
Magoli  mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza  katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika  dakika ya 90 ya mchezo yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe  la Kagame 2012 baada ya kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa  goli 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam.
Tanzania  ijnakila sababu ya kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya  Azam katika michuano hiyo ya mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa  michuani huyo iliingiza timu 4 zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa  katika hatua ya robo fainali.
Yanga  pia waliutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na  Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji  kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya kushambulia mwamuzi kwa ngumi.