Pages

Showing posts with label Pemba. Show all posts
Showing posts with label Pemba. Show all posts

Friday, August 17, 2012

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Afuturisha Mkoa wa Mjini Magharibi

Baadhi ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakianza kufutari kwa kunywa madafu kabla ya kula futari jana walipoalikwa katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa huo kila ifikapo mwezi kama huu kwa futari maalum.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Baadhi ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika futari iliyoandaliwa jana ,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa huo kila ifikapo mwezi kama huu kwa futari maalum.
Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar.
Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, (wa pili kushoto) akijumuika na akinamamawa wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Chakula cha Futari iliyoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, (wengine kulia) Mama Shadiya Karume, Mama Pili Balozi Seif na Waziri wa Muungano Samia Suluhu Hassan, (kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akijumuika na wananchi pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Futari, aliyowaandalia wananchi hao katika viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar jana, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amaan Abeid Karume,(kushoto) na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kufutari nao pamoja jana katika futari aliyowaandalia katika viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumalizika Futari waliyowaandalia katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, (kulia) akisalimiana na mke wa Rais mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume, baada ya Futari iliyoandaliwa kwa wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar

Thursday, August 16, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURIASHA WANANCHI WA KISIWA CHA PEMBA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya Viongozi na wananchi wa Kisiwa cha Pemba, katika Futari aliyowaandalia wananchi hao na kufuturu nao kwa pamoja katika Ukumbi wa Makonyo Chakechake Pemba.
Wake wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal (katikati) Mama Asha Bilal (wa pili kulia) wakijumuika na wananchi katika hafla ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais iliyofanyika katika Ukumbi wa Makonyo Chakechake Pemba jana Agosti 14, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi wa Kisiwa cha Pemba, baada ya hafla fupi ya futari aliyowaandalia wananchi hao na kufuturu nao pamoja katika Ukumbi wa Makonyo Chakechake Pemba. Picha na OMR

Monday, August 13, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ziarani Mkoa Wa Kisiwani Pemba

Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi ya mradi wa skuli ya Istiqama uliopo katika kijiji cha Mbuyuni Mkoani Pemba Ustadhi Mohd Omar Makame akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi huo
Mjumbe wa Kamai Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa shilingi 800,000/- kusaidia ununuzi wa saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Tawi la CCM la Makombeni Mkoani Kisiwani Pemba. Sambamba na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pia akakabidhi mchango wa shilingi 300,000/- kwa ajili yha mIlango ya Tawi hilo.
Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi la CCM, Makombeni wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif Ali Iddi aliyetembelea Tawi hilo kuangalia hatua iliyofikia ya ujenzi wa Tawi hilo.
--
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea mradi huo. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono miradi yote inayoanzishwa na Taasisi, Mashirika, Jumuiya na hata Wananchi katika lengo la kustawisha Maendeleo ya Jamii hapa Nchini.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo wakati alipokuwa akikagua mradi mkubwa wa ujenzi wa Skuli inayojengwa na kusimamiwa na Jumuiya ya Istiqama Tanzania hapo katika Kijiji cha mbuyuni Mkoani Kisiwani Pemba.

Balozi Seif aliuambia uongozi wa wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa mradi huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha kwamba miundo mbinu muhimu ya maji, umeme na bara bara inawekwa ili kuona lile lengo lililokusudiwa la kuanzishwa kwa mradi huo muhimu kwa jamii linafikiwa.

Aliuagiza Uongozi huo kumuandikia barua mara moja ya changamoto wanazopambana nzo ambazo zimo ndani ya uwezo wa Serikali Kuu ili iwe rahisikwake kuziagiza Taasisi husika kupanga mikakati ya kutekeleza miundo mbinu hiyo.

Balozi Seif alisema atatumia uwezo na nafasi aliyonayo kushawishi wahisani zikiwemo ofisi za Kibalozi kusaidia ujenzi huo uliolenga kwenda hadi ghorofa tatu ambao tayari hivi sasa umeshatumia karibu shilingiMilioni mia tatu { 300,000,000/- }.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Jumuiya hiyo ya Istiqama Tanzania kwa hatua yake ya kujenga mradi huo mkubwa ambao utasaidia kusukuma mbele Maendeleo ya Elimu ya Dini na Dunia.

Alisema Jumuiya hiyo inafaa kuungwa mkono na jamii yote Nchini kwa vile tayari imeshajipanga vyema kuweka mkazo zaidi katika suala la Elimu kwa kukiandalia mazingira bora kizazi cha sasa. “ Nimevutiwa sana na mradi huu wa Elimu wenye kuleta faraja si kwa wakaazi wanaouzunguuka hapa lakini kwa Wananchi wote Nchini. Naimani kwamba utakapokamilika bila shaka utachukuwa wananfunzi wa sehemu mbali mbali Nchini”.

Alionyesha furaha yake Balozi Seif. Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Mradi huo Ustaadhi Mohammed Omar Makame alimueleza Balozi changamoto wanazopambana nazo wakati huu wa ujenzi. Ustaadh Mohd Omar alizitaja changamoto hizo kubwa kuwa ni pamoja na ukosefu a huduma ya maji safi, umeme pamoja na Bara bara licha ya juhudi walizochukuwa za kuchimba kisima bila ya mafanikio.

Alisema ujenzi wa Skuli hiyo ulioanza tarehe 1/12/2010 utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 1575, Madarasa 45 , mabweni, nyumba za walimu pamoja na msikiti lengo likiwa kunyanyua elimu ya dini sambamba na kuibua vipaji vya wanafunzi.

Mapema asubuhi Balozi Seif akiwa pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alipata fursa ya kutembelea Tawi Jipya la CCM la Makombeni pamoja na kukagua uhai wa Chama hapo katika mtaa wa Mweneza.

Akizungumza na Viongozi na Wanachama hao Balozi Seif aliwatahadharisha katika kipindi hichi cha chaguzi zinazoendelea za chama hicho wahakikishe wanawachaguwa Viongozi safi watakaokuwa mahiri katika kutekeleza Sera za chama hicho.

Alisema wakati umefika kwa Wanachama wa chama hicho kuwakataa wanachama wasiokuwa na msimamo kwa kufikiria kujinufaisha binafsi pamoja na kuvuruga chama kwa makusudi. “ Wale wanaohisi kwamba sera za Chama cha Mapinduzi zimepitwa na wakati kwa hiyari yao wangeliamua mapema kwenda kwenye vyama vyenye Sera za Dot Com na kuiachia CCM Yetu inayoamini sera za Serikali mbili Ncchini Tanzania”. Alifafanua Balozi Seif. Katika kuunga mkono harakati za kukamilisha ujenzi wa Tawi la CCM Makombeni

Balozi Seif alichangia shilingi laki nane { 800,000/- } kusaidia ununuzi wa saruji na kuahidi shilingi 500,000/- za fundi pamoja na Seti ya TV na DVD yake wakati Mkewe alichangia shilngi laki 300,000/- kusaidia milango ya Tawi hilo.

Akitoa Taarifa fupi ya ujenzi huo pamoja na uhai wa Chama Katibu wa CCM WA Tawi la Makombeni Bibi Wahida Mbaraka Mohd alisema ujenzi wa Tawi hilo umekuja ili kwenda sambamba na hadhi ya chama chenyewe kilivyo.

Bibi Wahida alisema hadi sasa ujenzi huo uliolenga kufikia gharama ya shilingi milioni 13,920,000/- umeshafikia shilingi milioni 8,000,000/-.

Katibu wa Tawi hilo alimuhakikishia Balozi Seif kwamba Wanachama wa CCM wa Tawi hilo wataendelea kuunga mkono sera za Chama chao za kuamini mfumo wa Serikali mbili Nchini Tanzania.

Alisema Wanachama hao wamejiimarisha kutoghilibiwa na vurumai zinazojichomoza Nchini za baadhi ya watu kushawishi wananchi juu yamchakato wa utoaji wa maoni ya Katiba unaolenga kuvunja Muungano.

Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

Tuesday, July 31, 2012

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKIWASILI PEMBA LEO KUANZA ZIARA YA MIKOA YA KUSINI NA KASKAZINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali mbali,wa Chama na Serikali, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo akiwa katika ziara maalum ya Mikoa ya Kusini na Kaskazini.Picha na Ramadhan Othman,ORZ
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakisalimiana na Viongozi mbali mbali,wa Chama na Serikali, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo akiwa katika ziara maalum ya Mikoa ya Kusini na Kaskazini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wakuu wa Vikosi vya Ulinzi Pemba, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo akiwa katika ziara maalum ya mikoa ya Kusini na Kaskazini.

Tuesday, July 10, 2012

Waliokimbia na Kuomba Hifadhi ya Ukimbizi Nchini Somalia Wafikishwa Nyumbani Kwao Kisiwani Pemba

BoTI Ikiwasili Mkoani Pemba
Mmoja wa Viongozi wa UNHCR akiwa amembeba mtoto wa mmoja wa Wananchi waliokuwa Nchini Somali Wakimbizi walipowasili bandari ya Mkoani kwa Boti ya Sea Bus.
Mkuu wa Mkua wa Kusini Pemba Juma Kassin Tindwa akisalimiana na baadhi ya Wananchi waliokuwa Nchini Somali Wakimbizi walipowasili bandari ya Mkoani pembe kwa Boti ya Sea Bus.
Rashid Abdalla Said, akitowa shukrani kwa Uongozi wa UNHCR NA Serekali ya Tanzania kwa Ushirikiano na Serekali ya Somali na Serekali ya Zanzibar kwa kuwafikisha Nyumbani kwa usalama akiwa katika bandari ya Mkoani Pemba baada ya kuwasili Kisiwani Pemba hivi karibuni.

Popular Posts