Pages

Showing posts with label Jeshi la Polisi Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Jeshi la Polisi Tanzania. Show all posts

Wednesday, October 17, 2012

Maelezo Ya Jeshi La Polisi Kuhusiana Na Hatua Ya Kumkamata Sheikh Ponda


KATIBU WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU (T) SHEIKH PONDA ISSA PONDA AKAMATWA NA POLISI

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya tajwa hapo juu maarufu kama PONDA ISSA PONDA kwa makosa mbali mbali ya kuchochea vurugu na uvunjaji wa amani jijini Dar es Salaam.
Aidha hivi karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda aliongoza kundi la wafuasi wake na kuvamia kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika Manispaa ya Temeke mali ya Kampuni ya AGRITANZA ambayo ipo chini ya Kurugenzi ya Kampuni hiyo. Mnamo tarehe 12/10/2012 Ponda Issa Ponda aliwaongoza wafuasi wake walioteka eneo hilo wakidai kwamba wanakomboa.
Mali za Waislamu, zilizouzwa na BAKWATA, uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba kiwanja hicho kina hati miliki No. 93773 uliotolewa na Wizara ya Ardhi pamoja na mikataba mbali mbali ya kuuziana au kubadilishana kati ya BAKWATA na Kampuni tajwa hapo juu. Pia uongozi wa BAKWATA umeleta mashahidi kuthibitisha uhalali wa kiwanja hicho kumilikiwa na Kampuni tajwa. Hivyo watu wote waliovamia eneo hilo wakiongozwa na Sheikh Ponda wanakabiliwa na shtaka la kuingia kwa jinai pamoja na uharibifu wa mali katika eneo hilo. Sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda tarehe 16/10/2012 saa 4.00 usiku karibu na eneo la maficho yake ambapo aliletwa na pikipiki.
WATU 38 WAMEKAMATWA KWA KOSA LA  JINAI NA UHARIBIFU
Wakati huo huo sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda Polisi walifanya operesheni maalumu ya kuwaondoa wavamizi katika kiwanja tajwa hapo juu kinachomilikiwa na Kampuni AGRITANZA. Watu wapatao 38 walikutwa katika eneo la kiwanja hicho ambacho kati ya hao (7) ni wanawake na 31 ni wanaume.
Operesheni hiyo ilifanyika tarehe 17/10/2012 usiku wa manane kuanzia saa tisa hadi saa kumi na nusu usiku kwa muda wa dakika 90. Katika eneo hilo vilikutwa vielelzo mbali mbali vikiwemo visu na mapanga na pia nyenzo mbali mbali za ujenzi, pamoja na vifaa vya ujenzi, vielelezo hivyo vimehifadhiwa katika kituo cha Polisi tayari kwa ajili ya ushahidi mahakamani.
SHEIKH PONDA KUSABABISHA VURUGU NA VITISHO
Katika siku za hivi karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake chini ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kwa kufanya maandamano kinyume cha Taratibu na kuhamasisha umwagaji damu jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa ujumla.
Kwa ujumla Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania inayoongozwa na Sheikh Ponda haijasajiliwa kisheria lakini wanatihumiwa kwa uchochezi wa hali ya juu ambapo licha ya kufanya maadamano kinyume na sheria pia siku ya tarehe 12/10/2012 walisababisha kuvunja kwa makanisa zaidi ya manane, uharibifu wa magari na wizi au upotevu wa vifaa katika makanisa, yote hayo yameongozwa na Sheikh Ponda na madhara yake ni makubwa.
Sheikh Ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola pamoja na kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai watuhumuwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na kufikishwa mahakamani waachiwe mara moja kabla siku saba na kadhalika. Uchunguzi wa watuhumiwa wote 39 unaendelea na kufikishwa mahakamani mara baada ya kupitishwa na wakili wa Serikali kuthibitisha mashitaka.
S.H. KOVA – DCP
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUMU YA POLISI
DAR ES SALAAM
————————
Nukuu za matamshi ya Kamanda Kova alipokuwa akitoa taarifa:
  • “Sheikh ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola na kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai watuhumiwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na kufikishwa Mahakamani waachiwe mara moja kabla ya siku saba”
  • “Ponda alikamatwa juzi majira ya saa 4:30 usiku akiwa kwenye pikipiki kuelekea katika maficho yake maeneo ya Temeke”
  • “Juzi usiku sijalala kabisa kuhakikisha oparesheni ya kumkamata inakwenda salama, Ponda ni mjanja sana ila Serikali ina mkono mrefu kabla ajaingia katika maficho yake Temeke, alijaribu kukimbia ili atoroke lakini akakamatwa”
  • “Ponda akiwa na wafuasi wake walivamia kiwanja hicho cha agritanza na kudai kuwa wanakomboa mali za waislamu zilizouzwa na BAKWATA”
  • “kati ya watu 38 tuliowakamta wanawake ni saba na wanaume ni 31 na tuliwakuta na silaha mbalimbali kama visu, mapanga, sururu na vifaa vya kuvunjia na vya ujenzi, jenereta na kujenga jengo la haraka”
  • “Jeshi la Polisi limemvumilia Ponda kwa muda mrefu… watu wanaoandamana kinyume cha taratibu waache.”
  • “Nawasifu sana Wakristo ni wavumilivu, wana busara kwa tukio la Mbagala la kuchoma Makanisa la sivyo hali ingekuwa ya hatari na hata hivyo Jumuiya ya Taasisi za Kiislam haijasajiliwa kisheria”
  • “Wafuasi wengine wajisalimishe kwani opareheni inaendelea na watawachukulia hatua za kisheria”
  • “Nawaasa Wananchi kutumia akili zao binafsi na kuacha kufuata mkumbo kwa kuwa watashughulikiwa.”

Thursday, September 6, 2012

TBL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SH. MIL. 11 WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kuruthum Bambe (kushoto) akiwa na Mkaguzi wa Polisi, Zauda Mohamed wakati wa hafla hiyo.
Kamanda Mpinga (kulia) akiteta jambo na msaidizi wake, Kahatano wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia), akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga sehemu ya fulana 550, kofia 200 na stika 350 kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika hafla iliyofanyika, Dar es Salaam jana. Vifaa hivyo vina thamani ya sh. mil. 11.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga, akiangalia moja ya fulana baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia), akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga sehemu ya stika 350 kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika hafla iliyofanyika, Dar es Salaam jana. TBL pia ilikabidhi fulana 550 na kofia 200 vyote vikiwa na thamani ya sh. mil. 11.
Kamanda Mpinga akionesha stika hizo zenye ujumbe maalumu maadhimisho hayo
Kamanda Mpinga (kushoto), akitoa shukrani kwa TBL. Kutoka kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa kampuni hiyo, Steve Kilindo.

Sunday, September 2, 2012

Safari ya Mwisho ya Daud Mwangosi









Taarifa Ya Jeshi la Polisi Kabla ya Vurugu Baina ya Wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo, Mufindi,Iringa

JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.

Monday, August 27, 2012

FFU WALIVYODHIBITI MAANDAMANO YA CHADEMA MOROGORO

Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema

Askari waliokuwa katika eneo la tukio kabla ya kuanza kwa maandamano hayo

Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya chadema leo mjini morogoro




Gari la chadema lililokuwa likiongoza maandamano hayo

Mmoja wa kiongozi wa chadema akiwa amekamatwa akiwa ndani ya gari la polisi

Wafuasi wa chadema wakiwa na maandamao hayo mjini morogoro
Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada ya kutandikwa risasi na Polisi wakati wa vurugu za kuzuia maandamano ya chadema leo. Picha kwa hisani ya Father Kidevu

Popular Posts