Baadhi  ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  wakianza kufutari kwa kunywa madafu kabla ya kula futari jana  walipoalikwa katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni  kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa huo kila ifikapo mwezi kama huu  kwa futari maalum.
    Baadhi   ya Viongozi na Wananchi Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini  Magharibi,wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa  Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu Mjini  Zanzibar
    Baadhi  ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  wakiwa katika futari iliyoandaliwa jana ,katika viwanja vya Ikulu Mjini  Zanibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj  Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa  huo kila ifikapo mwezi kama huu kwa futari maalum. 
  Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika  viwanja vya Ikulu ya Zanzibar. 
    Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika  viwanja vya Ikulu ya Zanzibar. 
   Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, (wa pili kushoto) akijumuika na  akinamamawa wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Chakula cha Futari  iliyoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed  Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, (wengine kulia) Mama  Shadiya Karume, Mama Pili Balozi Seif na Waziri wa Muungano Samia Suluhu  Hassan, (kushoto). 
   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed  Shein,(wa pili kulia) akijumuika na wananchi pamoja na Viongozi wa Mkoa  wa Mjini Magharibi katika Futari, aliyowaandalia wananchi hao katika  viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar jana, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini  Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amaan Abeid  Karume,(kushoto) na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.
   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed  Shein, akisalimiana na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi  baada ya kufutari nao pamoja jana katika futari aliyowaandalia katika  viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar. 
   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed  Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi na  Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumalizika Futari  waliyowaandalia katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
   Mke  wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama  Mwanamwema Shein, (kulia) akisalimiana na mke wa Rais mstaafu wa  Zanzibar Mama Shadya Karume, baada ya Futari iliyoandaliwa kwa wananchi  wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed  Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar