Translate - Tafsiri
Labels
- Tamko kwa Umma - Press Release
- All Photos - Picha
- CCM CHAMA CHA MAPINDUZI
- Zanzibar
- IKULU - STATE HOUSE
- Sports - Michezo
- CHADEMA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
- Dodoma
- Editorial Opinion - Maoni Tahariri
- Tanzania
- Dar es salaam
- Habari za Kimataifa - International News
- Burudani - Entertainment
- Bungeni
- Katiba - Constitution
- Dini - Religion
- Mbeya
- SMZ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
- Vodacom
- Hotuba - Speech
- Arusha
- Iringa
- Tanzia - Msiba - Mazishi
- Afya - Health
- Ofisi ya Waziri Mkuu
- Singida
- Ajali - Accident
- Development Reports
- Morogoro
- Open Letters - Barua za Wazi
- Urembo - Beauty
- Kenya
- CUF Chama cha Wananchi
- Maonyesho ya Sabasaba
- Ofisi ya Makamu wa Rais
- Huduma za Usafiri - Transport Services
- Tanga
- Business Finance Money
- Masuala ya Elimu - Education
- Miundombinu -Infrastructure
- Mtwara
- Rukwa
- UVCCM
- Habari za Mahakamani
- Kilimanjaro
- Serengeti Breweries Limited
- Tourism - Utalii
- Habari za Nyumbani - Local News
- Jakaya Mrisho Kikwete
- Kagame Cup - Kombe la Kagame
- Katavi
- Lindi
- Nishati - Madini - Mining - Energy
- UN United Nations - Umoja Mataifa
- Yanga
- African Union - Umoja wa Afrika
- Bagamoyo
- Agriculture - Kilimo
- Azam FootBall Club
- Balozi na Ofisi za Balozi
- Baraza la Wawakilishi
- Human Rights - Haki za Binadamu
- Jeshi la Polisi Tanzania
- Kigoma
- Maonyesho ya Nane Nane
- Simba Sports Club
- Tabora
- East African Community
- HARUSI - WEDDINGS
- Kagera
- Mwanza
- Pemba
- Shinyanga
- Sumbawanga
- TFF Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
- Videos - Multimedia
- Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Kimataifa
- Wizara ya Nishati na Madini
- Afdb African Development Bank
- Airtel Tanzania
- Benki - Fedha - Uchumi
- Fiesta 2012
- GEITA
- Mafuta - Oil Issues
- Uganda
- Wizara ya Maliasili na Utalii
- BAJETI 2012 - 2013
- Burundi
- Climate Change - Mabadiliko ya Tabia Nchi
- FASHION - MITINDO - MAVAZI
- ICT Information and communications technology
- Kambi ya Upinzani
- London Olympic Games 2012
- Mambo ya Zamani - Archives
- Maonyesho ya Biashara - Trade Shows
- Mara
- Mobile - Telecoms
- NHIF National Health Insurance Fund
- Peace and Security
- Rwanda
- Sayansi na Tekinolojia
- Wizara ya Elimu na Ufundi
- Wizara ya Mambo ya Ndani
- Wizara ya Uchukuzi
- Zambia
- BOT Bank of Tanzania Benki Kuu ya Tanzania
- Events - Matukio
- Habari za Majimboni
- Mahojiano - Interview
- Makala - Articles
- Malawi
- Mkoa wa Pwani
- Musoma
- NJOMBE
- National Parks - Mbuga za Wanyama
- Ruvuma
- SONGEA
- Shirika la Nyumba laTaifa - NHC
- TBL Tanzania Breweries Limited
- Taifa Stars - Timu ya Taifa
- UDAKU UMBEYA GOSIP
- US EMBASSY - UBALOZI WA MAREKANI
- University of Dar es salaam - Chuo Kikuu cha Dar es salaam
- ABG African Barrick Gold
- BAKWATA
- Banks - Benki
- Environment - Mazingira
- Ilala
- Kilimo Kwanza
- Land and Land Grabbing Issues - Ardhi
- Love Relationships - Mapenzi Mahusiano
- MIKUTANO
- Mabondia - Boxing
- Manyara
- Miradi ya Maendeleo
- Misaada - Donations
- Mombasa
- NCCR MAGEUZI
- Nairobi
- People - Watu
- Picha ya Wiki - Photo of the Week
- Precision Air
- Procurement
- Ripoti Maalumu
- SANAA - ARTS
- Sensa ya Makazi na Watu 2012
- Sheria - Law
- Somalia
- South Africa
- South Sudan - Sudani Kusini
- Takwimu - Statistics
- Tigo
- Travel - Safari
- Ugaidi - Terrorism
- Ulinzi na Usalama - Security and Defence
- Wizara ya Afrika Mashariki
- Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
- Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo
- Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknologia
- Wizara ya Viwanda na Biashara
- Zimbabwe
Blog List
Saturday, January 5, 2013
TAMKO LA JUVICUF JUU YA UTAPELI WA KUTOA GESI MTWARA
NI HAKI YA MSINGI KABISA WANANCHI WA MKOA WA MTWARA KUANDAMANA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR ES SALAAM.WAKATI HAWAJUI HATIMA YAO.
TAREHE: 05/01/2013
Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaendelea kuunga mkono harakati zinazoendelea mkoani Mtwara za kupinga mpango wa serikali wa kujenga bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka mtwara hadi dare s salaam, jumuiya ya vijana CUF taifa inaamini gesi inahamishwa kwa matakwa ya watu Fulani na sio kwa manufaa ya taifa kama inavyoelezwa na serikali, jumuiya haioni sababu ya kiuchumi ya kuhamisha gesi Mtwara kupeleka Dar es salaam au sehemu nyingine yeyote ile kwa kuzingatia yafuatayo:-
1. Uamuzi wa kuhamisha gesi sio wa kiuchumi na haukuzingatia misingi ya kiuchumi kwani kama serikali ingeamua kujenga mitambo ya kufulia gesi (Plants) mkoani Mtwara ingeokoa mabilioni ya pesa yanayotumika kusafirishia gesi asilia toka Mtwara kwenda Dar es Salaam, inasemekana bomba moja la mita tano (5) inagharimu fedha za kitanzania takribani bilioni tatu (3), hii ni hatari tujiulize umbali uliopo kati ya Mtwara na Dar nikilometa ngapi? Kwani ni zaidi ya kilometa 560 mara hiyo bilioni 3 tunazani ni pesa kiasi gani zitatumika kwa ajli ya mradi huo?kwanini wasifanye opportunity cost ya kujenga hizo plants Mtwara? ili kuokoa gharama za usafirishaji wa gesi wanasafirisha na wanaenda kujenga plants nyingine Dar hivi hatuoni Taifa linaingia gharama mara mbili?
2. Ujenzi wa vinu vya kufulia gesi asilia Mtwara utasaidia kuchochea maendeleo ya mikoa ya kusini kwa kuwahakikishia ajira vijana ambao kila siku wanapanga mikakati ya kwenda Dar kutafuta ajira na maisha bora! Lazima Taifa lifanye diversification of economy kwani hata mataifa ya Ulaya na Marekani yalifanikiwa kwa kufanya diversification of economy sio kila mradi tuupeleke Dar es Salaam, tunasababisha population na kufanya uchumi kuwa concentrated in a single area hii ni hatari kwa mipango ya muda mrefu ya taifa hili.
3. Kujengwa kwa mitambo hiyo katika mikoa ya kusini itasaidia kuchochea maendeleo ya miundo mbinu mbalimbali kama barabara, bandari, na reli kwa lazima serikali itajenga miundo mbinu imara kwa ajili ya kusafirisha gesi iliyo tayari kwa kutumiwa na watumiaji mbalimbli kutoka mikoa tofauti tofauti, Taifa linahitaji mawazo yakinifu ya kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini hasa wanaotoka mikoa ya kusini.
Jumuiya ya vijana inashangazwa na kauli tata inayotolewa na viongozi wa Serikali ya CCM kwani ikumbukwe kuwa tarehe 25/07/2011 kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa Rais Kikwete aliwahutubia wananchi wa Mtwara na kuwahakikishia kuwa katika utawala wake atainua mikoa ya kusini kiviwanda na kumtaka Meya wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani kutenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji, wananchi wanahoji utawala wake unaelekea ukingoni hauna hata dalili ya kiwanda kimoja badala yake kunazoezi la kutaka kuhamisha gesi hiyo na kupelekwa Dar es Salaam, je hivi kweli Rais Kikwete na CCM yake wana mapenzi ya dhati na watu wa kusini?
Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaendelea kushangazwa na taarifa ya Waziri wa nishati na madini Mheshimwa Sospeter Muhongo kwa kudai kuwa eti asilimia kumi na nne (14%)tu ya gesi iliyogunduliwa ndiyo inatoka Mtwara, kwanini sasa wasipeleke mradi huo wa bomba la kusafirishia gesi sehemu nyingine badala ya Mtwara? Jumuiya inasisitiza kuwa wanamtwara hawapingi gawio la pato linalotokana na gesi kutumika sehemu nyingine yeyote ya nchi, kwani ikumbukwe kuwa hata kwenye ushuru wa zao la korosho ambalo limekuwa zao la pili kuingizia ushuru wa Taifa mwaka jana wananchi hawajahoji lolote juu gawio la ushuru huo?
Kwa hiyo Jumuiya ya vijana CUF Taifa inashangazwa na kauli ya viongozi wa CCM ya kusema kuwa wanamtwara wanahitaji gesi iwanufaishe wao wakati ukweli ukijulikana kuwa kilio cha wanamtwara nikutaka uwekezwaji unaotokana na gesi ufanywe Mtwara na Lindi kama ilivyofanywa kwenye viwanda vya sukari, kwani miwa inalimwa Tuliani, Mtibwa, na Kilombero – Morogoro na viwanda viko huko kwa nini gesi iwe Mtwara plant iwekwe Dar es Salaam?
Kwa hiyo Jumuiya ya vijana CUF Taifa inaunga mkono gesi kutosafirishwa kupelekwa Dar es Salaam.
Imetolewa na,
Jumuiya ya Vijana CUF Taifa,
Monday, November 19, 2012
ZIARA YA VIONGOZI WA CUF MKOANI KIGOMA
Monday, November 12, 2012
Maalim Seif alipohutubia K/Maiti
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2C02dZCWL
Friday, October 19, 2012
Chama cha Wananchi chasikitishwa na vurugu Zanzibar
Haki sawa kwa Wote
………………………..
Salim Biman
Kaimu Naibu katibu Mkuu Zanzibar
Thursday, September 6, 2012
UZINDUZI WA KAMPENI WA CUF JIMBO LA BUBUBU
Sunday, July 29, 2012
TAARIFA YA JUVICUF KWA VYOMBO VYA HABARI KUFUATIA KUJIUZULU MHESHIWA HAMAD MASOUD
JUVICUF – JUMYIYA YA VIJANA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
PONGEZI ZA JUVICUF KWA WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO KWA UWAMUZI WAKE MAKINI WA KUWAJIBIKA KISIASA
JUVICUF inatoa pongezi za dhati kwa Mhe Hamad Masoud kwa uwamuzi wake wa kujiuzulu ili kuonyesha spirit ya dhati ya kuwajibika kisiasa.
Tunaamini alikuwa mmoja wa mawaziri waliofanya makubwa ili kuleta mabadiliko katika sekta ya mawasiliano na miundombinu Zanzibar. Tulikuwa tunamshuhudia alivyokua Mbioni Ulaya kutafuta misaada kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa Barabara na vitega uchumi vya Bandari na viwanja vya ndege. Uwanja wa ndege wa Zanzibar hapo awali ulikua ni vurugu tupu hujui nani aningia na nani anatoka au nini kinaingia na nini kinatoka. Tunafahamu alikabidhiwa uoza uliokuwemo katika wizara hiyo iliyojaa Ubinafsi, rushwa, upendeleo na Ubadhirifu. Hata hivyo hakujali alijikaza na kufanya mabadiliko makubwa. Huu Ndio uungwana na uwajibikaji, vijana wa CUF na Wazanzibari wote tutakua nae akiwa ndani ya Serikali au Nje na daima tutazithamini jitihada zake.
Kujiuzulu kwa Mheshimiwa Hamad Masoud ni ishara tosha kwamba viongozi wa CUF si waroho wa madaraka bali wapo kuwatumikia watu. Hii ni heshma kubwa kwa chama chetu na picha kamili ya kuwaonyesha wazanzibari na watanzania kwamba CUF haipo serikalini kwa ajili ya kupata vyeo bali kuwatumukia wananchi.
Kutokana na dosari kadhaa wa kadhaa zifuatazo zilizofungamana na maafa haya tunawashauri viongozi wengine wa kisiasa waliohusika wajiuzulu kama alivyofanya mwenzao ili na wao kuonyesha dhati yao ya kuwajibika kisiasa.
1. Vikosi vya ulinzi vilikosa kutimiza wajibu wao kwa wakati. Kwa mfano kikosi cha KMKM kilifika katika eneo la tukio saa 12 jioni wakati kikosi cha wanamaji cha JWTZ kilifika katika eneo la tukio siku ya pili yake. Kwa kuwa ajali ilitokea kiasi cha saa 7.30 mchana, Jambo hili limepelekea watu wengi kukosa msaada wa kuokolewa.
2. Kikosi cha Wanamaji cha JWTZ kilipaswa kuwa na jukumu la uokozi wa meli hiyo lakini hata hivyo halikufanyika mapema kutokana na kutokuwepo na kikosi imara cha dharura (standby unit) pamoja na kukosa vifaa vya kutosha vya uokozi kama vile rubber boats na fibre boats. Badala yake vifaa hivi vilifika katika eneo la tukio na kuanza kutumika siku ya pili yake wakati watu tayari wameshafariki.
3. Pamoja na Tume ya Maafa na Mwenyekiti wake kufika katika eneo la tukio haikuweza kutoa msaada wa kutosha kutokana na kuwa haikuwa na wataalamu wa masuala ya maafa. Wengi wa waokoaji waliofika walikuwa ni raia wa kawaida. Aidha katika zoezi hilo hakukuwa na Kikosi cha Uokozi na kamanda wake jambo ambalo lilikuwa dosari kubwa na kusababisha zoezi hilo kukosa muongozo.
Kwa kuwa dosari hizo ziliongeza ukali wa tatizo tunamshauri sana Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais, Mheshimiwa Mohd Aboud ambaye anasimamia masuala ya maafa ajiuzulu kwa kushindwa kufanikisha zoezi la uokozi kwa wakati na kwa ufanisi pamoja na kwamba miezi kumi tu iliyopita kitengo hicho cha maafa kilipata funzo na msaada mkubwa wa kifedha kufuatia kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander.
HAKI SAWA KWA WOTE
Khalifa Abdalla Ali
Katibu wa Jumuiya ya Vijana CUF – Taifa
TAARIFA YA MWENYEKITI KWA VYOMBO VYA HABARI KUFUATIA AJALI YA KUZAMA MV SKAGIT
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT YA KAMPUNI YA SEAGUL NA MAAFA YA ABIRIA WALIOZAMA NA KUFAMAJI ILIYOTOKEA TEREHE 18/08/2012
1. CUF – Chama cha Wananchi tumepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa sana taarifa ya kuzama kwa meli Mv. Skagit iliyotokea Jumatano mchana, Julai 18, 2012 katika bahari ya Hindi, ambapo inahofiwa watu zaidi ya 100 wamefariki. Kwa niaba ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, Wanachama na wapenzi wa CUF, na kwa kweli kwa Watanzania kwa ujumla tunatoa pole kwa familia, ndugu, marafiki wa wafiwa, Wazanzibari na Watanzania wote kwa msiba wa kitaifa uliotokea kabla hata mwaka mmoja haujapita baada ya meli ya Mv. Spice Islander kuzama katika mkondo wa Nungwi Septemba 10, 2011 na watu zaidi ya 200 kupoteza maisha.
2. Mnamo tarehe 18/07/2012 kiasi cha saa 5:00 asubuhi meli ya Mv. Skagit inayomilikiwa na kampuni ya SEAGUL iliyosajiliwa Zanzibar iliondoka Dar es Salaam ikiwa na kiasi cha abiria 290 wakiwemo watoto wadogo wanaofika 40. Mpaka tunaandika taarifa hii idadi ya abiria waliookolewa imeripotiwa kufikia 145 na maiti waliopatikana ni 68.
3. Wakati meli hiyo inaondoka Dar es Salaam, hali ya hewa haikuwa nzuri sana. Hata hivyo iliendelea na safari na ilipofika eneo la Chumbe umbali wa nautical miles 3 kutoka katika kisiwa cha Chumbe meli hiyo ilipigwa na dhoruba kali jambo lililosababisha ilale ubavu kwa muda mfupi sana na baadae kugeuka kabisa juu chini, chini juu. Hali hii ilisababishwa na mawimbi makubwa yaliyosababishwa na upepo mkali.
4. Taarifa za vyombo vya habari vinaeleza Meli ya Mv. Skagit ilitengenezwa mwaka 1989 na kufanya kazi Seattle, Jimbo la Washington, Marekani. Iliachishwa kufanya kazi mwaka 2006. Hatimaye kuuzwa na kuletwa Tanzania. Inasemekana ilifanyiwa marekebisho Mombasa na kuongezwa urefu. Kuongeza urefu kuliifanya isiwe thabiti (stable) hasa abiria na mizigo ikiwa juu. Ilianza kufanya kazi Oktoba 2011. Kuna taarifa kuwa ilikuwa inayumba sana wakati wa safari ya kutoka Unguja kwenda Pemba na ilisimamishwa kufanya safari hizo.
5. Taarifa ya kupoteza muelekeo na kuzama meli hiyo iliripotiwa kwa Control Tower, Zanzibar na Dar es Salaam kabla ya meli hiyo kuzama. Aidha nahodha wa meli hiyo aliomba msaada kutoka kwa Control Tower pamoja na Harbour Master. Hata hivyo msaada wa uokozi ulishindikana kwenda kwa haraka kutokana na vyombo vilivyokuwepo bandarini kukosa mafuta.
6. Zoezi la uokozi lilikuwa gumu sana kutokana na sababu zifuatazo kwa sababu ya hali mbaya ya bahari na upepo mkali ilisababisha zoezi la uokozi kuwa gumu sana. Waokozi hawakuwa na taaluma ya uokozi kwani wengi wao walikuwa ni raia wa kawaida na vyombo vilivyotumika katika zoezi la uokozi vilikuwa ni vya kiraia ambavyo havikuwa na uwezo mzuri wa kuokoa. Na kwa sababu hiyo waokoaji walishindwa kuifikia na kuifunga mipira meli hiyo ili kuizuia isiendelee kuzama.
7. Pamoja na Tume ya Maafa na Mwenyekiti wake kufika katika eneo la tukio haikuweza kutoa msaada wa kutosha kutokana na kuwa haikuwa na wataalamu wa masuala ya maafa. Aidha katika zoezi hilo hakukuwa na Kikosi cha Uokozi na kamanda wake jambo ambalo lilikuwa dosari kubwa na kusababisha zoezi hilo kukosa muongozo.
8. Vikosi vya ulinzi vilikosa kutimiza wajibu wao kwa wakati. Kwa mfano kikosi cha KMKM kilifika katika eneo la tukio saa 12 jioni wakati kikosi cha wanamaji cha JWTZ kilifika katika eneo la tukio siku ya pili yake. Jambo hili limepelekea watu wengi kukosa msaada wa kuokolewa.
9. Kikosi cha Wanamaji cha JWTZ kilipaswa kuwa na jukumu la uokozi wa meli hiyo lakini hata hivyo halikufanyika mapema kutokana na kutokuwepo na kikosi imara cha dharura (standby unit) pamoja na kukosa vifaa vya kutosha vya uokozi kama vile rubber boats na fibre boats. Badala yake vifaa hivi vilifika katika eneo la tukio na kuanza kutumika siku ya pili yake wakati watu tayari wameshafariki.
10. Tatizo la kushindikana kuizuia meli isiendelee kuzama na hivyo kukosekana kuokolewa abiria lilitokana na uwezo mdogo wa uokozi waliokuwa nao waokozi waliofika katika eneo la tukio. Tuna vikosi vya baharini alau vitatu:- Kikosi cha Wanamaji cha JWTZ (Navy), Jeshi la Polisi la Wanamaji (Marine Police) na KMKM vyote havikufika mapema na kuwa na uwezo wa kuokoa abiria.
11. Kukosekana kwa mawasiliano baina ya Chombo kinachosimamia hali hewa na Chombo kinachosimamia usafirishaji, kwa ajili ya kupeana tahadhari itakayopelekea ikibidi vyombo kuzuiwa kutosafiri kwa siku husika visimamishwe, hususani vyombo vyenye uwezo mdogo wa kukabiliana na misukosuko ya mchafuko wa bahari.
12. Tuna wasiwasi na uwezo wa manahodha na mabaharia katika kujua uwezo wa chombo chao kama kinaweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa siku husika, na pengine hata SUMATRA na Wakala wa Meli Zanzibar (ZMA) haina sifa sahihi za manahodha na mabaharia hawa, na pia hakuna uhakiki ikiwemo kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa usalama wa chombo na abiria.
13. Nchi yetu ina mapungufu makubwa sana katika Kitengo cha Taifa cha Uokoaji, hawana vituo vya uhakika vya ukoaji, hawana zana na vyombo vya kisasa vinavyokwenda na wakati, lakini pia hawapati mafunzo sitahiki yanayokwenda na wakati katika uokoaji, kiasi ya kutegemea kuomba msaada wa uokoaji na zana kutoka Afrika Kusini pindi maafa yatokeapo, kama ilivyotokea wakati wa kuzama meli ya Mv. Bukoba Mei 21, 1996 katika ziwa Viktoria na meli ya Mv. Spice Islander katika mkondo wa Nungwi Septemba 10, 2012
14. CUF – Chama cha Wananchi tunaitaka Serikali iangalie upya uwajibikaji, utendaji na mwenendo wa SUMATRA, kwani imeshindwa kuwajibika ipasavyo. Kuwepo na chombo cha uhakika cha kusimamia usalama wa usafirishaji, kwa kuhakisha vyombo vinavyopasishwa kwa usafirishaji vinauwezo wa kukabiliana na machafuko ya hali ya hewa. Kuhakikisha vyombo vyote vinabeba abiria na mizigo kulingana na uwezo wa ujazo wa chombo husika.
15. Ni muhimu kuhakikisha kunakuwepo na mawasiliano kati ya Kituo cha Hali ya Hewa na Chombo cha kusimamia usafirishaji ili kuwepo na TAHADHARI pindi itokeapo mabadiliko ya hali ya hewa yanayoweza kuleta na kusababisha maafa kama ambavyo inavyofanyika kwa usafirishaji wa anga.
16. Vyombo vya Uokoaji vipewe mafunzo ya kisasa na vyombo/zana za kisasa za uokoaji zinazokwenda na wakati. Ili kujipanga kwa ajili ya kukabiliana na ajali hapo baadae, tunapendekeza serikali iunde kikosi maalum cha uokozi. Aidha kuwepo kwa Kamanda wa pamoja atakayesimamia na kuratibu vikosi vyote vitakavyoshiriki vikiongozwa na wataalamu wa maafa na uokozi. Kadhalika pawepo na vyombo maalum vya uokozi ambavyo wakati wote vitakuwa standby na viwe na mafuta ya dharura ya kutosha ili kurahisisha zoezi la uokozi kwa ajali nyingine.
17. Ni vyema serikali ikawa na meli za usafiri imara na za uhakika kama ilivyokuwa kwa Mv. Mapinduzi na Mv. Maendeleo. Meli za serikali ziendeshwe kibiashara ili zisiwe na gharama kwenye bajeti ya serikali na faida itumiwe kununua meli nyingine.
18. Baada ya ajali ya MV. Spice Islander Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaahidi Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla yaliyotokea katika ajali hiyo hayatarudiwa. Mpaka sasa serikali haijajipanga kuwa na utaratibu unaoeleweka wa uokoaji ajali ikitokea. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambayo ndiyo inayoratibu masuala ya maafa na uokoaji inapaswa kuwajibika.
19. Mwisho tunarudia kutoa rambirambi kwa ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu zao katika maafa haya, CUF tunaungana nao katika kipindi hiki kizito cha majonzi na kuwataka wawe na subira na watambue kuwa msiba huu ni wetu sote, na kila mmoja wetu ameguswa sana na tunawapa pole wale walionusurika pamoja na kuwatakia afueni njema ili warudi tuungane nao katika harakati za maisha na kulijenga Taifa letu, lakini pia Tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi AMIN!!!!!
HAKI SAWA KWA WOTE
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti Taifa
Tuesday, July 17, 2012
MAAMUZI YA BARAZA KUU CUF YATANGAZWA.JUMUIYA YA VIJANA YAFUMULIWA YASUKWA UPYA
MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UONGOZI
LA TAIFA KILICHOFANYIKA SHABAN HAMISS MLOO
MJINI DAR ES SALAAM TAREHE 14-15 Julai, 2012.
Yametangazwa leo tarehe 17/07/2012,Ofisi za CUF Buguruni mbele ya waandishi wa habari.
Baraza Kuu la Uongozi Taifa la The Civic United Front (CUF- Chama Cha Wananchi) limekutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kikao ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Prof Ibrahim Lipumba na kufanyika katika Ukumbi wa Shabani Hamisi Mloo , Dar es salaam, Tarehe 14-15 Julai, 2012. Katika kikao hicho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limepokea, limejadili na kuzifanyia maamuzi Agenda mbalimbali zilizowasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ikiwa ni pamoja na;
- 1. Utekelezaji wa Kazi za Chama kipindi cha Oktoba 2011-juni 2012
- 2. Maandalizi ya Uchaguzi mdogo Jimbo la Bububu
- 3. Msimamo wa Chama katika mchakato wa Maoni ya Wananchi kuhusu uandikaji wa Katiba mpya ya Tanzania.
- Uimarishaji wa Chama kupitia Jumuiya ya Vijana.
- Hali ya Kisiasa Nchini.
Baada ya Mjadala wa kina kuhusiana na agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:
Utekelezaji wa Kazi za Chama kipindi cha Oktoba 2011-juni 2012
- Baraza Kuu limepokea Taarifa ya Kazi za Chama kwa kipindi cha Oktoba 2011 hadi 2012. Baraza limeipongeza Kamati ya Utendaji kwa Kazi ilizofanya na kusimamia kwa kipindi pamoja na changamoto za kiutendaji zinazowakabili. Baraza Kuu limetoa msisitizo kwa Chama kuendelea kujipanga .
Kuhusu Maandalizi ya Uchaguzi Bububu
- Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeridhia lengo la Chama kushiriki katika Uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Bububu na kuhakikisha chama kinashinda kwa sababu jimbo hilo ni ngome kubwa ya CHAMA na hasa baada ya kutathmini matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Kuhusu uimarishaji wa Chama kupitia Jumuiya ya Vijana
- Baada ya kazi kubwa iliyofanywa na jumuiya za chama na kuonekana kuwa zinapaswa kuimarishwa zaidi, hususani jumuiya ya vijana taifa (JUVICUF), Baraza Kuu limejadili na kukubaliana kufanya mabadiliko katika nafasi mbali mbali za Uongozi ndani ya Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilisha baadhi ya wajumbe waliokuwepo awali. Viongozi walioteuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ni hawa wafuatao:-
S/N | JINA | NAFASI |
1 | Katani A.Katani | M/kiti |
2 | Yusuph K. Makame | M/Mwenyekiti |
3 | Khalifa A. Ali | Katibu |
4 | Thomas D.C. Malima | Naibu Katibu |
5 | Sonia Magongo | Mjumbe |
6 | Bonifasia Mapunda | Mjumbe |
7 | Kuruthumu Mchuchuli | Mjumbe |
8 | Said Maulid | Mjumbe |
9 | Ashura Mustapha | Mjumbe |
10 | Hamidu Bobali | Mjumbe |
11 | Ahmed Mudhihir | Mjumbe |
12 | Shomvi R Issa | Mjumbe |
13 | Faustin Khalfan | Mjumbe |
14 | Suleiman S. Abdallah | Mjumbe |
15 | Biubwa M. Mselem | Mjumbe |
14 | Pavu J. Abdallah | Mjumbe |
15 | Gora J. Hamis | Mjumbe |
16 | Hafidh A. Hafidh | Mjumbe |
17 | Ayoub Y. Khamis | Mjumbe |
Kuhusu mgomo wa madaktari nchini;
- Baraza kuu limesikitishwa na mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini kwa zaidi ya miezi saba sasa bila Serikali ya CCM kuwa na mkakati wenye malengo ya kuondoa tatizo lililopo. Kuendelea kwa mgomo huo kumesababisha kusuasua kwa huduma za Afya kunakowasababishia mateso makubwa wananchi wa tabaka la hali ya chini na wengine kufa kwa kukosa tiba katika kipindi muafaka.
- Baraza Kuu linawasihi Madaktari wote warejee kazini ili kuokoa maisha ya Watanzania wenzao wasio na uwezo wa kwenda kutibiwa hospitali zinazotoa pesa nyingi, sambamba na hilo tunaiomba Serikali iwaombe Madaktari wote waliosaini kuacha kazi warejee kazini.
- Kuendelea kuwafukuza na kuwatishia si kutatua tatizo hili kwa sababu limekuwepo muda mrefu na madaktari wana madai ya msingi ya kuboresha mazingira ya kazi na huduma kwa wananchi pamoja na mishahara yao, madai haya yasidharauliwe kwa sababu yana mantiki kubwa japokuwa hayapaswi kutumiwa kupoteza roho za watu kwenye mgomo. Tunaitaka Serikali ya CCM ihakikishe inatekeleza madai yote ya msingi yanayolalamikiwa na Madaktari, pia kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za Afya.
- Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limelaani kitendo cha kutekwa, kuteswa na kuhujumiwa kwa kiongozi wa madaktari ndugu. Ulimboka , Baraza Kuu linaitaka serikali iunde tume huru ya wataalam na isiyohusisha usalama wa taifa wala Jeshi la polisi ili suala hili lichunguzwe na matokeo ya uchunguzi yawekwe hadharani.
- Mgomo wa madaktari umechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari haidhuru ni sehemu ndogo ya huduma za afya. Watanzania wachache sana wanaopata fursa ya kuonana na daktari. Wengi wanategemea huduma za zahanati na vituo vya afya ambavyo vina hali mbaya sana. Hakuna huduma ya afya ya msingi ya kukidhi mahitaji ya wananchi. Maeneo mengi ya nchi yana theluthi moja tu au chini ya hapo ya mahitaji yao. Tanzania haina wahudumu wa afya wa kutosha. Shirika la Afya la Dunia linakadiria kuwa Tanzania inahitaji wafanyakazi wa sekta ya afya wasiopungua 92000 wakati wafanyakazi wote waliopo ni 25400. Sera ya serikali ni kuwa na wafanyakazi 140,500 ifikapo mwaka 2019. Vyuo vyote vya afya vinafundisha wafanyakazi 4000 kwa mwaka. Kwa sababu ya mazingira mabovu ya kufanyia kazi asilimia 30 ya wahitimu wote (wafanyakazi 1200) wa sekta ya afya wanaacha kazi mwaka wa kwanza baada ya kuhitimu. Zahanati, Vituo vya afya na hospitali nyingi hazina wafanyakazi wenye ujuzi na ari ya kutoa huduma.
- Uchambuzi wa mgawanyo wa matumizi halisi ya serikali kisekta yanaonyesha kuwa miaka yote sekta ya afya inatengewa chini ya asilimia 10 ya matumizi yote ya serikali na hakuna dalili ya jitihada zozote za kutenga asilimia 15 ya matumizi ya serikali katika sekta ya afya kama ilivyokusudiwa na sera ya afya ya 2007. Mgao wa matumizi ya serikali katika sekta ya afya umepungua toka asilimia 8.2 mwaka 2008/09 na kufikia asilimia 5.4 mwaka 2010/11.
- Watanzania wengi bado wanaathirika na maradhi mengi yanayoweza kuzuiliwa kwa gharama ndogo. Vipaumbele vya matumizi ya fedha za serikali viwe katika kinga na tiba ya maradhi ya kuambukiza na kuhakikisha watoto wote wanapata lishe bora. Maradhi yanayohusiana na kupumua, malaria, kuharisha na ukosefu wa lishe bora ndiyo chanzo cha vifo vingi vya watoto. Maradhi haya yanaweza kuzuwiwa kwa gharama ya wastani. Matumizi makubwa ya serikali yanatengwa kuwatibu watu wachache. Gharama kubwa inatumiwa kuwapeleka wagonjwa wachache hasa viongozi nje ya nchi.
Kuhusu suala la Bajeti ya Mwaka 2012-2013
- Baraza Kuu limebaini kuwa malengo ya bajeti ya 2011/12 hayakufikiwa. Katika hotuba ya bajeti ya juni 2011, ilieleza kuwa “Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wananchi katika kupambana na makali ya maisha. Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, pamoja na mambo mengine, inalenga katika kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo.” Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa wakati waziri wa fedha anasoma hotuba ya bajeti, mfumko wa bei Juni 2011 ulikuwa asilimia 10.9. Mfumko wa bei uliongezeka na kufikia asilimia 20 mwisho wa mwaka 2011 na umepungua kidogo sana na kuwa asilimia 18.2 mwezi Mei 2012.
- Mfumko wa bei wa vyakula ni wa juu zaidi. Takwimu za serikali zinaonyesha mfumko wa bei uliongezeka toka asilimia 12 mwezi Juni 2011 mpaka kufikia asilimia 26 mwezi desemba 2011 na Mei 2012 ulikuwa asilimia 24.5. Mfumko wa bei ni matokeo ya matumizi makubwa ya serikali yasiyokuwa na tija. Sekta ya kilimo haijatengewa fedha za kutosha kwa madhumuni ya kuongeza tija na uzalishaji wa chakula na mazao mengine ya kilimo. Mgao wa matumizi ya serikali kisekta unaonyesha kuwa sekta ya kilimo ilitengewa asilimia 2.92 mwaka wa fedha 2010/11 na asilimia 1.65 mwaka 2011/12. Taarifa za hali ya uchumi wa taifa zinaonyesha kuwa, kwa muda wa zaidi ya miaka 20 iliyopita, sekta ya Kilimo, misitu na uvuvi kwa pamoja imekuwa inatengewa chini ya asilimia 5 ya matumizi yote ya serikali. Makubaliano ya nchi za SADC ni kutenga alau asilimia 10 ya matumizi ya serikali kwenye kilimo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uzalishaji wa mazao ya chakula na kupunguza umaskini uliokithiri vijijini. Sekta ya kilimo imekua kwa asilimia 3.6 wakati ongezeko la watu linakadiriwa kuwa asilimia 2.9. Nafasi muhimu ya serikali katika kuleta mapinduzi ya kilimo ni katika maeneo ya utafiti wa mbegu bora, mbolea inayofaa kwa mazao katika maeneo mbali na madawa ya kuua wadudu, huduma za ugani na elimu kwa wakulima, miundombinu ya umwagiliaji maji na usafiri.
- Kilimo kipo hoi na bei ya bidhaa za wakulima ikiwemo korosho haiwasaidii wakulima na bado wanaendelea kukopwa kwa utaratibu wa ‘stakabadhi gharani.’ Bei ya pamba imepungua toka shilingi 1100 kwa kilo msimu uliopita na sasa ni shilingi 660/ kwa kilo msimu huu.
- Katika mwaka 2011/12 Serikali ililenga kukusanya asilimia 17.2 ya pato la taifa kuwa mapato ya serikali. Imefanikiwa kukusanya asilimia 16.9. Ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na mapato yasiyokuwa ya kodi ndiyo hayakufikia kiwango kwa asilimia kubwa. Serikali inalenga kukusanya asilimia 18 ya pato la taifa kama mapato yake. Inakadiriwa kuwa misamaha ya kodi ni asilimia 2.5 ya pato la taifa. Ukwepaji wa kulipa kodi ni asilimia 2-3 za pato la taifa. Sekta ya madini haichaingii ipasavyo katika mapato ya serikali. Serikali makini inaweza kukusanya asilimia 22-25 ya pato la taifa kuwa mapato ya serikali.
- Sera za kukusanya mapato zimejikita katika kodi za vinywaji na sigara. Sentensi moja inaniudhi kuisikia katika bajeti kila mwaka nayo ni “Ushuru wa “Cigar” unabaki kuwa asilimia 30.” Hivi cigar ngapi zinazovutwa Tanzania mpaka zistahiki kuwa ndani ya hotuba ya bajeti kila mwaka! Bajeti haizungumzii kabisa hatua zinazochukuliwa kuhakikisha sekta ya madini inachangia vya kutosha mapato ya serikali.
- Katika kukabiliana na upungufu wa umeme serikali iliahidi kuchukua “hatua kadhaa za kukabiliana na upungufu huu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100 Dar es Salaam na ule wa megawati 60 Mwanza.” Katika bajeti ya mwaka huu bado inaeleza “Serikali ilisaini Mkataba wa mkopo wa Euro milioni 61 na Benki ya HSBC. Mkopo huu umeelekezwa kugharamia ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawati 60 Nyakato Mwanza.” Bajeti tano mfululizo zimekuwa zinaeleza utekelezaji wa mradi huu. Mpaka sasa haujakamilika. Fedha zinazotengwa kila mwaka kukamilisha ufuaji wa umeme, Nyakato Mwanza zinakwenda wapi? Hali ya umeme bado ni tatizo kubwa nchini mbali na mwaka 2008 kutengwa 1.7 trilioni kama mfuko wa kichocheo cha kufufua uchumi (stimulus package) utekelezaji wake hauelezwi uliyeyukia wapi na fedha hizo zilizotengwa zimekwenda wapi! Serikali ya CCM, imeshindwa kutatua tatizo hili na kuisababishia nchi kupata hasara kubwa kwa kudhoofisha uchumi wa nchi. Hali hiyo imezorotesha uzalishaji viwandani na bidhaa zimepanda bei na kusababisha ukali wa maisha kwa watanzania, huduma za mahospitalini, katika sekta ya elimu, upatikanaji wa maji, KUPOROMOKA KWA SHILINGI na mengi mengineyo. CUF tunaamini bila ya umeme wa uhakika nchi haiwezi kupata maendeleo.
- Serikali pia iliahidi kuweka mazingira mazuri ya kuongezeka kwa ajira. Mpaka sasa tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa mno na halielekei kutatuliwa. Katika nchi yenye nguvukazi ya zaidi ya watu milioni 22, walioajiriwa katika sekta rasmi ya viwanda ni watu 115000 tu.
- Tatizo kubwa la bajeti yetu ni kuwa matumizi ya serikali hayatekelezi bajeti ya maendeleo iliyopitishwa na bunge. Matumizi ya miradi ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2011/12 yatakuwa chini kwa shilingi bilioni 600 ukilinganisha na bajeti iliyopitishwa na Bunge. Baadhi ya sekta, matumizi halisi ya maendeleo ni chini ya asilimia 50 ya fedha zilizoidhinishwa.
- Bajeti ya Maendeleo ya 2012/13 ni ndogo. Matumizi yote ya serikali yameongezeka toka shilingi trilioni 13.1 na kufikia shilingi trilioni 15.1 bajeti ya maendeleo imepunguzwa toka shilingi trilioni 4.9 mwaka 2011/12 na kufikia shilingi trilioni 4.5 mwaka 2012/13. Bajeti ya Maendeleo mwaka 2011/12 ilikuwa asilimia 36.4 ya matumizi yote ya serikali. Matumizi halisi ya bajeti ya maendeleo katika mwaka 2011/12 yatakuwa asilimia 33.3. Mwaka 2012/13 Bajeti ya Maendeleo ni asilimia 30 ya bajeti yote. Matumizi ya kawaida yameongezwa kwa asilimia 23.2 na bajeti ya maendeleo imepunguzwa kwa asilimia 8.1. Ukizingatia mfumko wa bei matumizi halisi ya bajeti ya maendeleo yatapungua mwaka 2012/13 ukilinganisha na mwaka 2011/12. Ili kuweka msukumo katika ukuaji wa uchumi bajeti ya maendeleo iwe alau asilimia 40.
- Matumizi ya kawaida yanakua kwa kasi kubwa kwa sababu ya kuongeza gharama za utawala kama vile kuanzisha wilaya na mikoa mipya, safari nyingi za nje za Rais na viongozi wengine wa serikali, ukubwa wa Baraza la Mawaziri, posho za semina na makongamano. Hatua za maksudi zinahitajiwa kuchukuliwa kubana matumizi ya utawala.
- Baraza kuu limeshtushwa na hali ya MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA kama ilivyoainishwa na taarifa iliotolewa na Msimamizi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Serikali Kuu, halmashauri mbalimbali nchini na mashirika ya umma, mabilioni ya shilingi ya fedha za walipa kodi wanyonge wa Tanzania zimetafunwa na watendaji wachache bila hatua stahiki kuchukuliwa dhidi yao. Baraza Kuu linaitaka Serikali ya CCM na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuchukua hatua za kuwakamata wahusika wote waliotajwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Matumizi ya Rasilimali za mafuta, gesi, madini
- Kuhusu matumizi ya Rasilimali za mafuta, gesi, madini ya uranium na madini mengine nchini, Baraza kuu linaitaka serikali kuweka utaratibu mzuri wa mchakato wa matumizi ya rasilimali hizi ili ziweze kuwanufaisha watanzania wenyewe kwani uzoefu inaonyesha kuwa nchi nyingi dunia zimeingia katika matatizo makubwa kutokana na ufisadi mkubwa wa watu wachache waliohodhi rasilimali hizo kwa maslahi yao.
- Baraza Kuu la linatoa wito kwa Watanzania wote, pale Tume ya Kukusanya Maoni itapopita kwenye Wilaya zao, kutoa Maoni juu ya sehemu ya Mapato yanayopatikana toka kwenye mauzo ya Mali ya Asili kama vile gesi, dhahabu na madini mengine yagawiwe kwa Wananchi moja kwa moja ili yaweze kupunguza makali ya maisha na kuleta ulinzi shirikishi wa Rasilimali za Nchi na mali ya Asili ya Nchi yetu katika kukuza na kuimarisha dhana ya Utawala Bora.
Mpasuko wa kisiasa ndani ya serikali ya CCM
- Kuhusu mpasuko wa kisiasa ndani ya serikali ya CCM unaathiri na kuiyumbisha nchi na ustawi wa maisha ya watanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na makundi makubwa ya nani awe mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015. Jukumu la msingi la chama kinachounda serikali inayounda kufahamu kuwa nchi yetu inahitaji mabadiliko. Baraza Kuu linatoa wito kwa Watanzania kuzinduka na kufahamu kuwa nchi yetu inahitaji mabadiliko. CUF na viongozi wake wako tayari kuwaongoza Watanzania kuelekea katika mabadiliko wanayoyataka. CCM imeshindwa kuiongoza Tanzania. Na tujiandae kuishughulikia kikamilifu mwaka 2014/15 ili CUF iweze kuunda serikali makini itakayoweza kuweka mipango thabiti ya kiuchumi na maendeleo ya Taifa yetu.
Kuhusu suala la Vitambulisho vya Mnzanzibar Mkaazi ZAIN ID
- Baraza Kuu la Uongozi Taifa linaipongeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar juu ya maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Wawakilishi kuhusu kushghulikia suala la Vitambulisho vya mzanzibari mkaazi ZAN-ID. Baraza Kuu linawaomba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuona haja ya kutatua tatizo hili la Vitambulisho vya Mzanzibar Mkazi ili kuendeleza Ummoja uliopatikana kwa siku za Karibuni.
Kuhusu suala la Sensa
- Baraza kuu linaitaka serikali kudhibiti utoaji wa Takwimu ili kuepusha migongano isiyo ya lazima ndani ya Nchi. Baraza kuu linaona kuwa mgogoro uliopo sasa baina ya Waislamu na serikali katika suala la Sensa unatokana na serikali kutodhibiti utoaji wa takwimu za idadi ya watu kwa taasisi zisizohusika. Baraza Kuu limesikitishwa na namna serikali imelishughulikia tatizo ikiwemo vyombo vya serikali kutoa takwimu potovu na kuwa na dodoso la sensa linalohesabu nyumba za ibada bila kuhesabu waumini wa madhehebu husika. Linatoa wito kwa Rais Kikwete kukutana na viongozi wa dini zote kuwasikiliza hoja zao na kutafuta maridhiano kuhusu dodoso la dini katika sensa kwani ikiwa sehemu ya jamii itahamasishwa na kususia sensa, zoezi hili lenye gharama kubwa halitafanikiwa na nchi itakuwa na takwimu zisizo sahihi.
Msimamo wa Chama katika mchakato wa kutoa Maoni ya Wananchi kuhusu uandikaji wa Katiba Mpya ya Jamuhuri Muungano
- Baraza Kuu limewapongeza Viongozi wa Chama kwa jitihada zilizofanyika za kudai Katiba Mpya na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na kufanikiwa kuishinikiza Serikali kuanzisha mchakato wa kukusanya Maoni ya wananchi juu mabadiliko ya Katiba mpya. Sera ya CUF ni kuwa na Muungano wa Serikali tatu. Sera hiyo imezingatia ukweli kwamba muundo Mpya wa Muungano ndio unaoweza kutoa ufumbuzi wa kudumu kwa changamoto (Kero) za muda mrefu za muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili. Serikali ya Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya mambo yake kuhusu Zanzibar. Ikiwemo uamuzi wa mwisho kwa matumizi ya mali asili (Mafuta, gesi na Madini) na matumizi ya kiuchumi ya bahari.
- Baraza kuu limeona ni vizuri Serikali ya Muungano ihusike na mambo ya jumla ambayo wananchi wa Serikali mbili zinazounda Muungano watakubaliana. Hata hivyo kwa kuwa Muungano sio wa vyama na umekuwepo kabla ya kuungana kwa TANU na ASP1977, na kwa kuheshimu demokrasia ya wananchi wa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar) waliofanya Muungano uwepo mwaka 1964, CUF- Chama Cha Wananchi kinasisitiza kuwa Tume isikilize na kuyaheshimu maoni ya Wananchi na isiyachakachue.
- CUF- Chama cha Wananchi tunawahimiza wanachama na wananchi kwa ujumla wao kutoa maoni yao kwa UHURU ili kufanikisha jambo hili kwa mustakabali wa Nchi yetu. Baraza Kuu limesisitiza kusimamia na kuheshimu Sera ya Chama ya kutaka Muundo wa Serikali tatu ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwepo na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Baraza kuu linawaomba Watanzania kushiriki kutoa Maoni yatakayowezesha kuandikwa Katiba Bora ikayotujengea Tanzania Tuitakayo.
Kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi
- Baraza Kuu linaitaka Serikali kuanzisha Mchakato wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi sambamba na Mchakato wa ukusanyaji wa Maoni ya Katiba ili Uchaguzi wa 2015 uweze kufanyika chini ya Tume itayokubaliwa na Watanzania wote ili kuipa muda Tume hiyo kuweza kupitia Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kuhusu suala la Haki ya Kumiliki Ardhi
- Baraza Kuu la uongozi linatoa wito kwa serikali kuwamilikisha Watanzania ardhi yao hasa ukizingatia mchakato wa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki na wimbi la kutafuta na kupora ardhi linalofanywa na nchi zenye fedha lakini zinaagiza chakula toka nje. Katiba mpya iwape Watanzania haki ya kumiliki ardhi yao.
Mwisho;
Baraza Kuu la Uongozi Taifa linawatakia watanzania wote ushiriki mwema katika utoaji wa Maoni yatakayowezesha kupatikana kwa Katiba Mpya.
Imetolewa na
Prof.Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti CUF Taifa
HAKI SAWA KWA WOTE
Thursday, July 12, 2012
MKUTANO WA CUF WA JUMAPILI 15/7/2012 WAAHIRISHWA
MKUTANO WA JANGWANI WA JUMAPILI TAREHE 15.07.2012 UMEAHIRISHWA.
Ndugu zangu, ule mkutano uliokuwa ukisubiriwa sana na WAPENZI NA WANACHAMA wa CUF pamoja na WANANCHI KWA UJUMLA umeahirishwa.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu kati yetu, kanisa katoliki na mamlaka za ILALA tumekubaliana kuwa wakatoliki waendelee na MKUTANO WAO WA KIMATAIFA WA UPONYAJI ambao utachukua takribani MWEZ...I MZIMA.
Maombi yetu na ya wakatoliki yalifika pamoja Sasa kilichofuata ni kukubaliana na kwa sababu chama chetu hakina makuu tumekubali kuwapisha wenzetu kwa sababu itakuw vigumu wao kukatisha mkutano wao halafu waendelee tena.
Tulitizamia kupata kiwanja kingine lakini utafiti umeonesha UWANJA UNAOWEZA KUHIMILI SHUGHULI YA CUF DSM NI JANGWANI, kwa hiyo tunasubiri wenzetu wamalize kisha tutafanya.
Hivi Sasa tunaendelea na oparesheni mbalimbali na wiki ijayo tutakuwa mkoa wa morogoro kwenye baadhi ya wilaya.
Poleni kwa usumbufu wowote ambao umejitokeza.
Monday, July 2, 2012
CUF KUFANYA MKUTANO JANGWANI JULAI 15 2012
Njooni mumsikilize Mwenyekiti wa Jopo la Magwiji wa Uchumi Duniani, Full Bright Visiting Economist Profesor, The International Figure, Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.
Sambamba naye atakuwepo Gwiji la Siasa Barani Afrika, The First Vice President of The Government of National Unity of Zanzibar, Katibu Mkuu wa CUF Taifa Mhe. Maalim Seif Sharif Hamadi
Njooni msikilize Sera adhimu na maridhawa za VISION FOR CHANGE, Njooni msikilize Mustakabali wa Uchumi wetu kama Taifa na nini cha kufanya hasa katika kipindi hiki cha Mchakato wa Katiba Mpya.
Njooni msikilize ufumbuzi mbadala wa 'mazonge' yanayoendelea hapa nchini kwa sasa
Confirmation ya kufika kwa wanabidii katika mkutano huo ni muhimu kwa ajili ya ku-observe protocals.
Shime wanabidii, kwa pamoja tulijenge Taifa letu, Tanzania yenye neema inawezekana
HAKI SAWA KWA WOTE
Friday, June 8, 2012
Mazishi Ya Mwenyekiti Mstaafu Wa CUF Marehemu Musobi Mageni


Wednesday, June 6, 2012
Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Wananchi CUF Yalaani Taarifa ya UVCCM
JUMUIYA YA VIJANA - JUVICUF
Office of the Secretary General
Party Headquarters, P.O. Box 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail:cufhabari.co.uk Homepage: www.cuftz.org
Our Ref: CUF/HQ/JUVICUF/003/2012/Vol 13 Date: 06/06/2012
Jumuiya ya vijana ya Chama cha Wananchi CUF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kikao cha baraza kuu la UVCCM iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu wake Martin Shigella kuhusiana na vurugu zilizotokea Zanzibar hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoitoa amesema, serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar inahusika na vurugu hizo.
Sisi vijana wa JUVICUF tunalaani kauli hiyo kwani juhudi za kuipata serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar haikuwa kazi nyepesi jambo ambalo linajulikana na wazanzibari, watanzania na ulimwengu mzima. Serikali ya umoja wa kitaifa imepataikana kwa taabu nyingi baada ya Zanzibar kupoteza muelekeo wake, ustawi wake na roho za watu wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe Dr Ali Moh’d Shein alitoa taarifa rasmi kuhusiana na vurugu hizo. Kauli hiyo ya UVCCM ambayo imejaa shutuma dhidi ya serikali ya Dr Shein anayoiongoza, ambayo imekuja mara baada Rais wa kutoa taarifa yake rasmi kuhusiana na vurugu hizo ni ya utovu wa nidhamu wa wazi unaopaswa kulaaniwa na kukaripiwa kwani inaweza kuwa ni sawa na cheche ya moto katika nyasi kavu. Kuvurugika kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ambayo inafanya kazi zake kikatiba na kuaminiana ni kurejesha nyuma umoja na maendeleo yaliyopatikana.
JUVICUF inatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao. Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.
Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi. Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.
HAKI SAWA KWA WOTE
…………………………………….
Khalifa Abdalla Ali
KATIBU MKUU
Popular Posts
-
South Sudan Vice-President to attend Business and Security Forum The Vice-President of South Sudan, HE Dr Riek Machar, will join senior mini...
-
Tarehe 6 mwezi wa Aprili, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, aliunda Tume ya ...
-
Baraza la Madaktari Tanganyika limepokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu , Wizara y a Afya na Ustawi wa Jamii kwamba , baadhi ya Madakt...
-
RIPOTI YA TUME YA KUCHUNGUZA AJALI YA KUZAMA M. V. SPICE ISLANDER I SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI 1.1 CHIMBUKO Usiku wa kuamkia tarehe 10...
-
This statement outlines how we handle any personal information we obtain PataHabari is committed to respecting and protecting the privac...
-
1. MWENYEKITI TAIFA 1 Asila Ali SALIM 2 Jamal K. ALI 3 Lulu Mcham ABDALLAH 4 Lusekelo W. MALEMA 5 Mbarouk M. MBAROUK 6 Mwana Amina Haji FARU...
-
Usomi wa ngazi mbalimbali si sifa ya mtu kufaa kuwa kiongozi, dunia katika historia yake ina majina lukuki ya baadhi ya viongozi ambao wa...
-
YAH: UTEUZI WA KUJAZA NAFASI YA UONGOZI KATIKA WIZARA YA UCHUKUZI Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Eng. Omar A. Chambo kwa Mamlaka a...
-
Mwananchi wa Kijiji cha Jambiani akiwasilisha maoni yake kwa njia ya Barua kwa Tume. Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wak...
-
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Manchester City ya Uingereza wakichuana vikali na mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Real...