Pages

Sunday, October 28, 2012

Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Mazishi Ya Aliyewahi kuwa mpambe wa Rais wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi Marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijiji cha Kiwangwa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani  jana jioni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa nyumbani kwa marehemu kijijini  Kiwangwa,wilayani Bagamoyo jana jioni wakati Rais Kikwete alipokwenda kushiriki mazishi ya Marehemu.Pichaa na Freddy Maro-IKULU-
----

Enzi za Uhai wake Marehemu Luteni Kanali Mtengwa aliwahi kuwa mpambe wa Rais wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi,kuanzia mwaka 1995.Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika Wizara ya Sheria na kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jeshi.

Marehemu alifariki juzi tarehe 25 Oktoba nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda na ameacha mjane, watoto wanne na wajukuu watatu

Popular Posts