Pages

Showing posts with label NHIF National Health Insurance Fund. Show all posts
Showing posts with label NHIF National Health Insurance Fund. Show all posts

Friday, August 17, 2012

NHIF YACHANGIA SH. MILIONI 3 UJENZI WA ZAHANATI YA SOMANGILA WILAYA YA TEMEKE DAR ES SALAAM

Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) , Mariam Wilmore (kulia) , akimkabidhi hundi yenye thamani ya sh. Milioni 3 Diwani wa Kata ya Somangila, Aisha Mpanjila (wapili kushoto), wengine ni Meneja wa NHIF Kanda ya Temeke, Imelda Likoko, . Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Somangila Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Somangila, Aisha Mpanjila (wapili kulia), akionesha hundi ya sh. Milioni 3 aliyokabidhiwa na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mariam Wilmore (kulia) kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Somangila. Wengine ni Meneja wa NHIF Kanda ya Temeke, Imelda Likoko (wapili kushoto) , na Meneja wa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Anjela Mziray.
Na Mwandishi Wetu
DIWANI wa Kata ya Somangila, Wilaya ya Temeke, Aisha Mpanjila amesema kitendo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya cha kusaidia Zahanati ya Mbutu kitahamasisha wananchi wengine kuchangia ujenzi unaoendelea katika zahanati hiyo na hatimaye kumaliza tatizo la miundombinu.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, jana ulikabidhi hundi yenye thamani ya sh. Milioni 3, kwa lengo la kusaidia ujenzi wa wodi ya akina mama na watoto.

Akipokea msaada huo, Diwani Mpanjila, alisema kuwa NHIF imeonesha njia na imekuwa mfano wa kuigwa hasa kwa kutambua mahitaji ya wananchi katika sekta ya afya.

“Kweli nyie ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya…pamoja na kusaidia wanachama wenu katika huduma za matibabu lakini mmekwenda mbali zaidi kwa kutoa hata msaada wa kuboresha vituo vya kutolea huduma msaada ambao unamgusa kila mtu…nawapongeza sana,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Diwani huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa maeneo hayo ambao ni wanufaika wa moja kwa moja na zahati hiyo kuunga mkono Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuchangia ili ujenzi wa wodi zilizopo zikamilike na zianze kutumika mara moja.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mariam Wilmore amesema NHIF imeguswa na matatizo ya wakazi wa kata hiyo hivyo itaendelae kusaidia kadiri ya uwezo wake.

Zahanati ya Mbutu inahudumiwa zaidi ya wakazi wa mitaa SITA inayozunguka kata hiyo.

Tuesday, July 17, 2012

NHIF YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU WA AFYA WA ZAMBIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba akizungumza na Ujumbe kutoka Zambia ambao umefika kwa lengo la kujifunza namna Mfuko huo unavyofanya kazi.
Ujumbe wa Wataalam kutoka Zambia ulioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Bajeti wa Wizara ya Afya, Mubita Lubelwa.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee akitoa maelezo ya namna NHIF inavyofanya kazi kwa ujumbe huo muda mfupi kabla ya kuanza mafunzo.
Wataalam wa Afya kutoka Nchini Zambia ,wakifuatilia mada zilizotolewa kuhusu Mifuko ya Afya hapa nchini (NHIF na CHF).
Baadhi ya Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya waliojumuika na ujumbe kutoka Zambia.

Sunday, July 15, 2012

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Yatembelea NHIF

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati kamati yake ilipofanya ziara katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu akisalimia wadau.
Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla nae akisalimia wadau.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Ndg. Emmanuel Humba akitoa maelezo mafupi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Mh. Deogratius Mtukamazina (kulia) akitoa salamu ya Bodi yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale jana kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi,Naibu Waziri wa Afya, Dk. Sirra Umbwa,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),Mh. Majaliwa K. Majaliwa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakifuatia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini hapo.
Meneja wa Idara ya Uanachama wa NHIF,Bi. Ellentruder Mbogoro akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii walipotembelea makao makuu ya Mfuko huo,Kurasini jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Nyaraka wa NHIF,Erastus Msigwa akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii moja ya mafaili ya Wanachama wa Mfuko huo yaliyohifadhiwa kwenye Masanduku ya Kisasa yanayotumia mfumo wa Umeme.

Popular Posts