Pages

Showing posts with label Singida. Show all posts
Showing posts with label Singida. Show all posts

Monday, September 10, 2012

Tamasha la serengeti fiesta 2012 Mkoa wa singida

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cirryl a.k.a Kamikazi akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shillole akijimwaya mwaya jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Singida (hawapo pichani),usiku huu.

Shillole akiwapa dole mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.
Rich Mavoco akiwaimbisha mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu,ambapo wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye tamasha hili.
Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka THT,Recho akiwa sambamba na dansaz wake jukwaani wakikamua vilivyo.
Pichani ni Ofisa Mahusiano wa kampuni Clouds Fm,Simalenga akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini,Mh Queen Mlozi pamoja na nduguze wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel,Mkoani Singida ambapo wakazi wa mji huo wameitikia wito wa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya
Anaitwa Ben Paul mmoja wa wasanii mahiri wa Bongofleva katika miondoko ya R&B
Pichani kulia ni Dj Zero akiwa amepozi mtangazaji wa kipindi cha XXL,wote wafanyakazi wa Clouds FM wakishoo love usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Singida Motel.
Pichani juu na chini Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea.

Sunday, August 26, 2012

BARABARA YA MLIMA SEKENKE ILIVYOHARIBIKA

Kutokana na kilichoelezwa kuwekwa kwa lami chini yakiwango katika mlima Sekenke mkoani Singida, imeharibika vibaya kama inavyoonyesha pichani magari yakipita kwa shida baada ya lami hiyo kubomoka kwa kipindi kifupi tangu iwekwe, kama ilivyokutwa jana.Picha na Joseph Senga

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa Kwenye Mkutano wa Kuwashukuru Wananchi wa Jimbo la igunga

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akisalimiana na aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo mwaka jana, kupitia Chadema, Mwalimu Joseph Kashindye, walipokutana katika mkutano wa kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, ambayo Chadema kiliibuka mshindi, uliofanytika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akikumbatinana na Mbunge wa Maswa Mashariki, Slyvester Kasulumbai, walipokutana katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa jimbo la Igunga kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga juzi.
Kutokana na kilichoelezwa kuwekwa kwa lami chini yakiwango katika mlima Sekenke mkoani Singida, imeharibika vibaya kama inavyoonyesha pichani magari yakipita kwa shida baada ya lami hiyo kubomoka kwa kipindi kifupi tangu iwekwe, kama ilivyokutwa jana.Picha na Joseph Senga

Monday, August 6, 2012

MKUU MKOA WA SINGIDA ATEMBELEA WIZARA YA FEDHA KATIKA MAONYESHO YA WAKULIMA YA NANENANE MJINI DODOMA

Meneja Mawasiliano na Kumbukumbu wa Shirika Hodhi la Mali ya Mashirika ya Umma (CHC) Joseph Mapunda (kushoto) akimpa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia) leo ,jinsi Shirika hilo linavyofanya tathmini ya mashirika ya umma yaliyobinafsishwa na utendaji wa mashirika hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi jinsi Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mchambuzi wa Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya TEKNOHAMA ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia) leo mjini Dodoma jinsi kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Monday, July 23, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA SECONDARY MTIPA WILAYA YA SINGIDA MJINI

Meneja Huduma kwa Jamii wa Kampuni ya Simu za Mikononi Tanzania ya Airtel, Hawa Bayuni (kushoto) akikabidhi vitabu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwakilishi wa Shule ya Sekondari
Mtipa iliyopo mkoani Singida, Bi. Mary Haiki ambaye alitembelea makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu ya Airtel jijini Dar es salaam
---
Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora nchini kote, leo imetoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari Mpita ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salam kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mtipa wilaya ya Singida mjini. Mwawakilishi wa shule hiyo ambaye ni mzawa wa eneo hilo bi Mary Hiki alikabidhiwa msaada huo wa vitabu na Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayuni. Shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilling milioni mbili.

Vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Hisabati, Phisikia, Biolojia, Kiswahili. ambapo vimekuwa na uhitaji mkubwa shuleni hapo.

Akiongea wakati wa makabithiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salaam Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayuni alisema" Airtel kwa kupitia kampeni yake ya kusaidia jamii imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule ya sekondari wilayani Singida na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hii Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza Bayuni.

Mwakilishi wa Shule hiyo bi Mary Hiki mzawa wa Singida alisema tunayo fuhara kuona Airtel inajito katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni
kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Singida anatoka graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika
kutimiza malengo tuliojiwekea.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, mwezi uliopita Airtel ilitoa msaada wa kutoa computer 4 na Vitabu vyenye dhamani ya millioni tano kwa shule ya sekondari Mazombe iliyokokilomita nne kutika Iringa mjini . Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.

Tuesday, July 17, 2012

WAFUASI WA CHADEMA WALIOPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWENYEKITI WA UVCCM

Afisa sera na utafiti CHADEMA Makao makuu, Waitara Mwita akifurahi na wanachama wa CHADEMA, baada ya kupata dhamana mjini Singinda
Mwita Waitara akizungumza na wanahabari mjini Singida baada ya kuwekewa dhamana ya wadhamini wawili
Mwita Waita (wa kwanza kushoto), akifurahi na wafuasi wa CHADEMA mahakamani mjini Singida, baada ya kupata dhamana ktk kesi ya mauaji.
VIJANA sita, Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti UVCCM Yohana Mpinga wa Kata Ndago Iramba Singida, wakipandishwa kwenye gari la polisi.Picha na Habari na Elisante John
--

WATU sita wamepandishwa kizimbani Mjini Singida, kujibu shitaka la mauaji ya Mwenyekiti UV-CCM Kata ya Ndago Wilaya Iramba,Yohana Mpinga, katika vurugu zilizohusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM.Wamesomewa shitaka hilo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Neema Mwanda mbele ya hakimu mfawidhi mahakama ya Mkoa Singida, RuthMassam.
Walioshitakiwa ni Manase Daudi (40), Williamu Elia (33), Frank Stanley (20), Charles Leonard (36), Tito Nintwa na Fillipo Edward (30), wakazi wa Ndago, Wilaya Iramba.
Wamedaiwa kufanya kosa hilo Julai 14, 2012 saa kumi alasiri, katika kijiji cha Nguvumali, kwa kutumia mawe na fimbo.
Hawakutakiwa kujibu lolote, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo na itatajwa tena Julai 30, 2012.
Pia kesi nyingine iliyosomwa na mwanasheria wa Serikali Seif Ahmad, imemhusisha afisa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Waitara Mwita (37) mkazi wa jijini Dar-es-salaam, akidaiwa kutoa lugha ya matusi mkutanoni.
Waitara anadaiwa kutoa lugha hiyo ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, Julai 14, 2012 saa kumi jioni katika kijiji cha Ndago, Wilaya Iramba Mkoani Singida. Yupo nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja mwenye Sh.800,000 na itatajwa tena Julai 30, 2012.

Monday, July 16, 2012

MWANAFUNZI WA MAREKANI ATOA ZAIDI YA MILIONI 30 KUSAIDIA UCHIMBAJI KISIMA SINGIDA

Mtambo wa kuchimba visima ukichimba kisima cha maji cha kijiji cha Sekoture jimbo la Singida Kaskazini.

Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na mke wake Faraja Kota, muda mfupi baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Sekoture.

Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini Mh. Lazaro Nyalandu akiwa kwenye picha ya pamoja na mwanafunzi Leah Singer (katikati) kutoka Marekani aliyetoa msaada wa shilingi milioni 30 za kugharamia uchimbaji wa kisima cha kijiji cha Sekoture. Wa kwanza kulia ni mke wa Nyalandu Faraja Kota.

Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikagua uchimbaji wa kisima cha maji cha kijiji cha Sekuture kata ya Ilongero.

Mwanafunzi aliyemaliza masomo yake kwenye shule ya High school Coval Reef Miami nchini Marekani Leah Singer, akichukua picha za hafla ya uzinduzi wa uchimbaji wa kisima cha maji cha kijiji cha Sekoture anachokigharamia kwa zaidi ya shilingi milioni 30. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Mwanafunzi wa shule ya Covel Reef High School ya jimbo la Miami nchini Marekani Leah Singer (18), ametoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kugharamia uchimbaji wa kisima kirefu cha kijiji cha Sekoture kata ya Ilongero jimbo la Singida Kaskazini.

Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini Mh. Lazaro Nyalandu amesema hayo muda mfupi baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya uchimbaji wa kisima hicho kitakachowakomboa wananchi 4,850 wa kijiji cha Sokoture ambao, wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na uhaba wa maji safi na salama.

Amesema mwanafunzi huyo kijana mdogo amefikia uamuzi huo wa kutoa msaada wa kuchimba kisima, baada ya kusoma taarifa ya hitaji la maji kwa wakazi wa kijiji hicho kwenye mtandao wake (Nyalandu).

“Leah baada ya kusoma habari hiyo, alitambua umuhimu wa hitaji hilo na mara moja alianza kuchangisha fedha na hatimaye amefanikiwa kutimiza lango lake na sasa tunashuhudia kisima hiki kirefu kinachimbwa” alifafanua Mh. Nyalandu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Katika hatua nyingine, mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwataka vijana nchini kuiga mfano wa Leah wa kuwa na moyo wa kujitolea.

Mh. Nyalandu amesema vijana wanapaswa kutambua kuwa kutoa misaada ni moyo na wala si kwa sababu mtu ni tajiri wa kiwango gani.

Akifafanua zaidi, amesema vijana wanao wajibu mkubwa wa kuanzia kuzisaidia familia zao kwa hali na mali na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Leah ambaye baadaye mwaka huu anatarajiwa kujiunga na chuo kikuu maarufu nchini Marekani cha Havard, amesema ataendelea na juhudi zake za kuchangisha fedha za kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji muhimu yakiwemo ya maji safi na salama.

Mwita Waitara Mwikabwe Mbaroni kwa mauaji ya Mwenyekiti wa UVCCM

Afisa wa sera na utafiti CHADEMA makao makuu,Mwita Waitara Mwikwabe,(wa kwanza kulia walioketi) akitoa tamko kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) la CHADEMA kutohusika na mauaji ya mwenyekiti wa umoja wa vijana (CCM) kata ya Ndago jimbo la Iramba Magharibi.

Afisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Mwita Waitara Mwikwabe (wa tatu kushoto) akitoka nje ya ofisi ya CHADEMA mkoa wa Singida, baada ya kumaliza kutoa tamko la CHADEMA kutohusika na mauaji ya mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM kata ya Ndago jimbo la Iramba Magharibi.

Na Nathaniel Limu.

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia Afisa wa sera na utafiti wa Chama cha CHADEMA Makao Makuu Waitara Mwita Mwikwabe, kwa tuhuma ya mauaji ya mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi Yohana Mpinga (30).

Kiongozi huyo wa CHADEMA alikamatwa muda mfupi baada ya kumaliza kutoa tamko la chama hicho kutokuhusika na mauajio ya kijana huyo kiongozi wa CCM kwa waandishi wa habari.

Waitara, mbunge wa jimbo la ubungo jijini Dar -es- salaam Mh. John Mnyika na mshauri wa CHADEMA na Mhadhiri wa chuo kiku cha Dar- es- salaam Dk. Kitila Mkumbo, inadaiwa walichochea mauaji hayo kwa kitendo chao cha kumkashifu mbunge wa wa jimbo la Iramba magharibi Mwigulu Lameck Nchemba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Linus Vicent Sinzumwa, kashifa hizo zimetolewa na viongozi hao wa CHADEMA, Julai kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi, pia karibu kabisa na kituo kidogo cha polisi cha Ndago, ambapo viongozi hao wanatuhumiwa kutoa kashifa hizo dhidi ya Mwigullu.

Sinzumwa amesema baada ya viongozi hao kuacha kueleza sera za chama chao na kuanza kumkashifu Mwigullu, baadhi ya wananchi waliwataka kuacha mara moja kumkashifu mbunge wao, lakini viongozi hao walipuunza maombi hayo ya wananchi.

Amedai kitendo hicho kilichochea kutokea kwa vurugu ambazo mwisho wake, ulipelekea kikundi cha wanachama wa CHADEMA kumuuwa Yohana Mpinga kwa kumpiga kwa fimbo na mawe.

Jeshi la polisi lilimkamata Waitara muda mfupi baada ya kutoa tamko kwa waandishi wa habari kuhusu yaliyojiri katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika kata ya Ndago julai 14 mwaka huuu.

Katika tamko hilo, Afisa huyo wa sera na utafiti, amesema wakati wanajiandaa kuanza hotuba, vijana wanane walianza choko choko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbali mbali.

Amesema kikundi hicho kiliwaogofya wananchi ambao waliondoka katika eneo hilo, lakini muda mfupi baadaye, walirejea na mkutano uliendelea kwa amani na utulivu hadi ulipomalizika.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wa CHADEMA, wamelaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinadai kuwa polisi wanawahusisha wao CHADEMA na tukio la mtu aliyeuawa kwenye vurugu zilizotokea Ndago.

Sunday, July 15, 2012

Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliandaa mikutano ya hadhara katika Jimbo la Iramba Magharibi. Mikutano hiyo ilitolewa taarifa polisi na jeshi hilo lilitoa baraka zake kama utaratibu wa sheria unavyotaka kwa barua yake ya tarehe 12 Julai 2012 Kumb. Na. KIO/B1/1/VOL.V/268

2. Mkutano wa kwanza ulipangwa kufanyika katika Kata ya Ndago katika viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi ambapo pia ni hatua chache karibu kabisa na Kituo cha Polisi Ndago. Mkutano huu ulipangwa kuanza saa nane mchana.

3. Msafara wa kitaifa unaofanya ziara ya ukaguzi wa chama, katika mkoa wa Singida chini ya uratibu wa Ofisa wa Sera na Utafiti Makao Makuu, Mwita Mwikwambe Waitara, (ikiwa ni maandalizi ya operesheni nyingine kubwa mkoani humo itakayofanyika baadae), uliwasili katika eneo la Mkutano majira ya saa tisa na nusu alasiri. Tulikuta wananchi wengi wakiwa wanatusubiri. Kabla ya Mkutano kuanza tulipewa taarifa kwamba kuna kikundi cha vijana kimeandaliwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA kwa kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe ili mkutano huo usifanyike. Suala hilo lilielezwa mkutanoni mapema na Mheshimiwa Waitara, mbele ya askari polisi.

4.
Wakati tukijiandaa kuanza hotuba, vijana wapatao wanane walianza chokochoko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbalimbali. Wakati fujo zinaanzishwa na kile kikundi, Mheshimiwa Waitara alikuwa bado anazungumza na wananchi kuwaandaa kusikiliza wazungumzaji wengine. Vurumai hiyo ilizimwa na wananchi wenyewe wa Ndago waliokuwa na hamu ya kusikiliza ujumbe wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.

5. Kwa kweli tunawashukuru wananchi wengi wa Ndago walioonesha ujasiri mkubwa kuweza kuwaondoa vijana wale eneo la mkutano, kisha mkutano ukaendelea, huku wananchi wakionesha kila hamasa ya kufurahia hoja kutoka kwa wazungumzaji, akiwemo Mheshimiwa John Mnyika, ambaye aliombwa ahudhurie ziara hiyo kwa nafasi yake ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

6. Mpaka tunamaliza mkutano huo ambao wananchi waliufurahia sana kwa namna ulivyohutubiwa kwa amani na utulivu huku wazungumzaji wakijenga hoja juu ya mstakabali wa jimbo na taifa lao kwa ujumla, mamia ya wananchi waliohudhuria walitaka tuendelea kuhutubia, lakini tulibanwa na ratiba ya kuwahi mkutano wa pili, eneo la Kinampanda.

7. Lakini kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikisababishwa na kikundi cha vijana ambao tayari ilishatolewa taarifa yao kwenye mkutano huo, lakini askari waliokuwepo hawakuthubutu kuchukua hatua, tulilazimika kuomba msaada kutoka kwa OCD na R.P.C, ambapo baadae wakati mkutano unakaribia kuisha tuliona gari la polisi kutoka Mjini Singida likiwa na askari waliojipanga rasmi kwa ajili ya kuzuia vurugu likifika pale eneo la mkutano, lakini wakati huo hali ilishatulia na hotuba zimetolewa vizuri.

8. Kutokana na hali hiyo ya vurugu, zilitolewa taarifa Kituo cha Polisi cha Ndago, ambapo lilifunguliwa jalada NDG/RB/190/2012. Katika jalada hilo tulitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa waliokuwa vinara wa kundi lililokuwa likifanya fujo kwenye mkutano mbele ya askari polisi. Majina hayo ni; 1. Daniel Sima, 2. Tito Nitwa, 3. Bakili Ayubu, 4. Yohana Makala Mpande, 5. Ernest Kadege, 6. Abel John, 7. Athuman Ntimbu, 8. Martin Manase, 9. James Ernest, 10. Simion Makacha, 11. Anton John, 12. Frank Yesaya

9. Kwa hakika askari polisi wa Ndago waliokuwepo mkutanoni mbali ya kutochukua hatua yoyote dhidi ya fujo tulizofanyiwa ikiwemo kupondwa mawe na kikundi kidogo cha wahuni, fujo zilipozidi askari wote walikimbia eneo la mkutano, akabaki OCS pekee ambaye naye alionekana dhahiri kutotaka kuchukua hatua stahili. Hakuonekana kufanya juhudi zozote za kuhakikisha amani inalindwa na ulinzi unaimarishwa katika eneo la mkutano na hatua zinachukuliwa dhidi ya watu walioonekana kudhamiria kufanya fujo. Mtu yeyote makini angeweza kuona kuwa askari wale walikuwepo pale mkutanoni ‘almuradi’ tu lakini kama vile walikuwa na maelekezo maalum ya kuhakikisha hawachukui hatua yoyote katika kuzuia mpango wowote wa kusababisha vurugu na kuvunja amani.

10. Baada ya kumaliza mkutano wa Ndago kwa amani, tulikwenda Kinampanda ambako tulifanya mkutano mwingine mzuri kwa amani kabisa, ambapo mbali ya wananchi kuwa wametusubiri kwa hamu kubwa na kutusikiliza kwa makini hoja zetu, polisi katika eneo hilo walitupatia ushirikiano mzuri tangu wakati tunafika mpaka tulipomaliza mkutano huo.

11. Jioni wakati tumerudi hotelini, tukasikia kuna taarifa zinasambazaa kuwa kuna mtu/watu wamekufa katika eneo la Ndago. Habari hizo zilikuwa zinakanganya kwa sababu zilikuwa zikitaja idadi tofauti tofauti. Lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli kuna tukio la mtu kufariki, CHADEMA tunasikitika sana kwa tukio hilo la uhai wa mtu.

12. Tunalaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinawataja polisi kuwa wanatuhusisha CHADEMA na tukio la mtu aliyefariki. Hii ni ajabu kubwa kwamba tumetoka kwenye mkutano ule kwa amani kabisa mpaka tumemaliza mkutano wa pili kwa amani na polisi wakiwepo sehemu zote mbili, kisha tunasingiziwa masuala ambayo wenyewe hatukuwa na habari nayo tangu mkutano wa kwanza ukiwa unaendelea mpaka mkutano wa mwisho ulipomalizika.

13. Kutokana na habari hiyo ya kifo cha mtu inavyoenezwa kwa kuihusisha CHADEMA, tumebaini kuwepo kwa mbinu na mikakati ya chama tawala pia vyombo vya dola vikihusika kutaka kuwatisha wananchi wa Singida, Watanzania wote wapenda mabadiliko na viongozi wa CHADEMA katika mkoa huu, wasifanye kazi ya kisiasa kwa kuwabambikizia tuhuma na kesi na pia kuwafanya waonekane ni watu wa vurugu.

14. Tunapenda kusema hapa kuwa njama hizo hazitafanikiwa. Zitashindwa kama zilivyoshindwa njama zingine zote ambazo zimekuwa zikifanywa na vyombo vya dola, viongozi wa serikali na chama tawala dhidi ya CHADEMA na vuguvugu la mabadiliko nchini.

15. Tunawataarifu wananchi kuwa ratiba ya kufanya Operesheni nyingine kubwa katika Mkoa wa Singida, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, itafanyika baadae kama ilivyoazimiwa na kikao cha Kamati Kuu.


Imetolewa leo Singida, Julai 15, 2012 na;

Waitara Mwita Mwikwabe

Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu

MWENYEKITI WA UVCCM KATA YA NDAGO AUWAWA

Aliyeuawa jana na wafuasi wanaaminika kuwa ni wa Chadema, ametajwa kuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Ndago, Yohana Mpinga mwenye umri wa miaka 30. Imeelezwa kutoka mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Linus Vicent Sinzumwa amesema leo kwamba, Mpinga amefariki dunia baada ya kupigwa kwa fimbo na mawe, na baadhi ya wafuasi wa Chadema, Julai 14 mwaka huu, saa kumi alasiri katika kijiji cha Ndago.

Alisema siku hiyo Chadema walikuwa na kibali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha Ndago na mgeni rasmi katika mkutano huo,alikuwa mbunge wa jimbo la Ubongo jijini Dar-es-salaam, John Myika.

Akifafanua,kamanda huyo, alisema mara baada ya Chadema kuanza mkutano huo,viongozi wake walianza kuporomosha kashifa dhidi ya mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba ,kitendo kilichowaudhi baadhi watu waliokuwepo kwenye mkutano huo.

Sinzumwa, alisema watu hao ambao walichukizwa na kitendo cha kukashifiwa mbunge wao,walianza kupiga kelele kuwa hawataki mbunge wao akashifiwe na badala yake wanataka kusikia sera za Chadema tu lakini viongozi hao waliendelea tu kuporomosha kashifa dhidi ya Mwingullu na kusababisha kuanza kwa vurugu.

Alisema kuwa vurugu hizo zilihusisha kundi la wanachama wa Chadema na wa CCM na zilisambaa haraka.Wanachama hao walianza kurusha mawe ovyo na askari wachache wa polisi waliokuwepo,walizidiwa nguvu na makundi hayo.

Amesema, Mwenyekiti wa UVCCM Yohana,yeye baada ya kuona vurugu zinaendelea kukua, akikimbilia kwenye nyumba ya Mwalimu Shume Manase Mpinga ili kuokoa maisha yake hata hivyo, kundi la wana-Chadema wakiwa wamebeba fimbo na mawe,walimpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusbabisha kifo chake papo hapo.

Alisema katika kundi hilo ambalo wamelikamata,watawahoji na wataobainika kuhusika,watafikishwa mahakamani wakati wo wote.

Aidha polisi wamefuta mikutano yote ya Chadema iliyokuwa iendelee katika kijiji cha Shelui na Kiomboi mjini jimbo la Iramba magharibi leo.

Tuesday, July 10, 2012

MAHAKAMA MKOANI SINGIDA YATEKETEZA BANDI YENYE THAMANI YA MILIONI 5

Matukio mbalimbali ya uchomaji wa Bangi yenye kilo zaidi ya 350 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.2 iliyokuwa ikisafirishwa na Pascal Dogii (31) mkazi wa Nzega mjini mkoani Tabora kuipeleka jijini Dar-es-salaam, ikiteketezwa kwa moto nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.Pascal hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka kumi jela baada ya kukiri kosa la kumiliki madawa ya kulevya aina ya Bangi.Picha na Nathaniel Limu

Friday, July 6, 2012

ZIARA YA CHADEMA JIMBO LA IRAMBA MAGARIBI

Chama cha CHADEMA kitafanya Ziara ya Mwezi Mzima katika Jimbo la Iramba Mangaribi ambalo ni Jimbo la Mh. Mwigulu Nchemba kwa ajili ya kuimarisha chama, Mada zitakazozungumziwa katika Ziara hiyo ni;

1. Utendaji wa BOT kati ya Mwaka 2006 - 2010
2. Wizi wa Fedha za EPA
3. Uhusika wa BOT na Taratibu za ufunguaji Akaunti nje ya nchi
4. Uhusika wa Wafanyakazi wa BoT na wizi wa pesa za EPA
5. Uhusika, usaidizi, ushauri wa kitaalamu wa wafanyakazi wa BOT uliosaidia kuibwa kwa Fedha za EPA
6. Ushauri Mbovu wa masuala ya Uchumi katika kipindi cha 2006 - 2010 ndani ya BoT
7. Ugumu wa maisha ya wananchi wa Iramba Mangaraibi, suluhisho la Matatizo yao.
8. Matatizo ya Elimu katika Jimbo la Iramba Magharibi,
9. Utendaji wa Kazi wa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi,
10. Serekali kushindwa kushughulikia Mauaji ya Raia baada ya uchaguzi wa Igunga na Arumeru Mashariki.
11. Hali ya Uchumi ya Nchi.

Wazungumzaji Wakuu:

1. Freeman Mbowe
2. Mchungaji Msigwa - Kiongozi wa Ziara
3. Mh. John Mnyika - Katibu wa Ziara
4. Dr. Wilbrod Silaa
5. Godbless Lema
6. Halima Mdee
7. Joshua Nassari
8. Mh. Wenje

Wazungumzaji Huru.

1. Ma Profesa wawili wa Uchumi - Chuo Kikuu Dar - Es - Salaam
watatoa elimu kwa umma kuhusu Uchumi na utekelezaji wa Mipango ya Taifa - Majina yanahifadhiwa kwa sasa.

2. Wanaharakati Mashuhuri Wawili - Majina yanahifadhiwa kwa sasa
3. Uongozi wa TAMWA - Taifa
4. Aliyekuwa Mgombea wa Ubunge Igunga
5. Mume wa Mwanamke aliyefumaniwa na kiongozi wa Juu wa CCM Igunga
6. Baba mzazi wa Kijana aliyekutwa amekufa Igunga mara baada ya Kampeni
6. Wazazi na Mke wa Kiongozi wa Chadema aliyeuwawa Arumeru mara baada ya Uchaguzi
7. Wazazi wa Vijana Wanne waliouwawa kwa kuvunjwa Shingo na kutupwa Jimbo la Arumeru Mashariki
8. Viongozi wa Dini kuu mbili za Kiislam na Kikristo
9. RPC Mstaafu
10. Ungozi wa Kitaifa LHRC (Haki za Binadamu) Tanzania
11. UONGOZI WA KITAIFA - TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA (THBUB)
12. Kiongozi wa wazee wa Iramba.

KAZI HII ITAKUWA NI YA MWEZI MMOJA.





Monday, July 2, 2012

ATEKELEZA FAMILIA BAADA YA MKE KUJIFUNGUA WATOTO WANAOFANANA NA NYANI.

Mtoto Alhaj.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mwanaharusi Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye shati Nyekundu na Abdulatifu.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha kuwa magumu.Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu. Pia aliondoka na matandiko yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).Alisema baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu aliozaa naye.Alisema katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.

“Mtoto wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa la saba mwaka huu. Ramadhani (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.

Mwanaharusi alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5) ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa kuanza shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi. Mawasiliano yao yanategemea ishara tu.

“Ukiacha matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu kubwa. Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.

Mwanaharusi alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na macho yao ni makubwa. Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.

Hata hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu na afya zao zikiwa njema kabisa. Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.

“Wakati bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika hospitali ya mkoa wa Singida. Alichunguzwa na alibainika kuwa na upungufu wa damu. Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi nyumbani”,alisema.

Alisema baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa, ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha magumu mno ambayo ni ya kuomba omba. Mnyawi pamoja na familia yake, amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea watoto wao pamaja, jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi kugoma kumrudia Mwanaharusi.

Naye mratibu elimu wa kata hiyo Mwekwa Mwekwa, alisema watoto hao wawili, shule inayowafaa ni ile ya watoto wenye mtindio wa ubongo na si hizi za kawaida.Jitihada ya kumtafuta Mnyawi ambaye anaishi kijiji hicho cha Ndulungu, hazikuzaa matunda baada ya kuelezwa kwamba baada ya kusikia waandishi wa habari watafika kijijini hapo, alifunga safari na kuelekea jijini Mwanza.

Tuesday, June 26, 2012

AJALI AJALI AJALI

Basi la abiria mali ya Summry likilipita basi lingine mali ya Kampuni ya SKY LINE katika kona kali jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria na mali zao. Madereva wa mabasi hawana budi kutambua dhamana waliyopewa ya kusafirihs roho za watu na kuhakikisha wanazilinda na kuepukana na ajali zisizo za lazima.

Popular Posts