Pages

Showing posts with label Kagame Cup - Kombe la Kagame. Show all posts
Showing posts with label Kagame Cup - Kombe la Kagame. Show all posts

Tuesday, July 31, 2012

TAMKO LA TASWA KUHUSU WAANDISHI KUNYANYASWA KATIKA MASHINDANO YA CECAFA


TAMKO LA TASWA KUHUSU CECAFA

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), kimesikitishwa na hatua ya Baraza la Michezo la Vyama vya michezo la Afrika Mashariki (CECAFA), kuwanyanyasa na kuwadhalilisha waandishi wa habari na wapiga picha katika mchezo wa fainali Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Kufuatia kudhalilishwa huko kwa waandishi katika fainali hiyo ya michuano ya kombe la Kagame kati ya Yanga na Azam, TASWA imelaani kitendo hicho na kuwaondolea utu, udhalilishaji na unyanyasaji kulikosababishwa na baadhi yao kutandikwa makofi na askari polisi mithiri ya vibaka.

Waandishi wa habari za michezo wa Tanzania wamekuwa wasikivu, waadilifu na watu wanaofuata taratibu, lakini katika fainali hiyo mara baada ya mchezo walifanyiwa vitendo ambavyo havikulingana na tabia yao.

Lengo la waandishi si kuleta vurugu bali kuhakikisha wananchi wanapata habari kwa kila tukio lilikuwa linatokea uwanja, badala yake walionekana hawana thamani mbele ya jamii inayowawakilisha.

TASWA inalaani kitendo cha Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye kwa kutoa agizo kwa polisi kuwazuia waandishi kuingia uwanjani kumalizia kazi zao za kuhoji makocha na wachezaji, hali iliyosababisha vurugu.

CECAFA walijenga urafiki wa karibu na waandishi kipindi chote cha mashindano hayo na Kagame kwa lengo la kuyatangaza , lakini mwisho wa yote walionekana kama taulo la deki limekuwa na thamini pale ambapo linahitajika kwa deki, lakini baada ya hapo halina thamani tena.

Lakini TASWA inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, kufuatia baadhi ya waandishi kuonesha utovu wa nidhamu kama baadhi ya viongozi wa TFF na CECAFA walivyodai kuwa walionesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kutoa maneno ya kashfa na kutaka kumpiga Musonye

Kufuatia hatua hiyo TASWA imechukua maamuzi yafuatayo
1.Kutoandika jambo lolote linahusu Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki (CECAFA).
2.Kutoandika jambo lolote linahusu mashindano yoyote yaliyo chini ya CECAFA.

Ili kuweza kufanya kazi pamoja na CECAFA,TASWA inataka kuombwa radhi na CECAFA kutokana na kitendo hicho na kuwalipa fidia waandishi ambao wamepoteza vifaa vya vya kazi na wengine kuhalibiwa vifaa vyao.

TASWA inatoa onyo kali kwa baadhi ya vyama,viongozi na makampuni wenye tabia ya kutotoa ushirikiano na dharau kwa waandishi wanapokuwa kwenye kazi zao.

Juma Abbas Pinto
CHAIRMAN
Julai 30, 2012
Committee Members: A. Lucas, S. Jaba, G. Hoka, E.Kambili, O.Kapinga, Z. Chande

Sunday, July 29, 2012

YANGA YA TANZANIA NDIO BINGWA WA KOMBE LA KAGAME 2012

Wachezaji wa Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakishangilia ubingwa wao wakiwa na Kombe la Kagame baada ya kukabidhiwa rasmi walipoibanjua timu ya Azam Fc kwa mabao 2-0, katika mchezo wa Fainali uliozikutanisha timu hizo katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo jioni.
*****************************

TIMU ya Yanga ya jijini ya Dar es Salaam, leo imewadhihirishia mashabiki wa soka kwa kutetea ubingwa wake na kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame 2012,katika mchezo wa Fainali za Kombe hilo dhidi yake na timu ya wauza Lambalamba Azam Fc, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa.

Yanga sasa imebakiza mara moja kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba kutwaa Kombe hilo, mara tano kwa sita. Yanga ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Hamisi Kiiza aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 44 na Said Bahanuzi aliyefunga la pili dakika ya 90+ katika dakika tatu za nyongeza.

Kiiza alifunga bao lake, baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kumpiga chenga kipa huyo kisha kuusukuma mpira nyavuni.

Bahanuzi aliuwahi mpira mrefu uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa Azam kabla ya kumtungua Dida.

Niyonzima, akichanja Mbuga.
Niyonzima, akimtoka beki wa Azam kwa spidi ya ajab na kumimina majalo.
Kipa wa Azm, Dida, akiokoa moha ya hatari langoni kwake.
Niyonzima, akiendelea kuwatesa mabeki wa Azam.
Beki wa Azam, Mouris akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi na kumpa nafasi kipa wake Dida kudaka mpira huo.
Mashabiki wa Azam waliochanganyika na wa Simba, wakiwa wamebeba Jeneza kuwakejeli mashabiki wa Yanga, kabla ya kuanza kwa mchezo huo.lakini hadi mwisho wa mchezo huo Jeneza hilo halikujulikana lilikopitia.
Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao ya As Vita yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi, dakika ya 67, wakati la kufutia machozi la timu ya APR ya Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya 89 na kufanya mshindi wa tatu katika michuano hiyo kuwa ni AS Vita.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la kwanza.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia na Kombe lao.
Kasuku nao walikuwapo kushuhudia mtanange huo huku wakiwa na rangi ya Yanga na Bendera ya Yanga.
Mashabiki wa Azam wakiwa Tuliiiiii, wakiwa kama wamemwagiwa maji baada ya timu yao kupokea kichapo kitakatifu jioni ya leo.
Said Bahanuz, akishangilia mbele ya mashabiki wake baada ya mchezo huo kumalizika.
Mashabiki wa Yanga....... Ebwana eeeeh!!!! ushindi mtamu bwanaaaaaa!!!!
Bahanuzi kama Kawa.......
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji akipita katikati ya Uwanja kuwapongeza wachezaji wake baada ya mchezo huo kumalizika.
Niyonzima (kushoto) akimfariji Ngasa, baada ya mchezo huo.

2012 CECAFA KAGAME CLUB CUP
Dar es Salaam, July 14-28
(Yellow cards after end of preliminary round)
2:
20. Derrick Walulya (Suspended Match No. 12)
4. Yusuf Makame Juma [Mafunzo]
5. Kadar Abaneh [AS Port]
1:
2. Edward Simon Jovan [El Salaam, Wau]
28. Maxime Sekamana [APR ]
11. Emery Ndikumana [Atletico Olympique]
7. Didier Kavumbagu [Atletico Olympique]
17. Amir Maftah [Simba]
15. Allan Munabu [URA]
21. Ahmed Mohdi [AS Port]
5. Ismail Khamis [Mafunzo]
25. Johnson Bagoole [APR]
17. Christopher Ndayishimiye [Atletico]
4. Hassan Hakizimana [Atletico]
13. Ismail Musa Juma [El Salaam, Wau]
13. Lema Mubidi [AS Vita]
17. Thiery Kasereka [AS Vita]
16. Vincent Agbor [AS Port]
1. Khalid Moursal [AS Port]
4. Jean Paul Niyibaraba [AS Port]
3. Francis Nongwe [Atletico]
15. Frederick Nsabiyumwa [Atletico]
15. Santino Makuei [El Salaam, Wau]
24. Jerry Santos [Tusker]
18. Said Musa Shaaban [Mafunzo]
14. Sula Bagala [URA]
22. Osman Wejuli [URA]
12. Suleman Ndikumana [APR]
4. Donatien Tuyizere [APR]
18. Joseph Shikokoti [Tusker]
13. Aggrey Morris [Azam]
19. John Bocco [Azam]
TOTAL: 29
QURTER FINALS
2:
21. Issa Mpeko [AS Vita Club] (2) R
4. Ibrahim Mwaipopo [Azam] (2) R
1:
15. Mohamed Abdoulrahman [Mafunzo]
20. Derrick Walulya [URA]
16. Augustine Nsumba [URA]
22. Jean Claude Iranzi [APR]
3. Albert Ngaboyisibo [APR]
16. Nelson Lukong [Vita]
23. Pierre Kwizera [Atletico]
3. Simbi Ebunga [AS Vita Club]
14. Mutombo Kazadi [AS Vita Club]
10. Felix Sunzu [Simba]
6. Erasto Nyoni [Azam]
26. Haruna Shamte [Simba]
25. Jabir Aziz [Azam]
TOTAL (from Quarter final stage only): 17 - Up to Match No. 20 (Yanga v APR semifinal)
OVERALL TOTAL: 36
Gishinga Njoroge
Managing Editor
www.kpl.co.ke
Brookside Grove
Westlands
P.O Box 5350, Nairobi, 00506 Kenya
Office Tel: +254 020 444 20 70
+254 020 444 20 72
email: gishinga@kenyanpremierleague.com
Personal cel phone: +254 722 79 77 49

Saturday, July 28, 2012

MABINGWA KOMBE LA KAGAME 2012 NI YANGA YA TANZANIA

Magoli mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika dakika ya 90 ya mchezo yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe la Kagame 2012 baada ya kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa goli 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tanzania ijnakila sababu ya kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya Azam katika michuano hiyo ya mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa michuani huyo iliingiza timu 4 zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa katika hatua ya robo fainali.

Yanga pia waliutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya kushambulia mwamuzi kwa ngumi.

Kikosi kilichoipeleka Yanga fainali kombe la Kagame 2012

Kikosi kilichoipeleka Yanga fainali mwaka huu; Kutoka kulia waliosimama Nadir Cannavaro, Kevin Yondan, Said Bahanuzi, Ally Barthez, Athumani Chuji na Oscar Joshua. Waliopiga magoti kutoka kulia ni Juma Abdul, David Luhende, Haruna Niyonzima, Godfrey Taita na Hamisi Kiiza.

Kikosi kilichoipeleka Azam fainali Ya Kombe la Kagame 2012

Kikosi kilichoipeleka Azam fainali, kutoka kulia waliosimama ni Said Mourad, Ibrahim Mwaipopo, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, John Bocco na Ramadhan Chombo. Walioinama kutoka kulia ni Jabir Aziz, Salum Abubakar, Ibrahim Shikanda, Kipre Tcheche na Deo Dida.

Thursday, July 26, 2012

TIMU ya Azam Fc Yatinga Fainali Kombe la Kagame 2012

Mpira uliopigwa na John Boko ukitinga wavuni na kuandika bao la kwanza.
Wachezaji wa Azam wakishangilia bao lililofungwa na John Bocco.

TIMU ya Azam Fc, leo imetinga hatua ya Fainali na kumsubiri mshindi kati ya Yanga ya Dar es Salaam ama APR ya Rwanda, baada ya kuichapa AS Vita kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa leo mchana mida ya saa nane katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, AS Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Mfongang Alfred, katika dakika ya 34, baada ya kuunasa mpira uliopigwa na Ibrahim Shikanda na kuichambua ngome ya Azam kabla ya kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Azam, Deo Munishi ‘Dida’.
Vita walipata pigo dakika ya 41, baada ya mchezaji wao, Issama Mpeko, kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Azam ilisawazisha bao hilo, kupitia kwa John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 68 aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Kipre Tchetche, kutoka wingi ya kulia.
Mrisho Khalfan Ngassa aliyeingia kutokea benchi kipindi cha pili aliifungia Azam bao la ushindi dakika ya 89, akimalizia pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Baada ya kufunga bao hilo, Mrisho alikwenda moja kwa moja kwa mashabiki wa Yanga na kushangilia nao, badala ya mashabiki wa Azam.

Wednesday, July 18, 2012

SIMBA YAICHAPA SPORTS MABAO 3-0 KOMBE LA KAGAME

Mshambuliaji wa Simba (kulia) akichuana na beki wa timu ya Sports katika mchezo wa Kombe la Kagame, ambapo mchezo huo umemalizika huku Simba wakiibua na ushindi wa mabao 3-0. Mabao ya Simba yamefungwa katika dakika 60 na 64,bao la kwanza likifungwa na Abdallah Juma na la pili likifungwa kwa mkwaju wa penati katika dakika hiyo ya 64, baada ya mchezaji wa Sports, kuunawa mpira akiwa ndani ya eneo la hatari.
Mwinyi Kazimoto (kushoto) akiwania mpira na beki wa Sports.

Sunday, July 15, 2012

YANGA YATANDIKWA 2 BILA NA ATLENTICO KAGAME CUP

Mchezaji wa timu ya Yanga, Juma Abdul, akichuana kuwania mpira na beki wa Atletico, Henry Mbazumutima, wakati wa mchezo wao wa fungua dimba ya michuano ya kombe la Kagame, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo inaandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA. Katika mchezo huo Yanga imeanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao 2-0 na Atletico, huku mabao hayo yakiwekwa kimiani na Olivier Ndikumana katika dakika ya 81 na 90+3.
Wachezaji wa timu za Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi wakichuana vikali katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.

Popular Posts