Pages

Monday, July 23, 2012

Wananchi wa Mgodi wa Buhemba Kuishitaki Serikali Ya Tanzania Kwa Jumuia za Kimataifa

Mgodi wa Buhemba
Diwani wa kata ya Buhemba Boniphace Masero akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
---
Augustine Mgendi, BUHEMBA
WANANCHI vijiji Vitatu wanaozungukwa na Mgodi wa Buhemba wilaya ya Butiama mkoani Mara wanakusudia kuishitaki Serikali ya Tanzania katika Taasisi za Umoja waMataifa zinazohusika na haki za binadamu ikiwa ni shinikizo la kulipwa fidia ya shilingi Bilioni 30.

Mbali na kusudio hilo la kuelekea umoja wa Mataifa lakini pia wananchi hao wamesema kuwa wanakusudia kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kumueleza madhara yaliyosababishwa na Mgodihuo ambao ulidaiwa kumilikiwa na Serikali kupitia Kampuni ya Meremeta.

Wananchi hao kutoka vijiji vyaTarani,Biatika na Magunga huku wakiomba Wabunge kuungana na kutoipitisha Bajetiya Wizara ya Nishati na Madini had hapo Serikali itakapo wafidia.

Akiongeana waandishi habari katika eneo hilo la Buhemba,Diwani wa kata ya BuhembaBoniphace Masero amesema kuwa Mgodi huo umeachia athari kubwa kutokana namachimbo yaliyoachwa kuleta athari kubwa huku Ardhi yao ikiwa haina rutuba kutokanana Kemikali zilizomwagwa katika eneo hilo

Amesema athari zingine zilizoletwa na Mgodi huo nipamoja na Shule iliyokuwa katika eneo hilo kubomolewa lakini walishindwakuijenga kama walivyokuwa wameahidi wahuska hao wa mgodi huku miundombinu yabarabara nao ikiwa haifai kutumika.



“Huu Mgodi umetuachia madhara makubwa sana maanaMashimo hayakufukiwa,Milima inaleta uchafuzi wa Mazingira,shule iliyokuwaimejengwa hapa ilibomolewa,Nyumba zikabomoka kutokana na Baruti za mgodi,katikahili sisi tunakusudia kumuona Rais ili tumueleze haya Manyanyaso tunayoyapata”alisema diwani huyo

Diwani Masero ameongeza kuwa athari nyingine nipamoja na baadhi nyumba za wakazi wa eneo hilo kubomoka kutokana na barutizilizokuwa zikipigwa katika Mgodi huo lakini mpaka sasa hawajalipwa fidia nahivyo wanawaomba Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakutoipitisha Bajeti ya wizara ya Nishati na Madini mpaka walipwe fidia yao

Aidha Pasta wa Kanisa la Anglikana SamweliNyakarungu alisema kuwa mgodi huo wa Buhemba ulikuwa ni Mgodi wa kitapeliambapo wahusika hao wamechuma raslimali za Taifa na kushindwa kufanya shughuliza Maendeleo katika Jamii.

Pasta Nyakarungu alisema kuwa mbali na wawekezajihao wa Kitapeli kuiba mali ya Watanzania lakini pia wamesababisha madharamakubwa kwa jamii ya Buhemba kwa kushindwa kujenga miundombinu ya barabara,kujengashule kama inavyotakiwa.

Kutoka na adha hiyo Pasta huyo alisema kuwa Serikaliimeshindwa kuwajali wananchi wake na hivyo wanawaomba Wabunge wa Bunge laJamhuri ya Muungano kutoipitisha Wizara ya nishati na Madini mpaka hapowananchi wa eneo hilo watakapopata fidia yao.

“Hawa wawekezajimimi naona hawakuja hapa kwa lengo la kumsaidia mtu wa Buhemba huu Mgodi naonaulikuwa wa Kitapeli kabisa,wamechuma raslimali za Taifa na kushindwa kumsaidiamtu anayezungukwa na mgodi na hata kurekebisha miundombinu huska na hiiinaonyesha jinsi Serikali isivyojali wananchi wake” alisema Pasta Nyakarungu

Naye Mwalimu mstaafu Sita Nyamhanga na bi HadjaYasini walisema kuwa mgodi huo umewaachia matatizo makubwa ikilinganishwawalivyokuwa wameahidiwa wakati wanaanza uchimbaji katika mgodi huo.

“Tunavyojuani kwamba wawekezaji wanapowekeza eneo lolote lazima watu wanaozungukwa naMgodi ule wanufaike lakini hapa Buhemba sisi wananchi ndiyo tumepat tabu kabisakwani mpaka sasa hatuna shule,barabara inayopitika muda wote,eneo letu limebakiJangwa huku wakina mama wanapata tabu kutafuta maji kutokana na vyanzo vingivya maji kuchafuliwa na mgodi” alisema Mwalimu mstaafu huyo.

Kwa upande wake Bi Hadja Yasini alisema kuwawanapata tabu hata kutafuta kuni kutokana na eneo kubwa la Buhemba kubakiJangwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Kulingana na adha hiyo Bi Hadja alisema kuwa nivyema Waziri mwenye dhama huska akawasaidia watu wa Buhemba ili waweze kupatafidia zao kutokana na madhara waliyoyapata kutokana na mgodi huo.

Mgodi wa Buhemba ambao ulianza kuchimbwa mwaka 2002ni moja ya mgodi ambao ulikuwa ni mkubwa hapa nchini ukielezwa kumilikiwa naSerikali na kufungwa mwaka 2006 huku ukiacha eneo hilo la Buhemba kupotezarutuba yake

Popular Posts