Pages

Monday, July 2, 2012

ATEKELEZA FAMILIA BAADA YA MKE KUJIFUNGUA WATOTO WANAOFANANA NA NYANI.

Mtoto Alhaj.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mwanaharusi Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye shati Nyekundu na Abdulatifu.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha kuwa magumu.Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu. Pia aliondoka na matandiko yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).Alisema baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu aliozaa naye.Alisema katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.

“Mtoto wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa la saba mwaka huu. Ramadhani (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.

Mwanaharusi alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5) ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa kuanza shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi. Mawasiliano yao yanategemea ishara tu.

“Ukiacha matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu kubwa. Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.

Mwanaharusi alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na macho yao ni makubwa. Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.

Hata hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu na afya zao zikiwa njema kabisa. Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.

“Wakati bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika hospitali ya mkoa wa Singida. Alichunguzwa na alibainika kuwa na upungufu wa damu. Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi nyumbani”,alisema.

Alisema baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa, ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha magumu mno ambayo ni ya kuomba omba. Mnyawi pamoja na familia yake, amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea watoto wao pamaja, jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi kugoma kumrudia Mwanaharusi.

Naye mratibu elimu wa kata hiyo Mwekwa Mwekwa, alisema watoto hao wawili, shule inayowafaa ni ile ya watoto wenye mtindio wa ubongo na si hizi za kawaida.Jitihada ya kumtafuta Mnyawi ambaye anaishi kijiji hicho cha Ndulungu, hazikuzaa matunda baada ya kuelezwa kwamba baada ya kusikia waandishi wa habari watafika kijijini hapo, alifunga safari na kuelekea jijini Mwanza.

Popular Posts