Pages

Showing posts with label TBL Tanzania Breweries Limited. Show all posts
Showing posts with label TBL Tanzania Breweries Limited. Show all posts

Tuesday, June 26, 2012

TBL YAKAGUA MRADI WA MAJI WA SH. MIL. 25 GEITA

Mkandarasi wa mradi wa visima vya maji, Enock Kangasa akisukuma pump ya moja ya visima vya maji mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie (kushoto), kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa gharama ya sh. milioni 25 katika Kijiji cha Mkolani I, wilayani Geita juzi.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (aliyeweka miwani kifuani) akifurahia jambo wakati Mkuu wa Wilaya ya Geita , Manzie Mangochie akijaribu moja ya pump ya visima vya maji katika mradi unaojengwa kwa sh. milioni 25 na TBL katika Kijiji cha Mkolani I, Geita, viongozi hao walikwenda kukagua mradi huo juzi
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie, akisistiza jambo wakati akikagua juzi mradi wa visima vya maji unaotekelezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kijiji cha Mkolani I wilayani Geita, Katikati ni Mhandisi wa Maji wilayani Geita, Enock Kangasa Mradi huo umegharimu milioni 25.

Monday, June 25, 2012

WAJASILIAMALI 16 KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM WAKABIDDHIWA RUZUKU ZA SAFARI WEZESHWA.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam akimkabidhi Mjasiliamali, Catherine Urio Cherahani wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam akimkabidhi Mjasiliamali, Elizabeth Chami Mashine ya kutengenezea keki inayotumia gas na umeme wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Ofisa mauzo wa Kanda wa TBL Victo Kavishe.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam akimkabidhi Mjasiliamali, Christabela Lyimo Compresor ya kupakia rangi inayotumia wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

Popular Posts