Pages

Monday, July 2, 2012

CUF KUFANYA MKUTANO JANGWANI JULAI 15 2012

Kwa niaba ya CUF- Chama Cha Wananchi natumia fursa hii kukukaribisheni wanajukwaa wenzangu katika MKUTANO MKUBWA NA WA KIHISTORIA WA CUF utakaofanyika katika viwanja vya jangwani mnamo Julai 15 mwaka huu.

Njooni mumsikilize Mwenyekiti wa Jopo la Magwiji wa Uchumi Duniani, Full Bright Visiting Economist Profesor, The International Figure, Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.

Sambamba naye atakuwepo Gwiji la Siasa Barani Afrika, The First Vice President of The Government of National Unity of Zanzibar, Katibu Mkuu wa CUF Taifa Mhe. Maalim Seif Sharif Hamadi

Njooni msikilize Sera adhimu na maridhawa za VISION FOR CHANGE, Njooni msikilize Mustakabali wa Uchumi wetu kama Taifa na nini cha kufanya hasa katika kipindi hiki cha Mchakato wa Katiba Mpya.

Njooni msikilize ufumbuzi mbadala wa 'mazonge' yanayoendelea hapa nchini kwa sasa
Confirmation ya kufika kwa wanabidii katika mkutano huo ni muhimu kwa ajili ya ku-observe protocals.

Shime wanabidii, kwa pamoja tulijenge Taifa letu, Tanzania yenye neema inawezekana

HAKI SAWA KWA WOTE

Popular Posts