Pages

Showing posts with label Sayansi na Tekinolojia. Show all posts
Showing posts with label Sayansi na Tekinolojia. Show all posts

Friday, July 6, 2012

IBM Supports Accelerated Adoption of Technology in Tanzania

President Jakaya Kikwete in a souvenir photo with Prof. Makame M. Mbarawa, the Minister for Communication, Science and Technology (Dr Makame Mbawara), Dr. Mark Dean, Chief Technology Officer and IBM Fellow, IBM Middle East (second left), Mr Jean-Christophe Knoertzer, General Manager IBM Central, East and West Africa and Africa and Country General Manager IBM Tanzania, Mr David Sawe (left) and their team when they paid him a courtesy call at the State House in the city on Wednesday July 4, 2012
President Jakaya Kikwete in talks with Dr. Mark Dean, Chief Technology Officer and IBM Fellow, IBM Middle East and Africa, Mr Jean-Christophe Knoertzer, General Manager IBM Central, East and West Africa and IBM’s Country General Manager, Mr David Sawe, when they paid him a courtesy call at the State House in the city on Wednesday July 4, 2012.
--
By a Correspondent
IBM has signed a collaboration agreement with the Tanzanian Ministry of Communication, Science and Technology to help accelerate the adoption of technology as part of Tanzania's ongoing development and strategy to increase its competitiveness in East Africa.

IBM will work with the Tanzanian Government to help achieve its vision of becoming a hub for trade in the wider East Africa region and to enhance sustainable economic development as outlined in the Tanzania National ICT Policy.

"This agreement supports the goals of the National ICT Commission to use innovative technologies and approaches to transform our infrastructures, build national data centers, increase cyber-security and invest in IT talent development," said Honourable Prof. Makame M. Mbarawa, the Minister for Communication, Science and Technology.

"Working with IBM will help to ensure that our initiatives are in line with international standards while positioning us to become competitive regionally and internationally, " he added.

IBM and the Government of Tanzania will co-operate to support the country's National ICT agenda developing simplified and more effective social and administrative systems for e-Government, e-Health and e-Education among other areas.

"IBM is a long-standing partner to the Tanzanian government and we are committed to supporting the country's economic growth and technical advancement," said Dr. Mark Dean, Chief Technology Officer and IBM Fellow, IBM Middle East and Africa. "A key part of our strategy in Africa is to build skills and a culture of innovation across the continent."

One of the focus areas of the agreement will be the port of Dar es Salaam which is the main point for Tanzania's imports and exports. The port also serves the neighboring landlocked countries of Zambia, Malawi, Burundi, Rwanda, Uganda, and the Democratic Republic of Congo.

By working with IBM, the Tanzanian government will explore the use of innovative technologies and approaches to help the port to operate more efficiently, transform revenue collection processes and strengthen regional trade links.

The agreement underscores IBM's commitment to Africa and builds on a similar agreement signed in March 2010 between IBM and the Tanzania Ministry of Education and Vocational Training to support the adoption of IT in the areas of education, research and development.


Significant progress has been made since that earlier agreement, including the provision of international guest lecturers, three academic awards, the donation of 37,000 technical reference books and journals to the University of Dodoma and the Dar es Salaam Institute of Technology, as well as international co-operation with Tanzanian academics.

IBM has also been actively engaged in Tanzania through its Corporate Service Corps program. Since 2009, 88 talented emerging leaders from more than 25 different countries have worked on one month assignments to Tanzania in projects aimed at social and economic development. Through this program IBM has dedicated over 10,000 hours of pro bono information technology and business consulting to Tanzania.

Sunday, June 24, 2012

TANZANIA NA CHINA ZAJIVUNIA MAFANIKIO YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na ubalozi wa China nchini Tanzania kuhusu mikakati ya serikali ya kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao wakati wa hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini.
Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ukiwemo ujenzi wa reli ya Uhuru (TAZARA) walioalikwa kwenye hafla hiyo Bw. Abdul Haji (kulia) na mama Roza Kangoma (kulia) ambaye ni mama wa balozi wa Zambia nchini Tanzania pia aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha mafunzo cha TAZARA.
Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule.
Raia kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kutoka nchini China katika miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania wakijipatia nakala mbalimbali za machapisho kuhusu shughuli za kilimo, siasa, Utamaduni, Teknolojia na masuala ya kijamii.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo katika ubalozi wa China nchini Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla hiyo.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Thursday, June 14, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Azindua Ofisi ya Tume Ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiof Ali Iddi akimpongeza Ndugu Said Omar Said { Sugu } kufutai ubunifu wake wa Gari iliyopewa jina la Sugu 11 .Balozi Seif aliikagua gari hiyo baada ya kukagua maonyesho ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na Ile ya Nguvu za Atomiki Tanzania hapo Tunguu.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia { actech } Bwana Saleh Mikidadi akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi aliyefungua rasmi Ofisi ya Tume hiyo pamoja na ile ya Nguvu za Atomiki iliyopo katika Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jmauhuri ya Muungano liliopo Tunguu.

Nyuma ya Afisa Mikidadi ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Muungano Mh. Makame Mnyaa Mbarawa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia bidhaa zilizotengenezwa na moja ya Kikundi cha wajasiri amali cha Kijiji cha Paje kwenye maonyesho ya uzinduzi wa Ofisi za Tume ya Sayansi na Teknolojia na Ile ya Nguvu za Atomiki hapo Tunguu

Bidhaa hizo zimetengenezwa kwa mali Ghafi ya Mwani chini ya usimamizi wa wataalamu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Sayansi ya Baharini ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
---
Uongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania {costech} umeombwa kushajiisha Wasomi hasa Vijana wa Vyuo Vikuu Nchini kupenda kufanya tafiti mbali mbali zitakazojenga Mazingira ya kumuondoa Mtanzania kwenye matatizo yanayomkabili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa ombi hilo katika Hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Tume hiyo ilyofanyika hapo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Balozi Seif alisema Tafiti kama hizo ambazo zitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mwananchi zinaweza kusaidia kupata Maendeleo kwa kasi zaidi katika Kipindi kifupi kijacho.

Alisisitiza kwamba Serikali kwa upande wake iko tayari kwa namna yoyote ile kutumia vyema matokeo ya Tafiti zinazofanywa na Wazomi wazalendo.

Hata hivyo Balozi Seif alieleza kuwa yapo baadhi ya matokeo ya Tafiti hubakia kuwa siri kwa Taifa lakini mengine yanastahiki kutolewa kwa Wananchi ili waelewe kinachoendelea kwenye maisha yao.

Balozi Seif alieleza kwamba wakati umefika kwa Makampuni pamoja na Viwanda vya hapa Nchini kujenga Utamaduni wa kutoa kazi zao za Utafiti kwa Tume hiyo ili ijipatie fedha za kuendesha shughuli zake za utafiti kama Nchi nyengine zilizoendelea.

Alieleza kwamba Tanzania imepania kuleta maendeleo kwa Wananchi wake kutokana na uamuzi wake wa kutenga Jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni Thalathini { 30,000,000,000/-} kwa ajili ya Utafiti na Maendeleo kwenye Bajeti yake ya Mwaka 2010/2012.

Balozi Seif alifahamisha kwamba Maendeleo bila ya Sayansi na Teknolojia hayapatikani kwani masuala hayo mawili yanakaribiana katika utekelezaji wake.

Akizungumzia Tume ya Taifa ya nguvu za Atomu Balozi Seif alielezea kufarajika kwake kutokana na mipango m,izuri ya Taasisi hiyo kuhudumia Zanzibar katika masuala ya usimamizi wa matumizi salama ya Mionzi.

Balozi Seif alisema ushirikiano wa pamoja wa Taasisi hiyo,Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika kuanzisha mradi wa Matibabu ya Saratani katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja unafaa kuungwa mkono.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa wa kusogeza karibu na Wananchi shughuli za Ofisi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomu.

Katika Taarifa yake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Iddi Suleiman Nyangarika Mkilaha alisema Taasisi yake itaendelea kutoa Elimu sahihi ya matumizi ya Mionzi.

Profesa Nyangarika alisema Taaluma hizo kwa sasa itazingatia zaidi katika sekta ya Viwanda pamoja na Vituo vya Afya ambavyo vinatumia Vifaa vyenye mazingira ya Nguvu za Atomiki.

Mkurugenzi huyo wa Tume ya Nguvu za Atomiki alifahamisha kwamba katika kupanua zaidi huduma zake Taasisi hiyo itaendelea kupima Mionzi katika Mimea ili kujua kiwango sahihi cha kulinda Vyakula kwa ajili yamatumizi bora kwa Wanaadamu.

Mapema Waziri wa Mawasiliano,Sayansina Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Makame Mnyaa Mbarawa alisema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Wataalamu wa ndani na nje ili kuona Tafiti zinazofanywa zinatmika kwa walengwa ambao ni Wananchi.

Alisema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Nguvu za Atomiki zimeanzishwa zikiwa na wajibu wa kusimamia tafiti na nguvu za Atomiki Nchini kwa kushirikiana na Taasisi za Kanda na zile za Kimataifa.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi Ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Popular Posts