Pages

Showing posts with label Kilimanjaro. Show all posts
Showing posts with label Kilimanjaro. Show all posts

Thursday, September 6, 2012

Bonite Bottlers yawazawadia washindi wa promosheni ya Vuta Mkwanja

Washindi 16 wa promosheni ya Vuta mkwanja wakifurahi zawadi ya pesa taslimu waliyo kabidhiwa kiwandani hapo.

Meneja uzalishaji wa Bonite Bottlers Leonard Mangupili akimkabidhi mshindi Hamid Nkya mkazi wa Ngaramtoni Arusha ,kitita cha shilingi milioni moja alichojishindia kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja
Mkuu wa masoko na mauzo wa Bonite Bottlers Christopher Loiruk akimkabidhi mshindi Rahim Hashim mkazi wa Majengo Moshi, kitita cha shilingi milioni moja alichojishindia kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja.

Mratibu wa mauzo wa Bonite Bottlers Boniface Mwasi akimkabidhi mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi laki moja kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja.


Mkuu wa masoko na mauzo wa kiwanda cha vinywaji baridi Bonite Bottlers,Christopher Loiruk akizungumza na wanahabari.

*******


Mwandishi Wetu ,Moshi.
KAMPUNI ya vinywaji baridi jamii ya Coca Cola ,Bonite Bottlers jana imekabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa washindi kumi na sita wa promosheni ya Vuta Mkwanja ambayo inafikia tamati mwezi huu.

Washindi katika promosheni hiyo iliyoanza mwezi Julai mwaka huu ni pamoja na Fredy Charles ,Hamid Nkya wote wakazi wa Arusha na Rahim Hashim mkazi wa Majengo mjini Moshi ambao kila mmoja amejinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.

Washindi wengine ni Goodluck Kessy ,Focus Njau ,Joseph Kauwedi,Samson Mushi na Fatuma Ibrahimu ambao walijishindia kaisi cha shilingi laki
moja kila mmoja.

Mkuu wa masoko na mauzo wa kiwanda hicho Christopher Loiruk aliwataja washindi wengine waliojishindia kiasi cha shilingi lakini moja kuwa ni Julius Michael,Christina Kessy,Dorin Masawe na Khadijah Said.

Aliwataja washindi wengine ambao wamepatikana katika mikoa ya Arusha, Kilimnjaro Singida na Manyara kuwa ni Lucas Sumari ,Magdalena John na Lilian Maro ambao wote walikabidhiwa fedha zao kiwandani hapo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi ,Loiruk alitoa wito kwa wateja wa Coca cola kuendelea kunywa kinywaji hicho na jamii yake ili waweze kuibuka washindi wa zawadi mbalimbali ambazo bado zipo katika kinywaji hicho.

“Shindano promosheni imemalizika ,lakini zawadi bado zitaendelea kutolewa kwa kuwa bado zipo katika mzunguko,kuna washindi ambao wamejishindia zawadi mbalimbali kwa kunywa soda za Coca cola ,Fanta na Sprite …kila soda unayokunywa una nafasi ya kuwa mshindi”alisema Loiruk.

Alisema promosheni hiyo imewezesha wateja wengi wa bidhaa hizo kujishindia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoaja na Sh 1000,000,sh 100,000,10,000,sh 5,000 ,sh 2,000 fulana za Coca cola pamoja na soda ya bure.

Monday, August 6, 2012

TAFRIJA YA KUMUAGA MKURUGENZI MTENDAJI WA SBL MJINI MOSHI

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (wapili kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda wakati wa tafrija maalum ya kumuaga Wells, iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
Mama Tundu Pinda, akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL aliyemaliza muda wake, Richard Wells, wakati wa tafrija ya kumuaga iliyofanyika kiwanda cha SBL mjini Moshio hivi karibuni.
Mama Tunu Pinda, akisalimiana na Mkurugenzi mpya wa SBL, Steven Gannon.
Richard Wells (kushoto) akiwa katika vazi la jadi la jamii ya Wamasai pamoja na Kisu cha sime baada ya kukabidhiwa na Wafanyakazi wa SBL mjini Moshi wakati walipomuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake na kumkaribisha Mkurugenzi Mpya Steven Gannon.
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Bia Serengeti Mjini Moshi wakipiga picha na viongozi wao.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dkt. Msengi
Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda, akitunzwa na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela, kwa kutoa burudani ya aina yake wakati wa tafrija hiyo ya kumuga Richard Wells.
Vijana wa Kalunde Band wakiwa kazini kutoa burudani.
Hapa kazi tu.....Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda, na Mkurugenzi wa Masoko, Ephraim Mafuru, wakiimba wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga Richard Wells.
Richard Wells, akicheza muziki na Wafanyakazi wa Kiwanda cha SBL mjini Moshi wakati wa tafrija ya kumuaga.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa SBL, Steven Gannon, akisakata rumba na wafanyakazi wa SBL Kiwanda cha Moshi.
Wafanyakazi wakiwa wanaendelea na vitu vya hapa na pale wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga Mkurugenzi Mtendaji aliyemaliza muda wake, Richard Wells, mjini Moshi.

Thursday, July 26, 2012

Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe Azindua Huduma Za Safari za Anga Za Qatar Aiways Kutoka KIA Kuelekea Sehemu Mbali Mbali

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh lakizungumza machache na pia kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo mapema leo iliofanyika kwenye uwanja wa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akimpa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison zawadi ya yenye nembo ya ndege ya shirika hilo la Qatar.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar zawadi ya picha yenye kivuli cha Mlima Kilimanjaro .
Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat,Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakijadiliana jambo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika hilo aina ya Ndege namba QR546,shoto kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki
Wakuu wa uzinduzi wakipga makofi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akipiga makofi wakati kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza,shoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat

Tuesday, July 10, 2012

JUU YA UZUSHI UNAOENEZWA NA MH. MWIGULU NCHEMBA JUU YANGU NA CHAMA CHANGU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UZUSHI UNAOENEZWA NA MH. MWIGULU NCHEMBA JUU YANGU NA CHAMA CHANGU


Ndugu zangu kwanza nachukua nafasi hii kuendelea kumshukuru Mungu kwa afya njema anayoendelea kunijalia mimi na Mke wangu hapa Hospitali ya KCMC. Pia niwashukuru wote walionifariji/wanaoendelea kunifariji katika kipindi chote cha matatizo yaliyotokea.

UTANGULIZI

Itakumbukwa kuwa tarehe 28/05/2012 nilipata mbaya ya gari. Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Boma karibu na chuo cha VETA. Watu wa kwanza kufika kwenye Eneo la ajali na kutupa msaada walikuwa ni Askari Polisi waliokuwa Doria karibu na eneo lile na Raia waliofika wa pia walikuwemo MWENYEKITI WA CHADEMA (W) YA HAI pamoja na MWENYEKITI WA BAVICHA (W) YA HAI. Walisaidiana na Polisi kuchukua majeruhi (Mimi nikiwemo) pamoja na marehemu waliofariki pale hadi Hospitalini.

Baada ya kufika hospitalini pia walifika MHE.MEYA WA MANISPAA YA MOSHI (AMBAYE PIA NI DIWANI WA CHADEMA) akiongozana na baadhi ya VIONGOZI WA CHADEMA WA KATA YAKE NA BAADHI YA MAENEO YA MOSHI MJINI.. Baadaye alifika KATIBU WA CHADEMA MKOA WA KILIMANJARO AKIONGOZANA NA BAADHI YA MADIWANI WA CHADEMA WA MOSHI NA ARUSHA na Viongozi wengine ambapo nakumbuka walitokea Wilaya ya Mwanga kwenye Mikutano ya Hadhara. Tulikuwa wote hadi tunapatiwa huduma na majeruhi tukapelekwa Wodini. Siku iliyofuata nilipokea Simu kutoka kwa MHE. FREEMAN MBOWE (MWENYEKITI WA CHADEMA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI) akiwa Mtwara kwa shughuli za Chama akinipa Pole kwa yaliyotokea na kunifariji.

Baadaye hali yangu ilipoimarika kidogo tukapanga taratibu za mazishi ya Marehemu Mama yangu Mzazi (R.I.P) na miongoni mwa watu waliohudhuria kwanza ni WANACHAMA WA CHADEMA, MADIWANI WOTE WA CHADEMA ARUSHA, MADIWANI WA MOSHI MJINI NA MOSHI VIJIJINI. Kutoka makao makuu ya CHADEMA waliwakilishwa na Mhe.Rwakatare na Ndg.Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Utawala) Pia walihudhuria Baadhi ya WWABUNGE WA CHADEMA wakieleza sababu za viongozi na wabunge wengine kutokuhudhuria (Na zilikuwa Sababu za Msingi kabisa) kwa sababu hata baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria walileta salam za wakubwa wao ambao nao walitamani kuhudhuria lakini kutokana na sababu mbali mbali walishindwa!..

Pamoja na hayo, MHAMA JOSEPHINE MUSHUMBUSI (MKE WA MHE.KATIBU MKUU WA CHADEMA) alinitembelea hospitalini akiwa na wajumbe kadhaa... Aliniletea salam za pole kutoka kwa KATIBU WANGU MKUU WA CHAMA. Nilifarijika sana kuona kuwa kiongozi wangu pamoja na kuwepo kwake safarini kikazi lakini bado aliweza kutuma ujumbe kwangu.

Baadaye nilihamishiwa MOI (Muhimbili) kwa ajili ya matibabu Zaidi. Nakumbuka walifika wabunge wengi sana wa CHADEMA lakini kubwa zaidi alifika MHE.FREEMAN MBOWE (MWENYEKITI WA CHADEMA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI).

KANUSHO

Nimekuwa nikisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Mwigulu Nchemba (Mb-CCM) Anatangaza kuwa Chama changu kimenitupa na hakina msaada wala Ushirikiano na mimi kwenye Matatizo yaliyojitokeza..

Kwanza: Sijawahi kumwajiri Mwigulu Nchemba kuwa msemaji wangu!.

Pili: Mwigulu Nchemba si mkweli na hajui chochote kuhusu mimi wala CHADEMA.

Tatu: Mwigulu Nchemba anataka nionekane sina shukrani kwa viongozi na Chama changu kwa Umoja na Ushirikiano wanaoendelea kunipatia hata sasa.

Nne: Viongozi wangu wanafuatilia kwa karibu sana matibabu yangu na Mke wangu.

MWISHO:

Naomba Mwigulu aelewe kuwa sitaki malumbano yasiyo na Tija kwangu wala kwa Wananchi wangu Walionichagua. Pia nisingependa kumtaja Marehemu Mama Yangu (R.I.P) kabla hata ya Arobaini. Zaidi ya yote akumbuke kuwa Viongozi na Wabunge wa CHADEMA wana mambo mengi ya kufanya na hawatakuwa tayari tena kujibu uongo na uzushi DHAIFU kama aliouzusha!!.

Ahsanteni Sana,
Mungu aendelee kuwabariki.
Joseph Selasini
(Mb) Rombo-CHADEMA.

via facebook.com/joseph.selasini

Sunday, July 8, 2012

Serengeti Soccer Bonanza yafana Mjini Moshi

Wachezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Barcelona wakishangilia mara baada ya mchezaji wao kufunga goli zuri katika dakika tisini dhidi ya timu ya Mashabiki wa timu ya Chealsea katika mchezo wao wa fungua dima kwenye bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza linalofanyika kwenye uwanja wa Memoriol mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mchana huu.
Bonanza limepamba moto ambapo kumekuwa na burudani mbalimbali zikishirikisha mpira wa miguu kutoka kwa timu za mshabiki wa timu mbalimbali za Ulaya ambazo ni Manchester United, Liver Pool, Chealsea, Arsenal, Baeryen Munichen na Manchester City, Barcelona na Real Madrid.
Kikosi cha timu ya mashabiki wa Manchester kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha Manchester City kikiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa Chealsea na Barcelona wakichuana vikali katika mchezo wao wa fungua dimba ambapo timu ya Barcelona imeshinda goli 1-0 dhidi ya Chealsea.
Kikosi cha mashabiki wa timu ya Barcelona kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Arsenal wakisubiri mchezo wao kuanza .
Timu ya Bayern Minicheni wakisubiri kuanza kwa mchezo wao.
Timu ya mashabiki wa Chealsea wakiwa katika picha ya pamoja .
Eneo hili likiwa limeandaliwa kwa ajili ya mashabiki maalum wa timu za mashabiki mbalimbali wa timu za Ulaya
Huduma ya kwanza imeimarishwa ili kuhakikisha wachezaji na mashabiki watakaopata matatizo yeyote katika bonanza hilo wanahudumiwa ipasavyo.
Mashabiki wa timu ya Barcelona wakiwa na jezi ya timu hiyo
Mashabiki mbalimbali wakiangalia matukio mbalimbali katika bonanza hilo
Mashabiki wa Machester United wakiangalia timu yao haipo pichani wakati ilipokuwa ikicheza.
Mtangazaji wa Clouds FM Mbwiga wa Mbwiguke akimpa kipaza sauti Said Bonge pia wa Kipindi cha Power Breakfast.
Mtangazaji wa Clouds FM Mbwiga wa Mbwiguke akiongea na mwalimu wa timu ya Chealsea ambaye aliamua kujipoza na muwa mkuuubwa mara baada ya kufungwa goli moja kwa bila na Barcelona katika mchezo wa fungua dimba.

Sunday, July 1, 2012

Chris Wilde Atoa ahadi ya kushiriki Kilimarathon mwaka 2013

Mmarekani Chris Wilde akiwa amesimama mahala alipomalizia mbio za kilometa 50 kama zawadi kwa uhuru wa Tanganyika. Kulia kwake ni mkimbiaji wa kimataifa wa Tanzania Nelson Brighton.
--

Chris Wilde raia wa Marekani aliyekimbia kilometa 50 kuipa Tanzania zawadi ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ameahidi kurejea tena mwakani kukimbia kilometa 51 katika mbio za kutimiaza miaka 23 tangu kuanzishwa kwa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.
Wilde ambaye ni mganga msaidizi kutoka jimbo la Minnesota amekuwa mtu wa kwanza kukimbia kilometa 50 kusheherekea uhuru wa Tanganyika alipokimbia katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili tarehe 24 mjini Moshi.

Mbio hizo zilifanyika kuanzia Moshi Club hadi Rau madukani na kurudi. Chris Wilde alirudi mara 9 na nusu ili kutimiza kilometa 50 kama zawadi kwa nchi ya Tanzania.
“Naipenda sana Tanzania na ili kuidhihirishia dunia kuwa mlima Kilimanjaro uko Tanzania, nakimbia mbio hizi kama zawadi kwa Tanzania” alisema mzungu huyo mwenye umbo la mwariadha wakati anajiandaa kukimbia mbio hizo jumapili tarehe juni 24.
Wilde aliongozana na mwanariadha wa kimataifa mtanzania Nelson Brighton na ambaye anakwenda nchini Marekani mwezi ujao kushiriki katika mbio mbalimbali zilizoandaliwa kwa ufadhili wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.

Kumiminika kwa wakimbiaji wa Kimarekani, Ulaya, Australia, Canada na Scandinavia katika mbio za Mt. Kilimanjaro marathon ni neema kubwa kwa taifa hili ambalo lina hazina kubwa sana ya wanamichezo wanaotakiwa kuendelezwa.Chris Wilde aliungana na mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon na kuzifanya kuwa mbio zinazovutia washiriki wa Kimataifa. Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances kutoka Bethesda nchini Marekani.

Ni mbio zilizokwisha kupewa tuzo na majarida mbalimbali yanayoheshimika duniani kama vile Wonders of World ambalo lina wasomaji zaidi ya milioni 5 ambalo lilizipa nafasi ya pili wakati ambapo jarida linaloheshimika la Forbes lilizipa nafasi ya kwanza kama mbio zinazovutia.

Imetumwa na;
Grace Soka
Afisa Uhusiano
Mt. Kilimanjaro Marathon 1991

Saturday, June 23, 2012

Deidre Lorenz Atembelea kituo cha Yatima wa Kituo cha Yatima cha Upendo

Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye alitua mjini Moshi jana kushiriki kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro Marathon leo alikaa na watoto wa kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa na masista wa shirika la Precious Blood mjini Moshi. Lorenz aliingia kwa kishindo katika Manispaa ya Moshi na kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini Marekni kwa kutumia usanii wake wa filamu.

Deidre Lorenz anashiriki katika mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza kutimua vumbi tarehe 24 Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na kurudi. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka katika mji wa Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja Tanzania kuanzisha mbio za marathon.

Deidre Lorenz anawakilisha kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto yatima cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto. Aidha, aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate na zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.

Lorenz ameshiriki pia katika mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza kuhusu nia yake ya kuitembelea Tanzania mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura nzuri sana. Aidha marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje katika mbio zinazofuata.

Klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 inakusudia kuwatumia watu maarufu kuja Tanzania ili waweze kuutangaza utalii pamoja na mazingira ya kuwekeza. Klabu hii ina lengo la kuanzisha marathon nyingine tena ambayo itajumuisha mbio na michezo mingine ya uwanjani.

“Tutakuwa na wiki nzima ya mashindanio ya uwanjani na siku ya saba tutafanya mbio za marathon” alisema Rais wa Klabu hiyo Onesmo Ngowi alipokuwa anazungumza na waandishi wa bahari hapa Moshi. Ngowi alieleza kuwa ni muhimu Moshi/Tanzania ikawa na mashindano ya michezo mingi itakayowavutia watalii na wawekezaji wengi kuja Tanzania.

Akielezea kuhusu mikakati ya klabu yake kuendeleza mchezo wa riadha Ngowi ambaye pia ni Rais wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi alisema kuwa wameweka mikakati mingi itakayoifanya mji wa Moshi kuwa kitovu cha utalii katika mkoa wa Kilimanjaro.
Hizi mbio ni sehemu tu ya mikakati ya kuendeleza michezo katika mkoa huu ambao miaka ya sabini ulikuwa unaongoza kwa michezo katika nchi hii. “Tutashirikiana na mashirikisho ya michezo ya ndani na nje kuinua viwango vya wanamichezo wetu” alisema Ngowi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo katika mkoa wa Kilimanjaro. Alisema kuwa wameandaa mikakati mingi na kumalizia kuwa Tanzania ni yetu sote kwa hiyo tuna jukumu la kuchangia katika maendeleo yake.

Deidre Lorenz atakimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili ijayo na ataondoka usiku wa jumapili kurudi nyumbani kwake New York jiji linajulikana kama “The Big Apple” na Financial Capital of the World (Jiji la Fedha Duniani)

Imetumwa na:


Grace Soka
Afisa Uhusiano


Mt. Kilimanjaro Marathon
Technology House
35-38 Ghalla Road
Moshi - Tanzania

Tuesday, June 19, 2012

JK ASIFIWA NA MWANZILISHI WA KILI MARATHON

Rais Kikwete na Marie Frances jijini Washington DC.
Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Akimkabidhi pesa za Visa mkimbiaji Nelson Brighton kwa niaba ya Mt. Kili Marathon kwenda USA.
-----
Mwanzilishi wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon Marie Frances mji wa Bethesda nchini Marekani amemsifu Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama kiongozi anayependa nchi yake na anayeona mbali. Marie Frances ametoa sifa hizo hapa mjini Moshi wakati Rais Kikwete akikutana na viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania (AT) kupanga mikakati ya kufufua riadha nchini hivi karibuni.

Frances ambaye aliwahi kukutana na Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa jengo la Tanzania House katika jiji la Washington DC amesema kuwa ni nadra sana kuona kiongozi wa nchi akikutana na viongozi wa chama cha mchezo wowote kuzungumzia maendeleo yake. Hii ni miujiza hata katika nchi kama Marekani.

Marie Frances amemuelezea Rais Kikwete kama mtu wa haiba ya kipekee mwenye akili na maono ya kuiendeleza Tanzania kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya Millenia. “Nilimpenda sana nilipokutana naye jijini Washington. Ni kiongozi mwenye haiba ya kipekee” alisema Frances ambaye aliombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za marathon nchini Tanzania mwaka 1990.

Marie Frances ambaye alikuwa mkuzaji (producer) wa Miss Universe pamoja na vipindi vya television huko Hollywwod nchini Marekani alihamia nchini Misri mwaka 1984 kuafanya kazi ya ABC kama mwandishi wa bahari. Akiwa nchini Mirsi, Marie Frances alianzisha mbio za Pyramid Marathon pamoja na Miss Universe ambazo ziitangaza sana nchi ya Misri. Ni wakati wa matamasha haya balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo alipomwomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon ili kuitangaza Tanzania.

Frances alikuja Tanzania mwaka 1990 na kutaka kuanzisha mbio za Mt. Meru Marathon lakini alipofika tu mjini Moshi alivutiwa sana na mlima Kilimanjaro na hivyo kuiamua kuanzisha mbio za “Mt. Kilimanjaro Marathon” mwaka 1991. Mbio hizi hukimbiwa kila jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita na zitatimiza miaka 22 tarehe 24 Juni mwaka huu.

Mt. Kilimanjaro Marathon zimeshapewa tuzo mbalimbali kama mbio za kimataifa. Gazeti la Wonders of the World lenye wasomaji zadi ya million 5 limezipa nafasi ya 2 kama mbio nzuri za kushiriki. Wakati jarida la kimataifa la Forbes limezipa nafasi ya kwanza kama mbio nzuri za kukimbia! Marie Frances pia ameanza kuwapeleka wanariadha wa Tanzania kukimbia nchini Marekani kwa kuwasaidia fedha za Visa za Marekani pamoja na tiketi za ndege kama inavyoonyesha picha ambapo mkimbiaji Nelson Brighton anapewa pesa na Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Benadetta Kinabo kwenda nchi Marekani mwezi ujao kwa ufadhili wake.Kwa sasa mbio hizi hufadhiliwa na shirika la ndege la Ethiopia.

Ni katika juhudi zake za kuutangaza mlima Kilimanjatro ndipo Manispoaa ya Moshi ikaipa jina la Marie Frances Boulevard barabara ya zamani ya Bustani Ale.

Mt. Kilimajaro Marathon itaanzia Moshi Klabu tarehe 24 Juni saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za kilometa 42, 21, 10 na 5 zitashindaniwa na watalii toka Marekani pamoja na wakimnbiaji toka Moshi na Arusha.

Wakimbiaji wanajiandikisha kwa wingi Bristol Cottages hotel iliyopo mkabala na benki ya Standard Chattered karibu na Kilimanjaro Hospital katika Manispaa ya Moshi.

Imetumwa na:
Grace Soka
Afisa Uhusiano
Mt. Kilimanjaro Marathon 1991

Popular Posts