Pages

Showing posts with label Kagera. Show all posts
Showing posts with label Kagera. Show all posts

Thursday, September 6, 2012

MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA

Marehemu Kardinal Laurean Rugambwa enzi ya uhai wake.
Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake.

*************
MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA

Kanisa katoliki nchini dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali Laurean Rugambwa, aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la Bukoba. Maziko ya Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6 mwaka huu.

Mwili wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi barani Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo Kashozi kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa.

Akizungumza katika kipindi cha Baragumu Channel ten na baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba Askofu Methodius Kilaini , amesema wanataka kumzika kardinali Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa alilopenda kuzikiwa kutokana na kukamilika kwake, lakini kabla ya kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa, alikobatizwa, sherehe zitakazoambatana na kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa kardinali Rugambwa tarehe 7 mwezi Octoba.

"tuna alika watu wengi kuhudhuria kwenye tukio hili..., na pia tunakaribisha michango itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu kwa mchango wake,alisema askofu Kilaini.

Naye mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo , James Rugemalira, alimwelezea Kardinali Rugambwa kama mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye jamii ya watanzania, kuanzia kwenye nyanja za elimu, afya na kiroho.

Marehemu Kardinali Rugambwa ana mambo mengi ya kukumbukwa na jamii ya watanzania hususani watu wa mkoa wa Kagera hasa kwa juhudi zake za kupeleka elimu mkoani humo kwa kuagiza ujengwaji wa shule za msingi na sekondari ikiwemo shule ya kwanza ya wasichana ya Rugambwa ambayo ujenzi wake ulikuwa ni mafanikio ya marehemu huyo kuomba msaada wa ujenzi wa shule hiyo alipohutubia bunge la Ujerumani akiwa mwafrika wa kwanza.

Licha ya mambo hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha mfuko rasmi wa kumuenzi kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la Kardinali Rugambwa ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

Padre Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10 Februari,1952. Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.

Thursday, August 16, 2012

BUS LA MUHAMED TRANS LAPATA AJALI BUKOBA MJINI

Lori lenye nambari T814 liliokua baada ya kugongwa na bus kwa kutokea nyuma.
Lori likiwa limeharibika vibaya.
RPC Kelenge kulia akijadili jambo na RTO Willy eneo la tukio
Bus la muhamed trans lenye nambari T884 likiwa limepinduka baada ya kupata ajali kwa kuligonga lori la mchanga. Ambapo bus hilo lilikua likisafiri kutoka bukoba mjini kuelekea Mwanza, na abiria wote wamenusurika.
Ajali hii imetokea asubuhi ya leo majira ya saa moja kasoro ni eneo la kyetema km 5 kabla ya kifika kemondo na ni umbali wa km 15 kutoka Bukob mjini. Shukrani za pekee ziwaendee BukobaWadau Blog

Thursday, July 26, 2012

MIKUTANO YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA - TSEGERA, ANGA, KYERWA, KARAGWE, MISENYI

Wiliam Wilbard Ishengoma, mkazi wa Kata ya Bwanjai, Wilaya ya Misenyi mkoani Kageraakitoa maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wake wilayani hapo hivi karibuni.
Mzee Idrisa Omary (70),mkazi wa kijiji cha Michungwani, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya Mpya katika mkutano wa kukusanya maoni kijijini hapo hivi karibuni.
Abdallah Mohamedi (31) mkazi wa kijiji cha Michungwani, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano wa kukusanya maoni kijijini hapo hivi karibuni.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Michungwani iliyopo kijiji cha michungwani, Kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tanga wakijisomea kitabu kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka1977 katika mkutano kukusanyaji maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya uliofanyika kijijini hapo hivi karibuni.
Bi.Teodezea John, ambaye ni mlemavu, mkazi wa Kata ya Kilimikile, Wilaya ya Misenyi,mkoani Kagera akitoa maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wake wilayani hapo. hivi karibuni.
Wananchi wa Kata ya Nkwenda, Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera wakiwa katika mkutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wa kukusanya maoni yao kuhusu KatibaMpya.Picha -Tume ya Mabadiliko ya Katiba (CRC))

Thursday, July 5, 2012

WASHIRIKI KATIKA SHINDANO LA KUMSAKA MISSS UTALII KAGERA 2012 WATEMBELEA BANDARI YA BUKOBA NA MELI YA MV. VICTORIA

Meneja wa Kampuni ya Kiroyera Tours akitoa maelezo kwa Warembo hawa.
Warembo wakiwa katika pozi.
Muandaaji wa Onyesho hili Bi Dinna akimshkuru AFISA wa Bandari ndg Msese.
Afisa wa Bandari Mdau Ajuaye Kheri Msese akiwapa somo walimbwende katika kuwapa uelewa zaidi wa mambo mbalimbali.
Warembo wakiwa wamejipanga kwa pozi.
Mkuu wa Bandari Ndg Ernest Nyambo akisalimiana na walimbwende hawa. Picha/BukobaWadau Blog.

Monday, July 2, 2012

ATEKELEZA FAMILIA BAADA YA MKE KUJIFUNGUA WATOTO WANAOFANANA NA NYANI.

Mtoto Alhaj.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mwanaharusi Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye shati Nyekundu na Abdulatifu.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha kuwa magumu.Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu. Pia aliondoka na matandiko yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).Alisema baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu aliozaa naye.Alisema katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.

“Mtoto wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa la saba mwaka huu. Ramadhani (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.

Mwanaharusi alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5) ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa kuanza shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi. Mawasiliano yao yanategemea ishara tu.

“Ukiacha matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu kubwa. Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.

Mwanaharusi alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na macho yao ni makubwa. Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.

Hata hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu na afya zao zikiwa njema kabisa. Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.

“Wakati bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika hospitali ya mkoa wa Singida. Alichunguzwa na alibainika kuwa na upungufu wa damu. Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi nyumbani”,alisema.

Alisema baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa, ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha magumu mno ambayo ni ya kuomba omba. Mnyawi pamoja na familia yake, amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea watoto wao pamaja, jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi kugoma kumrudia Mwanaharusi.

Naye mratibu elimu wa kata hiyo Mwekwa Mwekwa, alisema watoto hao wawili, shule inayowafaa ni ile ya watoto wenye mtindio wa ubongo na si hizi za kawaida.Jitihada ya kumtafuta Mnyawi ambaye anaishi kijiji hicho cha Ndulungu, hazikuzaa matunda baada ya kuelezwa kwamba baada ya kusikia waandishi wa habari watafika kijijini hapo, alifunga safari na kuelekea jijini Mwanza.

Popular Posts