Pages

Friday, August 3, 2012

Naibu Waziri Wa Viwanda Na Biashara Atembelea Maonyesho Ya Nanenane Mjini Dodoma

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Gregory Teu akitoa fedha kwenye Mashine ya kutolea fedha ya CRDB ambayo imefungwa kwenye gari la kisasa aina ya Mercedese Benzi ambalo linateknolojia ya kuzuia risasi wakati alipotembelea Maonesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Gregory Teu (kushoto) akipata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa Bw. Salum Mselem ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Farmers Center na FarmBase yanayotengeneza sumu za kuulia wadudu waharibifu wa mazao na mifugo na dawa za mifugo na mazao kwa kutumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini wakati wa maonesho ya Nane Nane.
Meneja wa shamba la mifugo la Kongwa (NARCO Kongwa RANCH) Bw. Hezron Kashalankoro (aliyevaa cap) akitoa maelezo ya Kitaalamu kwa Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Gregory Teu (aliyevaa suti) juu ya uzalishaji na ufugaji wa Ng’ombe bora wa Nyama wakati alipotembelea Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma.

Popular Posts