya nchi husika, watapata fursa ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Afrika ya Kusini mwezi Novemba mwaka huu.

Nchi zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na, Misri, Lesotho, Tanzania, Afrika ya Kusini na Qatar.Katika mashindano ya ndani, washiriki wanatakiwa kuendeleza ubunifu katika vipengele mbalimbali kama michezo, afya ya jamii, burudani, na simu.

Mshindi mmoja katika kila kipengele atapata dola 2000 za Marekani, na baada ya hapo kwa mshiriki ambaye atakuwa ametoa programu bora atapata nafasi ya kushiriki katika michuano ya kimataifa.Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, maombi yatawekwa na kusambazwa kupitia Hifadhi ya programu ya Vodacom na Vodafone na watu binafsi kuendelea kukusanya hadi mwisho wa muda wa kuwakilisha.

Twissa alibainisha kuwa mshindi wa awamu ya kwanza ambayo inalenga Watanzania tu, atadhaminiwa na Vodacom kushiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayo fanyika Afrika ya Kusini. “Awamu ya kwanza ni ya mashindano ya ndani na watengenezaji wa programu wanatarajiwa kuanza kujisajili kwa ajili ya mashindano kuanzia tarehe 7 mwezi 9 mwaka 2012 na wataweza kuziendeleza na kuzichapisha programu zao kwenye hifadi ya programu ya Vodacom,” alifafanua Twissa.

Alibainisha kuwa wakati wa michuano ya kimataifa, programu mbili zitakazoshinda zitapelekwa katika mchujo utakaofanywa na jopo la wataalam wa kimataifa wa masuala ya teknolojia kutoka Vodacom, zaidi ya hayo, wabunifu watapata nafasi ya kuonyesha kazi zao kwa njia ya vitendo mbele ya jopo la majaji.

“Mashindano haya yatamuwezesha mshidi kupata zaidi ya Dola elfu 20000 za Kimarekani. Tunajivunia kuwa sehemu ya mashindano haya makubwa. Ninaamini kuwa yatatoa nafasi kwa watengenezaji wa programu kuonyesha kile walichonacho, na ninatoa wito kushiriki katika mashindano haya na tunawatakia kila la kheri,”


Saturday, August 4, 2012

VODACOM TANZANIA WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA MTWARA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalila akisalimiana na ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh,wakati alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumuelezea mikakati mbalimbali ya Vodacom ya kusaidia jamii hususani elimu na vikundi mbalimbali vya wanawake mkoani humo,Ofisa huyo yupo mkoani humo kwa ajili ya kampeni ya Ramadhan Care & Share inayolenga kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule na katikati ni Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalila akisisitiza jambo kwa ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh(kushoto)wakati walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumuelezea mikakati mbalimbali ya Vodacom kusaidia jamii hususani elimu na vikundi mbalimbali vya wanawake mkoani humo,Ofisa huyo yupo mkoani humo kwa ajili ya kampeni ya Ramadhan Care & Share inayolenga kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,katikati ni Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalila akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumuelezea mikakati mbalimbali ya kampuni yao ya kusaidia jamii hususani elimu na vikundi mbalimbali vya wanawake mkoani humo,wafanyakazi hao wapo mkoani humo kwa ajili ya kampeni ya Ramadhan Care & Share inayolenga kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,kutoka kushoto Meneja Mahusiano ya umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu.Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule,Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh,Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalila akimsikiliza ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh(kushoto)akiongea wakati alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumuelezea mikakati mbalimbali ya Vodacom ya kusaidia jamii hususani elimu na vikundi mbalimbali vya wanawake mkoani humo,Ofisa huyo yupo mkoani humo kwa ajili ya kampeni ya Ramadhan Care & Share inayolenga kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,katikati ni Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalila akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumuelezea mikakati mbalimbali ya kampuni yao kusaidia jamii hususani elimu na vikundi mbalimbali vya wanawake mkoani humo,wafanyakazi hao wapo mkoani humo kwa ajili ya kampeni ya Ramadhan Care & Share inayolenga kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,kutoka kushoto Meneja Mahusiano ya umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu.Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule,Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh,Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja.

Popular Posts