Pages

Showing posts with label Maonyesho ya Nane Nane. Show all posts
Showing posts with label Maonyesho ya Nane Nane. Show all posts

Wednesday, August 8, 2012

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue atembelea Hazina katika maonyesho ya Nanenane 2012

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kulia) akisaini kitabu cha wageni jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma kuona shughuli mbalimbali za Wizara hiyo katika maonyesho ya nanenae.Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Fedha Ramadhan Omary.
Mkuu wa kitengo cha Menejimenti ya Mikataba kutoka Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] Mordecai Matto (kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) jana mjini Dodoma juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(wa pili kulia) akisamiliana na watumishi na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM)Mchambuzi wa Mifumo ya Komputya Ibrahim Sultan (katikati) na Afisa Taalum Mwandamizi Mkiramwene Msafiri(kushoto) jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma.

Tuesday, August 7, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL ATEMBELEA MABANDA YA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI DODOMA 2012

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakiangalia Mhogo aina ya Mumba wenye umri wa miaka (3) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Wa pili (kulia) ni Mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo jinsi ya uzalishaji wa zao la Zabibu kutoka kwa Ofisa Mtafiti Msaidizi wa Kilimo wa Kanda ya Kati Dodoma, Richard Malle, (wa pili kulia) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi mashine za kukamulia miwa zinavyofanya kazi, kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi ya uandaaji hadi kukamilika kwa Sukari tayari kwa matumizi,kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Wa tatu kutoka (kushoto) ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mbegu ya mizabibu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso (kushoto) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal,(wa pili kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya matrekta ya kuvunia mazao aina ya Mahindi, Ngano na Mtama, wakati Makamu alipotembelea katika maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiteta jambo na Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima wakati Makamu alipotembelea katika maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Atembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma 2012

Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu baada ya kuwasili katika banda la Wizara katika maonyesho ya Wakulima ya Nanenane kitaifa yanayoendelea mkoani, Dodoma. Wazir Mkuu Mhe. Mizengo Pinda atembelea maonyesho ya Nyuki katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii , katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Mhe. Waziri MKuu akitoa maelezo baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu anaendesha mafunzo maalam ya ufugaji nyuki yanaqyotolewa ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mhe. Waziri MKuu akiangalia sampuli za asali kutoka kwa moja ya wadau wa bidhaa za Nyuki wanaoshiriki maonyesho ya nane nane ndani ya banda la wizara ya Maliasili na Utalii.
Mhe. Waziri Mkuu akiangalia mzinga wa nyuki wasiouma katika shamba darasa la ufugaji nyuki

Monday, August 6, 2012

MKUU MKOA WA SINGIDA ATEMBELEA WIZARA YA FEDHA KATIKA MAONYESHO YA WAKULIMA YA NANENANE MJINI DODOMA

Meneja Mawasiliano na Kumbukumbu wa Shirika Hodhi la Mali ya Mashirika ya Umma (CHC) Joseph Mapunda (kushoto) akimpa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia) leo ,jinsi Shirika hilo linavyofanya tathmini ya mashirika ya umma yaliyobinafsishwa na utendaji wa mashirika hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi jinsi Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mchambuzi wa Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya TEKNOHAMA ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia) leo mjini Dodoma jinsi kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Friday, August 3, 2012

MAONYESHO YA NANE NANI DODOMA 03/07/2012

Mtunzaji Kumbukumbu na Mhasibu Abbas Mnyeto wa Wizara ya Fedha wakiwasaidia wazee wastafu upande wa Kilimo juu ya taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wanapostaafu jana mjini Dodoma walipokuwa kwenye banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (kushoto) akiwasidia Maafisa Polisi kujua kiwango michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma.
Kaimu Afisa Uhusiano wa wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Hawa Kikeke(kushoto) na Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (wa pili kutoka kushoto) wakiwasaidia Maafisa wa Polisi juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma.
Afisa Uhusiano wa Chuo Mipango Dodoma Sarah Mmari (kushoto) akimwelimisha Yulis Otto (kulia) utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho wakati mzee huyo alioptembelea banda la Wizara ya Fedha jana katika maonyesho yanayoendelea mjini Dodoma.
Afisa Uhusiano wa Chuo Mipango Dodoma Sarah Mmari (kushoto) akimwelimisha Yulis Otto (kulia) utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho wakati mzee huyo alioptembelea banda la Wizara ya Fedha jana katika maonyesho yanayoendelea mjini Dodoma.
Afisa Masoko kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) Said Mkomwa(kulia) akiwaelimisha wananchi faida za kuwekeza katika mifuko iliyoanzishwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania jana mjini Dodoma walipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Emilia Mkubulo(kulia) akimwelimisha mmoja wa wananchi faida za kununua hisa jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Kahenga Maulid( wa pili kutoka kulia) na Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (wa pili kutoka kushoto) wakiwasaidia watumishi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Monica Kung’aro (kushoto) na Mary Kulwijila(kulia) juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma.

Naibu Waziri Wa Viwanda Na Biashara Atembelea Maonyesho Ya Nanenane Mjini Dodoma

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Gregory Teu akitoa fedha kwenye Mashine ya kutolea fedha ya CRDB ambayo imefungwa kwenye gari la kisasa aina ya Mercedese Benzi ambalo linateknolojia ya kuzuia risasi wakati alipotembelea Maonesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Gregory Teu (kushoto) akipata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa Bw. Salum Mselem ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Farmers Center na FarmBase yanayotengeneza sumu za kuulia wadudu waharibifu wa mazao na mifugo na dawa za mifugo na mazao kwa kutumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini wakati wa maonesho ya Nane Nane.
Meneja wa shamba la mifugo la Kongwa (NARCO Kongwa RANCH) Bw. Hezron Kashalankoro (aliyevaa cap) akitoa maelezo ya Kitaalamu kwa Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Gregory Teu (aliyevaa suti) juu ya uzalishaji na ufugaji wa Ng’ombe bora wa Nyama wakati alipotembelea Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma.

Popular Posts