Pages

Showing posts with label FASHION - MITINDO - MAVAZI. Show all posts
Showing posts with label FASHION - MITINDO - MAVAZI. Show all posts

Monday, September 10, 2012

'ALLY REHMTULLAH 2013 COLLECTION'

Pichani Juu na Chini ni Models wakionyesha Vito vyenye Madini ya Tanzanite yanayochimbwa nchini Tanzania wakati wa raundi ya kwanza ya onyesho la 'Ally Rehmtullah 2013 Collection.(The Tanzanite Experience).

Pichani Juu na Chini ni Models wa kiume wakionyesha Mavazi ya Street Souls ambao ni mmoja wa wadhamini wa 'Ally Rehmtullah 2013 Collection'.
Pichani Juu na Chini ni Models wakionyesha 'Ally Rehmtullah 2013 Collection'.
Mbunifu mahiri wa mavazi nchini Ally Rehmtullah akijitambulisha baada ya Model kuonyesha Collection yake mpya ya Mwaka 2013 katika Onyesho la aina yake katika hoteli ya Serena jijini Dar.

Warembo waliokuwa wakikaribisha Wageni kutoka kampuni ya DULUX.

Mboni Masimba a.k.a Kim Kardashian wa Bongo na rafiki.

Evelyn na Eskado Bird.


MC Taji Liundi akitoa utambulisho wa 'Ally Rehmtullah 2013 Collection' iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya wadau kutoka ndani na nje ya nchi.

Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors ambao ni Wadhamini wakuu wa 'Ally Rehmtullah 2013 Collection kupitia Brand ya Mercedes Benz Tharaia Ahmed (wa tatu kushoto) sambamba na wadau wa tasnia ya urembo nchini wakati wa Onyesho hilo. Wa nne kushoto ni Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 2004 Faraja Kotta (Mrs. Nyalandu), Nancy Sumari (Miss World Africa 2005) pamoja Mkurugenzi wa Mtandao wa Bongo5.com Lucas.

Jennifer Bash (katikati) akiwa na marafiki.

Wengine walikaa kwa nje kushuhudia 'Ally Rehmtullah 2013 Collection' kupitia Big Screen zilizofungwa kwenye bustani ya hoteli ya Serena jijini Dar.

Msanii mkongwe wa Muziki nchini Diva Karola Kinasha akitoa burudani kwa wageni waalikwa.
Mbunifu wa mavazi anayechipukia Jokate Mwegelo a.k.a Kidoti akizungumzia show ya 'Ally Rehmtullah 2013 Collection'.
Designer Ally Rehmtullah, Super Model Fideline Iranga a.k.a Lagy Gaga na Sinta a.k.a JLO wa Bongo.
Warembo walipendeza sana.
Ally Rehmtullah katika picha ya pamoja na Designer wenzake walioshuhudia Collection yake mpya ya Mwaka 2013.
Mrs. Faraja Nyalandu, Ally Rehmtullah, Nacy Sumari na Sinta wakishow love mbele ya Camera yetu.
Belvedere Vodka walitoa huduma za vinywaji vya aina zote kwa wageni waalikwa.
Moja kivutio kikubwa kwa wageni waalikwa kwenye "Ally Rehmtullah 2013 Collection" ni hili gari aina ya Mercedes Benz M CLASS yanayouzwa na Kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar es Salaam.Kwa picha zaidi Bofya hapa BOFYA HAPA

Monday, August 27, 2012

AUDITION YA 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' JIJINI DAR .

Ally Rehmtullah.
Casting Coordinator wa ALLY REHMTULLA'S COLLECTION 2012 Audition Martin Kadinda akitoa mwongozo wa zoezi hilo kwa Models walioshiriki.
Baadhi ya Models wa kiume waliojitokeza Serena Hotel wakisubiri usaili.
Pichani Juu na Chini ni Models wa kike na wa kiume wakipita mbele ya Majaji wakati wa usaili.
Meza kuu ya Majaji kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Alliance Auto Bw. Alfred Minja akiwakilisha CFAO Motors wauzaji wa Magari ya Mercedes Benz ambao ndio wadhamini wakuu wa 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013', Aysha Mbarak Meghji kutoka Ayman Garage-Convolution Ideas Ltd, Administrative Assistant Mawalla Advocate na pia ni Model Myler Nyangasa, Mwasisi na CEO wa Missie Popular Blog Mariam Ndabagenga na Fashion Stylist wa Fashionnjukii.com Rosemary Kokuhilwa.
Pichani Juu na Chini Models wa kike wakionyesha umahiri wa Catwalk wakati wa Audition kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki "ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013".
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Models wa kiume wakipita jukwaani mbele ya majaji.
Baadhi ya Models wakiwa katika tafakari ya SIJUI NITAPITA wakati wa usaili huo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed ambao ni wauzaji wa magari aina ya Mercedes waliodhamini onyesho la 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' akielezea kuwa Mercedes Benz imedhamini Onyesho hilo kwa mara ya kwanza kwa sababu kwanza wanamkubali Ally Rehmtullah kama mmoja wa wabunifu wenye hadhi ya juu hapa nchini na kuwa wamechagua Brand ya Mercedes Benz kwa sababu ni magari yenye kiwango cha juu na Rehmtullah ana ubunifu wa hali ya juu.
Mercedes Benz imekuwa ikijihusisha na udhamini wa 'High and Fashion Show' duniani kote pia Orchestra, Baley na Sailing matukio ambayo yanaendana na hadhi ya magari ya Mercedes. Kulia ni Chief Editor wa MO BLOG Lemmy Hipolite.
Sales & Marketing Representative kutoka RAHA Preetkamal Bansal akielezea kuwa kampuni yake imekuwa na furaha kushirikiana na Ally Rehmtullah kwa kuwa ubunifu wake ni wa hali ya juu kama wao wanavyotoa huduma za Intaneti za hali ya juu na wamekuwa wakitoa huduma ya ISP (Internet Service Provider) kwa muda wa miaka 16 kwa kiwango kilekile.
RAHA wakiwa wadhamini muhimu watawezesha watu kuona Live 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' itakayofanyika September 8 mwaka huu ambapo Watu duniani kote wataona kupitia www.ar.co.tz
Amemalizia kwa kusema "On the day the Jungle puts on its show Our Broadband let you watch it Live".
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Quality Furniture Limited Bw. Mahad A Nur akisema wameamua kujihusisha kudhamini show hii ya Ally Rehmtullah ili kutoa ufahamu kwa umma juu ya ubora wa bidhaa wanazotengeneza na siku ya Onyesho hilo watatoa Furniture zitakazotumika sehemu ya wageni maalum (VIP).

Quality Furniture Limited wanatengeneza bidhaa zenye Quality kama lilivyojina lao na kama ilivyo show ya Ally Rehmtullah lakini pia Bw. Mahad amesema wako tayari kuwadhamini wabunifu chipukizi watakaokuja na ubunifu wenye Quality.
Majaji Aysha Mbarak Meghji na Rosemary Kokuhilwa wakibadilishana mawazo baada ya kazi kubwa ya kuchagua Models watakaoshiriki 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013'.
Hawa pia nao walikuwepo.

Popular Posts