Pages

Saturday, June 2, 2012

HOTUBA YA RAIS WA TANZANIA KWA WANANCHI JUNI 2 MWAKA 2012

Ndugu Wananchi,

Kama ilivyo ada, namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uhai na kutuwezesha kumaliza mwezi Mei salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza kwa njia hii kila mwisho wa mwezi, leo nitazungumzia mambo matatu.

Mkutano wa G-8
Jambo la kwanza, ni suala la usalama wa chakula na lishe. Duniani, inakadiriwa kuwa kuna watu milioni 925 wanaokabiliwa na njaa na lishe duni. Kati ya hao Afrika ina watu milioni 239 ambao ni karibu theluthi moja ya watu wote wenye tatizo la njaa na lishe duni kote duniani. Nchi za Afrika zenye tatizo la njaa kiasi cha kuhitaji msaada wa chakula kutoka nje ni 27. Kati ya hizo 11 zina matatizo makubwa zaidi. Tanzania siyo miongoni mwa nchi hizo, hata hivyo bado hatujafikia kiwango cha kujitosheleza kabisa. Hivi sasa tumefikia asilimia 95 na kila mwaka yapo maeneo nchini yanayopata msaada wa chakula kutoka Serikalini.

Mwaka 2009, katika mkutano wao wa L’Aquila, Italia, viongozi wa nchi nane tajiri kuliko zote duniani waliamua kuchukua hatua ya kuzisaidia nchi zinazoendelea duniani kukabiliana na tatizo la njaa na lishe duni. Katika mkutano ule waliahidi kutoa dola za Marekani bilioni 22 kwa ajili hiyo. Tanzania tunategemea kupata dola milioni 22.9.
Katika mkutano wa nchi hizo maarufu kwa jina la G-8 uliofanyika Camp David, Marekani tarehe 19 Mei, 2012, pamoja na mambo mengine walizungumzia suala la usalama wa chakula na lishe barani Afrika. Nia yao ni kuchangia katika juhudi zinazofanywa na mataifa ya Afrika zenye shabaha ya kutokomeza matatizo hayo. Tofauti na walivyofanya L’Aquila, safari hii waliamua kuchangia katika utekelezaji wa mipango na progamu za kuendeleza kilimo katika nchi za Afrika hasa zile zinazolenga kujenga usalama wa chakula na lishe.

Aidha, waliamua kuwa wataanza na nchi tatu na kuendelea kuziongeza kila baada ya muda fulani, badala ya kuanza na nchi zote mara moja. Hoja yao kubwa ni kwamba, wanataka kukusanya nguvu zao kwa nchi hizo chache ili kufanya kazi ambayo itakuwa na matokeo yanayoonekana katika kutokomeza njaa na kuboresha lishe. Hawakupenda kusambaza nguvu zao kwa nchi nyingi na kuishia kutokufanya kazi ya maana.

Ndugu wananchi;
Bahati nzuri katika programu na mipango ya nchi iliyokubaliwa kwa awamu ya kwanza ni Tanzania, Ethiopia na Ghana. Na, jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba mpango wetu wa kuendeleza kilimo katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania ulichukuliwa kuwa ni wa mfano. Maoni hayo ya nchi za G-8 ndiyo maoni ya WEF, Sekretariat ya NEPAD na Umoja wa Afrika, wote wameona kuwa mpango wetu unafaa kuenezwa barani Afrika kama mkakati sahihi wa kuendeleza kilimo, kujitosheleza kwa chakula na kupunguza umaskini.

Katika Bara la Afrika mkakati huo sasa unaitwa Grow Africa Partnership na tayari nchi saba zimeshajiunga nao. Nchi hizo ni Tanzania, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Ethiopia, Ghana na Burkina Faso.
Katika mkutano wa Camp David, nchi za Marekani, Japani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Urusi zimeahidi kuchangia nchi yetu katika juhudi zetu za kuendeleza kilimo na hasa zile zenye lengo la kujitosheleza kwa chakula na kuboresha lishe nchini. Ukichanganya na ahadi iliyotolewa na Umoja wa Ulaya katika mkutano huo, kiasi cha dola za Marekani milioni 897 zimeahidiwa kutolewa kwa nchi yetu kati ya sasa na mwaka 2015.

Ndugu Wananchi;
Mwaka 2006 tulizindua Programu Kabambe ya Kuendeleza Kilimo nchini maarufu kwa kifupi kama ASDP. Kwa kirefu kwa lugha ya Kiingereza ni the Agricultural Sector Development Programme. Programu hii ndiyo mwanzo wa safari yetu ya uhakika ya kuleta mapinduzi ya kilimo nchini Tanzania. Jambo la kwanza lililofanyika katika utayarishaji wa Programu hii ni kutambua vikwazo vinavyozuia maendeleo ya kilimo nchini na kupendekeza hatua za kuchukua za kuondosha vikwazo hivyo.

Mwaka 2008, katika tathmini iliyofanywa kwa ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi kwa uamuzi wa Baraza la Biashara Tanzania, ilidhihirika kwamba sekta binafsi ambayo ni wadau muhimu, haijahusishwa vya kutosha katika mikakati, mipango na programu za kuendeleza kilimo nchini. Kwa pamoja ilikubaliwa kuwa kasoro hiyo iondolewe ili wadau wote washirikishwe, yaani Serikali, wakulima wadogo, wakulima wakubwa na sekta binafsi. Vilevile, sote tulikubaliana kutoa kipaumbele cha juu kwa maendeleo ya kilimo. Kwa pamoja tuliafikiana kuwa mambo mengine yanaweza kusubiri isipokuwa kilimo. Matokeo ya maelewano hayo ndiyo yaliyozaa mkakati na kauli mbiu ya “Kilimo Kwanza”.

Ndugu Wananchi;
Tangu wakati huo, sekta binafsi nchini imekuwa inahusishwa na kushirikishwa kwa karibu katika utekelezajiwa ASDP na kuendeleza kilimo kwa jumla. Kwa upande mmoja sekta binafsi imekuwa inahusishwa katika upatikanaji wa zana na pembejeo za kisasa za kilimo kwa wakulima. Kwa ajili hiyo, wenzetu wa sekta binafsi wamekuwa wanategemewa kuleta na kuuza matrekta, mitambo na vifaa mbalimbali vya kilimo pamoja na mbegu, mbolea, dawa za kuua wadudu waharibifu wa mazao na za kukinga na kutibu maradhi ya mimea na mifugo. Hali kadhalika, wamekuwa wanajihusisha na ununuzi na usindikaji wa mazao ya mkulima na kuongeza thamani. Tunataka tuachane na kuendelea kuuza nje mazao ya kilimo kama malighafi na kununua bidhaa zilizotengenezwa na mazao hayo.

Upande mwingine tuliwategemea wenzetu wa sekta binafsi washiriki kulima mashamba makubwa. Wasiache kazi ya kilimo kufanywa na wakulima wadogo peke yao ambao uwezo wao si mkubwa wa kukabili matatizo ya kuongeza tija. Nafurahi kwamba wito wangu huo waliupokea vizuri na baadhi yao wameshaanza kufanya hivyo.

Ndugu Wananchi;
Swali kubwa walilouliza ndugu zetu hao siku ile ya tarehe 2 – 3 Juni, 2009 pale Kunduchi Beach Hotel ni kuhusu upatikanaji wa ardhi. Niliwaeleza kuwa upo utaratibu mzuri wa kuwapatia wakulima wakubwa ardhi ya kilimo na ufugaji. Utaratibu wenyewe ni kwamba kila wilaya imetakiwa kutenga ardhi kwa ajili ya wakulima wakubwa. Hilo likishafanyika, taarifa hutolewa kwa Kituo cha Uwekezaji na kuingizwa katika kitu kinachoitwa Benki ya Ardhi. Mwekezaji anapojitokeza, kulingana na aina ya kilimo anachotaka kujihusisha nacho, hugawiwa ardhi hiyo. Ardhi hiyo ni ile ambayo siyo inayotumiwa na wakulima wadogo. Katu hawanyang’anywi ardhi wakulima wadogo ili kuwapa wakulima wakubwa. Hiyo siyo sera wala madhumuni na malengo ya ASDP au Kilimo Kwanza.
Nalifafanua hili kuondoa hofu iliyokuwepo na upotoshaji uliokuwa unafanywa makusudi wa kuhusisha wakulima wakubwa na uporaji wa ardhi. Siyo makusudio yake hata kidogo.

Ndugu Wananchi;
Mwaka 2010 tukapanua wigo wa ushiriki wa sekta binafsi kwa kuihusisha sekta binafsi ya kutoka nje ya nchi. Mwaka huo pia, tukaamua kuipa sekta binafsi lengo maalum la kutekeleza nalo ni kushiriki katika kilimo cha kuhakikisha kuwa nchi yetu inajitosheleza kwa chakula na kupata ziada kubwa ya kuuza nje, kwa majirani zetu na kwingineko. Shabaha yetu hasa ilikuwa ni kujitosheleza kwa vyakula vikuu vya mahindi, mchele na sukari.

Aidha, tuliamua pia kuwa, kwa kuanzia tuelekeze nguvu zetu kwenye mikoa ya Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Iringa na Morogoro kwa vile mikoa hiyo ndiyo ghala la chakula la nchi yetu. Kwa vile mikoa hiyo ipo ukanda wa kusini ndio maana ikaja kuitwa Southern Agriculture Growth Corridor of Tanzania au SAGCOT. Tumeamua tukusanye nguvu za Serikali, wakulima, sekta binafsi na washirika wetu wa maendeleo kuwekeza katika kuendeleza kilimo katika mikoa hiyo.

Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa mpango wa kuendeleza kilimo katika ukanda wa SAGCOT una shabaha kuu mbili: Kwanza kabisa mpango unalenga kuboresha kilimo cha wakulima wadogo ili kitoke kuwa duni na cha kujikimu na kuwa cha kisasa na kibiashara. Chini ya mpango huu wakulima wadogo watasaidiwa na kuwezeshwa kupata na kutumia zana na pembejeo za kisasa za kilimo. Pia watawezeshwa kupata mikopo kwa ajili ya kilimo na masoko ya uhakika na yenye bei nzuri kwa mazao yao. Vile vile, huduma muhimu zitaimarishwa. Hapa tunazungumzia maafisa ugani na miundombinu ya umwagiliaji, barabara, umeme, maji safi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Pili, kwa pale inapowezekana kwa maana ya upatikanaji wa ardhi na aina ya mazao, kuihusisha sekta binafsi katika kilimo. Tayari utekelezaji wa mpango wa SAGCOT umeanza. Kamati ya Utendaji imeshaundwa na Sekretariati yake imeshateuliwa. Aidha, Mfuko wa Kuchochea Uwekezaji umeshaanzishwa na unaendelea kuchangiwa fedha.

Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa malengo ya SAGCOT kwa kilimo cha mpunga na kuongeza uzalishaji wa sukari yameanza kutekelezwa. Matayarisho yanaendelea kwa kilimo cha mahindi na mazao mengine.

Mpango huu utakapofanikiwa utakuwa na manufaa makubwa. Nchi yetu itajitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada kubwa ya kuuza nje. Inakadiriwa kuwa mapato yatokanayo na kilimo katika ukanda huu yatafikia dola bilioni 1.2 kwa mwaka, watu 420,000 watapata ajira na watu 2,000,000 wataondokana na umaskini uliokithiri.

Uwekezaji wake ni mkubwa na kwamba kiasi cha dola bilioni 3.4 kinahitajika kwa kipindi cha miaka 20. Kwa ushirikiano uliopo baina ya Serikali, sekta binafsi na wabia wetu wa maendeleo wakiwemo wa nchi za G-8, hayo yote yanawezekana.

Ndugu Wananchi;
Tukijitosheleza kwa chakula na kwa maana pana ya chakula chenye lishe bora tutakuwa tumefanikiwa kupata ufumbuzi wa tatizo kubwa la ukosefu wa lishe bora miongoni mwa wananchi wa Tanzania. Wanaoathirika sana na tatizo hili ni kina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. Ukosefu wa lishe bora huchangia asilimia 20 ya vifo vya kinamama wajawazito nchini na theluthi moja ya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano. Aidha, asilimia 42 ya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano wamedumaa na asilimia 16 wana uzito mdogo kulingana na umri wao na asilimia 59 wana upungufu wa damu. Kwa kina mama wajawazito asilimia 41 wana matatizo ya upungufu wa damu. Hali hii sio nzuri hata kidogo lazima tuibadili na tunaweza kufanya hivyo. Tunao mkakati wa kitaifa wa kuboresha lishe ambao kwa sehemu kubwa utanufaika sana na kufanikiwa kwa mkakati wa kujitosheleza kwa chakula.

Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
Ndugu Wananchi;
Jana tarehe 31 Mei, 2012 nilishiriki katika sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 47 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Mkutano wa 38 wa Mfuko wa Maendeleo wa Afrika. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Benki hii tangu ianzishwe mwaka 1964 kwa nchi yetu kuwa mwenyeji wa mikutano hii inayofanyika kila mwaka. Ni heshima kubwa sana kwa nchi yetu, nami kwa niaba ya Watanzania wenzangu wote, nimemshukuru sana Rais wa Benki hiyo, Dkt. Donald Kaberuka kwa ihsani kubwa aliyoifanyia nchi yetu.

Kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa kama huu ni jambo lenye manufaa mengi kwetu. Kwanza husaidia kuitangaza nchi yetu Barani Afrika na kwingineko duniani. Pili, ni fursa nzuri ya kuzungumza na viongozi wa Benki kuhusu mipango na miradi yetu ya maendeleo tunayohitaji msaada kutoka Benki hiyo.

Na, tatu, ni fursa nzuri ya watu wetu kufanya biashara. Mkutano huu umeshirikisha watu 2,500 ambao wametoka nje ya Tanzania na wanajitegemea kwa kila kitu. Wenye hoteli, migahawa, vyombo vya usafiri, huduma ya simu, internet na nyinginezo watakuwa wamefanya biashara nzuri katika wiki nzima kabla ya tarehe 28 Mei mkutano ulipoanza hadi 2 Juni, mkutano utakapofungwa. Ni kutokana na manufaa kama haya, ndio maana huwa tunahangaika kuvutia mikutano mikubwa kuja kufanyikia hapa nchini.

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

Watanzania Wenzangu;
Niruhusuni tena niwashukuru wenzetu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa mchango mkubwa waliotoa na wanaoendelea kutoa kuchangia maendeleo ya nchi yetu. Kwa miaka mingi Benki hii imekuwa inatupatia mikopo na misaada muhimu kwa maendeleo ya sekta mbalimbali nchini pamoja na zile za elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara, reli, umeme n.k.

Kwa msaada wa Benki hii tunajenga barabara ya Namanga – Arusha, Minjingu – Singida, Namtumbo – Tunduru, Iringa – Dodoma, Mayamaya – Babati, na Tunduru – Mangaka – Mtambaswala. Miaka ya nyuma pia walituwezesha kujenga barabara ya Mutukula – Muhutwe. Aidha, hivi sasa wanagharamia upembuzi yakinifu na usanifu wa reli mpya tunayotaka kuijenga kutoka Dar es Salaam hadi Rwanda na Burundi.

Matukio ya Uvunjifu wa Amani Zanzibar
Ndugu Wananchi;
Jambo la tatu ninalotaka kuzungumza nanyi leo ni matukio ya wiki iliyopita huko kwenye Jiji la Zanzibar katika mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Kama tujuavyo sote kulitokea ghasia zilizochochewa na viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu maarufu kwa jina la Uamsho. Taasisi hii imeanzishwa kwa madhumuni ya kidini, lakini hivi sasa viongozi wake wameamua kuyaacha madhumuni hayo na kubeba ajenda za siasa.

Siku za nyuma, ndugu zetu hawa walikuwa wakitumia muda mwingi kuilaumu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Baada ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa lawama hizo sasa hazisikiki. Lakini, mara tulipoanzisha mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mihadhara yao imeelekezwa kupinga Muungano na kuwakashifu viongozi waasisi wa Muungano na hata waliopo sasa. Isitoshe wamekuwa wakipandikiza chuki dhidi ya ndugu zao wa kutoka Tanzania Bara na wale wafuasi wa dini ya Kikristo.

Baya zaidi, katika uchochezi huo majengo na mali za Makanisa mawili zilichomwa moto, maduka ya watu kuvunjwa na mali zao kuibiwa. Kwa kweli vitendo hivi ni uhalifu ambao haukubaliki na wala hauvumiliki. Naungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kauli yake aliyoitoa jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ya kukemea vikali na kulaani uhalifu huo.

Ndugu Wananchi;
Ni jambo la kusikitisha na kushangaza kwamba, wenzetu hawa wamefanya uhalifu huo kwa hoja ya kupinga Muungano. Haiwezekani mtu anayepinga Muungano, akaitetea hoja yake kwa kuchoma moto makanisa au kuvunja maduka ya watu na kupora mali zao. Ukristo haukuingizwa Zanzibar na Muungano, bali ulikuwepo karne kadhaa kabla ya Muungano na wala haukutokea Tanzania Bara. Na kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais Ali Mohamed Shein jana, ukweli ni kwamba, dini ya Kikristo kama ilivyo ya Kiislamu imeenezwa Bara kutokea Zanzibar. Kanisa kuu la Anglikan Zanzibar lilijengwa kuanzia mwaka 1873 na lile la Katoliki kuanzia 1893 ni miongoni mwa Makanisa makongwe kuliko mengi kama siyo yote kwa upande wa Zanzibar na Bara.

Katika hotuba yake ya jana, Mheshimiwa Rais, Dkt. Ali Mohamed Shein,pamoja na kueleza kwa ufasaha ukweli huu, pia alisisitiza suala la haki na uhuru wa Kikatiba wa mtu kuchagua au kubadilisha dini au imani yake. Katika kutumia uhuru huo, mtu hastahili kuingiliwa au kulazimishwa na mtu yo yote. Hayo pia ndiyo matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kweli yanayofanywa na ndugu zetu wa Uamsho ya kuchoma moto makanisa siyo sawa hata kidogo. Na, wanapoyafanya kwa kisingizio cha Muungano ni jambo lisiloeleweka kabisa na wala halina mantiki. Labda wenzetu wana lao jambo.

Ndugu Wananchi;
Jambo lingine la kushangaza zaidi ni kule kutokea vurugu na ghasia hizi dhidi ya Muungano wakati ambapo Serikali imetoa fursa sasa kwa watu kutoa maoni yao kwenye mjadala wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Kama tujuavyo sote, Tume ya Katiba imekwishaundwa na inajiandaa kupita kote nchini kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya waitakayo. Kama mtu ana maoni yake kuhusu Muungano, hiyo ndiyo fursa ya kufanya hivyo. Utaratibu mzuri umewekwa kwa ajili yetu sote, vurugu za nini?

Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Mimi sioni sababu ya msingi ya kusababisha kuvurugika kwa amani kwa jambo ambalo limewekewa utaratibu muafaka wa kulishughulikia. Nawaomba tutumie utaratibu mzuri uliowekwa badala ya kufanya mambo yanayoleta mifarakano katika jamii na yanayosababisha uvunjifu wa amani na yanaharibu sifa na sura ya Wazanzibari na Watanzania isivyostahili.

Ndugu zangu,
Haipendezi wala haifurahishi kwa Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya raia wake. Lakini, kama hapana budi, Serikali lazima ifanye na haitasita kufanya hivyo. Narudia kuwasihi viongozi na wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho kurejea kwenye madhumuni ya msingi ya jumuiya yao. Wajiepushe na ajenda za kisiasa na kupandikiza chuki zitakazosababisha mifarakano baina ya wananchi wa pande zetu mbili za Muungano na baina ya Wakristo na Waislamu. Watanzania ni ndugu na wamekuwa wanaishi pamoja kwa upendo na furaha licha ya tofauti zao za rangi, makabila, dini na maeneo watokako. Kimeharibika kipi hata leo yatokee haya? Aidha nawaomba wenye maoni kuhusu Muungano wetu, muundo wake na uendeshaji wake watumie fursa ya mjadala wa Katiba kutoa maoni yao. Huhitaji kufanya ghasia kutoa maoni yako!

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia fursa hii pia kuwapa pole wale wote walioathirika na vurugu zilizotokea. Nawaomba wawe wastahamilivu, hiyo ndiyo mitihani ya maisha. Serikali zetu mbili zitafanya kila lililo kwenye mamlaka yake kuwahakikishia wananchi wote usalama wa maisha yao na wa mali zao.

Nawapongeza vijana wetu wa Jeshi la Polisi kwa juhudi kubwa waliyoifanya ya kudhibiti hali ambayo mwelekeo wake haukuwa mwema. Nawaomba waendelee kuwa macho ili watu wasioitakia mema nchi yetu na watu wake wasipate nafasi ya kutuvurugia amani na utulivu wetu. Naamini tukidumisha utamaduni wetu wa kuheshimiana, kuvumiliana na kuzungumza pale tunapotofautiana hakuna litakaloharibika. Haya shime tufanye hayo.

Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.

TAARIFA YA RAIS WA SMZ KUHUSU HALI YA ZANZIBAR

TAARIFA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA
TAARIFA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA
LA MAPINDUZI, MHESHIMIWA DKT. ALI MOHAMED SHEIN,
KWA WAANDISHI WA HABARI, WAHARIRI NA WANANCHI KUHUSU HALI YA NCHI, TAREHE 31 MEI, 2012

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Assalam Aleykum

Namshukuru Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, kwa kutupa afya njema tukaweza kuzungumzia mambo yenye mustakbal mwema wa hali ya nchi yetu kwa jumla.

Napenda kutanguliza shukurani zangu kwa wananchi wa Zanzibar kwa kuendeleza na kudumisha amani hasa tokea kupatikana kwa maridhiano ya kisiasa baina ya vyama viwili vikuu vya siasa hapa Zanzibar, Chama cha Mapinduzi na Chama cha CUF, yaliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa mnamo Novemba, 2010 kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Maridhiano hayo yalidhihirisha silka, ustaarabu na utamaduni wa Wazanzibari kuishi pamoja kwa kuheshimiana , kusikilizana na kushirikiana katika mambo yao ya kiuchumi na ya kijamii na maendeleo yetu.

Kama tunavyoelewa kwamba Zanzibar ina watu wa makabila na dini tofauti. Wazee wetu wa asili walisema “Zanzibar ni njema atakaye na aje”. Ustaarabu huu ulianza kutumika tangu ulipoanza kuingia Uislamu na kuendelea hadi kufika wageni kutoka Uajemi (washirazi), Ureno na Oman walioanzisha utawala wao katika karne mbali mbali hadi ya 18. Uislamu uliingia Zanzibar mara tu baada ya kuwepo katika nchi ya Saudi Arabia. Kadhalika, Ukristo uliingia Afrika Mashariki alipofika Mvumbuzi wa Kireno, Vasco da Gama mwaka 1498 na hatimae kuja Wamishionari wa kwanza wakiongozwa na Ludwig Krapf mwaka 1844. Mfalme wa wakati huo wa Zanzibar aliwaruhusu kujenga Kanisa la Anglikana la Church Missionary Society (CMS) liliopo Mkunazini. Krapf baadae aliruhusiwa kujenga mishionary Mombasa. Madhehebu mengine ya kikristo yaliingia Zanzibar katikati ya karne ya Kumi na Tisa na kuenea sehemu za bara kutokea hapa Zanzibar, na kanisa la pili kubwa la Minara Miwili lilijengwa katika eneo la Shangani Mjini Zanzibar.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,
Naelezea haya ili nikumbushe sifa ya Zanzibar kuwa ni pahala ambapo watu wa dini mbali mbali walifika na kuweka makazi yao na kuendeleza shughuli zao za maisha pamoja na kidini. Anayeijua Zanzibar vizuri atakumbuka kwamba ilikuwa taabu kumtambua Muislam au Mkristo kwa sababu wafuasi wengi wa dini hizo walikuwa na tamaduni za mavazi ya aina moja, wakicheza na kusoma pamoja. Baadhi ya ndugu zetu hao leo tunaishi nao pamoja.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,
Hii ndio hali ya dini ya Kiislamu na Ukristo hapa Zanzibar. Kuvumiliana na kuelewana kulikuwa ni chachu ya amani kwa muda mrefu na kulichangia kuondoa ubaguzi. Kwa mara nyingi sherehe zao zilikuwa zinahudhuriwa na watu wa dini zote. Aidha, wafuasi wa dini hizo walikuwa wakihudhuria shughuli za jamii kwa pamoja na kujadili mambo ya maslahi ya nchi kwa pamoja. Katika Afrika Mashariki ukiongelea uvumilivu wa kidini mfano mzuri ni wa hapa Zanzibar. Mnamo mwaka 1953 yalifanyika mashindano ya sanaa ya uchoraji katika eneo la Afrika Mashariki ya kuonesha uvumilivu wa kidini. Mshindi wa mashindano haya alitokea Zanzibar ambae mchoro wake ulionesha msikiti, kanisa na baina yake palikuwa na temple. Mchoro huu uliashiria mfungamano wa kidini wa watu wa Zanzibar tangu enzi .

Zaidi ya maelezo hayo ya kihistoria, Katiba ya Zanzibar ya 1984 kifungu cha 19(1) kimeelezea kuwa “kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani na wa uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa kubadilisha dini au imani yake”, ambapo pia, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nayo inazungumzia hayo hayo. Aidha, miongoni mwa masuala tunayokwenda nayo vizuri sisi viongozi ni hili suala la kuheshimu imani za dini mbali mbali hapa Zanzibar.

Mfano ni tarehe 16 Septemba, 2011, mimi nikiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi nilikutana na viongozi wa dini mbali mbali waliokuwa wakijihusisha na juhudi za kuendeleza amani nchini. Pia, nilihudhuria kutawazwa kwa Askofu Michael Henry Hafidh wa kanisa la Aglikana tarehe 15 Aprili mwaka huu na nilipewa fursa ya kuhutubia wafuasi na kuwaelezea msimamo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya imani za watu na kutobagua dini.

Kadhalika, mimi na viongozi wenzangu tumekuwa tukikutana na kujadiliana na viongozi kadhaa wa dini ya Kiislamu. Kwa mfano tarehe 25 Aprili, 2012 Kamati maalum ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikutana na viongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Maimamu na Mashekhe kuzungumzia hali iliyotokea nchini katika kufanya mihadhara ikiashiria kama kwamba kutatokea uvunjwaji wa amani tuliyonayo. Kamati hiyo ilifanya kazi nzuri sana. Tutaendelea na utaratibu huu wa kukutana na viongozi wa dini zote ili kujadiliana hali halisi katika jamii. Hivi majuzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed, Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi pamoja na IGP Said Mwema, wamefanya hivyo juzi na mikutano kama hiyo itaendelea kufanywa kwa utaratibu wake.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,
Tunaelewa vyema kwamba mustakabali wa nchi yetu umo katika mjadala mkubwa wa kisiasa. Msingi mkuu wa hayo ni mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maridhiano ya viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tulikubaliana kuwa na mchakato wa mabadiliko ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika kikao cha pamoja na viongozi wa dini zote Aprili 25, mwaka huu, iliwasihi sana viongozi hao watumie busara na wafuate taratibu zilizowekwa kuhusu marekebisho ya katiba. Walitakiwa kuwaomba wafuasi wao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjaji wa amani katika nchi yetu. Wote walitakiwa kushiriki ipasavyo katika mchakato wa mabadiliko ya katiba utakapoanza.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,
Wakati huo huo, kabla ya kuanza mchakato wa mabadiliko ya katiba, Serikali zetu mbili, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tangu mwaka 2006 tumekuwa tukifanya mazungumzo ya pamoja kuhusu mambo ya Muungano kupitia Kamati ya pamoja inayozungumzia mambo ya Muungano inayoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuzungumzia kero za Muungano. Mimi nilipata nafasi ya kuingonoza Kamati hii kuanzia mwaka 2008 hadi 2010. Hivi sasa Kamati hio inaongozwa na Mheshimiwa Dk. Mohammed Gharib Bilal ili kujadili kero na mapungufu katika mambo mbali mbali ya Muungano wetu.

Vikao mbali mbali vinaendelea kufanyika. Pande zote mbili zimekuwa zikiwasilisha mambo ambayo yanajichomoza na yanayoendelea kuchomoza kama kero kwa Sekretarieti ambayo ina wajumbe sita, watatu kutoka kila upande wa Muungano.

Sekretarieti hii ina jukumu la kuandaa ajenda za mikutano ya ngazi za Wataalamu, Makatibu Wakuu, Mawaziri na hatimae kikao cha juu kabisa kinachowajumuisha Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uwenyekiti wa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa vikao vilivyofanyika ni:
1. Vikao 4 vya Sekretarieti vilivyofanyika kwa lengo ka kuratibu utekelezaji wa yatokanayo katika kikao cha mambo ya Muungano.
2. Vikao 6 vya ngazi ya watendaji wa sekta mbali mbali husika kujadili utekelezaji na taratibu za kisheria kwa mambo yote ambayo yameainishwa katika kero za Muungano.
3. Vikao 4 vya ngazi ya Makatibu Wakuu kujadili maamuzi ya watendaji.
4. Vikao vitatu vya ngazi ya Mawaziri kwa ajili ya kuandaa mapendekezo ya kikao cha juu cha mambo ya Muungano.
5. Kikao kimoja kati ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichofanyika Dar es Salaam tarehe 28 Januari mwaka huu.

Wana ratiba ya kuandaa kikao chengine hivi karibuni.
Miongoni mwa mambo yaliyojitokeza hadi sasa na yaliyopata nafasi ya kujadiliwa ni haya yafuatayo:
1. Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia.
2. Ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
3. Uvuvi katika Ukanda wa Bahari Kuu.
4. Ushirikiano wa Zanzibar na Taasisi za Nje.
5. Ajira kwa Watumishi wa Zanzibar katika Taasisi za Muungano.
6. Uwezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukopa Ndani na Nje ya Nchi.
7. Kodi ya Mapato.
8. Usajili wa vyombo vya moto.
9. Ongezeko la gharama za umeme kutoka TANESCO kwenda ZECO.
10. Uharamia na utekaji nyara wa Meli.
11. Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo.
12. Taarifa ya utekelezaji wa masuala ya Muungano.
Changamoto zipo na zitafanyiwa kazi.

Nimeona haya niyaseme ili wananchi waelewe mambo haya muhuimu yanayofanywa na Serikali zote mbili juu ya suala hili.

Kutokana na jitihada hizi zinazochukuliwa na Serikali zote mbili, pamoja na kuitumia vizuri fursa tuliyopewa ya kuweza kuwasilisha maoni yetu katika marekebisho ya Katiba, matumaini yangu ni kuwa kwa pamoja tutaweza kuondosha kero hizi na kuandaa Katiba mpya itakayotuletea maendeleo makubwa nchi yetu. Haya ni masuala muhimu kwa ustawi wa nchi yetu. Nawasihi wananchi wayakabili wakiwa na subira na busara ili tuijengee mustakbali mzuri nchi yetu katika mambo 12 niliyoyaorodhesha hapo juu mambo mengi tayari yamepatiwa ufumbuzi na yapo baadhi ambayo yanafanyiwa kazi.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar alitangaza majina ya Tume ya mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Jaji Agostino Ramadhani. Naelewa kuwa hadi sasa sio wananchi wengi wanaoijuwa sheria hiyo. Tume inafanya utaratibu wa kuwaelimisha wananchi juu ya sheria hii ili wapate kutoa maoni yao kwa njia bora zaidi.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yo yote ile, wako huru kutoa maoni yao kwa njia ya amani na salama kwa Tume hiyo itakapokuja kuanza kazi zake. Aidha, wananchi hawajawekewa vizuizi katika kutoa maoni yao, ila tu ni kuzingatia sheria za nchi na taratibu zake. Tume nayo imepewa uhuru wa kusikiliza maoni ya wananchi kwa kuzingatia sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83 (Toleo la mwaka 2012).

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Ni jambo la kusikitisha sana na kutia majonzi kuwa katika siku chache zilizopita kumezuka vitendo vya uvunjaji sheria. Tumeshuhudia maandamano na mikutano yenye sura ya dini lakini yenye ujumbe wa siasa, hasa kwa kuuzungumzia Muungano wetu. Vitendo hivyo vilikuwa chachu ya machafuko yaliyojitokeza tarehe 26 Mei, 2012.

Viongozi na wafuasi wao wasiojali sheria, ustaarabu na utamaduni wa kihistoria wa Kizanzibari walichoma moto majengo, mali za watu wasio na hatia na makanisa, wamevunja maduka ya raia na kuiba mali zao na wamekuwa wakitoa matamshi ya vitisho na ubaguzi ambavyo vimejenga khofu kwa wananchi. Nimeshangaa sana uhusiano gani uliopo kati ya kuzungumzia muungano na matukio hayo ambayo hatukuyatarajia kutokea. Haya ni kinyumbe na Katiba na sheria zetu – lakini yametokea.

Mtakumbuka kwamba hivi karibuni, tarehe 21 Machi, 2012 nilikuwa na ziara kwenye mikoa mitano ya Zanzibar. Katika mikutano yangu ya majumuisho wakati wa ziara ya wilaya zetu zote za Unguja na Pemba, nilikuwa nikitahadharisha sana na kueleza kwamba hatutovumilia kwa hali yoyote uvunjaji wa sheria. Nilisema katika Mkutano wangu wa mwisho wa majumuisho, tarehe 9 Mei, 2012 baada ya ziara ya Mkoa wa Kusini Unguja, kwamba Serikali haitomuonea muhali mtu yeyote atayethubutu kuharibu amani yetu. Hilo lilikuwa ni onyo kwa kila mmoja wetu. Maana ishara tuliziona kupitia mihadhara yao na Serikali ilichukua jitihada za kukabiliana nayo kwa kuzungumza nao.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Kutokana na matokeo hayo ya siku ya tarehe 26 Mei, 2012, Jeshi letu la Polisi lilichukua hatua za haraka kuidhibiti hali iliyojitokeza, wengi wenu mliiona hali ilivyokuwa. Kadhalika, Jeshi la Polisi walihakikisha kwamba wale wote waliohusika na vitendo hivyo vya uharibifu na aibu kwa nchi yetu na jamii ya Kizanzibari wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kuzingatia sheria za nchi ziliopo hapa Zanzibar. Hakuna atakaeonewa wala kudhulumiwa na kila mmoja atahukumiwa kwa kesi inayomuhusu na kwa mujibu wa sheria ziliopo.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Nachukua fursa hii kwanza kutoa pole kwa ndugu zetu waliotiwa hasara ya mali zao. Pia, nawapa pole wananchi wote kwa usumbufu wote uliojitokeza. Naelewa vyema kuwa wananchi wamepata hasara kubwa ya kiuchumi kwa baadhi ya wananchi kuvunjiwa maduka yao, kuibiwa na pia kukatizwa shughuli zao za kujitafutia riziki na maisha yao. Kwa bahati mbaya, wako pia waliofikwa na matatizo ambayo hawakuyategemea wala kuyazowea wakati polisi wakifanya kazi zao. Serikali inaendelea kufanya tathmini ya hasara zilizotokea na pia inazingatia hatua za kuchukua katika hasara hizo.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Baada ya hayo, napenda kuwaarifu wananchi wote kwamba hatua za Serikali zetu mbili kuidhibiti hali ya usalama zitaendelea, ili amani idumu na usalama wa wananchi, mali na maisha yao uwepo wakati wote. Kwa wale wanao vunja sheria na viongozi wao tunawataka watambue kwamba Serikali hatovumilia vitendo walivyovifanya. Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu ye yote atakayevunja sheria na yule mwenye lengo la kuiharibu amani na utulivu wetu. Amani ambayo haikuja kwa bahati tu, bali imehangaikiwa kwa muda mrefu, tutailinda hali hiyo kwa nguvu zetu zote.

Kadhalika, nataka wananchi waelewe kwamba Serikali haitoingilia shughuli za kweli za kidini au vitendo halali vya viongozi na wafuasi wa dini yoyote. Kwa wale wenye maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tungewasihi sana wasubiri utaratibu wa kutoa maoni kama Tume ya Mabadiliko ya Katiba itavyotangaza. Wafahamu fika kwamba kwenda kinyume na sheria iliopo ni kosa la jinai, kwa sababu ni sheria iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama ilivyozoeleka, shughuli za ibada za pamoja zifanywe katika nyumba za ibada na ikiwepo haja ya kufanya nje, iwe kwa kufuata taratibu zilizowekwa nchini haya yanajulikana na lazima yazingatiwe. Kwa kutunza amani na utulivu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imetangaza hatua kadhaa, miongoni mwa hatua hizo ni kupiga marufuku mikusanyiko ya aina mbali mbali, maandamano na mihadhara ambayo haijapata kibali cha Serikali hili ni lazima kila mmoja wetu azingatie, huu sio wakati wa kubeza, na kila mtu azingatie sheria. Mikutano ya halali ya kijamii haitaingiliwa hata siku moja na pale pa kutaka ulinzi Jeshi la Polisi litafanya hivyo. Napenda kuwatoa hofu waumini wa dini zote kwamba shughuli za ibada hazitoingiliwa na waumini wa dini hizo wataendelea na ibada zao kama Katiba ya Zanzibar ya 1984 na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Pamoja na kudhibiti amani na kuwahakikishia usalama wananchi, juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea pia kudumisha sifa ya kuendeleza amani ambayo kama itapungua seuze kuondoka kwake kutaathiri utalii ambao ni tegemeo la uchumi wetu, ni jukumu letu kuendeleza amani na ni jukumu letu kuwalinda wageni wetu wanaokuja kututembelea. Kuathirika kwa utalii kutawaathiri wananchi ambao kwa kiasi ya asilimia 60 za shughuli zao zinahusiana na sekta hiyo. Wananchi hawa ni pamoja na wakulima, wavuvi na wafanyabiashara mbali mbali zikiwemo zile biashara za usafiri, mikahawa na hoteli. Nimeshabainisha katika mikutano mbali mbali kuwa sekta ya Utalii inachangia zaidi ya asilimia 80 ya fedha za kigeni tunazoingiza nchini. Tutambue kwamba hao wanaofanya fujo ni waharibifu wa uchumi wetu na kamwe tusiwape nafasi katika kutimiza malengo yao.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Natoa wito kwa wananchi wote wanaopenda amani washirikiane na Serikali yao katika kudumisha amani hiyo. Wafuasi wa dini wazitumie nyumba za ibada kwa kufanyia ibada na kutumia wakati wa ibada zao kuamrishana mema na kukatazana mabaya. Wazazi wachunguze myenendo ya watoto wao na wachukue dhamana yao ya kuwalea watoto hao katika maadili mema na kila wakati wawatahadharishe juu ya kutokushiriki katika vitendo vya uvunjaji wa sheria. Viongozi wa jamii nao wanajukumu la kuisaidia jamii katika kufikia misingi ya kuwa raia wema na kutojiingiza kwenye vitendo vya uvunjaji wa sheria. Ni jukumu letu sote kuilinda na kuitekeleza misingi ya haki za binadamu na utawala bora, hili ni jukumu la kila mmoja wetu si Serikali tu.

Ni jukumu letu sote tuidumishe misingi ya ustarabu na mila zetu, kwa hakika si vizuri kutaka kuiga kila tuliloliona katika nchi za nje. Lakini tuyaige yaliyo mazuri yenye kujenga uadilifu na utamaduni bora, lakini katu mabaya tusiyaige hayana maana kwetu. Aidha, wakati Serikali inaendelea kudhibiti usalama, nawataka viongozi hasa viongozi wa jamii wawache kutoa lawama zisizokuwa na msingi katika hali hii. Viongozi wa dini, siasa na jamii wawe waangalifu wa matamshi yao, kwani Zanzibar na Tanzania ni yetu sote. Linapoharibika ni letu sote na linapotengamaa ni letu sote.

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Kwa kumalizia, natoa tena pole kwa wananchi wote wa Zanzibar na ndugu zetu wa kikristo walioathirika na vitendo viovu vilivyotokea hivi karibuni. Pia, nawapa pole wale wote walioathirika kwa njia mbali mbali.

Nawasihi sana wananchi tuendelee kuvumiliana, tuheshimiane na tushirikiane katika shughuli hasa zile za kuiletea maendeleo nchi yetu na kila mmoja wetu kupata manufaa. Tuendele kupendana na tudumishe umoja wetu kama ulivyo utamaduni na silka zetu. Jeshi letu la Polisi litaendelea na kutimiza wajibu wao kwa faida yetu na amani ya nchi yetu. Nataka niwahakikishie wananchi wote kwamba tutaendelea kuyalinda Mapinduzi, tutayaendeleza kwa ajili ya maslahi ya kila mmoja wetu na Wazanzibari wote. Nataka niwahakikishie wananchi wote kuwa Mapinduzi yetu tutayalinda kwa maslahi ya wananchi wetu wote.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Friday, June 1, 2012

KUAHIRISHWA KWA MKUTANO WA MADAKTARI WOTE NCHINI

Kwa Madaktari wote

YAH: KUAHIRISHWA KWA MKUTANO WA MADAKTARI WOTE NCHINI

Chama cha madaktari Tanzania (MAT) na Kamati ya Jumuiya ya Madaktari nchini tunapenda kuwataarifu madaktari wote kuwa ule mkutano wa mrejesho wa mazungumzo ya kamati ya Rais ya kushughulikia mgogoro wa madaktari na serikali uliopangwa kufanyika jumamosi tarehe 2/6/2012 umeahirishwa hadi jumamosi tarehe 9/6/2012.

Hii ni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kukamilika kwa taarifa ya kikao cha leo (cha kamati ya rais) (31/05/2012), pia kamati inaendelea kukusanya taarifa muhimu kuhusu msimamo wa mwisho wa serikali katika madai yetu yote ili tuweze kuwa na mrejesho uliokamilika.

Madaktari wote tunaombwa kuhamasishana na kuhudhuria kwa wingi kikao hicho cha tarehe 9/6/2012 kwani kitakuwa kikao muhimu sana kwa mustakabali wa fani yetu, huduma kwa wagonjwa na maisha yetu.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Dr. Namala P. Mkopi
MAT, President

TAMKO LA MAASKOFU KUHUSU MACHAFUKO NA HALI YA VITISHO ZANZIBAR

Sisi Maaskofu, Mapadre, Wachungaji na Waumini tunaoishi Zanzibar,
tumekutana leo tarehe 30 Mei 2012 kufutia hali ya machafuko, uvunjifu
wa amani, uchomaji wa Makanisa, uharibifu wa mali za Kanisa na vitisho
dhidi ya Wakristo na mali zao.

Tumekutana na tunatoa tamko baada ya muda mrefu wa kimya na uvumilivu
tuliosafiri nao kwa takribani miaka 11, kwa kumbukumbu zetu tangu
mwaka 2001. Tunajua na tunauambia umma wa wapenda amani kuwa matukio
ya tarehe 26 hadi 28 Mei 2012 ni matokeo ya mahubiri na mihadhara
ambayo imekuwa ikiendeshwa iliyolenga kwa makusudi kuutukana na
kuukashifu Ukristo hapa visiwani Zanzibar na hivi kupandikiza hofu
miongoni mwa waumini wa dini ya Kikristo. Tunashawishika kusema kuwa
ufadhili na ushawishi wa vurugu na vitisho hivi vina udhamini wa ndani
au nje ya nchi yetu.

Tumefikia hatua hiyo baada ya matukio mbalimbali yaliyokuwa yanafanywa
dhidi ya Kanisa na mali zake tangu mwaka 2001 hadi hivi majuzi
yalikuwa yakitolewa taarifa kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa
visiwani Zanzibar lakini ushirikiano umekuwa mdogo na kwa sehemu kubwa
dhaifu sana. Kwa maelezo na vielelezo ni kwamba, jumla ya makanisa
yasiyopungua 25 yamevunjwa na kuchomwa moto tangu mwaka 2001, pamoja
na ahadi za Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo
yote yaliyopata kutolewa taarifa hakuna hata moja lililothibitika
wahusika kukamatwa, kufikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua za
kisheria.

Kumekuwa pia na vitendo vya kuchoma magari huko Pemba na hapa Unguja,
na Serikali kwa upande wake imeshiriki hata kupora ardhi na majengo ya
Kanisa hapa Unguja na huko Pemba.

Tumebaini pia hasa baada ya matukio ya vurugu za tarehe 26 hadi 28 Mei
2012 kuwa kuna mikakati ya makusudi ya kuwafanyia Wakristo vurugu.

Mikakati hiyo inajumuisha mambo kama vile kuchoma Makanisa zaidi,
kuharibu mali za Makanisa yakiwemo mashule, vituo mbalimbali vya
Kanisa vinavyotoa huduma za kijamii hapa Visiwani.

Mkakati au mpango huo umepangwa na unakusudiwa kutekelezwa kati ya
tarehe 1 na 2 Juni, na tarehe 8 na 9 Juni mwaka huu. Tunazo taarifa
tunazoweza kuzithibitisha kuwa baadhi ya Wakristo wamekuwa wakitumiwa
jumbe za simu za mkononi (SMS) zikiwatisha na kuwataka waondoke
visiwani humu mara moja hata kama ni wazawa.

Sehemu ya pili ya mkakati ni kuwasaka Wakristo nyumba kwa nyumba kwa
ajili ya kuwaangamiza, kuwabaka na kuwalawiti.

Chakusikitisha zaidi ni pale ambapo baadhi ya walinzi wa Usalama wa
raia hasa Polisi wenye asili ya hapa Visiwani Zanzibar kusikika
wakisema kuwa wataunga mkono vurugu kila zitakapotokea.

Kufuatia maelezo hayo yote, Sisi Maaskofu, Wachungaji, Mapadre na
waumini tuliokutana leo, tunapenda kwanza kutoa neno la shukrani kwa
uongozi wa Serikali kwa ushirikiano iliyotuonyesha kufutia matukio ya
hivi majuzi, na hasa kwa kupewa fursa za kukutana na viongozi na
kusikilizwa.

Tunatamka kuuelezea umma wa wapenda Amani wote tukisema, tumechoswa
kuishi na kuchukuliwa kama raia wa daraja la pili katika nchi yetu.

Tunaonya kuwa hatuko tayari tena kuvumilia vitendo vya uvunjaji wa
amani na haki zetu na tabia za kufanywa tuishi kwa hofu.

Kadhalika tunaiomba seriakli yetu ituhakikishie usalama wa maisha
yetu, mali zetu pamoja na majengo yetu ya ibada.

Wito wetu kwa viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini ni kuwa, kila
mmoja anawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa kwa
mujibu wa sheria za nchi na kwmba kila mmoja ahubiri kwa lengo la
kukuza amani, utulivu na usalama wa kila mtu na mali zake.

Mwisho, tunapenda kuhitimisha tamko letu kwa kuwaalika wakristo wote
kuiombea nchi yetu amani, utulivu na mshikamano ambazo ni tunu
tulizoachiwa na waasisi wetu.

Ni imani yetu pia kwamba viongozi wetu wataendeleza wajibu wao na
mamlaka waliyopewa na Mungu pasipo upendeleo wa aina yoyote.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Zanzibar.

Kwa niaba ya Wakristo wote;

Ni sisi Maaskofu wenu

1. Michael Hafidh
Askofu wa Kanisa Anglikana Zanzibar

2. Augustine Shao
Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar

3. Pastor Timothy W. Philemon
Makamu Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji wa Makanisa ya Pentekoste
Zanzibar

SOURCE: Kiongozi [Toleo Na: 22 Juni 01-07,2012 (uk 2)].

Dear Mandela - We Are Still Not Free

With the ANC's attempt to legalise this regime, are we making a return to apartheid or could it be just as true that for rural South Africans as well as shackdwellers, history was never left behind?'

On the 27 April, Freedom Day (a South African national holiday) was marked throughout the country with political party rallies, NGO commemorations and thousands of now customary non-political braais (BBQs). It is a holiday that has come to signify something different to each and every South African - most of whom barely recognise the history and political implications of the day.

Freedom Day also marked a milestone for the South African shackdwellers' movement, Abahlali baseMjondolo. As they took to the streets once again for an 'UnFreedom Day' march through central Durban, the award winning documentary on the movement, Dear Mandela, was also aired for the first time on South African television.

Even though it was broadcast on satellite TV (thereby excluding the vast majority of South Africa's poor), it quickly set off a fire-storm of chatter on local twitter accounts with #DearMandela trending for hours as many viewers decided to write their own UnFreedom Day tweets to Nelson Mandela. The struggle of the shackdwellers of Durban had struck a chord even amongst those South Africans privileged enough to have access to private TV.

A FILM ABOUT UNFREEDOM

The film charts the struggles and activism of three distinctive young members of Abahlali as they take up the cause of development and the fight for dignity with their communities. Putting aside their personal aspirations, they unwittingly place their lives at risk when the inevitable backlash brings them face to face with ruthless political repression.

In 2009, Zama Ndlovu, a single mother of two and one of the main protagonists in Dear Mandela, went into hiding after a vigilante group of self-identified ANC supporters attacked Abahlali activists in the Kennedy Road Informal Settlement. Three years later, Zama and her family have returned to Kennedy Road, but still live in fear of another attack. In the meantime, shack fires, another violent and politicised force plaguing shackdwellers, have claimed her family's home three times.

Yet, Zama remains unwavering in her commitment to the struggle. She reminds others that they should think twice before discriminating against poor communities like hers'. "Middle class people tend to look at the people from the shacks, like people who are not like human beings. Living in a shack doesn't mean that you cannot think for yourself," she says.

Mazwi Nzimande, 18 years old when the documentary was filmed, has since suffered numerous death threats, with groups of strangers showing up at his mother's home in Joe Slovo to make explicit threats: leave the movement or suffer the consequences.

Mazwi echoes Zama's words and the belief that the poor must lead their own struggles. He exclaims that "being poor in life, doesn't mean that you are poor in mind".

'NOTHING FOR US WITHOUT US'

What I found invaluable about the film Dear Mandela is that, beyond the misleadingly narrow service delivery discourse that currently dominates South African political party and NGO politics, the members of Abahlali baseMjondolo recognise that they are fighting for much more than toilets and a roof over their heads. They are demanding, not just services, but also ownership of the development process itself.

Zama and Mazwi, like thousands of other members of the Abahlali baseMjondolo movement, want to be active participants in everything that affects their lives. To them, democracy isn't something that only takes place every five years at the ballot box where you vote for others to do development for you. Democracy must be an everyday process by which people constitute their own power over their circumstances.

BUILDING UHURU

The need for grassroots activism as a prefiguration of freedom is clearly evident as opposition towards the proposed Traditional Courts Bill grows in South Africa. The lack of effective resistance at the local level has meant that authoritarian means of governance in rural areas remained even while they were off the legal books. The Post-1994 era brought us "democracy" without democratisation. This bill, like the apartheid laws enacted to prop up the Bantustan apartheid system, will formalise the despotic power that chiefs claim over the rural poor.

With the ANC's attempt to legalise this regime, are we making a return to apartheid or could it be just as true that for rural South Africans as well as shackdwellers, history was never left behind?

Dear Mandela reminds us on UnFreedom day that freedom must be about more than just a farcical electoral ritual used by political parties to placate us.

Electoral politics tries to convince us that its better to be a shackled welfare recipient surviving day-to-day on the crumbs of capitalism than to recognise that these handouts are, in fact, an expression of oppression which exists to ensure a co-opted hegemony over the 'rebellious masses'.

We need to be aware that freedom cannot be quantified statistically. Freedom is not only about service delivery and having access to a plot of land or a small government house.

A house means nothing if it was just given to you. It means everything if it is something you have spent your life fighting for; something you been instrumental in achieving because you have recognised your own human dignity and your own self-worth in the process of living that struggle.

Through the process of working together, communities that mobilise around important issues tend to empower themselves to address other issues which affect them. For example, drug abuse and other forms of crime are often reduced substantially when communities are united and engaged in self-organised struggles.

As Biko said "the most potent weapon in the hands of the oppressor is the mind of the oppressed." Freedom cannot exist unless we reclaim our consciousness from those that oppress us and want to speak for us, without us. We must recognise that a person becomes a person through other people; that none of us are free until all of us are free.

Looking forward towards future struggles, it is therefore critical that we keep questioning our freedom in a deeper sense through a continuously evolving bottom-up process. Instead of tweeting to Tata Madiba (aka Nelson Mandela, who we must realise had chosen long ago to take up the mantle of government and put aside his previous disposition as a freedom fighter), let us write instead to one another demanding that we all sit down and engage on how to fight for more authentic freedom.

Jared Sacks is a Cape Town-based activist working with community-based social movements and the Take Back the Commons movement. He is also the co-founder of Children of South Africa. He writes in his personal capacity.

The Militarisation of Poverty in Africa

analysis

Increasing the rewards for those forces able to capture the state, by any means necessary, inevitably leads to war.

KINGSTON, CANADA - Over the past year, Africa has seen the decomposition of states from coast to coast. A belt of war, coups and large-scale spontaneous demonstrations has emerged across the Sahel, from Guinea-Bissau to Somalia. The situation represents a significant global security threat, which for some will justify the increasing militarisation of the continent. These political processes have a variety of localised causes, yet they have some commonalities. All of them emerge in a context of failed agricultural markets and a boom in mineral and oil extraction. Fundamentalist Islam is merely a complicating factor: not a cause, so much as a response to the destabilisation we are seeing.

It is not a coincidence that African governments are falling apart while Europe and North America are facing financial crisis. We are witnessing are the declining hegemony of African states at the same time the competition for spoils intensifies, while the potential rewards of capturing the centre become ever more valuable. Capital is not withdrawing from Africa, but instead, the processes of extraction are becoming more obvious as the economic basis of societies are under severe strain. This is the context in which the US is devoting more resources to its AFRICOM division.

Frantz Fanon wrote in 1959 that:

'Colonialism hardly ever exploits the whole of a country. It contents itself with bringing to light the natural resources, which it extracts, and exports to meet the needs of the mother country's industries, thereby allowing certain sectors of the colony to become relatively rich. But the rest of the colony follows its path of underdevelopment and poverty, or at all events, sinks more deeply into it.'

This is the basis of "combined and uneven" development: a state in which most of the continent still finds itself. The aid industry has masked some of these effects, yet in the current moment it has been forced into retreat, as country contributions are cut away in austerity budgets.

"While they debated whether or not [neoliberal economic] policies had brought growth to the continent, the only point they agreed on was the fact that they have resulted in growing inequalities and increasing poverty."

NEOLIBERALISM'S LEGACY

At a recent launch of The Oxford Companion to the Economics of Africa in Accra, the editors of the esteemed volume were at odds over how to assess the consequences of three decades of "Washington Consensus" neoliberal economic policies. While they debated whether or not these policies had brought growth to the continent, the only point they agreed on was the fact that they have resulted in growing inequalities and increasing poverty throughout Africa.

Elections have therefore only offered the electorate a chance to choose politicians who continue to impose increasing poverty upon them. As a result, in some places, people are actually nostalgic about the years they were living under dictatorships - because they remember them as times when they had more food.

What we are witnessing now is, in part, the blowback from years of neoliberalism and military interventions in places such as Somalia and Libya. This blowback is revealing the shallowness of the "Third Wave" democratisation processes in Africa that the US political science establishment was so keen to ride. Larry Diamond, for example, influenced much of the Clinton administration's thinking about the democratic transitions and now boasts having authored 27 books on it.

The liberal triumphalist thinking of the 1990s was, of course, forced into revision from events that ensued. Neoliberal thinkers in places like the World Bank had thought movements for democracy, supported by Washington, would chop away the burdensome state, freeing natural propensities to trade, allowing capitalism to flourish. The reality is that neoliberal policies destroyed existing local markets while highly sinister elements flourished.

Thinking at the World Bank then turned policy orientation toward building "institutions for markets", "capacity building" and eventually a complete about-face to "statebuilding". The occupations in Iraq and Afghanistan were most influential in forcing this shift cutting back the sate, to now build them up as bulwarks against Islamic fundamentalists, rampant corruption and those who might want to consider re-nationalisation as a development tool.

GOVERNANCE REGIMES IN AGRICULTURAL SOCIETIES

While US political scientists were obsessed with liberal triumphalism in the 1990s, others were offering far more powerful tools for understanding African states, even if the empire had no use for them. Some of the most powerful analyses have been published in Review of African Political Economy. Works by people such as Catherine Boone, Mahmood Mamdani, and the late Chris Allen among others, examine ways that material processes of extraction impact political processes.

African state borders contain a wide variety of variables. They have diverse geographies, cultural histories and economic foundations. Nevertheless, Boone's work (along with others such as Mamdani, Jean-Francois Bayart and Robert Fatton) shows that peasant-based economies have integrative tendencies. Hegemony is more firmly rooted in land-tenure patterns and cultural institutions of labour mobilisation (ie: unpaid family labour, or working for the chief or marabout). These patterns stem from various alliances and forms of indirect-rule set in place between colonial governments and "strong men". Alternately, extractive industries around valuable commodities have greater tendency toward disintegration.

Along with agro-pastoralism, states in West Africa have forms of mercantilism that have extended back many centuries. Mining has also taken place there for hundreds of years. Until very recently, in most cases, it has been conducted by artisanal miners, who find sustenance largely through farming and herding.

AGRICULTURAL CRISIS

One does not need to look far to see that agriculture across the region is in crisis. Famine has already been declared in Somalia. The Sudans are at war, while refugees have fled their herds and any crops they could scrape from the ground after years of drought. UN FAO notes that last year the Horn of Africa experienced a food crisis that left an estimated 13 million people dependent on humanitarian assistance. Currently there are 15 million people facing food insecurity in the countries of the Sahel.

These famines are compounded by refugee crises. Altogether some 284,000 Malians have fled Northern Mali, according to the UN Office for the Coordination of Humanitarian Affairs: 107,000 of them are thought to be displaced within Mali; 177,000 in neighbouring countries. New arrivals have pushed refugee numbers to 56,664 in Burkina Faso, to 61,000 in Mauritania, and to 39,388 in Niger, according to UNHCR.

Around 810,000 Senegalese are facing hunger, according to a joint study in February 2012 by the Senegalese government and the World Food Programme (WFP). In the 2011 harvest season, cereal production fell by 36 per cent compared with 2010, and the production of peanuts, Senegal's main cash crop, fell by 59 per cent. One figure shows the latest harvest was 120,000 tons, down from a previous yearly average of 800,000.

It is tough to say what is happening in Guinea in the midst of its protracted electoral crisis, though it seems recent demonstrations called by opposition candidates tap into spontaneous displays of anger among a large population of highly disenfranchised youth. These demonstrations are acts of desperation among people whose anger can be easily exploited by self-serving politicians with fiery rhetoric. In this way, it holds some similarities to the more sophisticated Senegalese movements that emerged last year against former president Abdoulaye Wade. The Ivory Coast's Laurent Gbagbo is an example of how unsavoury they can become.

Guinea Bissau's coup has disrupted the marketing of cashews - an important plantation crop in that country - but the story not being told is that the indigenous rice economy has already been seriously battered. This is the case with all the rice-growing economies in West Africa, as shown by USDA figures. Burkina Faso, Ivory Coast, Mali, Ghana and Senegal all show declines in production. In the past year, imports have soared to meet local consumption. Mali's importation has risen 50 per cent. The Ivory Coast is importing a massive 80 per cent of their consumption.

"Sudden market shocks, gradually worsening terms of trade, market disincentives ... led to a process of de-agrarianisation ... [and] 'de-peasantisation', whereby 'peasant households and communities have lost their coherence as social and economic units'." - Deborah Bryceson, University of Glasgow

In these countries, 3,500 year old rice economies are being destroyed in a period of less than 20 years. Of course, it is not simply the rice that has been impacted, but also the cultures that came into being alongside them - along with the complementary grains that comprised a diverse agroecology suited to local conditions. This is what dispossession means. There are certainly positive aspects of breaking feudal regimes, but if people's labour fails to be absorbed into new forms of work, they simply become a surplus. This then pulls down labour conditions for many - who now also lack the protective aspects of a feudal economy (while you may work out of obligation, rather than for a wage, you are at least ensured your sustenance).

Reforms of the 1990s battered the agricultural sector throughout Africa. Deborah Bryceson at the University of Glasgow notes how these reforms greatly expanded the productivity gap between small-scale and large-scale production. Studies show that production rates of growth in African rice have begun to rebound in the past decade, but they are not keeping up with that of the population. More importantly, they are not meeting the same rates as highly capitalised farmers in North America and Europe (who have remained subsidised).

As Bryceson noted in 2009, sudden market shocks, gradually worsening terms of trade, market disincentives, "continue to undermine personal welfare, leading to social upheavals and political destabilisation". This has led to a process of de-agrarianisation, or more specifically, "de-peasantisation", whereby "peasant households and communities have lost their coherence as social and economic units".

These patterns fuel burgeoning global unemployment rates. A recent report of the International Labour Organisation shows that youth are particularly badly hit. Between 2007 and 2010, youth unemployment increased by 5.1 million.

AUSTERITY, DECLINING AID AND 'OVER-CONSUMPTION'

Africa is experiencing the most grotesque contradictions of Europe's financial crisis. The immediate consequences in the south have been a drop in aid funding, while at the same time, the world's wealthiest are hoarding gold. The Africa Report cites a 2.7 per cent drop in global development aid between 2010 and 2011, or a drop of $3.4bn. More importantly, it is the first drop in aid since 1997, after growth of 63 per cent between 2000 and 2010.

"There is no doubt that many of the earth's resources are being used to create unnecessary products for high-consumption lifestyles... Capitalist societies are producing simply for the sake of production, not need."

As declining peasant production, increased war and climate change fuel dislocation, there are fewer aid organisations to fill in the gaps for people to meet bare necessities. These people are the easiest to recruit into armies and gangs of banditry and piracy.

Amidst this, environmentalists at the World Wildlife Fund in a recent report, claim the world suffers from over-consumption. This, however, seems to fit too easily with an ideology where those in the affluent parts of the world are told they need to tighten their belts. Austerity is being enforced to "cut the waste" in workplaces where we are told people have been taking too much - retiring too early, expecting pensions and healthcare from employers. There is no doubt that many of the earth's resources are being used to create unnecessary products for high-consumption lifestyles in much of the world. The problem, however, is that the World Wildlife Fund has the matter up-side-down. Capitalist societies are producing simply for the sake of production, not need.

The current crisis of capitalism is that there is "surplus liquidity". In other words, the rich have so much wealth they have exhausted places to store it. If it is not invested its value depreciates. This is what has led to land grabbing and investment in grain futures markets. This is why we see record amounts being spent on art (ironically art that depicts the pain and isolation of capitalist society being imposed on Europeans). This is why we see car companies pushing zero per cent financing.

While workers are having their jobs and wages cut and governments are enforcing austerity, companies have never held so much cash. As one author reports: "Globally, companies are sitting on more than $5 trillion." This is a classic case of "over-production". When investors cannot sell more cars and condos, they turn to purchasing gold and minerals.

AFRICA'S MINING BOOM AND THE POLITICS OF SPOILS

There are few places in Africa where mineral industries have had a positive impact. 27 years of warfare in Angola is a case in point. More than a million people lost their lives, while another million were displaced in just the last decade of the war - a war that saw the country divided between factions fueled respectively by oil and diamond wealth.

Currently, Mining Weekly reports that "with commodity demand soaring, the world's mining companies are increasingly turning to Africa to deliver resources to growing economies". Foreign investment on the continent has grown 87 per cent in the past decade.

At this moment, rising mineral prices and increased production complicates all of the problems that states are confronting from declining agricultural production. The Sudans are amassing arms and moving ever-closer to full-scale war. The South was no-doubt emboldened by the first round of contracts it signed for mineral exploration. Coupled with the resulting cash, South Sudan was able to re-fit its army to push into Heglig, situated within territory situated in the North according to the 2009 peace treaty.

The ink from Chad's 2007 peace treaty was barely dry before Chad announced a new investment charter in 2008, in attempts to lure companies searching for gold, silver and even diamonds. Further attempts to sway prospective investors included a glitzy conference last year under invitation by Chad's president.

"The reason we need to worry about these mining investments is not simply because of their human rights violations ... mining increases the rewards for those forces able to capture the state."

The impact of gold on Nigeria has led to the largest recorded lead poisoning in human history as small-scale and artisanal miners step up their production, scattering lead-laden dust into children's play areas. The results are painfully tragic, killing 460 children and contaminating a further 4,000. The contamination will cause numerous ongoing problems for the country in years to come. This is of course in a country where the draw of Islamic fundamentalism has the entire country on edge. As much as those of us on the left would like to believe otherwise, this degree of poverty rarely produces pleasant political responses.

In Mali, mining companies will no doubt be increasing private security force protection of their mining concessions in the west of the country. The companies involved are also those that are participating in the mineral exploration rush on the same geographic feature that crosses into Guinea and Senegal. There are so many companies clamouring for mines in Guinea right now that the prices of poor-quality hotel rooms in Conakry are reportedly often $300 or $400 a night.

The reason we need to worry about these mining investments is not simply because of the human rights violations, the displacement of populations and the pollution of land that accompany them. More than that, we need to be aware of the fact that mining increases the rewards for those forces able to capture the state - regardless of how they go about accomplishing it. Warlords have little need to control the productive activities; they just need to have some control over the proceeds - or at least portions of them.

Guinea has seen one coup after another, with Burkina's Blaise Campaore often involved in some way. In Guinea Bissau, the proceeds from drug-running are beginning to have the same effect, with factions in the military and state colluding to exact spoils (and why would they want to collaborate in the "war on drugs" when drug smuggling is practically the only competitive advantage they have?).

The consequences of the processes I have described here are that, within the past year we have seen a corridor of insecurity emerge that leaves large areas, from coast to coast, where there is effectively no functioning government. Although African states have often done little to protect their citizens, the circumstances in refugee camps and in rebel held territory are far worse for everyone. They are especially bad for women; as the situation in Northern Mali is making clear.

The US, under AFRICOM, however, is not likely to be as concerned with women's safety as they are their oil and mineral operations, and the draw of fundamentalist Islam. Yet interest in Islamic fundamentalism is that much more appealing to people who've lost everything for the sake of the one per cent intent on taking it all. Armies are not signs of hope for those who have recently lost their land in mining concessions and land grabs, because in the experiences of the disposed, militaries have tended to come in to support those who are taking from them.

Militarisation is not taking place to resolve impoverishment, but enforce it. A more systemic solution would be to curb the appetites of the richest and invest human energies into building a more egalitarian global economy.

* Toby Leon Moorsom teaches at Queen's University in Canada and is an editor of Nokoko Journal of African Studies.

PICHA MBALIMBALI ZA MKUTANO WA AFDB ARUSHA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31. 2012
Ukumbi wa AICC wakati wa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31. 20
Rais Kikwete akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana Mh Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa Dkt Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Morroco Bw Omar Kabbaj (kushoto) , Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (wa pili kuhsoto) katika picha ya pamoja na Marais wastaafu wa Benki ya Afrika.Picha na IKULU

SHEIN : TUTALINDA AMANI NA UTULIVU ZANZIBAR KWA NGUVU ZOTE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein ,alipokuwa akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Bara na Visiwani,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar Jana.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,na Mawaziri wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk. AliMohamed Shein akizungumza na Waandishi Ikulu Zanzibar.
Mawaziri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar
--
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya vurugu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar jana,Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote, atakayethubutu kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”

Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji wa stamp ya uvumilivu wa kidini.

“Kwa masikitiko makubwa nataka kusema kuwa vitendo vilivyotokea vya kuvunja amani ni vya aibu, vimetusononesha sana na haya wananchi lazima wajue kuwa amani yetu ni muhimu kuliko jambo lolote lile” Alisema Rais Dk. Shein.

Alisema ameshangazwa na vitendo vya uchomaji makanisa moto vilivyofanywa wiki iliyopita akihoji kwamba kulikuwa na uhusiano gani baina ya Muungano na makanisa “Mie nilikuwa nashangaa sana hivi kuna uhusiano gani kuzungumzia Muungano na kuchoma makanisa,kupora mali za watu”

Alisema Dk. Shein. Rais Dk. Shein alisema matatizo ya Muungano yanashughulikiwa chini ya utaratibu uliokubaliwa na Serikali mbili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kuna kamati ya kushughulikia kero za Muungano na hadi sasa kuna mambo 12 yanafanyiwa kazi ikiwemo suala la mafuta na gesi asilia.

“Taratibu za kutatua kero za Muungano zinaendelea, kuna mambo 12 yamewasilishwa katika kamati na yanafanyiwa kazi, miongoni mwa hilo ni suala la mafuta na gesi asilia, sisi tumeshaamua, SMT bado haijaamua ,lakini sisi tumeamua kuyaondoa katika Muungano, lakini nasema ndugu wawili hawagombani…tutakubaliana” Alisema Rais Dk. Shein.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao na akielezea kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa Wazanzibari kueleza wanataka katiba iweje na kuwatoa wasiwasi kuwa hakuna atakayetishwa na wasiogope,lakini akasisitiza ni lazima wasubiri Tume ndipo watoe maoni yao maana wakieleza sasa hakuna anayewasikiliza.

“Wanaotoa maoni yao kuhusu Muungano kwa hivi sasa wanapoteza muda wao, ni sawa na kusema na ukuta tu kwani hakuna anayewasilikiza, hakuna anayechukuwa maoni yao maana Tume haijaanza kazi,wasubiri itakapoanza wakatoe maoni yao”

Alisema Rais Dk. Shein. Rais Dk Shein alitoa ufafanuzi huo akijibu swali la waandishi waliohoji kuwepo kwa kamati ya kutatua kero za Muungano na mjadala wa katiba mpya kwamba Serikali ingesubiri matokeo ya Tume ya Katiba kuhusu Muungano maana inawezekana mambo yakabadilika.

“Sheria ya Tume ipo wazi, lazima wafuate sheria na taratibu hatazuiwa mtu kutoa maelezo yake,lakini kero za Muungano zinaendelea kushughulikiwa kuwepo kwa Tume ya Katiba hakuzuii kamati iliyo chini ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kushughulikia kero za Muungano.

Katika hatua nyengine, Rais Dk. Shein ameipongeza Polisi kwa busara na hatua walizochukua kushughulikia vurugu zilizotokea wiki iliyopita Visiwani Zanzibar ” Nilipopigiwa simu nikauliza kuna alijeumizwa,vifo nikaambiwa hakuna nikasema Alhamdulillah salama”

Alisema Dk Shein. Alisema kwamba licha ya Polisi kuchokozwa na vijana waliokuwa wakichoma moto matairi ya magari barabarani, kuweka mawe na magogo kuziba njia,lakini Polisi ambao walikuwa na silaha hawakutumia silaha hizo,zaidi ya kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi.

”Jeshi la Polisi halibebi lawama,linastahili sifa na kupongezwa…Polisi wana busara sana wanafanya kazi vizuri hawa ndugu zetu wa Polisi kwa kweli lazima tuwapongeze” Alisisitiza Rais Dk. Shein wakati akijibu swali kwamba Polisi wanastahili kulaumiwa, Rais alisisitiza kuwa Polisi walitimiza wajibu wao kwa uzalendo mkubwa wa kuepusha madhara kwa jamii.

”Mimi nilikuwa natoka mazikoni, nilipita barabara ya amani, mwanakwerekwe, nimejionea namna vijana walivyoweka mawe,magogo, kuchoma matairi,lakini Polisi hawakutumia nguvu zaidi ya kuwatawanya kwa kutumia mabonu ya machozi, tuwapongezeni Polisi wetu wamejitahidi sana” Aliongeza.

Rais Dk Shein alisema kwa wale wote waliokamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria,haki itatendeka kwa kila mtu na kwamba hakuna atayakeonewa wala kudhulumiwa.

Pia alisema Serikali inafanya tathimini kuweza kuelewa athari za matukio yaliyotokea. Pia alitumia fursa hiyo kuwapa pole wale wote waliopatwa na matatizo ya vurugu zilizotokea.

Popular Posts