Pages

Showing posts with label Ofisi ya Makamu wa Rais. Show all posts
Showing posts with label Ofisi ya Makamu wa Rais. Show all posts

Thursday, November 8, 2012

MAKAMU WA RAIS DK.GHARIB BILAL AMJULIA HALI KATIBU MKUU WA MUFTI WA ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI NA WATU WASIOJULIKANA SHEIKH SORAGA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI



Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (wa tatu kulia) wakati akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Katibu Mkuu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga aliyemwagiwa tindikali jana huko visiwani Zanzibar.
Makamu wa Rais na msafara wake wakitoka katika wodi aliyolazwa Sheikh Soraga.
Makamu wa Rais akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kumjulia hali Sheikh Soraga.
...Akiingia kwenye gari tayari kwa safari.
Aliyewahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Business Times, John Mapinduzi ambaye hivi sasa ni mwandishi wa habari wa Mhe. Bilal akilifuata gari tayari kuondoka eneo hilo.
Mwanausalama akihakikisha kiongozi huyo anaondoka kwa usalama hospitalini hapo.(PICHA HABARI NA HARUNI SANCHAWA GPL-
--
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amefika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam kumjulia hali Katibu Mkuu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga aliyenusurika kifo baada ya kumwagiwa tindikali jana huko visiwani Zanzibar.

Kufuatia tukio hilo, amesema kuwa kitendo alichofanyiwa Sheikh huyo ni cha kinyama na hakitavumiliwa na kwamba serikali inafanya juu chini kuwabaini waliohusika na tukio hilo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.“Hatutavumilia kitendo hicho hata kidogo kwa sababu huu siyo utamaduni wetu tuliojiwekea,” alisema Makamu wa Rais.Jana, Rais Jakaya Kikwete alifika hospitalini hapo kumjulia hali Sheikh Soraga.

Saturday, September 1, 2012

Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal Akutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Dk. Mohammad Reza Rahimi Jijini Tehran

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Dk. Mohammad Reza Rahimi, walipokutana jana mjini Tehran na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliohudhuri Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na upande wowote uliomalizika jana mjini Tehran, Iran.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Sunday, August 26, 2012

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA DR BILAL ASHIRIKI SENSA YA MAKAZI NA WATU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro, wakati ofisa huyo alipofika nyumbani kwa Makamu akiwa na Karani wa Sensa na msimamizi wake kutoka Kituo cha Oysterbay, kwa ajili ya kukamilisha zoezi la Sensa, leo asubuhi Agosti, 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi, lililoanza leo nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Karani wa Senza, Happyness Masaka, baada ya kukamilisha zoezi la kujibu maswali husika katika zoezi hilo, leo asubuhi nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msimamizi wa Sensa wa Kituo cha Oysterbay, Daria Kailembo (kushoto) ni Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Ttifa, Stanley Mahembe. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
---
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Agosti 26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makazi akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bilal, ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley Mahembe na Radegunda Maro.

Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.

Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Box 5380
Dar es Salaam.

Tuesday, August 7, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL ATEMBELEA MABANDA YA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI DODOMA 2012

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakiangalia Mhogo aina ya Mumba wenye umri wa miaka (3) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Wa pili (kulia) ni Mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo jinsi ya uzalishaji wa zao la Zabibu kutoka kwa Ofisa Mtafiti Msaidizi wa Kilimo wa Kanda ya Kati Dodoma, Richard Malle, (wa pili kulia) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi mashine za kukamulia miwa zinavyofanya kazi, kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi ya uandaaji hadi kukamilika kwa Sukari tayari kwa matumizi,kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Wa tatu kutoka (kushoto) ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mbegu ya mizabibu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso (kushoto) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal,(wa pili kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya matrekta ya kuvunia mazao aina ya Mahindi, Ngano na Mtama, wakati Makamu alipotembelea katika maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiteta jambo na Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima wakati Makamu alipotembelea katika maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

Monday, August 6, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL AFUTURISHA IKULU NDOGO MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano kutoka kulia) akijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika swala ya Magharibi wakati wa hafla ya Futari aliyowaandalia na kushiriki nao pamoja katika futari hiyo iliyoandaliwa Ikulu ndogo mjini Dodoma jana Agosti, 5, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana, Agosti 5, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mhe. Juma Kapuya, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana, Agosti 5, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Maliasili na Utalii, Hamis Kagasheki, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana, Agosti 5, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana, Agosti 5, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana, Agosti 5, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

Sunday, July 29, 2012

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA ROTARY TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rotary Tanzania na Rais wa Rotary Interantional 2012-13, Sakuji Tanaka, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam kwa mazungumzo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Rotary International 2012-13, Sakuji Tanaka, baada ya kumaliza mazungumzo wakati Rais huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam jana, akiwa na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Rotary Tanzania, na Rais wa Rotary International 2012-13, Sakuji Tanaka, baada ya mazungumzo wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, jana.

Friday, July 27, 2012

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA CHUO CHA NELSON MANDELA MKOANI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo na Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kwa pamoja wakifurahia mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Video unaowawezesha wanafunzi kuonana na kuzungumza na kuchangia masomo kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya mkoa huo wa Arusha, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo, kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Chuo kipya cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati leo akitembelea mazingira ya Chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni kilichopo Jijini Arusha. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati akimfafanulia kuhusu kazi za maabala mpya inayoandaliwa katika Chuo hicho wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo, kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho. Kushoto kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.

Thursday, July 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANAO LA KWANZA KUHUSU UGONJWA WA KISUKARI KWA NCHI ZA AFRIKA, ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo jijini Arusha.
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa ‘International Diabetes Federation’, Jean-Claude Mbanya, baada ya kumaliza hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha.
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya watoto wanaishi na ugonjwa wa Kisukari kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika, wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio na ugonjwa wa kisukari, baada ya kufungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamanao hilo.
Watoto hao wakiimba wimbo maalum wa mshikamano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa ‘International Diabetes Federation’, Jean-Claude Mbanya, baada ya kufungua rasmi Kongamano la kwanza kuhusu Ugonjwa wa Kisukari kwa Nchi za Afrika, lililoanza leo, jijini Arusha.

Sunday, July 15, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Wafanya Mkutano wa Kamati ya Sensa ya Kitaifa

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif wakiteta katika Mkutano wa Kamati ya Sensa ya Kitaifa uliofanyika Mjini Zanzibar , Julai 14,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kamati ya Sensa ya Kitafa, Mjini Zanzibar Julai 14,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wednesday, July 11, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SINCHUAN HONGDA GROUP KUTOKA CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti aliyeongozana na ujumbe Kutoka Hongda Group ya Beijing China, Quan Zhezhu, wakati ujumbe huo ulipofiak ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 11, 2012 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe Kutoka Hongda Group, Beijing China, wakati ujumbe huo ulipofiak ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 11, 2012 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia zawadi ya picha wakati akikabidhiwa zawadi ya picha na Mwenyekiti wa umoja wa Hongda Group ya Beijing China, Quan Zhezhu (katikati) na Mjumbe, Liu Canglang, wakati ujumbe huo ulipofiaka ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 11, 2012 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Hongda Group, kutoka Beijing China, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Julai 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

Popular Posts