Pages

Wednesday, August 8, 2012

Vodacom Tanzania Yazindua Kinyang’anyiro Cha Watengeneza Programu Wa Kujitegemea

Vodacom yazindua mashindano mapya kwa watengenezaji wa programu wa kujiteg emea. Mashindano yatatoa fursa kwa watengenezaji hao kuonyesha vipaji vyao.Mashindano kuwa katika awamu mbili, ndani na nje ya nchi.

Mshindi kupata dola 20,000. zaidi ya shilingi Milioni 30 za kitanzania. Dar es Salaam, Waendelezaji wa programu za kiteknolojia wa Tanzania sasa watapata fursa ya kuonesha vipaji vyao katika mashindano yaliyo anzishwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, yaliyopewa jina la AppStar Challenge.

Mashindano hayo yameanzishwa ili kuwapa motisha washiriki ambao wanaendeleza ubunifu wa kiteknolojia katika simu na mawasiliano na kutoa nafasi kwa washiriki kuonyesha uwezo katika kuvumbua vifaa mbalimbali vya kiteknolojia ambavyo vinaweza kutumika katika nchi zinazoendelea na kutatua matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii.Washindi watakao patikana katika mashindano ya awali ndani ya nchi husika, watapata fursa ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Afrika ya Kusini mwezi Novemba mwaka huu.

Nchi zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na, Misri, Lesotho, Tanzania, Afrika ya Kusini na Qatar.Katika mashindano ya ndani, washiriki wanatakiwa kuendeleza ubunifu katika vipengele mbalimbali kama michezo, afya ya jamii, burudani, na simu.

Mshindi mmoja katika kila kipengele atapata dola 2000 za Marekani, na baada ya hapo kwa mshiriki ambaye atakuwa ametoa programu bora atapata nafasi ya kushiriki katika michuano ya kimataifa.Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, maombi yatawekwa na kusambazwa kupitia Hifadhi ya programu ya Vodacom na Vodafone na watu binafsi kuendelea kukusanya hadi mwisho wa muda wa kuwakilisha.

Twissa alibainisha kuwa mshindi wa awamu ya kwanza ambayo inalenga Watanzania tu, atadhaminiwa na Vodacom kushiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayo fanyika Afrika ya Kusini. “Awamu ya kwanza ni ya mashindano ya ndani na watengenezaji wa programu wanatarajiwa kuanza kujisajili kwa ajili ya mashindano kuanzia tarehe 7 mwezi 9 mwaka 2012 na wataweza kuziendeleza na kuzichapisha programu zao kwenye hifadi ya programu ya Vodacom,” alifafanua Twissa.

Alibainisha kuwa wakati wa michuano ya kimataifa, programu mbili zitakazoshinda zitapelekwa katika mchujo utakaofanywa na jopo la wataalam wa kimataifa wa masuala ya teknolojia kutoka Vodacom, zaidi ya hayo, wabunifu watapata nafasi ya kuonyesha kazi zao kwa njia ya vitendo mbele ya jopo la majaji.

“Mashindano haya yatamuwezesha mshidi kupata zaidi ya Dola elfu 20000 za Kimarekani. Tunajivunia kuwa sehemu ya mashindano haya makubwa. Ninaamini kuwa yatatoa nafasi kwa watengenezaji wa programu kuonyesha kile walichonacho, na ninatoa wito kushiriki katika mashindano haya na tunawatakia kila la kheri,”


Popular Posts