Pages

Thursday, November 8, 2012

HAJJAT REHEMA AOMBA MSAADA KULEA YATIMA NA WAJANE


 Hajjat Rhema Amir Gama
--
Assalam alleykum! Kwa jina naitwa Hajjat Rhema Amir Gama, ambaye mwaka huu nilikuwa miongoni mwa wanawake wa kiisilamu waliopata nafasi ya kupelekwa kuhiji Makka. Naishi Ilala Mtaa wa Nzasa, nyumba namba 17, jijini Dar es salaam.
Nina madrasa yangu inaitwa Al-Jannatu Islamiya na pia nalea watoto yatima na wajane, ambao wako shambani, Wiliya ya Kisarawe eneo la Masanganya, nimewahifadhi msikitini kwa sababu bado sijapata mfadhili wa kunisaidia kujenga makazi yao ya kudumu.
Wazee  wa msikiti wa Kisarawe wamenipa eneo la kujenga kituo cha watoto yatima na wajane, lakini sina uwezo wa kifedha wa kujenga makazi hayo.
Sasa naomba msaada wa hali na mali kwa yeyote ataeguswa na hawa watoto na wajane ili niweze kuwalea na kuwapa makazi ya kudumu wakiwa nao ni viumbe wa Mwenyezi Mungu. Moyo wa upendo ninao, ila sina uwezo. 
Kama kuna mtu anaguswa na jambo hili naomba awakilishe msaada wake katika akaunti namba2052529708 NMB au kwa Tigo Pesa na M-pesa kwa numba zifuatazo au afike Ilala Mtaa wa Nzasa, nyumba namba 17 aonane na Bi Hajjat Rehema Gama.
Simu na:
0714 230163,  
0713 558222
0754 414270

WABILLAHI TAUFIQ!

Popular Posts