Pages

Showing posts with label Yanga. Show all posts
Showing posts with label Yanga. Show all posts

Saturday, August 4, 2012

WACHEZAJI WA YANGA WAKIJINOA KATIKA UWANJA WA LOYOLA

KOCHA wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet, akikinoa kikosi cha timu yake katika Uwanja wa Shule ya sekondari Loyola iliyopo Mabibo jijini Dar es Salaam hii leo. Yanga inajinoa kwa michuano ya Ligi Kuu ya tabnzania bara inayotaraji kuanza baade mwezi huu. Lakini imezusha maswali kwa wadau wa soka nchi na wapenzi wa timu hiyo kwa kutokushiriki kwake michuano ya Super8 inayotaraji kuanza Agosti 5, 2012 katika viwanja mbalimbali nchini. Picha na Rachel Pallangyo-FK Blog.

Sunday, July 29, 2012

JERRY TEGETE NA MRISHO NGASA NDANI YA WHITE HOUSE KIMARA KOROGWE

Mwanamuziki nguli wa Bendi ya Mashujaa Musica Chaz Baba akiimba kwa furaha kubwa ndani ya Ukumbi wa White House Kimara Korogwe usiku wa kuamkia leo.
Rapa maarufu wa Bendi ya Mashujaa Fagasoni akiimba ndani ya ukumbi wa White house Kimara Korogwe.
Mrisho Ngassa na Chaz Baba wakifurahia kwa pamoja Ushindi waYanga, Mrisho ngassa ni Mshambuliaji mahiri wa Club ya Azam.
Kutoka kulia Chaz Baba, Mrisho Ngasa Mchezaji wa Azam na Gerry Tegete Mchezaji wa Yanga wakiwa ndani ya viunga vya White House Kimara Korogwe jana baada ya kutoka kwenye Mechi kali baina ya timu zao, ya kombe la Kagame ambayo Yanga waliibuka mabingwa kwa mabao 2 kwa bila.
Kulia Gerry Tegete akishoo luv na Mchezaji mwenzake Mrisho Ngassa anayechezea club ya Azam.
Mpiga tumba namba moja Afrika mashariki MCD akiwakimbiza washabiki wao ndani ya White house Kimara.
Tegete, Henry na kulia Mrisho Ngassa ndani ya White House Kimara.
--
Jana jioni kulikuwa na mechi ya fainali ya kombe la Kagame kati ya Yanga afrikani na Azam FC ndani ya uwanja wa Taifa ambapo Yanga waliibuka mabingwa

Ngassa na Tegete kwa kuonyesha mpira sio ugomvi walisherehekea pamoja ushindi wa Yanga baada ya mechi katika viwanja vya White House Kimara korogwe wakati bendi ya Mashujaa ilipokuwa inatumbuiza

YANGA YA TANZANIA NDIO BINGWA WA KOMBE LA KAGAME 2012

Wachezaji wa Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakishangilia ubingwa wao wakiwa na Kombe la Kagame baada ya kukabidhiwa rasmi walipoibanjua timu ya Azam Fc kwa mabao 2-0, katika mchezo wa Fainali uliozikutanisha timu hizo katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo jioni.
*****************************

TIMU ya Yanga ya jijini ya Dar es Salaam, leo imewadhihirishia mashabiki wa soka kwa kutetea ubingwa wake na kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame 2012,katika mchezo wa Fainali za Kombe hilo dhidi yake na timu ya wauza Lambalamba Azam Fc, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa.

Yanga sasa imebakiza mara moja kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba kutwaa Kombe hilo, mara tano kwa sita. Yanga ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Hamisi Kiiza aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 44 na Said Bahanuzi aliyefunga la pili dakika ya 90+ katika dakika tatu za nyongeza.

Kiiza alifunga bao lake, baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kumpiga chenga kipa huyo kisha kuusukuma mpira nyavuni.

Bahanuzi aliuwahi mpira mrefu uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa Azam kabla ya kumtungua Dida.

Niyonzima, akichanja Mbuga.
Niyonzima, akimtoka beki wa Azam kwa spidi ya ajab na kumimina majalo.
Kipa wa Azm, Dida, akiokoa moha ya hatari langoni kwake.
Niyonzima, akiendelea kuwatesa mabeki wa Azam.
Beki wa Azam, Mouris akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi na kumpa nafasi kipa wake Dida kudaka mpira huo.
Mashabiki wa Azam waliochanganyika na wa Simba, wakiwa wamebeba Jeneza kuwakejeli mashabiki wa Yanga, kabla ya kuanza kwa mchezo huo.lakini hadi mwisho wa mchezo huo Jeneza hilo halikujulikana lilikopitia.
Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao ya As Vita yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi, dakika ya 67, wakati la kufutia machozi la timu ya APR ya Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya 89 na kufanya mshindi wa tatu katika michuano hiyo kuwa ni AS Vita.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la kwanza.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia na Kombe lao.
Kasuku nao walikuwapo kushuhudia mtanange huo huku wakiwa na rangi ya Yanga na Bendera ya Yanga.
Mashabiki wa Azam wakiwa Tuliiiiii, wakiwa kama wamemwagiwa maji baada ya timu yao kupokea kichapo kitakatifu jioni ya leo.
Said Bahanuz, akishangilia mbele ya mashabiki wake baada ya mchezo huo kumalizika.
Mashabiki wa Yanga....... Ebwana eeeeh!!!! ushindi mtamu bwanaaaaaa!!!!
Bahanuzi kama Kawa.......
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji akipita katikati ya Uwanja kuwapongeza wachezaji wake baada ya mchezo huo kumalizika.
Niyonzima (kushoto) akimfariji Ngasa, baada ya mchezo huo.

2012 CECAFA KAGAME CLUB CUP
Dar es Salaam, July 14-28
(Yellow cards after end of preliminary round)
2:
20. Derrick Walulya (Suspended Match No. 12)
4. Yusuf Makame Juma [Mafunzo]
5. Kadar Abaneh [AS Port]
1:
2. Edward Simon Jovan [El Salaam, Wau]
28. Maxime Sekamana [APR ]
11. Emery Ndikumana [Atletico Olympique]
7. Didier Kavumbagu [Atletico Olympique]
17. Amir Maftah [Simba]
15. Allan Munabu [URA]
21. Ahmed Mohdi [AS Port]
5. Ismail Khamis [Mafunzo]
25. Johnson Bagoole [APR]
17. Christopher Ndayishimiye [Atletico]
4. Hassan Hakizimana [Atletico]
13. Ismail Musa Juma [El Salaam, Wau]
13. Lema Mubidi [AS Vita]
17. Thiery Kasereka [AS Vita]
16. Vincent Agbor [AS Port]
1. Khalid Moursal [AS Port]
4. Jean Paul Niyibaraba [AS Port]
3. Francis Nongwe [Atletico]
15. Frederick Nsabiyumwa [Atletico]
15. Santino Makuei [El Salaam, Wau]
24. Jerry Santos [Tusker]
18. Said Musa Shaaban [Mafunzo]
14. Sula Bagala [URA]
22. Osman Wejuli [URA]
12. Suleman Ndikumana [APR]
4. Donatien Tuyizere [APR]
18. Joseph Shikokoti [Tusker]
13. Aggrey Morris [Azam]
19. John Bocco [Azam]
TOTAL: 29
QURTER FINALS
2:
21. Issa Mpeko [AS Vita Club] (2) R
4. Ibrahim Mwaipopo [Azam] (2) R
1:
15. Mohamed Abdoulrahman [Mafunzo]
20. Derrick Walulya [URA]
16. Augustine Nsumba [URA]
22. Jean Claude Iranzi [APR]
3. Albert Ngaboyisibo [APR]
16. Nelson Lukong [Vita]
23. Pierre Kwizera [Atletico]
3. Simbi Ebunga [AS Vita Club]
14. Mutombo Kazadi [AS Vita Club]
10. Felix Sunzu [Simba]
6. Erasto Nyoni [Azam]
26. Haruna Shamte [Simba]
25. Jabir Aziz [Azam]
TOTAL (from Quarter final stage only): 17 - Up to Match No. 20 (Yanga v APR semifinal)
OVERALL TOTAL: 36
Gishinga Njoroge
Managing Editor
www.kpl.co.ke
Brookside Grove
Westlands
P.O Box 5350, Nairobi, 00506 Kenya
Office Tel: +254 020 444 20 70
+254 020 444 20 72
email: gishinga@kenyanpremierleague.com
Personal cel phone: +254 722 79 77 49

Saturday, July 28, 2012

MABINGWA KOMBE LA KAGAME 2012 NI YANGA YA TANZANIA

Magoli mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika dakika ya 90 ya mchezo yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe la Kagame 2012 baada ya kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa goli 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tanzania ijnakila sababu ya kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya Azam katika michuano hiyo ya mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa michuani huyo iliingiza timu 4 zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa katika hatua ya robo fainali.

Yanga pia waliutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya kushambulia mwamuzi kwa ngumi.

Kikosi kilichoipeleka Yanga fainali kombe la Kagame 2012

Kikosi kilichoipeleka Yanga fainali mwaka huu; Kutoka kulia waliosimama Nadir Cannavaro, Kevin Yondan, Said Bahanuzi, Ally Barthez, Athumani Chuji na Oscar Joshua. Waliopiga magoti kutoka kulia ni Juma Abdul, David Luhende, Haruna Niyonzima, Godfrey Taita na Hamisi Kiiza.

Tuesday, July 17, 2012

Yusuf Manji Ashinda nafasi ya mwenyekiti wa Klabu Ya Yanga Kwa Kura 1876 Sawa na 97.0%

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti Yusuf Manji wakati akiomba kura kwa wanachama wa Yanga kabla ya uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana.
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga akiomba kura kwa wanachama wa Yanga kabla ya uchaguzi uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Yusuf Manji (Kulia) na Clement Sanga (Kushoto) wakiteta kabla ya uchaguzi wa klabu ya Yanga uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana.Picha zote na mdau Dande Francis
--
NAFASI YA MWENYEKITI WA KLABU

Yusuf Manji (kura 1876) - 97.0%
John Jembele (kura 40) - 2.6%
Edgar Chibura (kura 4) - 0.24%

NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI

Clement Sanga (kura 1948) - 62.6%
Yono S Kevela (kura 475) - 23%
Ayoub Nyenzi (kura 288) - 14%

NAFASI YA UJUMBE

Abdallah Bin Kleb (kura 1942)
Moses Katabaro (kura 1068)
Aaron Nyanda (kura 922)
George Manyama (kura 682)
Beda Tindwa (kura 391)
Edgar Fongo (kura 295)
Graticius Ishengoma (kura 247)
Jumanne Mwamenywa (kura 251)
Justine Baruti (610)
Lameck Nyambaya (kura 425)
Omary Ndula (kura 170)
Peter Haule (441)
Ramadhan Said (249)
Yono Kivela (123)
Kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni

MWENYEKITI: Yusuf Manji,
MAKAMU MWENYEKITI: Clement Sanga

WAJUMBE: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda, Geroge Manyama

Sunday, July 15, 2012

YANGA YATANDIKWA 2 BILA NA ATLENTICO KAGAME CUP

Mchezaji wa timu ya Yanga, Juma Abdul, akichuana kuwania mpira na beki wa Atletico, Henry Mbazumutima, wakati wa mchezo wao wa fungua dimba ya michuano ya kombe la Kagame, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo inaandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA. Katika mchezo huo Yanga imeanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao 2-0 na Atletico, huku mabao hayo yakiwekwa kimiani na Olivier Ndikumana katika dakika ya 81 na 90+3.
Wachezaji wa timu za Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi wakichuana vikali katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.

Sunday, July 8, 2012

WABUNGE WA SIMBA WAWAKANDAMIZA WATANI WAO WA YANGA KWA PENALTI 3-2

Wachezaji wa Simba (Wabunge) wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga watani wao wa Yanga (Wabunge) kwa penalti 3-2.
Yanga baada ya kipigo hicho.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga (Wabunge) wakati wa TAMASHA LA MATUMAINI ambapo wabunge wapenzi wa timu ya Simba wameibuka kidedea kwa penalti 3-2. Simba wamefunga penalti 3 wakati Yanga wakifunga 2.
(PICHA ZOTE NA GPL)

Popular Posts