Pages

Showing posts with label Arusha. Show all posts
Showing posts with label Arusha. Show all posts

Monday, November 19, 2012

AIRTEL TANZANIA NA UNESCO WAZINDUA RADIO JAMII LOLIONDO MKOANI ARUSHA


Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akifungua jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa radio kijijini Ololosokwani. Uwekwaji wa redio hiyo  ya jamii umezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilo la kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi. Beatrice Singano na wakwanza shoto muwakilishi wa UNESCO Bi. Vibeke Jensen
Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbaraw akijaribu mtambo wa radio kwa kutangaza moja kwa moja (live) kupitia radio ya jamii LOLIONDO FM mara baada kumalizika kwa  hafla ya uzinduzi rasmi  wa radio hio ya jamii iliyowezeshwa kwa ushirikiano
kati ya Airtel na shirika lisilola kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi  Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani.

Picha Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akitoa wito kwa wanafunzi na wanakijiji wa Ololosokwani  kuhakikisha wanatumia vyema kituo cha mtandao wa Internet (multi media center) katika shughuli za masomo yao mara baada ya waziri huyo kuzindua mradi wa radio ya jamii LOLIONDO FM, mradi wa mtandao pamoja na kampeni ya
kuwafundisha jamii ya wamasai kujenga nyumba za kisasa katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi  Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani
Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akisalimiana wananchi wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ambapo waziri huyo alikuwa mgeni rasmi wa katika ufunguzi  wa radio ya jamii pamoja na miradi mingine ilikiwemo ujenzi wa nyumba za kimasai za kisasa

Wadau wawezeshaji wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa mara baaada ya uzinduzi wa radio hiyo kijijini 
Ololoskwani
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na shirika lisilo 
la kiserikali UNESCO kwa pamoja wamezindua Radio jamii katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na kufanywa na Waziri wa mawasiliano sayansi na technologia Mh Makame Mbarawa.

Mradi wa Radio za jamii ni program maalum inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na UNESCO yenye lengo la kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu, elimu duni, ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni , ukandamizaji wa wanawake na watoto na changamoto zinginezo. Maeneo hayo pia mbali ya kuwa na changamoto huduma za mawasiliano ni duni na upatikanaji wa huduma za radio kwaajili ya kuelimisha jamii ni changamoto kubwa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa radio hiyo, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Technologia Mh Makame Mbarawa alisema” ninawapongeza Airtel na UNESCO kwa jitihada zenu hizi katika kuendeleza mawasiliano nchini hasa vijijini, mimi nimefurahishwa sana kuona wadau hawa wanavyojiunga najamii ya kijijini hapa na kuwaunganisha na sehemu nyingine za dunia
kwa kuweka radio hii ya Loliondo FM ili kuwawezesha kupata habari na taarifa muhimu kwa maendeleo ya taifa”.

Hii ni fulsa ya pekee kwenu wakazi wa kijiji cha ololosokwani pamoja na vijiji jirani kuinua shughuli zetu za kiuchumi, kutumia radio hii kutoa maoni na elimu, Naamini vipindi vitakavyorushwa vitakuwa vimelenga jamii husika na kuwa chachu ya kuleta ufanisi mkubwa katika mabadiliko na maendeleo kwa ujumla”. Aliongeza Mbarawa Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurungezi wa Mawasiliano Bi Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel inajisikia furaha kuwa nafasi ya kuchangia maendeleo jamii  nchini Tanzania, tunaamini kwamba kupitia
redio hii na kwa kupitia mtandao wetu ulioenea zaidi wananchi wamaeneo haya na vijiji takribani 14 vya jirani watanufaika na kuwepo kwa redio Loliondo fm hapa ololosokwani. Tunategemea kuona maisha ya ndugu na jamaa zetu wa jamii ya wamasai na wageni waliopo hapa yakibadilika kwa kasi katika Nyanja zote”

“sasa Wakazi wa ololosokwani watapata nafasi kwa kupitia radio hii, kutangaza utamaduni wao, kuboresha na kupata uongozi bora, kutangaza biashara zao na kukuza soko huku wakitumia huduma ya Airtel money kupata malipo na kuhifadhi pesa zao kwa usalama zaidi” alisema Singano Singano aliongeza kuwa “Mbali na Radio tumeweza pia kuwawezesha wakazi
wa kijijini hapa kupata huduma ya internet kupitia Multimedia center tuliyoijenga na kuiwekea mtandao wetu wenye spidi wa 3.75G, Aliongeza Singano.

Naye mwakilishi kutoka UNESCO bw,  Ali-amin Yusuph alisema “UNESCO inayofuraha kuona mradi wa radio unakuwa na kuwafikia wananchi wengi nchini kwa ushirikiano wa Airtel,  kuwepo kwa radio hii kutaunganisha wakazi wa Ololosokwani na wale wa maeneo mengine nchini na dunia kwa ujumla. UNESCO tunayo miradi mingi sana ya kusaidia jamii na Mradi wa Radio hapa Olosokwani umetusaidia kuona maeneo mengine mengi  ya kuweza kusaidia jamii hii ya kimasai, leo tunayo miradi mbalimbali tuliyoianzisha  hapa ikiwemo Mradi wa Solar (umeme wa jua) ambao utawawezesha akina  mama kupata kipato. kwa kupitia mradi huu wakazi wa hapa wamepata sehemu za kuchajia simu zao na kuweza kufanya shughuli zinazohitaji umeme kwa malipo kidogo”.

“Halikadhalika tumeweza kurekebisha nyumba za kimasai na kuzifanya ziwe na muundo wa kisasa unaotoa moshi nje ya nyumba na kuzifanya ziwe na kiwango bora” Alimaliza kwa kusema mwakilishi kutoka UNESCO bw, Ali-amin

Uzinduzi wa kituo hicho cha radio ijulikanayo kama LOLIONDO uliambatana na ugawaji wa vitabu  vya masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kijijini humo kutoka kwa kampuni ya Airtel  ikiwa ni kuwahamasisha wanafunzi wengi kupenda fani ya sayansi wakiwa tangu wadogo kitu ambacho kitachangia kuongeza idadi ya wataalamu wa sayansi hapa nchini.

Airtel kwa kushirikiana na UNESCO inaendelea na mradi  wa radio jamiiunaotegemea kufikia maeneo mengi zaidi nchini ikiwemo Sengerema Mwanza,  Karagwe Kagera,  Chake Chake Pemba, Makunduchi Unguja , Pangani Tanga,  Kyela Mbeya , na Kalama Shinyanga.

Thursday, November 8, 2012

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI DHIDI YA RUFAA YA LEMA



IMG-20121108-WA0003
Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mhe. Godbless Lema wakiwa mahakamani leo.
IMG-20121108-WA0007
Godbless Lema akiwasili katika viwanja vya Mahakama ya Kuu jijini Dar leo.
Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai  ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.

Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za waliokata rufaa. Mawakili wa Mhe. Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.

Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi. Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu.
IMG-20121108-WA0006
Wapenzi wa Chadema wakimlaki Mhe. Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama leo.
IMG-20121108-WA0004
Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi.
IMG-20121108-WA0002
Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
IMG-20121108-WA0005
Katibu wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama Kuu leo. Habari / Picha kwa hisani ya ARUSHA255 BLOG

Tuesday, September 11, 2012

MKUTANO WA 14 MAWAZIRI WA MAZINGIRA BARANI AFRIKA KUANZA KESHO MKOANI ARUSHA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na maandalizi ya mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka barani Afrika Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.
---
Na.MO BLOG -Arusha
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania Mh. Theresia Huviza anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Rais wa Mazingira kwa Afrika katika Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa mazingira unaofanyika Arusha nchini Tanzania kuanzia kesho hadi tarehe 14 mwezi huu.
Waziri Huviza ataongoza kwa kipindi cha muda wa miaka miwili ambapo baada ya hapo nafasi hiyo itachukuliwa na nchini nyingine.
Mkutano huo umefanikishwa na European Union, Ubalozi wa Norway, Global Environmental Facility, UNEP na UNDP na wajibu mwingine ukifadhiliwa na serikali yenyewe.Bajeti ya maandilizi ya mkutano huo imegharimu takriban dola za kimarekani 350,000 sawa na shilingi za Tanzania zaidi ya milioni mia 6.
Pichani juu na chini ni Watoto wakifanya mazoezi ya wimbo maalum watakaoimba kesho kwenye mkutano wa 14 wa mawaziri wa mazingira barani Afrika mbele ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania Mh. Theresia Huviza.
Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(kushoto) akitoa maelezo mmoja wa wadau wa mazingira aliyefika katika banda la Umoja wa Mataifa lililopo katika jengo la AICC utakapofanyika mkutano wa 14 wa mawaziri wa Mazingira.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu aktioa maelezo kwa mmoja wa wadau ya namna Umoja wa Mataifa inavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika utunzaji wa Mazingira kupitia mpango wa mazingira (UNEP) uliopo chini ya Umoja wa Mataifa.
Banda la ROA OZONE ACTION PROGRAMME chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na UNEP wakitoa maelezo katika kutunzaji wa mazingira kwa wananchi.

Sunday, August 26, 2012

KIKUNDI CHA SERENGETI CHAJIUNGA NA CHADEMA


Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha Mh Samson Mwigamba.
Katibu wa Chadema wa mkoa wa Arusha Mh Amani Golugwa.
Mmoja wa Viongozi wa Kikundicha Serengeti akikabidhiwa katiba ya Chadema.
Wasanii wa kikundi cha Serengeti walioamua kujivua gamba na kujiunga na Chadema.Picha na Habari na CHADEMA
---
Sanaa kama moja wapo ya vyanzo vya ajira nchini haina budi kusimamiwa kikamilifu na serikali ili kuwezesha taifa kupunguza tatizo la ajira. Ni wakati muafaka hivi sasa kwa serikali kuhakikisha inaandaa utaratibu mzuri wa kukulinda maslahi ya wasanii kwa kusimamia uendeshwaji mzima wa biashara ya kazi hizo.Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Arusha, Mwigamba Samson wakati akiwapokea wanachama zaidi ya 40 ambao ni wasanii wa kikundi cha Serengeti Art Group kama wanachama wapya wa chama hicho.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa inashangaza kuona wasanii wengi wa Tanzania wana hali mbaya kiuchumi licha ya kazi kubwa na nzuri wanazozifanya na kuongeza kuwa hali hiyo inasababibshwa na serikali iliyopo madarakani kutojali kazi hizo. Amesema kama chama na kupitia wabunge wa chadema wamefanya kazi kubwa ya kuishinikiza serikali kuliona hilo na kulifanyia kazi.

Kwa upande wake Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Amani Golugwa, amesema sera ya chama chake kuhusu sanaa ni kuona kuwa sanaa haibakii kutumbuiza peke yake bali ni kuhakikisha kuwa inakua ajira rasmi kwa wasanii na wadau wanaojihusisha nayo kwa namna moja ama nyingine.

Katibu huyo ameongeza kuwa vuguvugu la mabadiliko linaloendelea hivi sasa lina lengo la kuzidi kukiimarisha chama na kwamba mkoani Arusha vuguvugu hilo litafanyika mnamo mwezi wa kumi na moja hivyo amewataka wanacham hao wapya kuanza kazi ya kuleta mabadiliko kama lengo la vuguvugu hilo linavyosema.

Saturday, August 4, 2012

MBUNGE WA MONDULI ATOA TENDE NA KANZU KWA WANANCHI

Mh Lowassa akimkabidhi sheikh Simba sehemu ya tende hizo.Wengine pichani kushoto ni Sheikh wa Mto wa Mbu Sheikh Nasib Idd Nasib Mnyema Kkatibu wa Bakwata wilaya ya Monduli Idd Idoya na Ustadh Swalehe Ramadhan .
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa, ametoa katoni kadhaa za tende pamoja na jozi 100 za kanzu kwa ajili ya Waislam wa Monduli.Akipokea msaada huo, sheikh wa wilaya ya Monduli Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni Salum Simba, alimshukuru mh Lowassa kwa utaratibu wake huo ambao amekuwa akiufanya kila mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Waislam wa Monduli.

Wananchi Wa kata ya Tarati wilaya ya Simanjiro watoa maoni ya Katiba mpya

Bw. Godson Luya, mkazi wa kata ya Terati wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kata hiyo hivi karibuni.
Wakazi wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani hapo hivi karibuni.

Friday, August 3, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AGAWA NGOMBE 500




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto kwake ni WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli mchana wa leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa shukrani kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa kuweza kuwakumbuka wananchi wa Wilaya ya Mbonduli.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa Ng'ombe kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.



Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng'ombe.


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipowasili katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kwa ajili ya kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Arusha waliofika katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kumlaki.Rais Kikwete leo amefika katika kijiji hicho cha Makuyuni na kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake zilizotokea mwaka 2008/2009.





Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.



Rais Kikwete akielekea kwenye Jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Monduli

Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni Wakizungumza
Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng'ombe.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipatiwa maelezo ya Mifugo hiyo kabla Rais Kikwete hafafika na kuigawa kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake uliozikumba wilaya hizo mwaka 2008/2009.



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika Mazungumzo na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka.Picha na IKULU
---
SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Ahadi hiyo imetolewa jana, Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika Makuyuni wilayani humo.
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.
Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.
Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo

Popular Posts