Pages

Monday, June 11, 2012

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete Wakagua Mahindi Shambani Kwao

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakikagua mahindi shambani kwao kijijini Msoga,Chalinze,wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki.Picha na Freddy Maro-IKULU

KHADIJA KOPA NA MWANAHAWA ALLY WALIVYOPELEKESHANA

Zuhura Shaaban wa Melody akiimba.
Mashabiki wa bnuruidani waliofika katika ukumbi wa Dar LIVE, Mbagala jana walipata burudani ya nguvu kutoka kwa magwiji wa taarab nchini – Khadija Kopa, malkia wa kundi la TOT, na malkia wa kundi la Melody, Mwanahawa Ally. Burudani hiyo ilisindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa.
Mwanahawa Ally akiimba wimbo wa ‘Kinyago cha Mpapure’.
Wanamuziki wa bendi ya Mashujaa, Gado ‘Field Force’ (kushoto) akiimba na Chalz Baba.
Abdul Misambano wa TOT akiimba.
Chalz Baba akiwapa raha mashabiki.
Wanamuziki wa TOT wakiitikia ‘mashairi’ ya Khadija Kopa.
Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakiwajibika.
Mkurugenzi wa ukumbi wa Equator, Hamis Slim, akimtunza Khadija Kopa.
Rapa wa Mashujaa, Ferguson, akighani na kunengua na mpiga gitaa wa bendi hiyo.
Mwanamuziki wa Mashujaa, Gado, akitoa burudani.
Khadija Kopa akiwa na mumewe kabla ya kupanda jukwaani kutoa burudani.
Mashabiki waliofurika ukumbini humo wakijimwayamwaya na burudani.

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA WAJITOLEA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi na timu yake nzima wakati walikuja kufungua zoezi la kujitolea damu kwa hiari kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) zoezi lililoandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuoni Hapo
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe akitoa neno fupi kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma waliofika katika Zoezi la Kujitolea Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula (Wa Pili Kushoto) akiwa amesimama wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe aliyeongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma, Na Balozi Job Lusinde katika zoezi la kujitolea damu kwa hiari lililofanyika siku ya leo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na Kuandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuo Hapo.
Afisa Mahusiano wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi Beatrice alipokua akitoa damu kwa hiari katika Zoezi la Kuchangia Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo huku Akishuhudiwa na Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Manongi(Mwenye Miwani)
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao Pia Wamemaliza Muda wao rasmi leo Wakiwa katika zoezi la Uchangiaji Hiari wa Damu zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo ambalo liliandaliwa na Taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosoholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO). Kutoka Kushoto Ni Emmanuel Mwakibinga akifuatiwa na Stefano Saimon.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akiaga wanafunzi na wafanyakazi waliojitoa katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) lililofanyika chuo hapo leo.Picha Zote Na Josephat Lukaza wa
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa Wanasubiri Kwenda Kutoa damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma

Kichanga kikiwa kimetupwa katika Dampo la Takataka Soweto Mbeya

Kichanga kikiwa kimetupwa katika Dampo la Takataka Soweto Mbeya
Baadhi ya akina Mama na watu wengine waliofika eneo hilo kutazama kichanga hicho ambapo Mama Mzazi hajafahamika. Hata hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi. Picha na Allt Kingo

VIONGOZI WA SERIKALI WAAGA MWILI WA BOB MAKANI

Waombolezaji mabo wengi wao ni makada wa CHADEMA wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Bob Makani wakati mwili huo ulipofikishwa katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kutolewa heshima za Mwisho.
Vioongozi wa juu wa Serikali akiwepo Rais Jakaya Kikwete (watatu kuli) Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilali(wapili kulia) Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (wa nne kulia) walihudhuria.

Popular Posts