Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu ombi lililotolewa na Katibu wa Tamico 
(Geita) kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu mafao 
  ·         Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na 
Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 
Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na 
imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini 
mwetu bila kubagua sekta yoyote ile. 
  ·         Kwa mujibu wa marekebisho hayo mafao ya kujitoa (withdrawal 
benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa 
yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko 
atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu  kwa hiari (miaka 
55) au kwa lazima (miaka 60). 
  ·         Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili 
kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa 
mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya 
uzeeni  wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya 
kujitoa yanapunguza kama si kuondoa kabisa kinga hii ya mfanyakazi 
anapofika uzeeni. 
  ·         Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao 
ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa 
kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu 
tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu 
kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena 
muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na 
Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika 
  ·         Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi 
kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi 
watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa 
hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. 
Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya 
wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi 
na waajiri ili kupata maoni yao. 
  ·         Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama 
yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. 
  Imetolewa na Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii. 
  KWA UFAFANUZI HUU TOKA MAMLAKA HUSIKA, 
  (i) Hakuna shaka kwamba sheria tayari imeaanza kutumika. 
  (ii) Hakuna shaka kwamba Bunge na Serikali wamekaa kimya kwa sababu wanajua 
kwamba sheria waliyotunga na kupitisha ni pigo kwa wafanyakazi hawa wa 
sekta binafsi hasa ukizingatia kwamba 
  - sekta binafsi ndo wachangiaji wakubwa wa mifuko hiyo. 
  - Usalama wa Ajira wa wafanyakazi wa sekta binafsi ni asilimia zero maana 
waajiri wamekuwa wakiwafukuza kama Popo au senene.serikali hajaiweka kinga 
madhubuti kwa wafanyakazi hawa.sheria ya kazi iliopo inawasaidia zaidi 
waajiri. 
  - Mazingira ya kazi kwa sekta binafsi sio rafiki kwa afya na usalama wa 
wafanyakazi.Hivi unategemea kijana aliye na miaka 25 kwa sasa na anafanya 
kazi migodini,viwanda vya chuma,Ujenzi NK afanye kazi hadi astaafu kwa 
mazingira haya? NADHANI HUU NI UVIVU WA KUFIKIRI KWA WATU TULIOWAPA DHAMANA 
KUBWA NA HILI NASEMA HALIKUBALIKI HATA KIDOGO!!!!!!!!!!!!!!!!! 
  NINI KIFANYIKE? 
  TUNASUBIRI MAJIBU TOKA SERIKALINI NA BUNGENI 
  Kama kweli wametunga na kupitisha sheria hii kandamizi,nasema kitu hiki 
hakikubaliki hata kidogo.Nguzo ya wafanyakazi ni UMOJA NA 
MSHIKAMANO.Wafanyakazi wote sekta binafsi tutapiga kura ya maoni kukataa 
sheria hii kisha tutapeleka suala hili mahakamani na iwapo mahakama itaamua 
ndivyo sivyo nadhani hatua itakayofuata ni kuprotest against this ACT. 
  Nimeguswa sana na Jambo hili kwa sababu Sheria hii imetungwa kukandamiza 
masilahi ya wafanyakazi wanyonge wa nchi hii na kwa pamoja tutahakikisha 
sheria hii inafutwa hata kama watatu Kolimba,mwakyembe,ulimboka NK. 
  MSHIKAMANO DAIMA - SOLIDARITY  FOREVER 
  Benjamin Daudi Dotto 
  Katibu wa Tamico wilaya ya Geita, 
  SLP 335, 
  Geita – Tanzania. 
  Simu: ofisi +255 774 866635 
  Simu:mkononi + 255 767 715116 alt.+255 784 715116