Pages

Monday, August 13, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ziarani Mkoa Wa Kisiwani Pemba

Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi ya mradi wa skuli ya Istiqama uliopo katika kijiji cha Mbuyuni Mkoani Pemba Ustadhi Mohd Omar Makame akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi huo
Mjumbe wa Kamai Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa shilingi 800,000/- kusaidia ununuzi wa saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Tawi la CCM la Makombeni Mkoani Kisiwani Pemba. Sambamba na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pia akakabidhi mchango wa shilingi 300,000/- kwa ajili yha mIlango ya Tawi hilo.
Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi la CCM, Makombeni wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif Ali Iddi aliyetembelea Tawi hilo kuangalia hatua iliyofikia ya ujenzi wa Tawi hilo.
--
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea mradi huo. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono miradi yote inayoanzishwa na Taasisi, Mashirika, Jumuiya na hata Wananchi katika lengo la kustawisha Maendeleo ya Jamii hapa Nchini.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo wakati alipokuwa akikagua mradi mkubwa wa ujenzi wa Skuli inayojengwa na kusimamiwa na Jumuiya ya Istiqama Tanzania hapo katika Kijiji cha mbuyuni Mkoani Kisiwani Pemba.

Balozi Seif aliuambia uongozi wa wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa mradi huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha kwamba miundo mbinu muhimu ya maji, umeme na bara bara inawekwa ili kuona lile lengo lililokusudiwa la kuanzishwa kwa mradi huo muhimu kwa jamii linafikiwa.

Aliuagiza Uongozi huo kumuandikia barua mara moja ya changamoto wanazopambana nzo ambazo zimo ndani ya uwezo wa Serikali Kuu ili iwe rahisikwake kuziagiza Taasisi husika kupanga mikakati ya kutekeleza miundo mbinu hiyo.

Balozi Seif alisema atatumia uwezo na nafasi aliyonayo kushawishi wahisani zikiwemo ofisi za Kibalozi kusaidia ujenzi huo uliolenga kwenda hadi ghorofa tatu ambao tayari hivi sasa umeshatumia karibu shilingiMilioni mia tatu { 300,000,000/- }.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Jumuiya hiyo ya Istiqama Tanzania kwa hatua yake ya kujenga mradi huo mkubwa ambao utasaidia kusukuma mbele Maendeleo ya Elimu ya Dini na Dunia.

Alisema Jumuiya hiyo inafaa kuungwa mkono na jamii yote Nchini kwa vile tayari imeshajipanga vyema kuweka mkazo zaidi katika suala la Elimu kwa kukiandalia mazingira bora kizazi cha sasa. “ Nimevutiwa sana na mradi huu wa Elimu wenye kuleta faraja si kwa wakaazi wanaouzunguuka hapa lakini kwa Wananchi wote Nchini. Naimani kwamba utakapokamilika bila shaka utachukuwa wananfunzi wa sehemu mbali mbali Nchini”.

Alionyesha furaha yake Balozi Seif. Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Mradi huo Ustaadhi Mohammed Omar Makame alimueleza Balozi changamoto wanazopambana nazo wakati huu wa ujenzi. Ustaadh Mohd Omar alizitaja changamoto hizo kubwa kuwa ni pamoja na ukosefu a huduma ya maji safi, umeme pamoja na Bara bara licha ya juhudi walizochukuwa za kuchimba kisima bila ya mafanikio.

Alisema ujenzi wa Skuli hiyo ulioanza tarehe 1/12/2010 utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 1575, Madarasa 45 , mabweni, nyumba za walimu pamoja na msikiti lengo likiwa kunyanyua elimu ya dini sambamba na kuibua vipaji vya wanafunzi.

Mapema asubuhi Balozi Seif akiwa pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alipata fursa ya kutembelea Tawi Jipya la CCM la Makombeni pamoja na kukagua uhai wa Chama hapo katika mtaa wa Mweneza.

Akizungumza na Viongozi na Wanachama hao Balozi Seif aliwatahadharisha katika kipindi hichi cha chaguzi zinazoendelea za chama hicho wahakikishe wanawachaguwa Viongozi safi watakaokuwa mahiri katika kutekeleza Sera za chama hicho.

Alisema wakati umefika kwa Wanachama wa chama hicho kuwakataa wanachama wasiokuwa na msimamo kwa kufikiria kujinufaisha binafsi pamoja na kuvuruga chama kwa makusudi. “ Wale wanaohisi kwamba sera za Chama cha Mapinduzi zimepitwa na wakati kwa hiyari yao wangeliamua mapema kwenda kwenye vyama vyenye Sera za Dot Com na kuiachia CCM Yetu inayoamini sera za Serikali mbili Ncchini Tanzania”. Alifafanua Balozi Seif. Katika kuunga mkono harakati za kukamilisha ujenzi wa Tawi la CCM Makombeni

Balozi Seif alichangia shilingi laki nane { 800,000/- } kusaidia ununuzi wa saruji na kuahidi shilingi 500,000/- za fundi pamoja na Seti ya TV na DVD yake wakati Mkewe alichangia shilngi laki 300,000/- kusaidia milango ya Tawi hilo.

Akitoa Taarifa fupi ya ujenzi huo pamoja na uhai wa Chama Katibu wa CCM WA Tawi la Makombeni Bibi Wahida Mbaraka Mohd alisema ujenzi wa Tawi hilo umekuja ili kwenda sambamba na hadhi ya chama chenyewe kilivyo.

Bibi Wahida alisema hadi sasa ujenzi huo uliolenga kufikia gharama ya shilingi milioni 13,920,000/- umeshafikia shilingi milioni 8,000,000/-.

Katibu wa Tawi hilo alimuhakikishia Balozi Seif kwamba Wanachama wa CCM wa Tawi hilo wataendelea kuunga mkono sera za Chama chao za kuamini mfumo wa Serikali mbili Nchini Tanzania.

Alisema Wanachama hao wamejiimarisha kutoghilibiwa na vurumai zinazojichomoza Nchini za baadhi ya watu kushawishi wananchi juu yamchakato wa utoaji wa maoni ya Katiba unaolenga kuvunja Muungano.

Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

Popular Posts