PRESS STATEMENT
HOTUBAYA MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) TAIFA- SANGOGUNGU KASERA
2August 20112
Ndg:Wanahabari
Ndg: wanaUVCCM wenzangu
Kwa  heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kutoa salamu zangu za dhati kwa  Watanzania na vijana wenzangu wanchi hii pamoja nanyi waandishi wa  Habari kwa kushiriki nami katika safari hiiinayolenga kuunganisha na  kujenga hatua za mabadiliko ya maisha ya Vijana waTanzania. Kwa namna ya  pekee kabisa niwashukuru na kuwaomba mshikamano vijanawenzangu wa Chama  cha Mapinduzi ambao kupitia kwao ninatumia nafasi hii kuomba ridhaa yao  ili nipate nafasi ya kuwa chemchem ya mafanikio na mabadiliko katika  maisha yetu kwa kuanzia na chama chetu. Leo hii naungana na vijana  wenzangu hawa wa ndani ya CCM, kufanya jambo moja kubwa, jambo la  kuchukua fomuya kuwania moja ya nafasi kubwa katika jumuiya ya Vijana wa  CCM Tanzania. Ninafanya kazi hii leo nikitambua mambo yafuatayo:
Kwanza, ninalenga kuleta mabadiliko yanayotazama aina ya vijana tuliopo  sasa, aina ya maisha tunayoishi na aina ya changanoto zinazotukabili  mimi nikiwa mmojawapo.
Pili kwa upekee mkubwa, nachukua fomu hii nikibaini hali ya vijana huko  tulikotoka na , changamoto tulizopitia na hatari inayotukabili mbele   kama hatua stahiki hazitaanza kuchukuliwa na vijana wa aina yangu ambao  tuna uzoefu wa kutosha wa maisha ya kawaida ambayo yanahitaji nguvu na  akili zetu na za wenzetu waliotutangulia katika kuboresha maisha yetu  ili tuweze kuwa raia wema katika nchi yetu na wanachama waadilifu wa  chama chetu na jumuiya zake.
Ndugu Waandishi wa Habari;
Kazi  hii ya kuchukua fomu ninayoifanya leo hii na kisha kuanza zoezi la  kutafuta kuungwa mkono. Ni kazi inayohitaji ushirikiano mkubwa kwa  uongozi wa Jumuiya yetu pamoja na vijana mbalimbali bila kujali itikadi  zao za vyama vya siasa. Nasema hivi kwa kutambua kuwa UVCCM ndiyo  Jumuiya pekee yenye kubeba taswira  na matarajio ya vijana wa Tanzania  na ambayo siku zote inatakiwa kusimamia maslahi na matakwa ya vijana wa  Tanzania na kwakuwa jumuhia hii ni jumuhia ya chama kinachoongoza si  chama tawala .
Ndugu zangu wanahabari na wana CCM tunafahamu tofauti kati ya kuongoza  na kutawala ndio maana nimetumia neno kuongoza, na Kama kazi hii ilikuwa  haifanyiki huko nyuma na kama ilifanyika bila kuridhisha, mimi nimeamua  kwa moyo mkunjufu kuingia kuonesha namna jumuiya yetu itakavyoweza  kuwatumikia vijana wa Tanzaniana kukiboresha chama cha Mapinduzi ili  kitambue wajibu wake kwa vijana wote waTanzania na kwa kufanya hivi  kiweze kusimamia misingi iliyolijenga Taifa hili na kuachwa na waasisi  wa Taifa letu  Hayati Baba Wa Taifa na Hayati Rais Karume ambao  walilijenga taifa letu katika misingi ya haki, usawa na ustahimilivu.
Ndugu wana habari; Katika kipindi hiki chakutafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi hii nitabakia kuongozwa na Moto isemayo: Vijana kwanza kwa taifa lenye amani na maendeleo.  Bila vijana kuangaliwa na kupewa yale wanayostahiki, ni wazi taifa  lenye amani na maendeleo halitakuwepo. Natambua fika kuwa vijana wa  Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa ile inayolenga kubaini  ndoto ya maisha yao ya sasa na siku zijazo. Naamini mimi ni mmoja wa  vijana hawa ambaye pia ninahitaji kuona vijana walio katika kilimo basi  wanaweza kupata soko la mazao yao. Vijanawabeba mikokoteni nao wanafanya  kazi hiyo kwa miaka kadhaa na kisha kuboreshaajira zao.
 Vijana wanaosoma basi wanahitimu vema na kupata ajira wanazostahiki na  pia walio makazini na waliopata nafasi za kuongoza wanaonesha mfano  wakufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii ili kuonesha kuwa vijana  tunaweza na hatuwezi kuliangusha taifa. Natambua haya ninayoyazungumza  ni mambo magumu lakini pia natambua yanahitaji mbinu nyingi ili  kukabiliana nayo. Kwa sasa natumia nafasi hii kukiomba Chama changu,  kuiomba Jumuiya Yetu ya Vijana kutambua kuwa nina  dhamira, nina nia,  nina sifa za kutosha, nina uwezo wa kufanya majukumu haya ninayoyaomba  na ninafahamu kazi za majukumu haya.
Tena nina rekodi katika umri wangu huu wa kufanya mambo ya kutukuka  ambayo rekodi yake inaweza kutazamwa pote nilipobahatika kutoa utumishi  wangu. Kwa namna isiyoonyesha kuyumba naomba kuwaeleza vijana wenzangu  kuwa kutokanana mshikamano wa vijana wenzangu kwangu ni wazi tumejiandaa  kushinda katika nafasi hii ili tuweze kuleta mwanga wa mabadiliko  katika jumuiya yetu na chama chetu katika maandalizi ya chaguzi zijazo.  Ndugu wanahabari ninatambua zipo changamoto nyingi zinazoikabili UVCCM  na changamoto hizi zinahitaji kiongozi ambaye atakuwa na uthubutu  wakuweza kukabiliana nazo, changamoto  kuuni kitaswira, kimuundo,  kiimani, kimadhumuni kama ambavyo zimehainishwa kwenyekanuni za ummoja  wa vijana.   Nina maanisha nini ninapozungumzia taswira ya UVCCM.Taswira  ya UVCCM  Taifa leo siotaswira ya kimapambano.
Historia yetu ipo wazi jumuiya ya vijana ilishiriki katika mapambano ya  kuleta Uhuru, Umoja na mshikamano mtakumbuka wakati TANU Inahangaika na  kutafuta Uhuru wa Tanganyika na Afro-Shirazi party ikipambana kuleta  Uhuru wa Zanzibar vijana waliunganishwa na jumuiya za umoja wa vijana wa  vyama hivi viwili ambavyo ni TANU YOUTH LEAGUE na ASP YOUTH LEAGUE,  zinafahamika kazi zilizofanywa na wabeba mizigo  wa Kariakoo mfano  Mzee  Rajabu Diwani, leo UVCCM sio tena yawabeba mizigo, sio tena ya   wamachingasio tena ya wakulima ,sio tena jumuiya  ya wafanyakazi ni  jumuiya  ya wafanyabiashara, watoto wa vigogo ama wenyenasaba nao ama  rafiki zao, inahitaji viongozi wenye dhamira ya dhati ambao watarudisha  jumuiya  hii kwa vijana wakitanzania na kurudisha taswira ya kimapambano  ambayo ni mapambano ya kiuchumi, kazi ya Uhuru imeshafanyika imebakia  jukumu la kuleta Uhuru wa kiuchumi na  kuwa kimbilio la vijana wote.
Ni dhamirayangu  ya kugombea nafasi hii ni kuhakikisha  awamu ya pili ya  mapambano ya kiuchumi ya umoja wa vijana inaanza rasmi. Nafahamu zipo  changamoto za kiutawala, kiuchumi na jumuiya  kuendelea kuishi kwa  kutegemea misaada na Ruzuku kutoka kwenye chama, nafahamu watendajiwana  hali mbaya kiuchumi hasa katika mawilaya, nafahamu ofisi zetu za wilaya  zina upungufu wa vitendea kazi ni dhamira yangu kubadili mwelekeo wa  utendajiwa jumuiya yetu kutoka “Business as usual” kuvalisha skafu  viongozi  na kuimba nyimbo, kuwa jumuiya yenye dira namwelekeo sahihi wa  kuwaunganisha na  kumkomboa kijana wa kitanzania.
Ndugu waandishi wa Habari; Ninafahamu matarajio yavijana wa kitanzania  yatafikiwa kupitia CCM imara na CCM inatokana na uimara wajumuiya  zake  kuwa imara na hili inawezekana kwa kupatikana viongozi Imara na mimi  nina amini ni mmoja waviongozi ambao wataifanya jumuiya yetu kuwa Imara.
Kwa kuhitimisha Hotuba yangu naomba kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi  Mungu kwa kunifanikisha kuwananyi hapa, niwashukuru wana familia yangu,  marafiki na nyie ndugu zanguwaandishi wa Habari kwa kukubali kujumuika  nami kunisikiliza leo. Niwaombe Vijana wenzangu wa CCM kuniunga mkono  katika azma hii kubwa niliyo nayo na niwakumbushe tu kuwa, zoezi hili la  kuchukua fomu nililofanya hapa leo si langu bali la vijana wote wa  Tanzania wakiwakilishwa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi.
Ni imani yangu kuwa, wana UVCCM hawatakubali kuangusha taa  hiiwaliyoiwasha kule Rorya mkoa wa Mara wao wenyewe na badala yake  wataungana namibega kwa bega ili kuufikia ushindi. Tutapitisha fomu hii  pamoja nao, tutachujwa pamoja nao na kisha tutashinda pamoja nao na  kisha kuanza kuwaongoza vijana wa Tanzania pamoja nao. Mwenyezi Mungu  Mwingi wa Rehma atubariki na kutupa nguvutufanikishe azma hii muhimu  pamoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi
Asanteni kwa kunisikiliza.
Mimi Ndg Sango Gungu  Kasera- Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM (W) Rorya
Kauli mbiu  Mbiu “Vijana kwanza kwa taifa lenye amani namaendeleo’’.
                      -