Translate - Tafsiri
Labels
- Tamko kwa Umma - Press Release
- All Photos - Picha
- CCM CHAMA CHA MAPINDUZI
- Zanzibar
- IKULU - STATE HOUSE
- Sports - Michezo
- CHADEMA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
- Dodoma
- Editorial Opinion - Maoni Tahariri
- Tanzania
- Dar es salaam
- Habari za Kimataifa - International News
- Burudani - Entertainment
- Bungeni
- Katiba - Constitution
- Dini - Religion
- Mbeya
- SMZ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
- Vodacom
- Hotuba - Speech
- Arusha
- Iringa
- Tanzia - Msiba - Mazishi
- Afya - Health
- Ofisi ya Waziri Mkuu
- Singida
- Ajali - Accident
- Development Reports
- Morogoro
- Open Letters - Barua za Wazi
- Urembo - Beauty
- Kenya
- CUF Chama cha Wananchi
- Maonyesho ya Sabasaba
- Ofisi ya Makamu wa Rais
- Huduma za Usafiri - Transport Services
- Tanga
- Business Finance Money
- Masuala ya Elimu - Education
- Miundombinu -Infrastructure
- Mtwara
- Rukwa
- UVCCM
- Habari za Mahakamani
- Kilimanjaro
- Serengeti Breweries Limited
- Tourism - Utalii
- Habari za Nyumbani - Local News
- Jakaya Mrisho Kikwete
- Kagame Cup - Kombe la Kagame
- Katavi
- Lindi
- Nishati - Madini - Mining - Energy
- UN United Nations - Umoja Mataifa
- Yanga
- African Union - Umoja wa Afrika
- Bagamoyo
- Agriculture - Kilimo
- Azam FootBall Club
- Balozi na Ofisi za Balozi
- Baraza la Wawakilishi
- Human Rights - Haki za Binadamu
- Jeshi la Polisi Tanzania
- Kigoma
- Maonyesho ya Nane Nane
- Simba Sports Club
- Tabora
- East African Community
- HARUSI - WEDDINGS
- Kagera
- Mwanza
- Pemba
- Shinyanga
- Sumbawanga
- TFF Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
- Videos - Multimedia
- Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Kimataifa
- Wizara ya Nishati na Madini
- Afdb African Development Bank
- Airtel Tanzania
- Benki - Fedha - Uchumi
- Fiesta 2012
- GEITA
- Mafuta - Oil Issues
- Uganda
- Wizara ya Maliasili na Utalii
- BAJETI 2012 - 2013
- Burundi
- Climate Change - Mabadiliko ya Tabia Nchi
- FASHION - MITINDO - MAVAZI
- ICT Information and communications technology
- Kambi ya Upinzani
- London Olympic Games 2012
- Mambo ya Zamani - Archives
- Maonyesho ya Biashara - Trade Shows
- Mara
- Mobile - Telecoms
- NHIF National Health Insurance Fund
- Peace and Security
- Rwanda
- Sayansi na Tekinolojia
- Wizara ya Elimu na Ufundi
- Wizara ya Mambo ya Ndani
- Wizara ya Uchukuzi
- Zambia
- BOT Bank of Tanzania Benki Kuu ya Tanzania
- Events - Matukio
- Habari za Majimboni
- Mahojiano - Interview
- Makala - Articles
- Malawi
- Mkoa wa Pwani
- Musoma
- NJOMBE
- National Parks - Mbuga za Wanyama
- Ruvuma
- SONGEA
- Shirika la Nyumba laTaifa - NHC
- TBL Tanzania Breweries Limited
- Taifa Stars - Timu ya Taifa
- UDAKU UMBEYA GOSIP
- US EMBASSY - UBALOZI WA MAREKANI
- University of Dar es salaam - Chuo Kikuu cha Dar es salaam
- ABG African Barrick Gold
- BAKWATA
- Banks - Benki
- Environment - Mazingira
- Ilala
- Kilimo Kwanza
- Land and Land Grabbing Issues - Ardhi
- Love Relationships - Mapenzi Mahusiano
- MIKUTANO
- Mabondia - Boxing
- Manyara
- Miradi ya Maendeleo
- Misaada - Donations
- Mombasa
- NCCR MAGEUZI
- Nairobi
- People - Watu
- Picha ya Wiki - Photo of the Week
- Precision Air
- Procurement
- Ripoti Maalumu
- SANAA - ARTS
- Sensa ya Makazi na Watu 2012
- Sheria - Law
- Somalia
- South Africa
- South Sudan - Sudani Kusini
- Takwimu - Statistics
- Tigo
- Travel - Safari
- Ugaidi - Terrorism
- Ulinzi na Usalama - Security and Defence
- Wizara ya Afrika Mashariki
- Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
- Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo
- Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknologia
- Wizara ya Viwanda na Biashara
- Zimbabwe
Blog List
Saturday, June 23, 2012
TAMKO LA TAASISI ZA KIISLAMU KUHUSU KUVUNJWA KWA MUHADHARA DONGE
BISMILLAH RAHMANI RAHIM
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR
Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W.T), Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), watu wake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar baada ya kufuatilia kwa hatua za awali na kufanya tathmini ya hali ya mambo namna ilivyotokea tarehe 17 juni, 2012 inatoa tamko RASMI kama ifuatavyo:
Siku ya tarehe 17 juni, 2012 majira ya saa nane na nusu za mchana waislam waliondoka viwanja vya malindi eneo la mjini magharibi na msafara wa gari, vespa na Pikipiki ukielekea kwenye muhadhara Kaskazini Unguja eneo la Donge sambamba na wenzao wengine waliotoka mashamba yote ya Unguja kuelekea hukohuko Donge katika Msikiti uliopo eneo linalojulikana kwa jina la Donge pwani, tulipofika Mahonda msikiti wa Ijumaa ambao upo karibu na kituo cha polisi cha mahonda, majira ya saa tisa na dakika kumi jeshi la polisi lililovalia sare za askari wa FFU liliwazuia wananchi hao kuendelea na safari yao ya Donge nakusababisha mkusanyiko usio wa lazima.
Watu waliokuwa katika msafara huo walilazimika waingie msikitini huku wakisubiri viongozi wao wa jumuiya na taasisi za kiisilamu wawaongoze, wakati viongozi wa jumuiya na taasisi za kiisilamu walipofika eneo hilo walitoka kwenye gari ili kwenda kufanya mazungumzo na askari, ndipo FFU walipoaza kurusha mabomu ya machozi ovyo na kuwatawanya waumini hao, huu ni uvunjaji wa katiba zote mbili na ukiukwaji wa haki ya raia na uhuru wake wa kuabudu kama inavyoelezwa na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 19 (2) ambayo inasema “Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada, kueneza dini itakua huru na jambo la hiari ya mtu binafsi na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakua nje ya shuguli za mamlaka ya nchi…” rejea pia katiba ya Jamhuri ibara. 19 (1), (2), (3).
Pia kufanya hivyo ni kwenda kinyume na katiba ya Zanzibar ibara ya 16 (1) kwa kuwazuwia watu kwenda watakapo ndani ya Zanzibar…, sheria kama hii pia inaelezwa ndani ya katiba ya Jamhuri…
Ibara ya 17(1) inatamka wazi kwamba “…Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano…”. Pia kifungu kidogo cha (2) (b)(i),(ii),(iii) vimetoa maelezo zaidi.
Jeshi la Polisi limekwenda kinyume na kifungu cha 18 (1) cha sheria ya Zanzibar kwa kuzuwia uhuru wa maoni Sambamba na Kwenda kinyume na Sheria ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Tanzania ibara ya 18 (1) “…kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari…”
Isitoshe, juu ya ukiukwaji wote huo askari hao wamefanya unyama na uhalifu wahali ya juu kwa kuunajisi Msikiti wa Ijumaa wa Mahonda kwa kuwahujumu Raia wasio na silaha ndani ya Msikiti kwa kuwarushia mabomu ya machozi yasiojulikana idadi yake ambapo hadi hii leo msikiti huo hausaliki ndani kutokana na harufu kali ya mabomu. Pia askari hao walipiga risasi pamoja na kuingia ndani ya Msikiti na viatu na kuvunja kwa makusudi vyombo (Vespa, Pikipiki, Baskeli n.k) vilivyoegeshwa eneo la msikiti huo wa Ijumaa.
Sambamba na hilo, polisi wamevunja taa ya mbele na nyuma ya vespa ya mwandishi wa habari wa jumuiya pamoja na taa za gari inayobeba vifaa vya mihadhara kichuki baada ya kuikamata mapema tu na kuifikisha polisi, hali hii ilitokea wakati gari ikiwa kituoni chini ya kizuizi cha polisi baada ya kuikamata tokea saa saba nanusu za mchana kabla ya kufika kwa misafara inayokwenda kwenye mihadhara hadi leo hii gari hiyo inashikiliwa na polisi kituoni mahonda.
Pia katika jumla ya matukio ni kuandamwa na kufukuzwa kwa gari ya kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Sh. Farid Hadi Ahmed yenye Namba ya usajili Z 628 DJ aina ya NISAN X-TRAIL iliyofukuzwa kwa pikipiki inasadikiwa na watu ambao walitumwa na jeshi la polisi kwa lengo la uhalifu dhidi ya Amir Farid kitendo ambacho kilisababisha ajali ya kupinduka kwa gari hiyo na kusababisha kujigonga na mti huko Dole tukio ambalo liliripotiwa kituo cha polisi cha Muembe Mchomeke. Haya yote yaliyofanywa na Jeshi la Polisi kuwajeruhi watu wasiokua na hatia pamoja na kuharibu mali yanakwenda kinyume na katiba na sheria za nchi.
Jambo la kushtusha zaidi ni kitendo cha kuwadhililisha wanawake na kufikia hadi kuwakashifu kwa kuwachania nguo zao na kuwavua mashungi yao pia hata watoto wadogo mitaani wako walopata kipigo, kitendo cha kuwatimba wanawake kwa viatu bila ya huruma na kuwapiga marungu na kuwajeruhi vibaya sehemu za usoni na mwilini kwa ujumla, huo wote ni unyama na ukiukwaji wa haki za binaadamu.
Ilipofikia wakati wa laasiri jeshi la polisi walianza pia kupiga mabomu ndani ya msikiti wa donge pwani pamoja na kuuhujumu msikiti na waumini wakiwa wanaswali katika msikiti wa Donge skuli na kuvunja vioo vya msikiti huo, huu wote ni udhalilishaji wa dini ya Kiislamu pamoja na waumini katika eneo hilo.
Vile vile, askari wa jeshi la polisi walikata kwa visu mipira ya vyombo vya wananchi kama vile vespa na baskeli zilizokua zimeegeshwa msikitini hapo na askari hao walivunja heshma ya msikiti kwa kuingia na viatu ndani ya misikiti hiyo.
Sambamba na hilo, walimkamata mzee Kassim Shekha mwenye Umri wa miaka 50 aliekua akiswali swala ya laasir walimjeruhi vibaya miguuni kwa mlipuko wa bomu la machozi akiwa ndani ya swala, pia kijana Othman Ali (22) aliamriwa aingie Msikitini na hatimae kujikuta akipigwa kwa mateke, vibao na kuchaniwa nguo huku akiamriwa lazima atembee kwa magoti pamoja na wenziwe hadi kituoni Mahonda.
Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar kupitia vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo gazeti la serikali la Zanzibar leo toleo nambari 3789 la tarehe 18 Juni, 2012 lilisema likimnukuu Kamishna huyo ndugu Mussa Ali Mussa eti hakuna alie jeruhiwa wakati taarifa za kuaminika zimeripoti watu thalathini na nne ambapo wanaume ni 27 na wanawake 9. Upotoshaji huo wa jeshi la polisi ni kuonesha namnagani jeshi la Polisi lisivyo wajali wananchi, roho na mali zao na jinsi linavyopotosha ukweli wa mambo. Pia kutokujali hata kwenda kinyume na viapo vyao vya uaminifu wanapoingia kwenye ajira, Kwa kiongozi wa Jeshi la Polisi kwa nafasi kama hiyo ya kamishna alipaswa awe mfano mzuri kwa walio chini yake.
Matukiyo yote hayo ya kunajisi Misikiti na kudhalilisha waumini wakiwa ndani ya nyumba za ibada yanazidi kujenga imani kua ni kweli yale yanaosemwa kua jeshi la Polisi linahusika kwa njia moja au nyengine katika suala zima la unajisi na uchomwaji wa Makanisa kiushiriki na ufichaji wa wahalifu kisha kutoa taarifa za uongo na kuwafanya Waislamu ndio chaka lao.
Baada ya hayo machache yaliyotangulia hapo juu pamoja na kukutana na waathirika na wananchi wa Donge, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu inatamka kwamba:
- Jumuiya inasikitishwa sana na taarifa za uongo zisizo kuwa na ukweli na inalitaka jeshi la polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kwa ukweli na uaminifu kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu wakitambuwa umuhimu wa jukumu lao la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu. Kwa maana hiyo tunalitaka jeshi la polisi litueleze kwa katiba gani na sheria ipi iliyotumika kuzuia uhuru wa kuabudu na kutoa mihadhara na kukusanyika waumini wa kiisilamu misikitini? Tunavyofahamu sisi jumuiya, ni kuwa jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote bila ya ubaguzi.
- Wananchi wa Donge wanasema wamechoshwa na ubaguzi na udikteta wa Shamhuna na wanaitaka serikali ya umoja wa kitaifa kupitia baraza la wawakilishi itoe ufafanuzi wa wazi kabisa, ni kwa sheria gani wananchi wa Donge wananyimwa fursa ya kufaidi uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni pamoja na uhuru wa kuchanganyika na ndugu zao wazanzibari? vile vile haki ya kutumia TV na DVD zao mitaani uhuru ambao unaingiliwa na masheha kwa kuwazuia watu kutizama watakacho na kufikia hadi kuwatisha kuwapeleka Polisi na hata kuwanyang’anya mali hizo jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati inafahamika kuwa haki zote hizo zinalindwa na katiba ya Zanizbar kwenye ibara zifuatazo 17, 18, 19 na 20.
- Wananchi wa Donge pia wanomba ufafanuzi kutoka baraza la wawakilishi kwani kwa miaka yote wanajiona kuwa wanabaguliwa wakati wananchi wenzao wa mashamba yote mengine katika wilaya tofauti wakipata haki kikamilifu, jee wao si wazanzibari? Ni dhambi gani waliyotenda hata wakabaguliwa kiasi hicho? Au Donge ni nchi yenye mfalme kama wafalme wa ki-Misri wakijulikana kwa jina laFIRAUNI?
- Wananchi wa Donge wanaliomba baraza la wawakilishi tukufu ndani ya siku kumi na nne (14) litoe ufafanuzi wa haki juu ya masuala yao yote, ikishindakana hivyo wasije wakalaumika kwa maamuzi watakayochukua. Pia wanaviomba vyama vyote vya siasa viwe makini sana kuwatetea haki zao.
- Jumuiya na taasisi za kiislamu zinawaahidi wananchi wa Donge kuwa ziko tayari kuwaunga mkono kwa maamuzi yoyote watakayo yachukuwa na kuwataka waislamu wote wawe tayari kwa hilo.
- Jumuiya za kiisilamu zinawapa pole waathirika wote na kuwapa hongera wazanzibari wote kwa uimara na kutotetereka katika kudai haki zao pamoja na kutoa wito wa kudumisha amani na utulivu, pamoja na kuwa na subra na kutolipiza kisasi.
Mwisho, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zinapenda ifahamike kwamba, inatoa na kupaza sauti ya ukombozi wa Zanzibar kwa njia za amani bila ya kutumia nguvu za silaha bali kwa kutumia nguvu za hoja na inaendesha harakati zake hizo za ukombozi juu ya misingi ya sheria za nchi na katiba.
Hivyo basi, wananchi wa Zanzibar kudai uhuru wa kujiamulia mambo yetu ni haki yetu ya msingi, na kwa hilo HATUNA MJADALA (MPAKA TUTAKAPOIPATA NCHI YETU INSHA-ALLAH), tutaendelea kudai haki zetu kwa kila hali bila ya kuvunja sheria za nchi.
Tunasisitiza kuendelea na kuidai Zanzibar yetu huru ingawa tunaelewa gharama ya kufanya hivyo ni kubwa ikiwemo kupoteza roho zetu na mali zetu. Na tunatamka wazi yakwamba tumechoka na ukoloni wa watanganyika wachache wasioitakia mema Tanganyika na Zanzibar.
Tutaidai nchi yetu kwa gharama yoyote mpaka kuipata Zanzibar yetu huru.
“…FREE ZANZIBAR…”
“TUACHIWE TUPUMUE”
WABILLLAH TAWFIQ
Deidre Lorenz Atembelea kituo cha Yatima wa Kituo cha Yatima cha Upendo
Mt. Kilimanjaro Marathon
Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi ngazi ya kitaifa
PICHA MBALIMBALI TOKA VIWANJA VYA BUNGE
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole- Sendeka (kushoto) na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 22,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (kushoto) na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Juni 22, 2012.
MAHAKAMA YAZUIA MGOMO WA MADAKTARI
UMOJA WA WATANZANIA WA BRAZIL WAKUTANA NA MAKAMU WA RAIS
Rais Jakaya Kikwete Akiifariji Familia ya Aliyekuwa Mkuu wa Utawala CCM Makao Makao Makuu Dodoma Marehemu Mwangunza Kinyamagoha
Wagombea Mbalimbali wa Uongozi Klabu ya Yanga
shule ya msingi Mgulani na Chemi & Cotex watembelea kituo cha Yatima cha Friends of Don Bosco Kimara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani Azungumza Kuhusu Maadhimisho ya Siku ya utumishi wa Umma
Timu ya Cricket ya Totteridge Yatoa Msaada wa Vifaa vya Michezo kwa Tanzania
Thursday, June 21, 2012
MABADILIKO YAFANYIKA BARAZA KIVULI LA MAWAZIRI
No. | WIZARA KIVULI | WIZARA YA SERIKALI | KAMATI HUSIKA YA BUNGE | WAZIRI KIVULI | NAIBU WAZIRI |
1. | OFISI YA WAZIRI MKUU | OFISI YA WAZIRI MKUU | -SHERIA NA KATIBA, -FEDHA ,UCHUMI +MIPANGO | KUB- FREEMAN A.MBOWE | |
2. | WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU | 1.SERA,URATIBU NA BUNGE 2.UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI 3. TAMISEMI— ELIMU -TAWALA ZA MIKOA | -do- | DAVID ERNEST SILINDE | - |
3. | MIUNDOMBINU | UJENZI NA UCHUKUZI | MIUNDOMBINU | SAID ARFI | PAULINE GEKUL |
4 | WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS | OFISI YA RAIS 1-UTAWALA BORA 2-MAHUSIANO NA URATIBU 3- MENEJIMENT YA UTUMISHI WA UMMA | -SHERIA NA KATIBA. -FEDHA NA UCHUMI | PROF. KULIKOYELA KAHIGI | - |
5. | FEDHA UCHUMI NA MIPANGO | WIZARA YA FEDHA | FEDHA NA UCHUMI | ZITTO KABWE | CHRISTINA MUGHWAI |
6. | KATIBA SHERIA NA MUUNGANO | KATIBA NA SHERIA+OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO | SHERIA NA KATIBA | TUNDU A.LISSU | - |
7. | MALIASILI,UTALII NA MAZINGIRA | MALIASILI NA UTALII+OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA | MALIASILI NA MAZINGIRA | MCH.PETER MSIGWA | - |
8. | MAMBO YA NDANI YA NCHI | MAMBO YA NDANI | MAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA | VICENT NYERERE | - |
9. | MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI | MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA+ USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI | MAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA | EZEKIAH D.WENJE | RAYA IBRAHIM KHAMIS |
10. | ULINZI NA JKT | ULINZI NA JKT | MAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA | MCH.ISRAEL NATSE | - |
11. | MAJI,MIFUGO NA UVUVI | MAJI NA UMWAGILIAJI+ MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI | KILIMO ARDHI NA MAJI | SYLVESTER M.KASULUMBAYI | SABREENA HAMZA SUNGURA |
12. | KAZI,HABARI,UTAMADUNI NA MICHEZO | HABARI,VIJANA NA MICHEZO+ KAZI NA AJIRA | MAENDELEO YA JAMII | JOSEPH O.MBILINYI | CECILIA PARESSO |
13. | NISHATI NA MADINI | NISHATI NA MADINI | NISHATI NA MADINI | JOHN MNYIKA | - |
14. | VIWANDA NA BIASHARA | VIWANDA NA BIASHARA | VIWANDA NA BIASHARA | HIGHNESS KIWIA | - |
15. | AFYA, JINSIA NA JAMII | AFYA NA USTAWI WA JAMII+MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO | -HUDUMA ZA JAMII -MAENDELEO YA JAMII | DR. GERVAS MBASSA | CONCHESTA RWAMLAZA |
16. | ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA | ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI + SAYANSI TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO | -HUDUMA ZA JAMII -MIUNDOMBINU | SUZAN A.LYIMO | JOSHUA NASSARI |
17. | KILIMO NA USHIRIKA | KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA | KILIMO, MIFUGO NA MAJI | ROSE SUKUM KAMILI | - |
18. | ARDHI,NYUMBA NA MAKAZI | ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI | ARDHI, MALIASI NA MAZINGIRA | HALIMA MDEE | - |
Popular Posts
-
Tarehe 6 mwezi wa Aprili, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, aliunda Tume ya ...
-
Nakala ya barua ya askari Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo ...
-
YAH: UTEUZI WA KUJAZA NAFASI YA UONGOZI KATIKA WIZARA YA UCHUKUZI Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Eng. Omar A. Chambo kwa Mamlaka a...
-
1. MWENYEKITI TAIFA 1 Asila Ali SALIM 2 Jamal K. ALI 3 Lulu Mcham ABDALLAH 4 Lusekelo W. MALEMA 5 Mbarouk M. MBAROUK 6 Mwana Amina Haji FARU...
-
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Manchester City ya Uingereza wakichuana vikali na mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Real...
-
Katibu Msaidizi wa CCM Bi. Anastazia Mwonga kulia akimkabizi fomu ya ugombea Ukatibu wa Siasa na Uenezi wa Wilaya ya Temeke kwa Yahaya Nd...
-
Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akihutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro katika mkutano wa hadha...
-
This statement outlines how we handle any personal information we obtain PataHabari is committed to respecting and protecting the privac...
-
Zitto Kabwe NDUGU Watanzania, r Ninawaandikia barua hii ya wazi kujieleza kwenu kuhusu mjadala mkali uliolitikisa taifa siku chache ...
-
Mwananchi wa Kijiji cha Jambiani akiwasilisha maoni yake kwa njia ya Barua kwa Tume. Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wak...