Pages

Showing posts with label SMZ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Show all posts
Showing posts with label SMZ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Show all posts

Wednesday, October 17, 2012

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI SHEIN AWAAPISHA MJUMBE (MBM), NAIBU MAWAZIRI NA NAIBU KATIBU WAKUU WA WIZARA MBALI MBALI IKULU ZANZIBAR


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mhe,Saidi Mohamed Said,kuwa Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, wakaati wa  hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, leo mchana.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha CDR Julius Nalimy Maziku,kuwa Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Idara Maalum za SMZ katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Bw Juma Ameir Hafidh,kuwa Naibu Katribu Mkuu Ofisi ya Rais (Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo), katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Bw Mustafa Aboud Jumbe,kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi,Maji na Nishati, katika haflailiyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Bw Tahir M. Abdulla,kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,wakati wa hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, leo mchana.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mhe.Shawana Bukheti Hassan, kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi wakati wa hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mhe, Mtumwa Kheir Mbarak,kuwa Naibu Waziri Kilimo na Maliasili,  wakati hafla iliyofanyika Ikulu MjiniZanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

SMZ YAWATAKA WANANCHI KUENDELEA NA SHUGULI ZAO


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wananchi kuendelea na shughuli  zao kama kawaida na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti hali  ya ulinzi na imeimarishwa katika maeneo yote ya Zanzibar.
Taarifa ya Serikali iliyotolewa leo usiku na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu  wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed imesema Zanzibar bado  ni shwari na inaendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu.

Akizungumzia tukio la vurugu zilizofanywa na wananchi wachache, Waziri  Mohamed Aboud alisema vikundi vya vijana vinavyosadikiwa kuwa ni wafuasi  wa Sheikh Farid Hadi walifanya vurugu hizo katika mitaa ya Darajani,  Michenzani, Muembeladu,Magomeni,Amani wakidai Sheikh wao haonekani  na kudhani amekamatwa na vyombo vya Dola na kuwekwa ndani.


Waziri Mohamed Abud alisema Serikali imewasiliana na vyombo vya  Dola ikiwemo Polisi,Jeshi la wananchi wa Tanzania, Idara ya Usalama wa Taifa,  Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,KMKM,JKU,Chuo cha Mafunzo, Zimamoto na Valantia ambapo vyombo vyote hivyo vimeeleza kutoelewa  chochote kuhusu Sheikh Farid.
  Waziri huyo alisema kwamba Jeshi la Polisi limepokea taarifa ya  kutoonekana kwa Sheikh Farid ambapo kwa sasa Jeshi hilo linaendelea  kumtafuta na kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ili kupata ukweli wake  na kuchukua hatua zinazofaa.
Alisema kwamba wakati Jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi wake,  wananchi wameombwa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo kwa vituo vya Polisi  au kupitia Masheha, Ofisi za Wilaya na Mikoa katika maeneo yao.
Waziri Mohamed Aboud amesema Serikali inawasihi wwananchi waache  kujiingiza katika vitendo vya fujo na vurugu kwani kutenda hivyo ni kosa  kwa mujibu wa sheria na Serikali haitovumilia vitendo hivyo.
 
Katika tukio la leo mchana, vijana hao wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa  Sheikh Farid Hadi walifanya vitendo vya vurugu ikiwemo kuchoma moto  Maskazini za CCM,kuvunja maduka,kupora mali za watu na kuharibu  miundombinu ya barabara na kusababisha hasara kubwa.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
17/10/2012
ZANZIBAR,TANZANIA

Monday, August 27, 2012

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA JUMUIYA YA ULAYA NCHINI TANZANIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiagana na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kusalimiana na Rais. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein na Familia Yake Washiriki Zoezi la Sensa ya Watu na Makaazi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein, akijiandikisha na familia yake kwa Karani Asia Hassan Mussa, (kushoto) katika zoezi la Sensa ya Watu na Makaazi, lililoanza leo nchini kote,Rais akiwa katika Shehia ya Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,(kulia ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

Friday, August 17, 2012

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Afuturisha Mkoa wa Mjini Magharibi

Baadhi ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakianza kufutari kwa kunywa madafu kabla ya kula futari jana walipoalikwa katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa huo kila ifikapo mwezi kama huu kwa futari maalum.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Baadhi ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika futari iliyoandaliwa jana ,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa huo kila ifikapo mwezi kama huu kwa futari maalum.
Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar.
Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, (wa pili kushoto) akijumuika na akinamamawa wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Chakula cha Futari iliyoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, (wengine kulia) Mama Shadiya Karume, Mama Pili Balozi Seif na Waziri wa Muungano Samia Suluhu Hassan, (kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akijumuika na wananchi pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Futari, aliyowaandalia wananchi hao katika viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar jana, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amaan Abeid Karume,(kushoto) na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kufutari nao pamoja jana katika futari aliyowaandalia katika viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumalizika Futari waliyowaandalia katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, (kulia) akisalimiana na mke wa Rais mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume, baada ya Futari iliyoandaliwa kwa wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar

Tuesday, August 14, 2012

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI SHEIN AFANYA MAZUNGUMZA NA MABALOZI WA KOREA NA DENMARK IKULU YA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Kim Young Hoon, alipofika kumuaga Rais, Ikulu mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Johnny Flento,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana, baada ya mazungumzo yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Johnny Flento, alipofika Ikulu mjini Zanzibar jana, kwa mazungumzo na Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Johnny Flento, alipofika Ikulu mjini Zanzibar jana, kwa mazungumzo na Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Korea Nchini Tanzania, Kim Young Hoon,alipofika kumuaga Rais,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Kim Young Hoon, alipofika kumuaga Rais, Ikulu mjini Zanzibar jana.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar

Balozi wa Marekani nchini Tanzania amtembelea makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiitikia dua baada ya kushiriki futari iliyoandaliwa na Masjid Iman iliyoko Mbweni Zanzibar.Katikati ni Sheikh Habib Ali Kombo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akifurahi pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt, aliyefika nyumbani kwake Mbweni kwa ajili ya kubadilishana mawazo. Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
---
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt ameahidi nchi yake itaunga mkono juhudi za Zanzibar kuwa na mipango madhubuti ya uokoaji wakati yanapotokea majanga, ili kunusuru maisha ya watu pale inapotokea hali kama hiyo.

Amesema msaada wa Marekani utaelekezwa zaidi kuiwezesha Zanzibar kuwa na mfumo wa kisasa wa mawasiliano utakaosaidia kujua eneo la tukio na kumudu kufika kwa haraka, kwa nia ya kuokoa maisha ya watu wengi zaidi iwezekanavyo.

Balozi Alfonso amesema hayo leo alipokuwa na mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad huko nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar kuzungumzia tukio la kuzama kwa meli ya MV. Skagit, pamoja na mambo mengine mbali mbali. “Msaada huu wa kuepusha maafa wakati yanapotokea majanga, utakuwa ni kwa Tanzania nzima, lakini tutahakikisha Zanzibar inanufaika nao na inajijengea uwezo wa kuokoa maisha ya watu wake, wakati wa maafa kama haya ya kuzama kwa meli na mengineyo”, aliahidi Balozi Lenhardt.

Hata hivyo, Balozi huyo wa Marekani alisifu mshikamano wa wananchi wa Zanzibar pamoja na serikali yao, wakati wa maafa ya kuzama kwa MV. Skagit mwezi uliopita, hali ambayo ilisaidia kuokolewa baadhi ya watu waliokuwemo kwenye meli hiyo.

Naye, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amekaribia azma hiyo ya Marekani kuisaidia Zanzibar katika kukabiliana na majanga mara tu yanapotokea. Katika hatua nyengine Balozi Lenhardt ameisifu Zanzibar kwa hatua kubwa iliyoweza kufikia kudhibiti ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa ukisababisha vifo vya watu wengi wakiwemo watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Balozi huyo amesema Zanzibar imejijengea heshima na hivi sasa imekuwa mfano Duniani na wataalamu kutoka sehemu mbali mbali wanakuja Zanzibar kujifunza mbinu za kutokomeza ugonjwa huo. Akizungumiza mafanikio hayo, Maalim Seif alisema suala la elimu kwa wananchi juu ya kutokomeza ugonjwa huo limechangia kwa kiasi kikubwa kuwa na uelewa wa hali ya juu kujilinda wasipate maradhi hayo.

Maalim Seif alisema baada ya wananchi walio wengi kuelewa mbinu za kujikinga na Malaria imekuwa rahisi kuweza kuzitumia njia wanazoshauriwa na wataalamu.

Alizitaja baadhi ya mbinu hizo kuwa ni matumizi ya vyandarua, kupuliziwa dawa kwenye nyumba zao, kuweka mazingira yao katika hali ya usafi pamoja na kufika kwenye vituo vya afya kwa uchunguzi na kutibiwa mara wanapoona dalili za kuwa na maradhi hayo.

Balozi huyo wa Marekani pia amemhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa nchi hiyo itaendelea kufanikisha miradi mbali mbali inayofadhiliwa na Marekani hapa Zanzibar.

Miongoni mwa miradi hiyo ni utandikaji wa laini kuu ya umeme kutoka Dar es Salaam hadi Fumba kupitia chini ya bahari na ujenzi wa barabara tafauti, ambayo yote ipo katika hatua nzuri za utekelezaji.

Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais jana alijumuika katika futari iliyoandaliwa na masjid Iman iliyoko mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Futari hiyo iliwajumuisha wananchi mbali mbali wanaosali katika msikiti huo pamoja na viongozi kadhaa wa dini na siasa wakiwemo Sheikh Habib Ali Kombo na Makamu Mwenyekiti wa CUF Machano Khamis Ali.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

Monday, August 6, 2012

Rais wa Zanzibar Azindua Mashine ya Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Uongozi wa Wzara ya Kilimo na Maliasili,baada ya kuzindua rasmi mashine za Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) katika hafla iliyofanyika leo huko shamba la Kilimo la Serikali, Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(wa sita kushoto)akiangalia Mashine ya Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) baada ya kufanya uzinduzi waMashine hizo,zilizonunuliwa na Serikali ya Mapinduzi zikiwa jumla 14 katika kuboresha hatua za Mapinduzi ya Kilimo,katika Shamba la Mbegu Bambi ,Wilaya ya Kati Mkoa waKusini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akiwasha Mashine ya Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mashine hizo,zilizonunuliwa na Serikali ya Mapinduzi zikiwa jumla 14 katika kuboresha hatua za Mapinduzi ya Kilimo,katika Shamba la Mbegu Bambi ,Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiangalia Mpunga Ukitoka katika mashine ya Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) baada ya kuzindua mashine hizo katika shamba la Kilimo la Serikali huko Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiangalia Mpunga Uliovunwa kwa kutumia mashine ya Kuvunia Mpunga,(Combine Harvester) baada ya kuzindua mashine hizo katika shamba la Kilimo la Serikali huko Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi na wakulima wa Mpunga wa Maeneo mbali mbali baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa mashine za Kuvunia Mpunga (Combine Harvester) huko Shamba la Kilimo la Serikali huko Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo na Maliasili Suleiman Othman Nyanga,(katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Othman Affan Maalim, baada ya kumalizika hafla ya kuzindua mashine za (Combine Harvester) leo katika shamba la Kilimo la Serikali huko Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

Popular Posts