Pages

Thursday, November 8, 2012

SERIKALI YA JAPAN YATIA SAINI MSAADA WA SHILINGI MILIONI 380 MIRADI MIPYA LINDI NA MTWARA


Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya TALIA ya mjini Mtwara, Ayubu Samuel wakitiliana saini mkataba wa makubaliano kati ya ubalozi wa japan na TALIA kwaajili ya ujenzi wa mradi wa  upanuzi wa shule ya wenye ulemavu Dinyecha Wilayani Mtwara utakao gharimu zaidi ya shilingi Milioni 192 na ujenzi. Anaeshuhudia kulia ni Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia.
 Mkurugenzi wa taasisi Women in Social Entrepreneurship (WISE) ya mkoani Lindi, Astronaut Bagile (kushoto) akitiliana saini na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada (wa tatu kulia) msaada wa ujenzi wa bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu shilingi Milioni  188. Wengine wanaoshuhudia utiaji saini huo kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Lindi, Frank Maghali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Nassor Hamid Nassor na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi,  Ashimun Mnzava.Utiaji saini huo wa makubaliano hayo ya msaada ulifanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Novemba 7, 2012.
 Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia, akizungumza jambo wakati wa utiliaji saini huo uliofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Novemba 7, 2012. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada
 Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada akisoma hotuba yake kwa viongozi wa mkoa wa Lindi na Taasisi ya Women in Social Entrepreneurship (WISE) ya mkoani Lindi wakati wa utilianaji saini mkataba wa makubaliano kati ya Ubalozi wa Japan na Taasisi ya WISE msaada wa ujenzi wa bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu shilingi Milioni  188. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Nassor Hamid Nassor.
Balozi wa Japan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Lindi na viongozi wa taasisi ya WISE baada ya kutiliana saini. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Meya wa Lindi, Frank Maghali,  Balozi wa Japan,  Masaki Okada , Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila,  DC wa Lindi, Nassor Hamid Nassor na Makurugenzi Mtendaji wa WISE, Astronaut Bagile.

Popular Posts