
  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia)  akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na ubalozi wa China nchini  Tanzania kuhusu  mikakati ya serikali ya kuboresha  kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania.
 
  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia)  akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing  wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini.
 
  Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ukiwemo ujenzi wa  reli ya Uhuru (TAZARA) walioalikwa kwenye hafla hiyo  Bw.  Abdul Haji (kulia) na mama Roza Kangoma (kulia) ambaye ni mama wa  balozi wa Zambia nchini Tanzania pia aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha  mafunzo cha TAZARA.
   Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza  hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio  ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China  na Tanzania kwenye  miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni  balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na  Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule.
 
  Raia kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio  ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kutoka nchini China katika miradi  mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania wakijipatia nakala mbalimbali za  machapisho kuhusu shughuli za kilimo, siasa, Utamaduni, Teknolojia na  masuala ya kijamii.
 
  Wageni  mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo katika ubalozi wa China nchini  Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla hiyo.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO