Pages

Thursday, November 8, 2012

BENDI YA MSONDO KUZINDUA VYOMBO VIPYA LIDAZ CLUB


BENDI Kongwe ya muziki wa dansi nchini Tanzania, Msondo Ngoma Music Band,  inatarajia kuzindua vyombo vyake vipya, walivyokabidhiwa hivi karibuni na Kampuni ya KONYAGI.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema ''Tumeshapewa vyombo na Kampuni ya Konyagi ambavyo tutavizindua mbele ya mashabiki wetu siku ya Ijumaa pale Leaders Club, siku ya Ijumaa hivyo wapenzi wote wa bendi ya Msondo mnaombwa kuhudhuria kwa wingi ili kuona vyombo vipya'' alisema Mhamila
Pamoja na kupata burudani za bendi hiyo zikiwemo nyimbo za zamani na za sasa kwa ajili ya kuanza burudani za mwisho wa wiki, Super D aliongeza kwa kusema wapenzi watakaokuja siku hiyo watapata burudani za radha tofauti tofauti kwani wamepanga kukonga nyoyo za mashabiki wao kwa kutumia vyombo vyao vipya. 

Bendi hiyo siku ya Jumapili itamaliza burudani za wik end katika ukumbi wa Max Bar Ilala bungoni.

Mkurugenzi wa Bendi hiyo Muhidini Maalimu Gulumo ataongoza kundi zima la wana msondo ngoma akiwemo Said Mabera,Shabani Dede, Romani Mn'gande, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hassani Moshi na wendine kibao kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki.

Popular Posts